Habari Njema 100%

Habari Njema 100% Njooni tumrudie Bwana HOSEA 6:1-3

2:7 "Yeye aliye
na sikio, na alisikie neno
hili ambalo Roho
ayaambia
makanisa.Yeyey
ashindaye, nitampa kula
matunda ya mti wa
uzima, ulio katika
bustani ya Mungu"

12/10/2014
29/10/2013

Somo la Leo

Waroma 8
Kuishi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu

1Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu kwa wale ambao katika maisha yao wameungana na Kristo. 2Maana, sheria ya Roho iletayo uhai kwa kuungana na Kristo Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo. 3Mungu ametekeleza jambo lile ambalo sheria haikuweza kutekeleza kwa sababu ya udhaifu wa binadamu. Mungu alimtuma Mwanae akiwa mwenye mwili sawa na miili yetu sisi wenye dhambi, ili aikabili dhambi, na kwa mwili huo akaiangamiza dhambi. 4Mungu alifanya hivyo kusudi matakwa ya haki ya sheria yatekelezwe kikamilifu ndani yetu sisi ambao tunaishi, si kwa nguvu za kibinadamu, bali kwa nguvu ya Roho. 5Maana, wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya mwili, hutawaliwa na fikira za mwili. Lakini wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya Roho Mtakatifu, hutawaliwa na fikira za Roho. 6Fikira za mwili huleta kifo; fikira za Roho huleta uhai na amani. 7Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii. 8Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

9Lakini nyinyi hamuishi kufuatana na matakwa ya mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo. 10Lakini k**a Kristo yumo ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, kwenu Roho ndiye uhai kwa sababu mmefanywa kuwa waadilifu. 11Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka kwa wafu ataipa uhai miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

12Hivyo basi, ndugu zangu, tunalo jukumu, lakini si la kuishi kufuatana na maumbile ya kibinadamu. 13Kwa maana, k**a mkiishi kufuatana na matakwa ya maumbile ya kibinadamu, hakika mtakufa. Lakini, k**a kwa njia ya Roho mnayaua matendo yenu maovu, basi, mtaishi. 14Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni watoto wa Mungu. 15Kwa maana, hamkumpokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watumwa tena na kuwatia hofu, bali mmempokea Roho mwenye kuwafanya nyinyi watoto wa Mungu, na kwa Roho huyo, sisi tunamwita Mungu, “Aba,” yaani “Baba!” 16Naye Roho mwenyewe anathibitisha na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu. 17Basi, kwa vile sisi ni watoto wa Mungu, tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo pamoja na Kristo; maana, tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake.
Utukufu ujao

18Naona kuwa mateso ya wakati huu wa sasa si kitu kamwe k**a tukiyalinganisha na ule utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhihirishe watoto wake. 20Kwa maana, viumbe viliwekwa katika hali ya kutojiweza kabisa, si kwa hiari yao, ila vilifanywa hivyo kwa mapenzi ya Mungu. Hata hivyo yapo matumaini, 21maana hivyo viumbe navyo vitaokolewa kutoka katika utumwa wa uharibifu, vishiriki uhuru mtukufu wa watoto wa Mungu. 22Kwa maana tunajua kwamba mpaka hivi sasa, viumbe vyote vinalia kwa maumivu k**a ya kujifungua mtoto. 23Wala si hivyo viumbe peke yake, bali hata sisi tulio na huyo Roho, aliye wa kwanza wa zawadi za Mungu; sisi pia tunalalamika ndani yetu, tukingojea tufanywe watoto wa Mungu, nazo nafsi zenu zikombolewe. 24Maana kwa matumaini hayo sisi tumekombolewa. Lakini tumaini halina maana ikiwa tunakiona kile tunachotumainia. Maana ni nani anayetumaini kile ambacho tayari anakiona? 25K**a tunakitumaini kile ambacho hatujakiona bado, basi, tunakingojea kwa uvumilivu.

26Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka. 27Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu.

28Tunajua kwamba, katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao, yaani wale aliowaita kadiri ya kusudi lake. 29Maana hao aliowachagua tangu mwanzo, ndio aliowateua wapate kufanana na Mwanae, ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30Basi, wale ambao Mungu aliwateua ndio hao aliowaita; na hao aliowaita ndio hao aliowafanya kuwa waadilifu na hao aliowafanya waadilifu ndio hao aliowashirikisha pia utukufu wake.
Upendo wa Mungu

31Kutokana na hayo, tuseme nini zaidi? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, nani awezaye kutupinga? 32Mungu hakumhurumia hata Mwanae wa pekee, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote. Ikiwa amefanya hivyo, je, hatatujalia pia mema yote? 33Ni nani atakayewashtaki wateule wa Mungu? Mungu mwenyewe huwaondolea hatia! 34Ni nani atakayewahukumu? Hakuna! Maana Kristo ndiye aliyekufa, tena alifufuka kutoka kwa wafu na anakaa upande wa kulia wa Mungu. Yeye anatuombea! 35Ni nani awezaye kututenga na upendo wa Kristo? Je, ni taabu, au dhiki, au mateso, au njaa, au ukosefu wa nguo, au hatari, au kifo? 36 K**a Maandiko Matakatifu yasemavyo:

“Kwa ajili yako, twakikabili kifo kutwa kucha;

tunatendewa k**a kondoo wa kuchinjwa.”

37Lakini, katika mambo haya yote, tumepata ushindi mkubwa kwa msaada wake yeye aliyetupenda. 38Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; 39wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu.

14/10/2013

Ni nani ana Moyo mgumu wa kusamehe na kukupenda zaidi, wakati ulimsaliti na kumdhihaki yeye??
Mungu anao upendo wa dhati kwako na bado anakuita kwake!

13/10/2013

Kamwe hatokuacha, katika bonde la mauti, mtumaini yeye naye atakuponya katika ulimwengu wa mateso na shida. "Mungu ni wa Mapendo"

12/10/2013

Neema ya Bwana utaendelea kutawala daima, mpaka utimilifi wa dahali....

07/10/2013

"Mpendwa Endelea kutusaidia kuwajulisha hata Jamaa zako , Kuupenda Ukurasa wetu wa Facebook, Tuendelee kuzungumza zaidi kuhusu Habari Njema 100% kote ulimwenguni.

Mwenyezi Mungu anatupenda. Sote tutabarikiwa

Like and Share

Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu, hata kuna wakati wa kila jambo chini ya mbingu: wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa...
07/10/2013

Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu, hata kuna wakati wa kila jambo chini ya mbingu: wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa kilichopandwa;+ wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; wakati wa kulia na wakati wa kucheka; wakati wa kuomboleza na wakati wa kurukaruka; wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe; wakati wa kukumbatia na wakati wa kuepuka kukumbatia; wakati wa kutafuta na wakati wa kuacha kutafuta kilichopotea; wakati wa kuweka na wakati wa kutupa; wakati wa kupasua+ na wakati wa kushona, wakati wa kukaa kimya na wakati wa kusema; wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia; wakati wa vita na wakati wa amani.

Mtendaji ana faida gani katika jambo analofanyia kazi ngumu?

Yaliyotokea WestGate Kenya, Mwenyezi Mungu hatayafumbia kamwe, atatenda, na ataonesha Muujiza katika hili.Damu iliyomwag...
25/09/2013

Yaliyotokea WestGate Kenya, Mwenyezi Mungu hatayafumbia kamwe, atatenda, na ataonesha Muujiza katika hili.
Damu iliyomwagika italipwa kwa Sala zetu, Mungu hakawii kujibu Maombi.

Mwenyezi MUNGU Akawajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu tunachopita.

Ni mara ngapi Moyo wako Umekuwa na Hofu juu ya Hukumu Ijayo??Ni mara ngapi Umekuwa ukihisi Kujutia uovu na Dhambi ulizon...
25/09/2013

Ni mara ngapi Moyo wako Umekuwa na Hofu juu ya Hukumu Ijayo??

Ni mara ngapi Umekuwa ukihisi Kujutia uovu na Dhambi ulizonazo??

Yote yaweza kuwa ni Maswali Magumu kwako, Lakini Mwenyezi MUNGU Hajachoka kuwa na wewe, Kwa Moyo wakona MATENDO YAKO, Mrudie sasa na uwe katika kumbukumbu ya Kitabu cha Uzima.

04/06/2013

2:7 "Yeye aliye
na sikio, na alisikie neno
hili ambalo Roho
ayaambia
makanisa.Yeyey
ashindaye, nitampa kula
matunda ya mti wa
uzima, ulio katika
bustani ya Mungu"

[Huu ndo wakati wa kuitengeneza njia iliyo ya kweli katika Maisha.]

MUHIBIRI 4:8-138  Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake h...
03/06/2013

MUHIBIRI 4:8-13
8 Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.

9 Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

10 Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

11 Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?

12 Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

13 Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu.

Zaburi 231  Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.2  Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya ma...
03/06/2013

Zaburi 23

1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.

2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.

6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.

Address

Arusha
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari Njema 100% posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Habari Njema 100%:

Share