07/02/2024
Yona 1:3-6
[3]Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.
[4]Lakini BWANA alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.
[5]Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
[6]Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
Lisikie neno hili wapo watu wakiwa katika maisha yako lazma maisha yayumbe nini kinacho sababisha maisha yako hayaendelei
Umeshawai jiuliza hili swali nini kizuizi katika maisha yako??
Vipo vizuizi vingi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya maisha yako kuendelea vizuizi ivyo leo nina vipa jina la yona katika merikebu
Kuna vizuizi k**a ushirikina
Watuwengi wamefungwa na nguvu za giza katika maisha yao kiasi kwamba hakuna kitu chochote kinacho fanikiwa
Kizuizi cha dhambi kunawatu wamefanya dhambi na zile dhambi zimekuwa kizuizi cha Mungu kuwabariki maisha yao
Kuna watu wanamarafiki wabaya ambayo wamekuwa kizuizi katika maisha yao
Ndugu yangu waondoe kina yona wote katika maisha yako ili Mungu awe na nafasi katika kuyabariki maisha yako
Mungu hawezi kukibariki kukiwa na kizuizi kinacho mfanya yeye Ashindwe kukubariki
Mwondoe yona leo ili Maisha yako yaweze kuendele