boundlesslifeministry

boundlesslifeministry A place to learn and know more of your God. Commit to serve Him in a more intimate way. Also a place to bring more to Christ. Prayes _ Intercession

You have a need and you need prayers for God's intervention, you can contact us through available means

09/08/2026

Mungu anatukuzwa kwa wewe kutenda matendo mema ambayo aliyakusudia uenende katika hayo ndani ya Kristo!

09/08/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

2. Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako
Maisha ni kuzaa matunda
🍎 Zaa tunda la roho = upendo...
🍎 Zaa tunda la akili
🍎 Zaa tuna la mikono = chochote unachokifanya kwa mikono yako kizae
🍎 Zaa tunda la Neno = uwe Neno linaloishi
🍎 Zaa tabia ya Uungu

09/08/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

2. Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako

Katika Wakolosai Biblia inasema, Kristo Yesu ndie uhai wetu - kiini cha maisha yetu.
Tunaishi ili kufanya kile ambacho Kristo alifanya - kila mwamini ana sehemu yake ya kufanya katika kazi ambazo Yesu alifanya.
Wewe k**a mwamini una sehemu yako maalum ambayo ni wewe tu unaweza kufanya kwa namna yako kupitia Kristo anayeishi ndani yako.
Kristo ni Neno - Neno limekusudiwa liishi kupitia mazungumzo yako, mikono yako, huduma, shule, biashara, kazi, akili yako, karama na vipawa vyako.
Matunda unayozaa yanadhihirisha kile ulichobeba. Wewe umembeba Kristo, umebeba uzima, umebeba majibu na suluhisho la wengi.
Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako katika kila eneo la maisha yako kwa utukufu wa Mungu.

02/08/2026

Live the plan!!

02/08/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

2. Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako

🔥 Kristo alikuja kuzivunja kazi za Ibilisi ambazo zote kiini chake ni dhambi na kutokea hapo mengine yote yanazaliwa.
🔥 Kristo - maana yake ni aliyepakwa mafuta! Hivyo wewe ni kiungo cha aliyepakwa mafuta - maana yake kila aliye ndani ya Kristo amepakwa mafuta...umepakwa mafuta kuhubiri habari njema kwa masikini, kuwaweka huru waliofungwa, kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika...kuponya wagonjwa, kufufua wafu, kutakasa wenye ukoma - kueneza uzima wa Mungu katika ulimwengu wako kupitia Kristo anayeishi ndani yako.
🔥 Kristo alisema kila amwaminiye Yeye atafanya yote ambayo Yeye aliyafanya alipokuwa duniani na atafanya makubwa zaidi ya hayo. Yoh 14:12. Hii ni kwa sababu Kristo anaishi na kutenda kazi sasa hivi kupitia mimi na wewe tunaomwamini.
🔥 Kristo hakuja kutuonyesha namna ambavyo Mungu mbinguni anaishi bali alikuja kutuonyesha namna ambavyo Mungu anaishi na kutenda kupitia mwanadamu hapa duniani. Maisha ya Kristo ndio maisha yetu kupitia Roho wa Kristo anayekaa ndani yetu.
🔥 Kupitia Roho Mtakatifu - sisi tuko ndani ya Kristo na Kristo yuko ndani yetu; na Kristo yuko ndani ya Mungu na Mungu yuko ndani ya Kristo. Kwa maana hiyo Mungu yuko ndani yetu katika mwili mmoja - Mwili wa Kristo!! Glory Halellujah!

"Resource ambayo tunaitumia kuishi ni Kristo mwenyewe"

12/07/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

Sehemu ya 2: Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako.

Kristo anaishi kupitia mwili wako kutenda matendo mema.
Yale ambayo Kristo alikuwa anayafanya alipokuwa katika mwili anaendelea kuyafanya kupitia mwili wake, ambao mimi na wewe ni viungo vya huo mwili.
Sisi ni mawakala wa Kristo, watu wanapata huduma za Kristo kupitia sisi.
Hiyo ndio maana ya kuzaa matunda - tunamuwakilisha Kristo. Tunazaa matunda
1. Tunapoeneza uzima wa Kristo kwa wengine.
Sisi tumepewa Uzima tele na tunaupeleka kwa wengine. Wewe umetumwa katika ulimwengu wako k**a "mwokozi"
2. Tunapotafuta na kuokoa kilichopotea - kupitia wewe watu wamuone Mungu asiyeonekana akitenda kazi kupitia wewe.
3. Kristo anapoponya na kufufua wafu kupitia wewe
4. Tunapozivunja kazi za Ibilisi katika maisha ya watu na katika ulimwengu wetu.

Hii inawezekana kwa sababu Kristo na wewe ni mwili mmoja, mnashiriki Roho mmoja, nia moja na mwili mmoja. Wewe na Kristo ni 'mtu mmoja'. Ni ajabu lakini kweli.

12/07/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

Sehemu ya 2: Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako.

Kristo anaishi kupitia mwili wako kutenda matendo mema.

Katika Mwanzo 1: 26-28 Mungu alimuumba mwanadamu kimakusudi k**a mwakilishi wake ili atimize makusudi yake.
Katika Waefeso 2:10 inasema...Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Mungu ametuumba tena ndani ya Kristo kupitia kuzaliwa mara ya pili tutimize yale aliyoaandaa tangu mwanzo tunayoyaona katika Mwanzo 1:28
Tuko ndani ya Kristo k**a viungo vyake - sisi ndio vitendea kazi vyake, mikono na miguu yake hapa duniani
Kristo anatenda kazi leo hapa duniani kupitia sisi - huu ni mpango wa Mungu
Kuishi kwetu ni kumpa Kristo nafasi ya kutenda k**a Mungu alivyotukusudia

Katika mwanzo 1:28 kuna matendo mema kadhaa ambayo yameainishwa pale k**a kusudi la maisha.
1. Maisha ni kuzaa
Maisha ni kuzaa matunda ya haki
Tunaishi kwa imani ili kuzaa matunda ya haki kwa sababu sisi ni wenye haki wa Mungu ndani yake Kristo. Kazi yetu ya kwanza ni kuzaa matunda.

12/07/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

Sehemu ya 2: Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako.

✍️Maisha yako yanaendeshwa na Ufahamu wako.

Unaishi kulingana na kile unachofahamu, huwezi kuishi zaidi au kinyume na ufahamu wako.
Ufahamu wako unajenga picha ya ndani kuhusu maisha yako. Picha uliyonayo ndio inaongiza hatua zako.
Katika neema yake Mungu amekupa akili za kumjua Yeye pia amekupa mbegu ya imani ya Mwana wa Mungu.
Imani hii inakuwezesha kuona udhihirisho wa utendaji wa uungu ulio ndani yako.

28/06/2026

LESSON SERIES: MAISHA NI ZAIDI YA CHAKULA

2. Maisha ni Kristo kuishi kupitia mwili wako

Neema Juu ya Neema.

1 Yohana 4:9 inasema... Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
Tafsiri ya AMP inasema
1John.4.9 - In this the love of God was made manifest (displayed) where we are concerned: in that God sent His Son, the only begotten or unique [Son], into the world so that we might live through Him.

⭐️ Tulipookoka Mungu amewekeza "Yeye" mwenyewe ndani yetu kupitia Kristo anayekaa ndani yetu. Maisha yetu ni Kristo kuishi kupitia sisi; kweli ya kuwa Kristo anaishi ndani yetu inapaswa kuwa uhalisia na uzoefu wetu wa maisha kila siku.

⭐️ Paulo anasema katika Wagalatia 2:20 - Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.

⭐️ Huu ni upande muhimu wa neema inayotuwezesha kuishi maisha k**a mawakala wa Mungu duniani. Yohana 1:16 inazungumza namna ambavyo katika utimilifu wa Kristo tumepokea neema juu ya neema.
Maana mojawapo ya neema ni utendaji wa Mungu kupitia mwanadamu. Kupitia Yesu anayeishi ndani yetu tumekirimiwa kutembea katika kiwango kimoja cha utendaji wa Kiungu hadi kiwango kingine.

16/06/2026

Count yourself transformed eternally!!

1 day to go!

Contact us 0783711195

Address

Arusha

Telephone

+255758463340

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when boundlesslifeministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to boundlesslifeministry:

Shortcuts

Share