Catholic Archdiocese of Arusha

Catholic Archdiocese of Arusha Jimbo Kuu Katoliki Arusha

10/06/2020
22/05/2020

Utaratibu wa Novena;

1. Wimbo wa Roho Mt.
2. Sala ya Roho Mt.
3. Kuomba msamaha kwa Mungu
4. Kuomba maisha ya Rehema
5. Uje Roho Mfariji
6. Tafakari ya siku
7. Maombi ya siku
8. Shukrani kwa Mungu
9. Litania ya Roho Mt
10. Sala ya Bikira Maria

22/05/2020

Wapendwa Taifa la Mungu,
Tumsifu Yesu Kristo....
Ni matumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri.

Naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha leo tarehe 22.05.2020 katika utaratibu wa Liturujia tumeanza Novena ya Roho Mt. (PENTEKOSTE).
Naomba tushiriki vema tusali pamoja na familia zetu ili tuweze kupokea Ile ahadi ya Bwana Yesu ya kutuletea msaidizi.
Yh 15:26
Ahsante.

06/05/2020

TANZIA:
Aliyekuwa Wakili Paroko wa Parokia ya Njiro, Padre Modesti Makiluli ameaga dunia jana Jumanne tarehe 05/05/2020 saa nne asubuhi katika hospitali ya St. Elizabeti. Mazishi yatafanyika Leo siku ya Jumatano tarehe 06/05/2020 Oldonyo Sambu saa nane mchana.

Ibada ya Misa Takatifu itafanyika Jumanne ijayo tarehe 12/05/2020 saa nne asubuhi katika Parokia ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu.

Tumwombee apumzike kwa amani Mbinguni.

Wafanyakazi Jimbo Kuu Arusha wakiwa katika Mafungo. Dhana Kuu ya Mafungo ni kuhusu Kwaresma na Ekaristi Takatifu. Mafung...
16/03/2020

Wafanyakazi Jimbo Kuu Arusha wakiwa katika Mafungo. Dhana Kuu ya Mafungo ni kuhusu Kwaresma na Ekaristi Takatifu. Mafungo yaliendeshwa na Padri Paul Raia alifafanua kwamba Ekaristi Takatifu ndio chemchem na kilele cha hazina ya kiroho. Ekaristi Takatifu ni Kristu Mwenyewe (Mwili na Damu yake). Fumbo hili ndilo linatupa historia ya wokovu wetu. Pia alizungumzia kuhusu Toba na historia ya Jumatano ya Majivu. Binadamu sio kitu mbele ya Mungu k**a tutatanguliza kiburi. Katika kipindi hiki cha Toba Katekisimu ya kanisa Katoliki ituongoze kuishi matendo saba ya huruma.

Baadhi ya Wafanyakazi Jimbo Kuu Arusha wakiwa katika Mafungo
16/03/2020

Baadhi ya Wafanyakazi Jimbo Kuu Arusha wakiwa katika Mafungo

Baba Askofu Mkuu Isaac Amani akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo Cha watoto Kanaani
12/03/2020

Baba Askofu Mkuu Isaac Amani akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo Cha watoto Kanaani

Baba Askofu Mkuu Isaac Amani, Mapadre na Walezi wa watoto wakiwa katika picha ya pamoja na watoto katika kituo Cha watot...
12/03/2020

Baba Askofu Mkuu Isaac Amani, Mapadre na Walezi wa watoto wakiwa katika picha ya pamoja na watoto katika kituo Cha watoto Kanaani.

Address

P. O. BOX 3044
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Catholic Archdiocese of Arusha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share