30/08/2024
vimepangiliwa kwa kufuata mitindi ya kiuandishi. Vitabu vyenye muundo mmoja wa kiandishi vimewekwa katika fungu moja mfano vitabu vya torati, Historia, Ushahiri na unabii. CHATI YA MPANGILIO WA BIBLIA MPANGILIO WA VITABU VYA AGANO LA KALE Mtindo wa kiuandishi Majina ya vitabu Jumla Sheria Mwanzo – kumbukumbu la torati 5 Historia Yoshua – Esta 12 Mashairi Ayubu – Wimbo uliobora 5 Kinabii / manabii Isaya - malaki 17 Jumla ya vitabu vy agano la kale 39 Mtindo kiuandishi Majina ya vitabu Jumla Injili Mathayo – Luka 4 Historia Matendo ya Mitume 1 Barua Warumi – Yuda 21 Unabii Ufunuo wa Yohana 1 Jumla ya vitabu agano jipya 27 UANDISHI WA BIBLIA LA KALE Wanadamu walianza kuandika k**a mwaka 3200k.k. Kuandikwa kwa kwanza kulifanywa katika mabamba ya towe nyororo katika mawe na katika ngozi waliziunganisha ngozi na kuandika ngozi hizo ziliitwa “Parchment” kisha ngozi hizo baada ya kuziandika walizivingisha na kuitwa magombo “Scrolls’. Katika Biblia neno kuandika lilitajwa kwanza katika Kutoka 17:14 Mungu alipomwambia Musa kuandika mambo ya ushindi wa Israeli juu ya waamaleki k**a mwaka 1440k.k BIBLIA NA MIAKA Zamani za kale watu hawakuandika tarehe na miaka k**a tufanyavyo sasa hivi walikuwa wakitaja nyakati za wafalme wa zama zao wenyewe tu. Mfano katika Isaya 6:1 katika mwaka aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu sana na kuinuliwa na pindo la vazi lake vikalijaza hekalu.” Luka 3:1 – 2 “Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake kaisari Teberio Pontio Pilato alipoalipokuwa liwali wa Uyahudi na Herode Mfalme wa Galilaya na Filipo ndugu yake Mfalme wa Itulea na nchi ya Trakoniti Lisania Mfalme wa Abilene wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa.Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria jangwani.” Hivi ndivyo ilivyokuwa katika nchi zote na nyakati zote za zamani hawakutaja miaka k**a tunavyotaja sasa. Lakini iliandikwa hivi katika mwaka Fulani wa kutwala kwake Mfalme Sulemani. Hivyo wataalamu wa Biblia hufanya kazi ya kuchunguza na kuunganisha miaka na nyakati ya wafalme wanchi mbalimbali. Hii ni kutokana kwamba kila nchi ina hesabu yake yenyewe ya miaka. Hivyo wataalamu wa Biblia na Theologia hawakubaliani katika mambo yote kuhusu miaka, hivyo katika kutaja miaka tunatumia neno “Kama” kwa sababu hakuna anaejua mwaka kamili ila tunafanya makisio baada ya kufanya utafiti kwa kina. Kalenda tunayotumia sasa iligunduliwa na mtaalamu mmoja mtawa anaeitwa Dionysius Exiguus. Warumi walihesabu miaka tangu kujengwa kwa Rumi. Miaka kabla ya kuzaliwa kwa Kikristo huhesabiwa kwa kurudi nyuma toka kwa Yesu Kristo kurudi nyuma na inaitwa K.K / BC na baada ya kuzaliwa kwa Yesu huhesabiwa toka kwa Yesu kwenda mbele na inajulikana k**a BK/AD. TAFSIRI ZA BIBLIA ZA ZAMANI SANA Kutokana na kufifia kwa lugha ya kiebrania mpaka kufikia mwaka 200 K.K na lugha hii kusahaulika na wengi na kutotumiwa na wengi ndipo ilibidi Agano la kale litafsiriwe katika lugha za mataifa mengi k**a vile Kiaramu, Kisuria, Kigiriki, Kiarabu, Kimisri n.k. SEPTUAGINTI YA KIGIRIKI Mwaka 300 – 200 K.K. Agano la kale lilitafsiriwa k**a lugha ya Kigiriki iliitwa Septuaginti. kwa sababu inasemekana ilitafsiriwa na watu 70. Septuagintu haiwezi kufaa kutumika k**a asili ya kutafsiri Biblia tena katika lugha zingine kwa sababu tafsiri yake inajichanganya kunasehemu imetafsiriwa neno kwa neno na kupoteza mantiki{ maana} halisi na sehemu zingine hazifahaamiki vema. Ila inasaidia wataalamu wa Biblia na Theolojia kujua maana ya maneno ya kiebrania cha zamani zile. Septuaginti ilikuwa Biblia ya wakristo wa kwanza na ilisomwa siku za Bwana Yesu ilisaidia sana watu wengi kulielewa Neno la Mungu wale ambao hawakuweza kusoma kiebrania. TARGUMU ZA KIARAMU Ni Agano la kale ambalo lilitafsiriwa kwa kiaramu baada ya lugha ya kiebrania kupoteza mashiko na kufifia watu walianza kutafsiri maneno yake katika masinagogi ya wayahudi walisoma kwa kiebrania na mtumwingine alitafsiri kwa kiaramu. Baadae tafsiri hizo ndipo zilipoandikwa na kusomwa na zilipewa jina la Targumu lenye maana ya tafsiri k**a Kiaramu. KISHAMU (KISURIA) ni tafsiri za Biblia ambazo zilitafsiriwa kwa lugha ya kishamu. Wakristo walipoongezeka katika nchi ya Shamu walihitaji kuwa na Biblia katika lugha yao ya kishamu na hivyo Biblia ilitafsiriwa kwa Kishamu. VULGALE ZA KITATIRI Ni Biblia iliyokuwa imetafsiriwa kwa kilatini. Mwaka 329 alizaliwa mtu mmoja aliyeitwa Jerome alikuwa ni mtaalamu alitafsiri Biblia nzima kwa lugha ya kirumi ambay o ni kilatini tafsiri hiyo iliitwa Vulgate. Vulgate ni tafsiri nzuri na imefwatwa na watu wengi katika kutafsiri maandiko. KASORO NDOGO NDOGO ZA KIUANDISHI Kabla ya kuangalia kasoro ndogo ndogo za kiuandishi zilizopo katika Biblia tuna budi kutambua namna ya uandishi uliotumika katika kuandika Biblia zamani za kale na hata vitabu vinginevyo vya kawaida. Ni vyema kutambua kwamba mashine za kuchapia vitabu hazikuwepo wakati wa kale mpaka mwaka wa 1450 BK ndipo zilipogunduliwa kwa hiyo kwa muda wa miaka 2730.........inaendelea