𝗕𝗔𝗞𝗜 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗨

𝗕𝗔𝗞𝗜 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗨 We are the passenger in this world.And everyone knows his direction.We can be in different cars movi

11/06/2020

K**a bado ni mzima basi unaweza ukawa karibu na Mungu zaidi ya jana.
Mkaribie Mungu nae atakukaribia.

08/06/2020

Usichoke kumwomba Mungu k**a bado unaweza maana kuna wakati unaweza ukashindwa kabisa.

07/06/2020

Ulindwe na damu ya Yesu mbali na nguvu za giza.

02/06/2020

Wewe sio wa kawaida k**a utaanza kuliishi kusudi lako...!

17/04/2020

Tumia sekunde chache kusema MUNGU NINAOMBA UKAWE KINGA KWA NCHI YANGU JUU YA COVID-19 na magonjwa mengine.
Share

15/01/2020

Unahisi ukipewa nini unaweza kuridhika na maisha kabisa.!?

Mara ya mwisho kuimba huu wimbo ni lini.!?
13/01/2020

Mara ya mwisho kuimba huu wimbo ni lini.!?

19/10/2019

Mwaka Mpya sio tarehe 01/01 tuu.

Ikiwa una umri wa miaka 30 basi itakuwa umeshaona tarehe 01/01 mara thelathini

Wengi hufanya mipango kila Mwaka Mpya, lakini ni wachache waliojitolea kwa yale waliyopanga. Mwisho wa mwaka wewe ni mtu yule yule, hajabadilishwa hata kidogo.

Sasa mwaka mpya sio siku ya kwanza ya mwaka tu, lakini ni namna wewe unavyokuwa mpya na mtazamo mpya na mbinu mpya na bidii mpya huo ndio mwaka mpya.

Andika mipango yako chini, kisha anza hatua za pole pole k**a mtoto.
Nilipoanza chekechea nilianza kufundishwa herufi moja baada ya nyingine, na wewe anza kufanya pole pole.

Amka asubuhi na tandika kitanda chako, uwe smart (nguo na viatu).

Kwa hivyo fanya jambo lile lile siku inayofuata, na siku inayofuata.
Itabadilika kuwa tabia.

Mara tu ni tabia hautalazimika kujilazimisha kwa sababu utakuwa umezoea na utakuwa unafanya pasipo kusimamiwa.

Jitahidi kuwa mtu ambaye mara zote unatamani kuwa, mwaka huu usiishe kabla haujafanikisha uliyoyapanga. Nasikitika kusema kuna wengine hawakumbuki hata malengo waliyoanza nayo mwaka na wengine hawakuweka kabisa.

-tuanze-mwaka-mpya
034

17/10/2019

Hii picha inakufundisha nini?!!

Me nimeandika kwenye comment...

13/10/2019

Mwanangu nisikilize,
Najua hautamani kuwa k**a mimi baba yako maana maisha yetu uliyajua vizuri tuu, ila cha kushangaza hata mimi sitaka kuwa k**a nilivyo.
Natamani wajukuu zangu wasiteseke k**a nyie tulivyowalea. Nilipokuwa kijana k**a wewe niliambiwa maneno hayahaya na babu yako ila niliona k**a anajaribu kunifundisha maisha. Natamani mtu angenirudisha katika enzi zangu hakika ningefanya mambo makubwa hata wewe ungeshangaa.
tofauti ya kula ujana na kuharibu maisha yako ya baadae.Mimi nilikula ujana sasa uzee ulinitafuna kwa kasi.
DAIMA linalowezekana leo lisingoje kesho, acha kupenda kusingizia kesho kwa uvivu wako wa kufanya leo.
"Utelezi unaweza kukuangusha au kukusogeza mbele kwa haraka.
Majaribu yanaweza kukuangusha(kukurudisha nyuma) au kukupeleka mbele kwa haraka. Majaribu ni k**a gari na ukilitumia vizuri linaweza likakupeleka mbali au kinyume chake utajikuta hospitalini ukiwa maututi(ajali). Usiogope majaribu maana mchumia juani hulia kivulini..."
Ni kauli aliyopenda kuitamka mama yako.

uendelee kumtegemea Mungu na kuongeza bidii yako katika kazi. Licha ya matatizo yetu lakini bado hatukumwacha Mungu. Na bila matatizo hayo pengine tusingemtafuta Mungu. Ila apangalo Mungu hakika mwanadamu hawezi kulitangua.
Ukitaka kuniona baba yako jitahidi uje paradiso, ninatamani sana kukuona ukiwa hapa mwanangu. Kwa bahati mbaya nasikitika kukuambia mama yako alipokufa alipelekwa kuzimu... Sijui ni nini kilimsibu hata akaiacha imani.
Nashindwa kuvumilia kulia maana nilikuwa nampenda sana...
Ni ombi uwasikilize watumishi wa Mungu waliopo duniani, maana sio mda mrefu mwenye mji anakuja?!! Kubali kutubu na kuokoka kabisa maana mama yako k**a angepewa nafasi akusimulimie mateso anayoyapata sijui angeanza na nini?!!
Sijawahi kukudanganya! we mwenyewe unajua, ni jukumu lako kuchagua kabla hawajakuchagua.

Ni mimi baba yako
Vita nimevipiga, imani nimeilinda na mwendo nimeumaliza.

Dawa ni maombi
Ugonjwa ni kuomba.

Share na like page yangu.
035

11/10/2019

Kuna aina tatu za watu ninazozifahamu katika kipindi cha majaribu.
Nawaelezea kwa mifano.
1. Kiazi
2.Yai
3. Kahawa(majani ya chai)

Ni hivi majaribu tuchukulie ni k**a maji ya moto.
Ukiwa chukua wote ukawaweka kwenye majaribu(maji ya moto) matokeo yatakuja hivi...
1. Yai= Atakuwa mgumu(atatoka katika ulaini wa zamani)
2.Kiazi= Atalainika( atatoka katika ugumu aliokuwa nao)
3. Kahawa=Atabadilisha sura ya maji ila yeye atabaki vilevile.

Sasa ni hivi
Kuna watu ni k**a mayai yani wakikutana na changamoto zinawakomaza akili na kuwapa ujasiri na mbinu mpya za kupambanua mambo. Na watu wa aina hii ni rahisi sana kumgeukia Mungu katika nyakati zao za majaribu.

Kuna watu ni viazi yani wao wakikutana na changamoto wanalainika kabisa. Yani wanakata tamaa, wanakosa nguvu ya kuomba tena, wanashindwa kusoma neno la Mungu, wanakosa imani tena, wanaingiwa na hofu, wanakosa furaha lakini mwanzoni walikuwa wagumu. Na watu wa namna hii ni rahisi sana kumwacha Mungu katika nyakati hizo za majaribu.

Kahawa hawa wakiwekwa kwenye maji baridi/moto bado wao huleta mabadiliko. Hawa ni wale ambao hawaangalii jaribu k**a tatizo bali k**a fursa. Huwa hawana hofu na mara zote hujiamini na kuona kwamba kila kitu wanaweza kukumbana nacho na kufanikiwa. Na mtu wa namna hii huwa anamtegemea Mungu sana kuliko wanadamu.

Je wewe upo upande gani rafiki yangu?!!!

Ni mimi jirani yako,
Joseph Daud Makindi-Jodama
Tumia link hii ku-like page yangu ambayo nimeihamia karibuni.
038

10/10/2019

Nimeshindwa kuvumilia, acha nieleze hisia zangu kwako.
Hakika hukujali kudodondosha machozi ulipotaka kuonyesha upendo wako kwangu.
Nikikumbuka kuna kifo yani mimi ndio nazidi kukupenda kwa maana bado napumua.
Nikukumbuka siku uliyoonyesha upendo wako kwangu yani nazidi kuona hakuna cha kunitenga na upendo wako.
Nikikumbuka maneno yako uliyoniambia yani hata moyo wangu unahisi kuruka ruka japo siuoni.
Kweli upendo ni vitendo, yani unayonifanyia hata wengine hawawezi kabisa hakika wewe unanitoshaa.
Zawadi zako kwangu hakika siwezi hata kujaribu kuzilipa.
Ukadiriki hata kuacha kula na kunywa kwa ajili yangu, kweli nazidi kuona haujaangalia sura yangu ila moyo wangu.
Kamwe hujaacha kubeba aibu yangu ndio maana leo naonekana mtu.
Najua maadui wapo ila wewe hukusikiliza maneno yao hata ukanichagua.
Wengine huwekana kwa profile, status, na kwinginepo wewe umeniweka kwenye vitanga vya mikono yako na bado ukatangaza kwa ulimwengu kwamba wanipenda.
Nakupenda sana, naomba usiniache maana ntakufa kwa mateso mengi na maumivu ya milele.
Kamwe hauangalii makosa yangu tena pale niombapo msamaha
Wewe ni mzuri kupita wote.
Hakika kwako nimefika.
Natamani siku ukija kunichukua tukaishi wote basi unikute nimekuwa tayari kwenda na wewe.
Japo wengi hawakupendi kwa sheria na kanuni zako, ila mimi nakupenda.
Nashindwa niseme nini maana sijui nianzie wapi kukuelezea kwa rafiki zangu.
Nakupenda, kweli hii nimesema kutoka moyoni.Wewe waujua moyo wangu, sio uongo machozi yananitoka ninapoandika ujumbe huu kwenye dairy yangu.
Nimekuandikia wewe rafiki yangu YESU.
Ni mimi rafiki yako.

Dawa ni maombi.
Ugonjwa ni kuomba.
039

Address

Nyamagana
Arusha

Opening Hours

Monday 07:00 - 17:00
18:00 - 22:30
Tuesday 07:00 - 17:00
18:00 - 22:30
Wednesday 07:00 - 17:00
18:00 - 22:30
Thursday 07:00 - 17:00
18:00 - 22:30
Friday 07:00 - 17:00
18:00 - 22:30
Saturday 07:00 - 17:00
18:00 - 22:30

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when 𝗕𝗔𝗞𝗜 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗨 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to 𝗕𝗔𝗞𝗜 𝗡𝗝𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗨:

Share