Efatha Church Jerusalem

Efatha Church Jerusalem Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Efatha Church Jerusalem, Pentecostal Church, mbauda, Arusha.

NENO LA SIKU  NAMCH: MERCY GEORGE KOMBA SOMO: UPENDO WA KWELI1 Wakorintho 13:4–7“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hau...
12/09/2026

NENO LA SIKU NA

MCH: MERCY GEORGE KOMBA

SOMO: UPENDO WA KWELI

1 Wakorintho 13:4–7
“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari, haujivuni; haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, hauoni uchungu, hauhesabu mabaya…”

Upendo ni moja ya zawadi kubwa ambazo Mungu amempa mwanadamu. Lakini upendo wa kweli si maneno pekee; unaonekana kupitia matendo, uvumilivu, msamaha na kujali wengine.

Yesu alitufundisha kwamba kumpenda Mungu na kumpenda jirani ni msingi muhimu wa maisha ya kiroho.

Mathayo 22:37–39
“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote… Mpende jirani yako k**a nafsi yako.”

1. Upendo huvumilia

Mtu anayependa kwa kweli hujifunza kuwa mvumilivu. Si kila mtu atakuwa mkamilifu, na si kila jambo litakwenda tunavyotaka.

Upendo haukimbii haraka wakati wa changamoto; hujaribu kuvumilia na kujenga.

2. Upendo husamehe

Kushikilia maumivu na chuki kunaweza kuufanya moyo ukose amani. Mungu anatuita tujifunze kusamehe.

Wakolosai 3:13
“…msameheane, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; k**a Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo hivyo nanyi.”

Kusamehe hakumaanishi kwamba kosa lilikuwa sahihi, bali ni kuamua kutokubeba chuki moyoni.

3. Upendo hauhusudu

Upendo wa kweli haufurahii mwingine anaposhindwa. Badala yake, unafurahia mafanikio ya wengine.

Tunapompenda mtu, tunaweza kusema kwa moyo wa kweli:
“Ninafurahi kwa ajili yako.”

4. Upendo haujivuni

Upendo hauhitaji kujiona bora kuliko wengine. Unatufundisha kuwa wanyenyekevu, kusikiliza na kuheshimu watu wengine.

Wafilipi 2:3
“…kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.”

5. Upendo unaonekana kwa matendo

Si rahisi kusema “nakupenda” lakini matendo yetu yawe kinyume. Upendo wa kweli unaonekana katika kusaidia, kujali, kuheshimu, kusamehe na kuwa pamoja na wengine wakati wa shida.

1 Yohana 3:18
“Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.”

6. Mungu ndiye chanzo cha upendo

Upendo mkuu kuliko yote ni upendo wa Mungu kwetu. Mungu alitupenda hata kabla hatujawa wakamilifu.

Yohana 3:16
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee…”

Hii inatufundisha kwamba tunapopokea upendo wa Mungu, tunapaswa pia kujifunza kuwaonyesha wengine upendo.

Tafakari ya leo

Jiulize:
• Je, ninawapenda watu kwa maneno tu au pia kwa matendo?
• Je, ninaweza kusamehe nilipoumizwa?
• Je, ninafurahia mafanikio ya wengine?
• Je, upendo wangu unaonyesha tabia ya Kristo?

BARAKA ZA IJUMAAMungu akutangulie katika kila hatua utakayopiga leo. Akufungulie milango ambayo hakuna mwanadamu awezaye...
11/09/2026

BARAKA ZA IJUMAA

Mungu akutangulie katika kila hatua utakayopiga leo. Akufungulie milango ambayo hakuna mwanadamu awezaye kuifunga, akupe amani moyoni, furaha katika familia, afya, hekima na nguvu mpya.

Kila kilichokulemea, Mungu akibebe.
Kila unachokiomba kwa moyo wa imani, Mungu akijibu kwa wakati wake.
Kila mlango uliofungwa, Mungu akufungulie ulio bora zaidi.
Kila machozi ya jana, Mungu ayabadilishe kuwa ushuhuda wa kesho.

“Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana; tutashangilia na kuifurahia.” -Zaburi 118:24

NENO LA SIKU  NA MCH: MERCY GEORGE KOMBA SOMO: WAABUDUO HALISIYohana 4:23–24“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo w...
10/09/2026

NENO LA SIKU NA

MCH: MERCY GEORGE KOMBA

SOMO: WAABUDUO HALISI

Yohana 4:23–24

“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli; kwa maana Baba awatafuta watu k**a hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Kuabudu siyo kuimba tu.
Kuabudu siyo kuinua mikono tu.
Kuabudu siyo kwenda kanisani tu.

Kuabudu ni maisha yanayompa Mungu heshima, nafasi na utukufu.

Mtu anaweza kuimba vizuri mbele za watu lakini moyo wake ukawa mbali na Mungu. Anaweza kuinua mikono yake ibadani, lakini maisha yake yasimshuhudie Mungu.

Ndiyo maana Yesu alisema Baba anawatafuta waabuduo halisi.

1. Mwabuduo halisi humwabudu Mungu kwa moyo

Mungu haangalii tu tunachofanya kwa nje; anaangalia moyo.

1 Samweli 16:7

“Maana Bwana haangalii k**a mwanadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.”

Mwabuduo halisi hamwabudu Mungu kwa ajili ya watu kumuona.

Anaweza kumwabudu Mungu hata akiwa peke yake.

Ibada ya kweli inaanzia moyoni kabla haijaonekana midomoni.

2. Mwabuduo halisi humwabudu Mungu katika roho

Yesu alisema tumwabudu Mungu “katika roho.”

Hii inaonyesha ibada inayotoka ndani kabisa ya mtu, ikiwa na uhusiano wa kweli na Mungu.

Si desturi tu.

Si mazoea tu.

Si kwa sababu watu wengine wanafanya.

Ni kwa sababu moyo wako unampenda Mungu na unatamani kuwa karibu naye.

Zaburi 42:1

“Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, kadhalika nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.”

Mwabuduo halisi ana kiu ya Mungu.

3. Mwabuduo halisi humwabudu Mungu katika kweli

Kuabudu katika kweli maana yake ni kumwabudu Mungu kulingana na ukweli wa Neno lake na siyo kulingana na hisia zetu pekee.

Yohana 17:17

“Neno lako ndiyo kweli.”

Huwezi kusema unampenda Mungu lakini kwa makusudi ukaishi kinyume na Neno lake.

Mwabuduo halisi anatamani:
• Kusoma Neno la Mungu.
• Kulielewa.
• Kulitii.
• Kuishi kulingana nalo.
• Kumheshimu Mungu katika maamuzi yake.

Ibada ya kweli inaonekana pia katika maisha ya kila siku.

4. Mwabuduo halisi humwabudu Mungu hata katika nyakati ngumu

Ni rahisi kumwabudu Mungu unapopokea baraka.

Lakini je, utaendelea kumwabudu wakati mambo hayaendi k**a ulivyotarajia?

Ayubu alipoteza vitu vingi, lakini bado alisema:

Ayubu 1:20–21

“Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.”

Hii ni ibada ya kiwango cha juu.

Mwabuduo halisi hamwabudu Mungu kwa sababu ya kile anachopata kutoka kwake; anamwabudu kwa sababu Mungu anastahili kuabudiwa.

5. Mwabuduo halisi ana maisha yanayolingana na ibada yake

Ibada haiishii kanisani.

Inaendelea nyumbani.

Inaendelea kazini.

Inaendelea kwenye biashara.

Inaendelea katika mahusiano.

Inaendelea wakati hakuna mtu anayekuona.

Warumi 12:1

Paulo anatufundisha kutoa miili yetu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu.

Hii inatufundisha kwamba maisha yetu yote yanaweza kuwa ibada.

Namna unavyoongea, unavyowatendea watu, unavyofanya kazi na unavyofanya maamuzi inaweza kumtukuza Mungu.

6. Mwabuduo halisi ana moyo wa unyenyekevu

Hakumwabudu Mungu ili ajionyeshe.

Anajua kwamba kila alicho nacho kimetoka kwa Mungu.

Yakobo 4:6

“Mungu huwapinga wenye kiburi, bali huwapa wanyenyekevu neema.”

Ibada ya kweli inamfanya mtu amwinue Mungu, siyo kujitukuza mwenyewe.

ALHAMISI YENYE BARAKA Alhamisi hii iwe siku ya neema, amani na ushindi katika maisha yako. Mungu akutangulie katika kila...
10/09/2026

ALHAMISI YENYE BARAKA

Alhamisi hii iwe siku ya neema, amani na ushindi katika maisha yako.

Mungu akutangulie katika kila hatua utakayopiga, akufungulie milango ambayo hakuna mwanadamu awezaye kuifunga, na akupe nguvu unapohisi umechoka.

Kile kilichokwama, Mungu akifungue.
Kile kilichopotea, Mungu akirejeshe.
Kile unachokiomba kwa imani, Mungu akijibu kwa wakati wake.
Kila hofu iondoke na amani ya Mungu itawale moyoni mwako.

Hesabu 6:24-25 “Bwana akubariki, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili.”

Usiogope kuhusu kesho. Endelea kumtumaini Mungu, kwa sababu hata pale ambapo huoni njia, Mungu tayari anaiona.

NENO LA SIKU NAMCH: MERCY GEORGE KOMBA SOMO: MOYO WA SHUKRANIMoyo wa shukrani ni hali ya ndani ya mtu ya kumtambua Mungu...
09/09/2026

NENO LA SIKU NA

MCH: MERCY GEORGE KOMBA

SOMO: MOYO WA SHUKRANI

Moyo wa shukrani ni hali ya ndani ya mtu ya kumtambua Mungu, kuthamini wema Wake, na kumshukuru kwa yale aliyotenda, anayofanya, na hata yale ambayo bado tunayangojea.

1 Wathesalonike 5:18

“Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.”

1. Shukrani ni kumtambua Mungu katika maisha yetu

Wakati mwingine tunapokea baraka na tunaanza kufikiri kwamba tumefanikiwa kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini moyo wa shukrani unatukumbusha kwamba Mungu ndiye chanzo cha uzima, nguvu, afya, nafasi na mafanikio tuliyo nayo.

Zaburi 103:2

“Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote.”

Usisahau yale ambayo Mungu amekutendea.

2. Moyo wa shukrani hauangalii matatizo pekee

Mtu anaweza kuwa na jambo moja ambalo halijafanikiwa na akasahau mambo kumi ambayo Mungu amemsaidia.

Moyo wa shukrani unasema:

“Bado sijafika ninapotaka kufika, lakini namshukuru Mungu kwa hatua ambayo tayari nimefika.”

Kuna mambo ambayo tuliyachukulia kuwa ya kawaida ka bile kuamka, kupumua, kuwa na familia, kupata chakula, kuwa na nguvu, kupata nafasi nyingine ya kuishi lakini yote yanaweza kuwa sababu ya kumshukuru Mungu.

3. Shukrani si kwa wakati mzuri tu

Ni rahisi kumshukuru Mungu mambo yanapokwenda vizuri. Lakini shukrani ya kweli huonekana zaidi wakati wa changamoto.

Ayubu 1:21
Ayubu alipoteza vitu vingi, lakini bado alisema:

“BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.”

Hii haimaanishi kwamba tunapaswa kufurahia maumivu, bali tunajifunza kumtumaini Mungu hata katikati ya hali ngumu.

4. Shukrani hubadilisha namna tunavyoona maisha

Unapokuwa na moyo wa kulalamika, unaanza kuona kile ambacho huna.

Lakini unapokuwa na moyo wa shukrani, unaanza kuona kile ambacho Mungu tayari amekupa.

“Namshukuru Mungu kwa kile nilicho nacho na ninaamini kwa kile ninachokisubiri.”

5. Shukrani inapaswa kuambatana na maombi

Biblia inatufundisha kupeleka mahitaji yetu kwa Mungu pamoja na shukrani.

Wafilipi 4:6

“Katika kila jambo kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.”

Kwa hiyo unapomwomba Mungu, usianze na mahitaji pekee. Anza kwa kumshukuru Mungu kwanza.

JUMATANO YA BARAKA NA NEEMA Leo ni siku mpya ambayo Mungu ametupa kwa neema yake. Ninaibariki Jumatano hii iwe siku ya a...
09/09/2026

JUMATANO YA BARAKA NA NEEMA

Leo ni siku mpya ambayo Mungu ametupa kwa neema yake.
Ninaibariki Jumatano hii iwe siku ya amani, furaha, afya, mafanikio na milango mipya.

Kila jambo litakalofanywa leo na mikono yetu libarikiwe. Kila hatua tutakayopiga iongozwe na Mungu, na kila changamoto tunayokutana nayo ipate suluhisho kwa wakati wake.

Mungu atutangulie katika kila jambo, atulinde na mabaya, atupe hekima katika maamuzi yetu, na atufungulie milango ambayo hakuna mwanadamu awezaye kuifunga.

Jumatano hii iwe mwanzo wa ushuhuda mpya, majibu ya maombi na sababu mpya za kumshukuru Mungu.

Usikate tamaa; kile Mungu alichoanza katika maisha yako, bado anaendelea kukikamilisha.

NENO LA SIKUNA MCHUNGAJI MERCY GEORGE KOMBA SOMO: USIKATE TAMAA, MUNGU BADO ANA MPANGO NA MAISHA YAKO Kuna nyakati katik...
08/09/2026

NENO LA SIKU

NA MCHUNGAJI MERCY GEORGE KOMBA

SOMO: USIKATE TAMAA, MUNGU BADO ANA MPANGO NA MAISHA YAKO

Kuna nyakati katika maisha ambazo mambo hayaendi k**a tulivyotarajia. Unaomba, unasubiri, unafanya juhudi, lakini majibu yanaonekana kuchelewa. Wakati mwingine unaweza kujiuliza, “Mungu yuko wapi katika hali ninayopitia?”

Lakini leo nataka nikukumbushe jambo moja muhimu: Kuchelewa kwa jibu siyo kukataliwa. Mungu anaweza kuwa kimya, lakini hiyo haimaanishi kwamba hayupo. Kuna wakati Mungu huruhusu mchakato uwe mrefu kwa sababu anakuandaa kwa kile unachokiomba.

Usidharau kipindi cha kusubiri.

Mbegu inapopandwa ardhini, haionekani mara moja. Kwa nje unaweza kuona udongo tu, lakini chini ya ardhi kuna mchakato unaoendelea. Vivyo hivyo, kuna mambo Mungu anayafanya ndani ya maisha yako ambayo bado huwezi kuyaona.

Huenda leo unaona milango imefungwa, lakini Mungu anaweza kuwa anakuandalia mlango ambao hautahitaji kulazimisha. Huenda unaona umesimama, lakini Mungu anaweza kuwa anakuandaa kwa hatua kubwa zaidi. Huenda unalia leo, lakini kesho machozi yako yanaweza kuwa sehemu ya ushuhuda wako.

Isaya 40:31 “Wamtumainio BWANA watapata nguvu mpya; watapaa juu kwa mbawa k**a tai; watakwenda mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”

Kwa hiyo, usiache kuomba kwa sababu majibu yamechelewa. Usikate tamaa kwa sababu safari imekuwa ngumu. Usijione umesahaulika kwa sababu wengine wamefanikiwa kabla yako.

Kila mtu ana wakati wake. Mungu hakupangii maisha yako kwa ratiba ya mtu mwingine. Usijilinganishe na wengine; endelea na safari yako, kwa sababu Mungu ana wakati wake maalumu kwa ajili yako.

Leo amua kumkabidhi Mungu hofu zako, mipango yako, familia yako, kazi yako, masomo yako na ndoto zako. Mwambie:

“Mungu wangu, hata nisipoelewa kinachoendelea, bado nitakuamini. Hata nisipoona njia, bado nitaamini kwamba Wewe unaijua njia. Nipe nguvu ya kusubiri bila kukata tamaa na moyo wa kuendelea mbele bila kuogopa.”

Kumbuka:
Mungu hajachelewa.
Mungu hakusahau.
Mungu hajakuacha.
Mchakato unaendelea, na wakati wako utafika.

Leo tembea kwa imani, si kwa hofu. Tabasamu hata k**a unapitia changamoto, kwa sababu Mungu anayekushikilia leo ndiye atakayekufikisha kwenye ushuhuda wako kesho.

Warumi 8:28 “Mambo yote hufanya kazi pamoja kwa ajili ya mema kwa wale wampendao Mungu.”

BARAKA ZA SIKU:
Mungu akutangulie katika kila jambo. Akufungulie milango ya baraka, akupe amani moyoni, akulinde na mabaya, akubariki katika kazi ya mikono yako, na akufanye uone matunda ya uvumilivu wako.

Usikate tamaa. Endelea kuamini. Bado kuna jambo zuri Mungu analifanya katika maisha yako.

JUMANNE YA BARAKA NA NEEMALeo ni siku mpya ambayo Mungu ametupa kwa neema yake. Naibariki Jumanne hii kwa jina la Yesu. ...
08/09/2026

JUMANNE YA BARAKA NA NEEMA

Leo ni siku mpya ambayo Mungu ametupa kwa neema yake. Naibariki Jumanne hii kwa jina la Yesu. Kila hatua nitakayopiga iwe chini ya uongozi wa Mungu, kila mlango uliofungwa ufunguke, na kila jambo jema nililokusudiwa lipate kibali.

Ninaamini kuwa leo sitatembea kwa hofu, bali kwa imani. Sitatawaliwa na changamoto, bali nitashinda kwa nguvu za Mungu. Kila mpango wa kunikatisha tamaa ugeuke kuwa ushuhuda, na kila kilio kigeuke kuwa furaha.

Mungu atangulie mbele yangu, alinde njia zangu, aibariki kazi ya mikono yangu na anipe hekima katika kila uamuzi nitakaoufanya.

Jumanne hii iwe siku ya neema, favor, mafanikio, amani, afya, furaha na ushindi.

Zaburi 118:24 “Hii ndiyo siku aliyoifanya BWANA, tutashangilia na kuifurahia.”

JUMATATU YA NEEMA NA USHINDI Leo si mwanzo wa wiki tu, bali ni ukurasa mwingine ambao Mungu ameufungua kwa neema yake. K...
07/09/2026

JUMATATU YA NEEMA NA USHINDI

Leo si mwanzo wa wiki tu, bali ni ukurasa mwingine ambao Mungu ameufungua kwa neema yake. Kuna mambo ambayo macho hayawezi kuyaona, lakini moyo unaamini kwamba tayari yanaandaliwa.

Wiki hii sitatembea kwa kile ninachokiona, bali kwa kile ninachoamini. Maana wakati mwingine Mungu hufanya kazi kubwa katika ukimya, kabla matokeo hayajawa ushuhuda.

Kila hatua iwe na sababu yake.
Kila mlango unaofunguka uwe kwa wakati wake.
Kila kinachochelewa kinifundishe kusubiri.
Kila kinachopotea kiache nafasi ya kilicho bora zaidi.
Na kila machozi ya siri yapate tafsiri yake kwa wakati wa Mungu.

“Tazama, nimeweka mbele yako mlango uliofunguliwa, wala hakuna awezaye kuufunga.” — Ufunuo 3:8

TUNAELEKEA KATIKA KUSANYIKO KUU LA MWAKA 2026! Muda umefika wa kukusanyika pamoja katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya iba...
06/09/2026

TUNAELEKEA KATIKA KUSANYIKO KUU LA MWAKA 2026!

Muda umefika wa kukusanyika pamoja katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya ibada, ushirika, kujifunza na kupokea kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili yetu.

Mahali: Precious Center, Kibaha
2026 Annual Gathering

“Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja kwa umoja.”
Zaburi 133:1

Tunaelekea kusanyika! Usikose sehemu yako katika kusanyiko hili la mwaka 2026.

Address

Mbauda
Arusha

Telephone

+255768588885

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Jerusalem posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share