12/08/2026
Mratibu wa Vijana KKKT Mchg Frank Mexon Mng'ong'o amewakilisha ujumbe wa Vijana kutoka KKKT wanaoshiriki Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kitamaifa ambayo kwa Tanzania inaadhimishwa Jijini Dodoma ikiwa na kauli mbiu "Mazingira Tofauti, Fursa sawa kwa Vijana".
Ushiriki huu ni kupitia Mwaliko wa Mh. JOEL NANAUKA Waziri wa Maendeo ya Vijana nchini Tanzania aliposhiriki na kuhitimisha Kongamano la Vijana KKKT Kitaifa.
Mratibu wa Vijana ameambatana na Bw. Augustine Mkungile kutoka Dayosisi ya Kati, Bw. Charles John Silayo kutoka Dayosisi ya Dodoma ambaye pia ni Katibu wa 'Jukwaa la Vijana wa KKKT wafanyabiashara na wajasirimali', pamoja na Bi Fadhila Mjengy kutoka Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha). Dawati la Vijana KKKT tunathamini mwaliko wa Mh. Joel Nanauka Waziri wa Maendeo ya Vijana nchini. Heri ya Siku ya Vijana Kimataifa.