08/12/2023
TAREHE 07/12/2023
SEMINA
KUHANI ;DAVID MSHANA
SOMO: NGUVU YA MUNGU
(LUKA 10:1 ...)
(Kutoka 20 : 4-6)
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Yesu anapenda kufurahi Na kinacho mfurahisha Ni kumzalia matunda
Mungu anapenda watoto wa kiroho wachukue Na kuvuna watoto wa kimwili Na kuwasababisha wapate kibali mbele zake;Basi utakuwa umemfurahisha Mungu.
Furaha Na Kula vinono Ni matokeo ya nguvu. Na nguvu Ni matokeo ya kumfurahisha bwana
Kwahio kituvkikubwa Na cha msingi Ni kumfurahisha bwana maana nguvu anazo yeye
Ukipungukiwana Na nguvu hakuna kitu utaweza kufanya Wala kuongeza kitu kwenye Maisha yako
Ifanye furaha yako ya kumfurahisha Mungu ikuinue Na ikupe nguvu ya kusimama katika Maisha
(Luka 15 : 7-10)
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.