24/08/2026
Vijana, dunia ya leo imejaa fursa, tumia mitandao ya kijamii kwa hekima, jifunze, jenga mahusiano mazuri, tangaza vipaji vyako na tafuta njia za kujiongezea kipato,
popote ulipo iwe mjini au kijijini, tumia mazingira yako kujijenga na kujenga wengine,
mazingira yasiwe sababu ya wewe kutofikia ndoto zako, bali heshima, bidii na ubunifu viwe funguo za milango ya maendeleo yako,
Kanisa likupa nafasi ya kuonyesha vipaji na uwezo wako usiache fursa hizo zipite, tumikia, shiriki na tumia kipawa ambacho Mungu amekupa,
Zaidi ya yote, baki ndani ya Kristo, mshirikishe Mungu katika mipango yako, kwa sababu mafanikio ya kweli si mali pekee, bali ni kuwa na maisha yenye kusudi, heshima na imani, tumia fursa za leo kuijenga kesho yenye baraka na mafanikio!
"Jaribu Sala Inatenda" ~ Padre Patrick Peyton CSC.
Family Rosary Holy Cross Family Ministries