Winners Prayerful Center & Church

Winners Prayerful Center & Church Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Winners Prayerful Center & Church, Religious organisation, Arusha.

SOMO: MLINZI WA MJI*UTANGULIZI*• Kila mji una mlizi na kila mji una mamlaka yake• katika ulimwengu wa roho kunakua kuna ...
07/08/2022

SOMO: MLINZI WA MJI

*UTANGULIZI*

• Kila mji una mlizi na kila mji una mamlaka yake
• katika ulimwengu wa roho kunakua kuna ukuta wa kuingia mkoa fulani mfano Arusha ina malango yake ya kuingia na kutoka Arusha na malango hayo yanakua na walinzi wake
• kila mlinzi wa mjui kuna vitu anataka mji uwe vipi au mkoa uwe vipi eitha kielimu/kiuchumi/kiafya n.k mfano mlinzi wa mji anaweza akaamua mji fulani uwe na wasomi kiasi gani na hali yao ya uchumi ikae vipi
• walinzi wa mji wanaweza wakakaa ndani ya baba/mama au mlezi ili kuilinda familia yake au uzao wake usitoke hata k**a kwenye familia kuna mtoto wa k**e na wakiume ambae umri wake umefika wa kuoa au kuolewa lakini bado yupo nyumbani na hana sababu yoyote.
zaburi 127:1 imeandikwa “1 Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
• nyumba inajengwa na mji unalindwa
• ikiwa Mungu hausiki kwenye ujenzi wako anaelinda inakua ni bure, hivyo basi kwenye nyumba yako Mungu anatakiwa awe mlinzi mkuu

isaya 21:8 imeandikwa “8 Ndipo akalia k**a simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu.

Mwanzo 19:1 imeandikwa “1 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala.
4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote.
5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.
6 Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.
7 Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.
8 Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu.
9 Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango.
10 Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango.
11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango.
12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa;
13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu.
14 Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa k**a achezaye machoni pa wakweze.

• Lutu alikua na kuhani wake ambae ni ibrahimu
• Kuna vitu vinatokea ila hatujui k**a Mungu ndo kasababisha vitokee
• Kuna namna unapoingia kwenye mji wale wenyeji wanaweza wakawahi kukumiliki na kukufanya vile watakavyo
• Ili uweze kufanikiwa kwenye mji uliohamia lazima uwamilki wao kwanza
Mathayo 12:29 imeandikwa “29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.
• Mwenye nguvu akiweza kukuteka anaweza akauza kila ulichonacho mfano anaweza akauza akili/ mikono ya biashara au nyota ya biashara sasa ili kuweza kurudisha vitu hivyo lazima uwe na nguvu za kuuteka mji huo
Marko 3:27 imeandikwa “27 Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

• Mtu hawezi kuingia kwenye nyumba ya mtu bila kumteka Yule alindaye mji

Luka 11:21-22 imeandikwa “21 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama;
22 lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang'anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.

• Mtu anaweza kua na nguvu lakini asilinde pia anaweza akawa na silaha lakini asilinde na kumpa nafasi adui ya kumshambulia

UKIRI
Bwana Yesu ninakushukurun kwa ajiliya siku ya leo ambayo bwana umeifanya kwa kusudi lako na utukufu wako maana umeikusudia siku hii mimi na watu wa nyumbani mwangu nishiriki ibada hii ni nikaisikia sauti yako maana leo ni siku ya tofauti kwangu maana umenipa neema ya kulisikia neno lako kwa habari ya walizi wa mji na namna wanavyofanya kazi leo Bwana umeniweka mimi ili niwe baraka kwa wengine kupitia vitu ambavyo nimevitoa kwa ajili ya wengine maana Mungu umesema nikimvika mtu asie na mavazi nawe utanivika mimi asante mungu kwa ajili ya kibari chako ambacho umekiachilia kwangu.Bwana Yesu leo ninakuja mbele zako nianafanya vita na kila walinzi wa kipepo waliosimama kwenye mji wangu kwa mamlaka ya jina la Yesu leo ninawaamuru kila walinzi waliotumwa kulinda mji wangu teketea kwa jina la Yesu wachawi wote wasoma nyota wote waganga washirikina waliowatuma walinzi ili kuilinda hatua yangu, elimu yangu biashara yangu leo ninawateketeza wote kwa moto ulao. Leo ninawapiga walinzi wa mji wote imeandikwa “mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama;
leo natangaza mimi ni mwenye nguvu zaidi yao na mimi ni mtawala na mmiliki maana nmepewa neema nimiliki na nitawale na chochote walichoiba wakauza hazina na mafanikio leo wanaachia kwa damu Yesu leo kila ngome ya wakuu wa mji walionishikilia na kunifunga kwa nmna yoyote leo napiga ngome yao kwa jina la Yesu na kila ngome iliozuia huduma na mafanikio yangu leo ninaibomoa sasa hivi kwa damu ya Yesu kila walinzi wa mtaa wanaolinda hatma yangu maana wamejua Mungu ameweka nini ndani yangu leo ninawateketeza kwa jina la Yesu. kila waliponishikilia leo wananiachia kwa mamlaka ya jina la Yesu. Ewe mlinzi ulieshikilia hatma yangu na mafanikio yangu ninakuteketeza kwa jina la Yesu. Leo Bwana ninaifungua mipaka yangu ya kumiliki na kutawala kwa jina Yesu na leo ninamshambulia yule mlinzi wa mji alietumwa ili kuilinda hatma yangu na leo naweka ulinzi mkali kwenye mipaka ya mji wangu na Mipaka ya watu wa nyumbani mwangu kwa jina la Yesu .

01/08/2022

Natabiria wiki hii ni wiki Yako ya upendeleo 🙏

SOMO: ROHO YA KIBALI NA UPENDELEOUTANGULIZI Ukifanikiwa kuwa na kibali utafanikiwa kwenye maisha yako maana kibali kika...
23/07/2022

SOMO: ROHO YA KIBALI NA UPENDELEO
UTANGULIZI
 Ukifanikiwa kuwa na kibali utafanikiwa kwenye maisha yako maana kibali kikankukutanisha na wakuu, kibali kinamfanya mtu asihilishe sehemu ambayo alikua hastahili
 Mfano ester alikua na kibari kwa mfalme na kwa watu wengine .
 kutonana na kile kibali alichokua nacho ester alivikwa crown ya ufalme na vazi la kifalme
 ukipata kibali kuna nguvu fulani ndani yako ambayo inaweza ikaleta vitu chanya
 ukiwa na kibali kila kitu kinakufuata lakin i ukiwa huna kibari kila kitu unachotaka kukifanya kinakua na ugumu fulani mfano hata k**a unatafuta kazi inakubidi uombee roho ya kibari iwe juu yako ili upate kazi bila kutumia nguvu
 kibali cha mtu kikipatikana au kikiachiliwa kila kitu kinamfuata
zaburi 19:4 imeandikwa “14 maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, ee bwana, mwamba wangu, na mwokozi wangu.
 mfano kwenye ndoa maneno yakipata kibari ndoa inakua na amani
 KABLA YA KUTOA WAZI AU KUCHANGIA MADA OMBEA KIBARI KWENYE LILE WAZO ILI WAZO LAKO LIPATE KIBALI
ZABURI 106 :4-5 IMEANDIKWA “4 Ee Bwana, unikumbuke mimi, Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. Unijilie kwa wokovu wako,
5 Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.

MWAZO 19:19 IMEANDIKWA “19 Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa.
 S

LUKA 1:80 IMEANDIKWA “80 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.
 ni vema kujua kua uanataka kuongezeka
 neno la mungu ndilo linalomfanya mtu kukua na kuongezeka k= nguvu rohoni

Esta 2:15-16 imeandikwa “15 Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona. 16 Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake.

 esta alipata kibali kwa mfalme na kwa watu wote
 esta alipata neema na kibali machoni pa mfalme kuliko mabikira wote na akavikwa taji la kifamle na akamfanya kua malkia baaadala ya vasht
 esta alipata upendeleo kutokana na kibari alichokua nacho

Esta 8:4-5 imeandikwa “4 Ndipo mfalme alipomnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu. Basi Esta akaondoka, akasimama mbele ya mfalme.
5 Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme.
 tunapaswa kuyaombea maombi yote tuyaombayoyapate kibali mbele za mungu.

Mwanzo 4:1-7 imeandikwa “1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.
2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 K**a ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

 sadaka inamfanyanmtu apate kibari k**a habili alivyopata kibari kwa mungu kutokana na nsadaka yake pia sadaka inamfanya mtu akose kibari kutokana na sadaka alieitoa(kaini)

 ukitenda vyema unaopata kibali

mathayo 14:6-11 imeandikwa “6 Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode.
7 Hata akaahidi kwa kiapo ya kwamba atampa lo lote atakaloliomba.
8 Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.
9 Naye mfalme akasikitika; lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya wale walioketi chakulani pamoja naye, akaamuru apewe;
10 akatuma mtu, akamkata kichwa Yohana mle gerezani.
11 Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule kijana; akakichukua kwa mamaye.
 mlango wa kibari ukifunguka na ukatumia ile fursa vibaya inaaaaakupeleka kwenye laana k**a mtoto wa mfalme (herodia)

MALAKI 1:6 imeandikwa “6 Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, k**a mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na k**a mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? Bwana wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? 7 Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya Bwana ni kitu cha kudharauliwa.

 Sadaka inaweza iakaleta kibari na upendeleo pia inaweza ikaleta uharibifu

DALILI 7 ZA MTU ALIEPOTEZA/ALIEIBIWA KIBALI
 Alikua anakubalika saana sasa hakubaliki
 Anaaza kuporomoka kiuchumi-hata k**a alikua ana biashara nyingi zenye mauzo mauzo yatasuka kwa aslimia kubwa/mfano k**a alikua anaitwa kwenye semina zenye malipo mazuri ataaza kuitwa kwenye semina zisizo na malipo mazuri.
 Unaazish kitu au jambo na wakati wa kuaza watu wanalipokea vizuri na baadae lile jambo lako linakua halina soko na akitokea mtu mwingine akafanya k**a wewe ulivyofanya mtu huyo akapata kibari maradufu
 Alieibiwa kibari sura yake itaaza kuharibika hata akabadilisha kila ain ya mafuta lakini mtu Yule sura yake itaharibika
 Aliebiwa kibari cha kinywa atakachoongea chochote hakitakubaliwa na kinywa cha huyo mtu kinakua kinajaa mate muda wote mfano Mtu alieibiwa kibari pale anapotaka kujitetea basi huharibu kabisa pia chochote atakachoongea hatasikilizwa
 Usipokua na kibari hata ukipewa mamalaka huwezi kukubalika na kuheshimika kwa sababu huna kibali
 Kila utakacho fanya hata k**a ni chema huwezi kukubarika na watu

MAOMBI YA KUOMBEA KIBARI NA KUREJESHA KIBARI KILICHOIBIWA
Bwana Yesu ninakuja mbele zako nwaba siku hii yako ya leo ninkushukuru bwana kwa ajili ya maarifa ulionip leo na kwa jili ya pumzi na afya njema ulionipa leo Bwana nasema santé kwa ajili ya siku ya leo siku ya pekee maana umenipa neema ya kusikia neno lako leo ninakuja mbele zako Bwana ninaomba unisamehe mahali popote amabapo Bwana nilijikwaa nikaenda kinyume na sharia yako na magizo yako maana mimi ni mwandamu leo Bwana ninaomba msamaha kwa kila machukizo yote mbayo Bwana nmekutendab . leo ninainua mikono yangu mbele zako Bwana niaomba rehema zako na nimetambua kwa sababu ya uovu a na dhambi adui akapata nafasi ya kunisambulia kwenye kazi yangu/ masomo/ mahusiano leo bwana ninakuja mbele zako maana imeandikwa akusamehe maovu yako yoke naakuponye na magonjwa ee bwana ninaomba unisamehe dhambi zote na ninaomba uniondolee kila hukumu kwa jina lako takatifu. leo bwana ninaomba unitakase na kuniosha kwa damu yako bwana ninaomba takasa masikio yangu ambayo Bwana kupitia masikio yangu nimesikia vitu ambavyo vimelichafua hekalu lao bwana leo ninaomba safisha kinywa changu ambapo kupitia kinywa changu nikampa ibilisi nafasi ya kunishambulia na kunifunga leo bwana nmetambua nilipotenda dhambi nimetambua nilimpa ibilisi nafasi ya kunishambulia na kuiba kibali changu leo bwana ninaitumia damu yako takatifu ili kunyamazisha kila kafara zote zilizomwagwa sehemu yoyote ili kuiba kibari changu kwa malaka ya jina la Yesu. lro Bwana ninafanyanya vita na kila adui alieiba kibari changu ili nisifanikiwe/ nisifanye biashara leo ninawashambulia wote na ninawatekekteza kwa moto wa Mungu leo bwana nawwamuru achia kibari changu kwa mamlaka ya jina la Yesu.kwa damu ya Yesu kila alieshikilia kibari cha uso/ kinywa/ uso leo naamuru vyote viachiliwe kwa jina la Yesu.leo naamuru adui yoyote alieshikilia mikono/uso wa biashara ili nisifanye biashara leo ninaamuru achia kila kitu ambacho mmekishikilia kwa mamlaka ya jina la Yesu.ewe adui ulieshikilia kibari changu cha ndoa leo ninawaamuru achia kwa jina la Yesu ewe adui ulieiiba kibali cha elimu yangu ukashikilia akili yangu leo ninawahambulia wote walioshikilia akili yangu kwa jina la Yesu.leo ninaamuru ngome na kilamadhabau ambayo imeshikiliwa kwa jina la Yesu leo natangaza katika ulimwengu wa roho leo kibali changu elimu/kazi/ndoa/biashara kiachiliwe kwa jina la Yesu.

20/07/2022

Natabiri juu Yako Yale yaliyokuwa magumu kwako yakàonekane mepesi kuanzia sasa Kwa jina la YESU 🔥

TUOMBEE Kenya nimeonyeshwa ajali za helicopter mbili zitatokea na nimeonyeshwa kuwa Kuna utulivu na amani kwenye kipindi...
18/07/2022

TUOMBEE Kenya nimeonyeshwa ajali za helicopter mbili zitatokea na nimeonyeshwa kuwa Kuna utulivu na amani kwenye kipindi hiki Cha kampeni lakini kutatokea vurugu kubwa na wengi kuumia mara tu uchaguzi utakapo Anza 🔥🔥🙏

18/07/2022

Ombea Kenya

17/07/2022

Niwatakie Ibada njema yakufunguliwa sana

■}Unaweza onekana dhaifu machoni pa wanadamu lakini ukaonekana mwenye nguvu machoni pa Mungu ■}Unaweza onekana mgonjwa m...
13/07/2022

■}Unaweza onekana dhaifu machoni pa wanadamu lakini ukaonekana mwenye nguvu machoni pa Mungu
■}Unaweza onekana mgonjwa machoni pa wanadamu na ukaonekana mzima machoni pa Mungu
■}Unaweza onekana mjinga machoni pa wanadamu lakini Mungu anakuona mwenye Hekima
🙏🙏🙏furaha yangu nikuwa nawewe siku zote.

13/07/2022

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Winners Prayerful Center & Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share