Efatha Church Sharon - Arusha HQ

Efatha Church Sharon - Arusha HQ KANISA LA EFATHA ARUSHA. Huduma ya Uponyaji na Ukombozi kwa damu ya YESU KRISTO. Mark7:34

Nguvu ya maa lava insomnia uovu wako,ukiwepo uovu wa aina yeyote ile wewe unakuwa huru kwa huo, hivyo usimwachie ibilisi...
16/09/2020

Nguvu ya maa lava insomnia uovu wako,ukiwepo uovu wa aina yeyote ile wewe unakuwa huru kwa huo, hivyo usimwachie ibilisi akulaumu kwa mambo yaliopita.

Ezekiel 18:14- 19 “Na k**a yeye huyo akizaa mwana, naye ameona dhambi zote za Baba yake alizozitenda, akaogopa, asifanye...
09/09/2020

Ezekiel 18:14- 19 “Na k**a yeye huyo akizaa mwana, naye ameona dhambi zote za Baba yake alizozitenda, akaogopa, asifanye neno lolote k**a hayo. Hakula juu ya milima wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli wala hakumtia najisi wa jirani yake wala hakumdhulumu mtu wala hakutwaa kitu kiwekwe rehani wala hakumnyanganya mtu mali yake kwa nguvu bali amewapa wenye njaa chakula chake, na kuwafunuka nguo walio uchi”

Ni kweli Baba zetu walitenda uovu lakini tumetambua na kuukimbia uovu na utumishi wetu utaishi na uhai utatangazwa. Uhai wako na uhai wa maisha yako utatangazwa juu yako maana umeijua sheria ya Mungu.

Sasa ili kutoka kwenye utumwa wa nchi na utumwa wa nyumba ya Baba yako kuna kutoka na hapo ndipo kunako kutoka katika utumwa wa nchi. Mwanzo 12:1 Sasa anza kuomba kutoka katika utumwa wa nchi au kijiji ukitoka omba kutoka katika utmwa wa nyumba ya baba yako kisha ombkuijua sheria ya Bwana.

Warumi 8:15 “kwakuwa hamkukmpokea tena Roho wa utumwa wa utumwa iletayo hofu, bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hio twalia, Aba, Yaani Baba”

Tunapopiga hizi roho za utumwa wa nchi pamoja na utumwa wa nyumba ya Baba yako pia omba kupokea roho ya Baba.

1samwel 16:12-15
Basi akatuma, naye akamleta kwao, naye alikuwa mwekundu mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza, Bwana akasema, ondoka, umtuie nmafuta; maana huyu ndiye”

Sasa roho ya Baba ilitoka kwa samweli na kuwa juu yake na leo roho ya baba inaenda na mtu mmoja kwa maana mafuta katika pembe yalimiminika juu yangu nami leo naiachilia juu yako.

2. Utumwa wa nyumba ya baba yakoKuna watu wanakuwa wametoka katika utumwa wa nchi lakini wamekandamizwa katika utumwa wa...
09/09/2020

2. Utumwa wa nyumba ya baba yako
Kuna watu wanakuwa wametoka katika utumwa wa nchi lakini wamekandamizwa katika utumwa wa nyumba za baba zao. kwahiyo wanahitaji kukombolewa. Kwahiyo kuna vifungo na utumwa unaotoka na utumwa wa familia.

Ndio maana anasema nakukomboa kutoka katika nyumba ya utumwa hii ni ule uovu unaotokana na nyumba ya utumwa sasa inahitaji ukombozi. Kwahiyo ukishabatizwa katika nchi ya utumwa unahitaji kukombolewa katika utumwa wa nyumba ya Baba yako.

Maombolezo 5 :7 “Baba zetu walitenda dhambi, hata hawako na sisi tumeyachukua maovu yao”

Anazungumzia maovu ya Baba, kwahiyo uovu wa nyumba unawafuata wana. Kuna utumwa wa nyumba, Ibrahimu na watu wake aliwapelekwa utumwani kwasababu Alizaa na kijakazi wake na huu ndio ulikuwa utumwa wa familia, ukombozi wa nyumba ya utumwa unakombolewa leo maana damu ya Yesu inatosha na leo tunanunuliwa kwa damu na kutoka katika utumwa wa nyumba ya Baba yako.

Hatuhitaji sasa kusema ohoo unajua Baba yangu alikuwa mganga wa kienyeji lakini leo tunatoka japokuwa tulichanjwa chale leo tunakombolewa kwa damu ya mwanakondoo. Kila utumwa wa nyumba ya baba yangu,

utumwa wa ulevi lakini leo nakombolewa toka nyumba ya utumwa pamoja na uzao wangu unakombolewa na leo lazima ahadi ya Bwana inatimia kwangu maana uovu wa baba yangu unakombolewa toka nyumba ya utumwa.
Unapokuwa kwenye utumwa wa nyumba ya utumwa ni nini kinatokea

Maombolezo 5:7-10 “Baba zetu walitenda dhambi, hata hawako na sisi tumeyachukua maovu yao. Watumwa wanatutawala, hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu kwasababu ya upanga wa nyikani, ngozi yetu ni nyeusi k**a tunuu, kwasababu ya hari ya njaa ituteketezayo”

Unakuwa unatawaliwa hata ukiensda kazini lakini hauoni pendo, sio k**a unataka hapana ni utumwa. Pili chakula kinaleta shida hii huu nao ni utumwa.

IBAYA YA KUTOKA UTUMWANI (JIONI) KANISA LA EFATHA– SHARON, ARUSHAMCHUNGAJI: JAMES NYANSIKASOMO: AHADI ZA KUTOKA KATIKA U...
09/09/2020

IBAYA YA KUTOKA UTUMWANI (JIONI) KANISA LA EFATHA– SHARON, ARUSHA
MCHUNGAJI: JAMES NYANSIKA
SOMO: AHADI ZA KUTOKA KATIKA UTUMWA WA NCHI PAMOJA NA NYUMBA

Mika 6:4 “kwa maana nalikupandisha kutoka nchi ya misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami naliwapeleka Musa na Haruni na Miriamu watangulie mbele yako”
Hapa tunaona mambo makubwa matatu

1. Nailikupandisha kutoka katika nchi,
Kuna utumwa unaotokana na kuwa katika nchi, ndio maana anasema nalikupandisha kutoka katika nchi, hii ina maana gani? Kuna utumwa ambao watu wanakwenda kutokana na nchi huu unatokana na maagano ya ibilisi au sharia za nchi zilizo kinyume na matakwa ya Mungu.

Yapo maagano yaliopo katika nchi yafanyayo watu wake kwenda utumwani, zipo ibada zilizopo katika nchi ambazo zinafanya watu wake wawe katika utumwa.

Yapo makosa yaliofanya watu wawe katika utumwa na chanzo chake ni nchi, vijiji vinakosa mvua kwasababu ya kuwa katika utumwa. Ndio maana anasema anakupandisha kutoka katika nchi kwahiyo ni muhimu sana fahamu zako ziondokane na utumwa wa nchi pamoja na tumaini na utendaji kazi wako uondokane na utumwa wa nchi.

Akili yako lazima ipande kutoka katika fikra za nchi. Ukiwa na Mungu na umetoka katika utumwa nchi kamwe huwezi kufa maskini, ukiwa na yesu ndio mtaji maana utaziamrisha fedha. Sera za nchi elimu sheria na matangazo ya nchi yanawafunga watu katika utumwa.

Makosa ya uonevu wa nchi yanaweka watu utumwani ndio maana Mungu anasema ninakupandisha katika utumwa wa nchi. Sasa katika kufunuliwa haya ni muhimu sana kujua ni utumwa gani unaupitia k**a taifa, k**a kijiji, k**a mkoa,au k**a nchi ili uweze kutoka.

MADHARA YA KUSIKILIZA ROHO ZA MASHETANI.Hali hii inawapata Wakristo wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji, kushiriki ibada...
08/09/2020

MADHARA YA KUSIKILIZA ROHO ZA MASHETANI.

Hali hii inawapata Wakristo wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji, kushiriki ibada za wafu na ibada za sanamu. Mfalme Sauli alipoona Mungu amemnyamazia, alikwenda kwa wenye pepo la utambuzi. Wapo watu wanaosikiliza roho zidanganyazo kwa kupandisha mapepo na kuandika habari zinazotolewa na mapepo halafu wanafundisha wengine kana kwamba ni sehemu ya neno la Mungu.

Dalili ya watu waliosikiliza mafundisho ya jinsi hii ni:-
-Wamejawa na hofu isiyotokana na Mungu,
- Ni waoga na wenye mashaka kwa kila shauri lililo jema,
-Ni wapinzani wa Imani ya kweli ikiwemo miujiza, ishara na nguvu za Mungu wa kweli,
-Hawapendi kukaribia uwepo wa Mungu na wana mapepo daima.

Hofu ni mlango wa mapepo kuingia na kutoka ndani ya mtu, ambapo mara nyingi ukikemea mapepo kwa mtu wa aina hii, baada ya muda mfupi yanarudi. Hata wakiponywa na nguvu za Mungu, uponyaji unakuwa sio wa kudumu kwa sababu uponyaji hutunzwa ndani ya mtu na nguvu za Mungu.

YOUR TUDAY IS BLESSED.
08/09/2020

YOUR TUDAY IS BLESSED.

Jumatatu yako imebarikiwa na bwana.
07/09/2020

Jumatatu yako imebarikiwa na bwana.

Address

KIMANDOLU
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Sharon - Arusha HQ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Efatha Church Sharon - Arusha HQ:

Share