Jukwaa la Maombi Tanzania

Jukwaa la Maombi Tanzania JUKWAA LA MAOMBI LA TANZANIA KWA HUDUMA YA MAOMBI NA MAOMBEZI YA NCHI NZIMA IKIJUMISHWA NA VITUO VYOTE VYA MAOMBI NA MAOMBEZI PAMOJA NAMAOMBI YA KILA SIKU

20/04/2026
20/04/2026

INJILI NI UWEZA WA MUNGU ULETAO............
MALIZIA KWA ANDIKO UPATE VOCHA MUDA HUU

20/04/2026

EWE MUOMBAJI WA TAIFA
WEKA NAMBA YAKO TUKUADD GROUP LA MAOMBI LA NCHI NZIMA
ANDIKA UJUMBE
MOAMBI YA TAIFA
KWENDA NAMBA 0742484348

EWE KIJANA LETA NAMBA YKAO TUKUADD GROUP LA VIJANA TANZANIA  NZIMATUMA MAJINA YAKO WHATSAPPANDIKA MIMI KIJANA TANZANIAKW...
20/04/2026

EWE KIJANA LETA NAMBA YKAO TUKUADD GROUP LA VIJANA TANZANIA NZIMA
TUMA MAJINA YAKO WHATSAPP
ANDIKA MIMI KIJANA TANZANIA
KWENDA NAMBA 0742484348

*SIKIA NDEGE PEKEE ANAYE THUBUTU KUMNG'ATA TAI NI KUNGURU.**_Kunguru anakaa juu ya mgongo wa tai  na kuuma shingo yake._...
30/12/2024

*SIKIA NDEGE PEKEE ANAYE THUBUTU KUMNG'ATA TAI NI KUNGURU.*

*_Kunguru anakaa juu ya mgongo wa tai na kuuma shingo yake._*

*_Tai hajibu, wala hapigani na kunguru; hatumii muda wala nguvu kwa kunguru._*

*_Tai anafungua tu mbawa zake na kuanza kupanda juu zaidi mbinguni._*

*Kadiri Tai anavyoruka juu zaidi ndivyo inavyokuwa vigumu kwa kunguru kupumua na kisha kunguru huanguka kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni na hufa*

*Jifunze kutoka kwa tai na kamwe usipigane na kunguru.*

*Endelea tu kupanda, endelea kufungua mbawa zako na kwenda juu zaidi*

_Wanaweza wakawa wanajaribu kushindana na kupigana na wewe kwa sasa, lakini wataanguka kwa kadiri unavyopanda kwenda juu zaidi_

*ONGEZA UWEZO WAKO WA KUPAA! JUU ZAIDI*

ONGEZA KIWANGO CHAKO CHA KUMTAFUTA MUNGU ZAIDI
ONGEZA MUDA WA KULISOMA NENO LA MUNGU ZAIDI
ONGEZA KIWANGO CHAKO CHA MAOMBI
ONGEZA KUTUMIKA
ONGEZA KUTOA ZAKA NA SADAKA
ONGEZA USHILIKA WAKO NA MUNGU

*_Wakati NGUVU/uwezo wako unapoongezeka katika eneo lolote, unakua na uwezekano mkubwa wa kushinda vita, changamoto, zinazoonekana au zisizoonekana_*

*“bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa k**a tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.”*
*_— Isaya 40:31 (Biblia Takatifu)_*

*ENDELEA KUPANDA JUU*
*ENDELEA KUPIGA MBIO*
*ENDELEA KUFUNGUA MBAWA ZAKO*
*ENDELEA KUNG'AA*
*USIKATE TAMAA*

Nimekuombea kwamba Nguvu zako hazitapungua kwa kadiri unavyozidi kupanda juu zaidi ndivyo nguvu Zako zitaongezeka zaidi na ndivyo itakavyokuwa katika Jina la Yesu kristo alie hai sema ameeeeeniii

Na Apostle & Evangelist
Charles Chazya Sichilima
0719123504
0683352535

30/12/2024

*VUKA MWAKA NA NGUVU KWA NENO NA KWA MAOMBI YA SIKU 40*
LEO TUKIWA SIKU YA 18(Tarehe 30 Disemba
Wacha Tujifunze
Kuhusiana
Na UTII.
*SOMO:SIRI YA UTII*

Dokezola Utii “Naye Samweli akasema, Je! BWANA huzipenda sadaka za kutekeketezwa na dhabihu sawasawa na kutii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya bebeeru.” 1 Samweli 15:22 Ukimuwekea Mungu machaguo mawili ili achague mojawapo kati ya hayo; upande mmoja uweke sadaka na upande mwingine uweke utii. Uwe na uhakika Mungu huchagua utii. Hata hivyo, ni heri ukijua ya kwamba sadaka ni udhihirisho wa utii wetu kwa BWANA.Sadakayoyote inayowasilishwanje ya kigezo cha utii, Mungu huiona k**a “hela” tu! Haisemi chochote mbele zake. K**a utii ni muhimu kiasi cha mvutia Mungu hivyo, utii ni nini basi?  Utiini kukubali na kutendea kazi maelekezo ya Mungubila kuyatilia mashaka.
 Namna tunavyohusiana na Mungu na kumwendea ni kwa utii. Hii ni kwa sababu kwenye mahusiano hayo, Mungu hutoa maelekezo na si mapendekezo. Mapendekezo hupokelewa kwa majadiliano. Wakati maelekezo hupokelewa kwa utii tu na si pungufu ya hapo.  NenonamaelekezoyaMunguhupokelewakwa utii na si kwauchaguzi.“NenolaMungunikwa ajili ya utekelezaji na si uchambuzi.” Dr. Sam Adeyemi  Upendeleo ya kiungu uko ng’ambo ya pili ya barabara ya utii unakusubiri. Je, utavuka mwaka 2024 ukiwa na hali yako ya kiburi na majivuno?
Ngazi nne za Utii: 1. Utiikuyaelekeamaandikomatakatifu(Biblia). “2. Katika mwaka wa kwanzawa kumiliki kwake, mimi Danieli, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka,ambayoenolaBWANAlilimjiaYeremianabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini. 3. Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguozamagunia namajivu,” Danieli 9:2-3 Kile alichokisoma Danieli kinapatikana kwenye vitabu vifuatavyo: Yeremia 25:11-12; 29:10; Ezra 1:1; 2 Nyakati 36:21. Angeweza kusoma k**a machapisho tu au vitabu vya historia ya taifa lake au masimulizi kutoka kwa waandishi wazuri na wema wa taifa lake zuri la Israeli. Lakini aliuvuka huo mtego. Aliposoma, alichukua kile alichokisoma kwa uzito na heshima ya hali ya juu sana. Alijua ya kwamba anachokisoma ni neno la BWANA.

Mwitikio wake juu ya kile alichokisoma unatuambia hali nya moyo wake kuyaelekea maandiko matakatifu, “…Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi…” . Hii ni heshima na mwitikio wa hali ya juu sana kwa neno la Mungu. Halikuwa neno lililoishia kumpa taarifa tu, bali liliyakunja magoti yake. Hakuna mahali kwenye unabii huo ambapo Danieli alitajwa kwa jina ya kwamba ana wajibu wa kuomba au kutenda chochote ili litokee na kuwa halisi kwenye maisha ya watu wake. Kilichoyakunja magoti yake, ni hali ya utii uliokuwa ndani yake kuliekea neno la Mungu. Iko hivi, kila ukisoma maandiko matakatifu ukagundua yanamuhusu kila mmoja isipokuwa wewe, ujue kuna upungufu wa utii ndani yako kuyaelekea maandiko. Kabla haujaanza kutafuta kusikia sauti ya Roho Mtakatifu, hakikisha umemaliza kuisikia iliyomo ndani ya neno lake; na k**a unapenda sana unabii,
hakikisha umeupokea unabii wako wote tena uliokwisha kutimilizwa uliomo ndani ya maandiko matakatifu. 2. NenolaMungulililovuviwa “31. Tena kwa habari ya kiyama ya watu, hamjalisoma neno lililonenwa na Mungu, kusema, 32. “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka , na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai.” Mathayo 22:31-32 (SUV). Ukisoma andiko hilo kutokea tafsiri ya NENO utagundua kuna msisitizo tofauti, “Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamkusoma kile Mungu alichowaambia, kwamba,” Utaona si tu kwambaMungualisema ujumbe ukaenda hewani, bali alikuwa anasema na hawa ndugu waliokuwa wanaongea na Bwana Yesu. Tafsiri nyingi za lugha ya kiingereza zinakubaliana kabisa na wazo hili ya kwamba si tu Mungu alisema ujumbe bali alisema na watu hawahuuujumbe. “But about the resurrection of the dead– have you not read what Godsaidto you,” (NIV)

“But as touching the resurrection of the dead, have ye not read that which was spoken unto you by God saying,” (ASV) “And as for whether the dead are resurrected, haven’t you read what Godsaidtoyou,” (CJB) Kwa msingi huo basi, twaweza kufikia hitimisho ya kwamba ndani ya neno la Mungu lililoandikwa kulikuwa na ujumbe ulimwendea Musa k**a msikiaji wa awali. Hata hivyo halikuishia hapo, bali limebeba pumzi ya kukihudumia na kukifaa kizazi kilichokuwa kimesimama mbele ya Yesu… na halikuishia hapo, linasema hata hivi leo. Kwahiyo, unaposomamaandikomatakatifu, kumbuka kuizingatia pumzi na sauti iliyo nyuma na maandiko hayo. Utagundua waliyoandikiwa ya kwamba maandiko Wakorintho, Wathesalonike, Wagalatia, Waebrania na wengineo yanakufaa wewe mtanzania (na mtu mwingine yeyote) hivileo! “Maana Neno la Munguli hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena

lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” Waebrania 4:12 Kila wakati unapofungua maandiko matakatifu kuyasoma, huwa yamefunuka kukusoma wewe. Huo ni uthibitisho wa pumzi iliyomo ndani ya neno. Usisome maandiko k**a kitabu cha historia, bali ni pumzi hai ya Munguhatahivi leo! 3. MaongoziyaRohoMtakatifu “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, haondio wanawaMungu.” Warumi8:14 “Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.” Wagalatia 5:18 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.” Yohana 16:13

Nimekusudia uone ya kwamba moja wapo ya kiashairia cha uana wa Mungu ni kuongozwa na Roho waMunguaambayeameachiliwakwaajili hiyo. Kumbuka neno linamtambulisha Roho Mtakatifu k**a msaidizi na si mlazimishaji. Kwa hiyo, namna yake ya kuongoza ni ile ya kutusaidia kuliko kutulazimisha zaidi. Nafasi hii ya “msaidizi” ndiyo mtegowenyewe.Unahitajikautii wa haliyajuusana ili kuongozwanamsaidizi! 4. Mamlakahalalijuuyangu: Katika kuyaongoza na kuyaratibu maisha ya mwanadamu hapa duniani, Mungu ameyaweka chini ya mamlaka. Kunamamlakanyingiambazozikojuuya maisha yako. Hata hivyo, kwa minajiri ya kitabu, ninatambulisha kwako mamlaka nne ambazo unapaswakuzitii. a) Wazazi wa kimwili: Hawa si tu kwamba ni watu waliokuleta duniani na kukupatia utambulisho wa kibaiolojia/vinasaba na kukupaukoo. Hawanimamlaka!
Tazama ni kwa namna gani maandiko yamewaambatanisha na aina fulani ya uheri. “Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.” Wakolosai3:21 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki 2. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 3. Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.” Waefeso 6:13 Kutotii mamlaka hii ya wazazi wa kibaiolojia ni kuchagua kutopokea thawabu iliyoambatanishwa pamoja nao. b) Wazaziwakiroho “Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.” Filemoni 1:21

Moja ya mifano ya mahusiano ya mzazi wa kiroho na mtoto wake na swala la utii ni katika ya mtume Paulo k**a baba kwa upande mmoja; na Filemoni k**a mwanakwaupandewapili. Kwenye waraka huu wenye sura moja, utaona malekezo ya baba kwamwanae:  Kumpokea Onesimo k**a ndugu yake katika Kristo. Hapo awali Onesimo alikuwa ni mtumwa wa Filemoni na inaonekanaaliotoroka naaliiba sehemuya mali ya bwanawake(Filemoni 1:16)  Kufuta madeni yote ya mali yaliyopita juu ya Onesimo. Lakini ikiwa ni muhimu sana kuendelea kuyadai, basi amdai baba yake, yaani mtumePaulo (Filemoni 1:18)  Amuandalie baba yake mahali pa kukaa ambapo atafikia baada tu ya kumaliza kifungo chake gerezani (Filemoni 1:22)  Tahadhari: Filemoni anakumbushwa na baba yake ya kwamba yeye anadaiwa nafsi
yake kabisa, siyo hata fedha au mali. Hii ni kwa sababu ya uwekezaji wa kiroho wa Paulo kwa mwanae(Filemoni 1:19b) Sasa, ni vizuri uelewe ya kwamba ujasiri wa kutoa malekezo alionao Paulo kwa mwanae Filemoni ni kwa sababu ya kiwango cha utii wake si tu kwa sababu ya mamlakayakiroho ya Paulo. “Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maanawaowanakeshakwaajili yarohozenu, k**a watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.” Waebrania 13:17 Mwitikio wetu kwa wanaotuongoza ni utii na unyenyekevu. Kwenye andiko hili, wanaoongoza ni wale wanaokesha kwa ajili ya roho zetu na wenye wajibu wa kutoa hesabu juu ya maisha yetu. Ni nani mwingine afanye hivyo ispokuwa mzazi wako wa kiroho? Unadhani kuna mtu mahali fulani anaweza kukesha kwa ajili yako? Unadhani kuna mtu mahali fulanianawezakujiwekakwenyejukumulakujakutoa
heshabu kwa ajili yako? Ni kwa nini ajiingine kwenye majukumumazitohivyo? c) Mume Mume ni mamlaka kwa mke wake! K**a mke atatambua hivyo, atachukua neno la Mungu k**a lilivyo na atatekeleza neno basi atavuna thawabu ya kutii kwake. Maandiko yanasema hivi kuhusu mamlakahii. “22. Enyi wake, watiini waume zenu k**a kumtii Bwana wetu. 23. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe,k**aKristo nayeni kichwachakanisa; naye ni mwokozi wa mwili 24. Lakini k**a vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.” Waefeso 5:22-24 Kwenye kitabu kiitwacho NYWILA nimefundisha kwa upana wake sana msukumo wa kiungu nyuma ya utii wa mwanamke kumuelekea mumewe. Mwanamke ameaminiwa Mungu kumfundisha mume wake utii kwa kuwa kilelezo cha huo utii wenyewe. Na mume, ambaye ni sehemu ya kanisa la Kristo, atatenda
inavyotarajiwa awapo kwenye nafasi yake ya bibi arusi wa Kristo. Hata hivyo, ni vizuri kujua ya kwamba Mungu ndiye aliyeweka mtiririko huo wa kimamlaka si kwa ajili ya hasara au kutuonea bali ni kwa faida na ustawi wetu. Hili ni jambo ambalo linabishaniwa sana miongoni mwa tamaduni na mapokeo kiasi kwamba mtu anayeamini katika njia hii anaonekana kuwa ni wa kizamani na amepitwa na wakati. Atukuzwe Mungu kwambavitu vyotevitapita, neno litasimama! “Ninyi wake, watiini waume zenu, k**a ipendezavyo katika Bwana.” Wakolosai 3:18 “Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi. Ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendowawakezao,pasipolile Neno.” 1Petro 3:1 d) Kiongoziwakazi Kuelewa muktadha kidogo, ni kwamba wakati wa kanisa la mwanzoni kulikuwa kuna uatamaduni wa utumwa kwenye jamii za wakati huo. Lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa. Ikafikia wakati ambapo watumwa wanaiamini injili na wanaokoka… wanfunguliwa kutoka katika utumwawadhambi(siyo utumwa wa kazi). Wengine walianza kuhoji ya kwamba, maadamu wamewekwa huru na Kristo kuna umuhimu gani tena wakuendelea kuwa chini ya utumwa wa bwana zao? Sasa ikumbukwe ya kwamba utumwa ndiyo ulikuwa mfumo wa kiuchumia wa uzalishaji (means of production)– ni k**a ilivyo ajira kwa zama zetu. Kulikuwa na utaratibu na miongozo ya namna ya kukombolewa (kulipiwa deni au kujilipia deni la kutoka utumwani) au kuachilia huru kwa utashi wa bwana. Tofauti na hapo ilionekana kuwa ni uasi na athari zake zingekuwa kubwa. Maandiko yanaelekeza ya kwamba watumwa wawaone bwana zao k**a mamlaka ambayo hata k**aumeokokaunapaswakuiitikia kwautii. “Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwanazenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, k**a wajipendekezao kwa wanadamu, bali
kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.” Wakolosai 3:22 “Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali.” 1 Petro 2:18 Ni sawa na zama hizi baada tu ya kuokoka usemi ya kwamba hupendi kuwa chini ya mtu, hupendi maelekezo yake, hupendi kubanwa… unataka umtii Kristo tu na neno lake! Hiyo siyo sawasawa. Ukiokoka, hakikisha viongozi wako wanauona mwenendo wako mwema kiasi cha kuwavuta kwa Yesu Kristo.
**************************************
NAOMBA TUENDELEE NA SOMO HILI KESHO.
JITAHIDI KUTII.
SOMA NENO
OMBA
FUNGA
TOA SADAKA.
USIPOVUKA MWAKA NA NGUVU YA KUMILIKI UJUE MUNGU NINAYE MTUMIKIA SIO MUNGU WA KWELI.
---------------------------------------------
Zaburi50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.-"*
Kwa iyo
Ikiwa Unayo sadaka.
*Tuma kwa namba 0719123504.
Jina: Charles John Chazya*

*Au Airtel Lipa namba. 0088881.
Jina: Jukwaa la Maombi Tz*

Naomba Ubarikiwe ikiwa utasimama kwa Uaminifu katika yote Hayo
*_NENO_*
*_MAOMBI_*
*_SADAKA_*

Waweza pia share link hii kwa wtu wengine na utakua umehubiri Injili pamoja nasi.
https://whatsapp.com/channel/0029VaDFjlC1CYoQJaAeA40T
Group letu
https://chat.whatsapp.com/E6mbIkETWaMK7JTIoMIU9G

______________________________________________

30/12/2024

MAOMBI YA VUKA MWAKA NA NGUVU SIKU 40

Bwana Yesu Asifiwe
Tuko Na maombi ya siku 40 na tuko wiki ya 03 Wikii hii Tunasimama na Maombi ya UREJESHO
leo ikiwa ni siku ya
18 (JUMATATU Tarehe 30 Disemba 2024 )
Tunasimama KUOMBA UREJESHO(Ayubu 20:15)
Job 20:15
[15]He hath swallowed down riches, and he shall vomit them up again: God shall cast them out of his belly.
Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.

Kwenye maeneo haya:-

>Urejesho wa Nguvu za Mungu katika Maisha yetu
-Nguvu ya Uamsho
>Mahusiano Yetu
>Elimu .
-Masomo Tetu
-Programms zetu
> Afya katika Maisha yetu
>Uchumi wa Huduma na mtu mmoja mmoja
-Urejesho wa mali,vitu,samani n.k
>Mamlaka ,kibali ,Nguvu ya
- nafasi,
- Huduma
- Maono
>Karama, vipawa na Nguvu ya Roho mt.
-Nguvu ya Kumtafuta Bwana
-Kiu ya Mungu
-Moto wa mungu
Urejesho juu ya
>kazi na hudumaa
>Biashara
> kila kilichoibiwa na adui kuanzia kuumbwa kwako

Simama
Ukaombe Uresho
Kua na hasira na Shetani mpaka arejeshe Aliyo yaiba kwetu Jukwaa la Maombi Tanzania
Weka Bidii zaidi
Weka imani.
Omba katina Roho na Kweli( Yohana 4:23-24)
Yakobo 5:16
James 5:16
[16]Confess your faults one to another, and pray one for another, that ye may be healed. The effectual fervent prayer of a righteous man availeth much.
Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Proverbs 23:8
[8]The morsel which thou hast eaten shalt thou vomit up, and lose thy sweet words.
Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.

Matthew 27:3-4
[3]Then Judas, which had betrayed him, when he saw that he was condemned, repented himself, and brought again the thirty pieces of silver to the chief priests and elders,
Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.
[4]Saying, I have sinned in that I have betrayed the innocent blood. And they said, What is that to us? see thou to that.
Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.
------------------------------------------
Zaburi50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.-"*
Kwa iyo
Ikiwa Unayo sadaka.
*Tuma kwa namba 0719123504.
Jina: Charles John Chazya*

*Au Airtel Lipa namba. 0088881.
Jina: Jukwaa la Maombi Tz*

Naomba Ubarikiwe ikiwa utasimama kwa Uaminifu katika yote Hayo
*_NENO_*
*_MAOMBI_*
*_SADAKA_*

Waweza pia share link hii kwa wtu wengine na utakua umehubiri Injili pamoja nasi.
https://whatsapp.com/channel/0029VaDFjlC1CYoQJaAeA40T
Group letu
https://chat.whatsapp.com/E6mbIkETWaMK7JTIoMIU9G
__________________________________________

26/12/2024

Utatu sio fundisho la uongo bali ni fundisho la biblia.

1 Yohana 5:8
Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

Utatu ni sifa kuu 3 za Mungu zilizo ndani ya Mungu (Baba yetu aliye mbinguni, Neno lake na Roho yake Takatifu) na sio mungu 3.

Mungu, Neno lake na Roho yake Takatifu ni Mungu mmoja yuleyule na alituumba kwa mfano wake. Hata wewe, neno lako na roho yako sio watatu bali ni wewe mmoja, vyote ni sifa zilizoko ndani yako na si nje yako.

Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Yohana 14:
[7]K**a mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
[8]Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
[9]Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

Matthew 4:1-11
[1]Then was Jesus led up of the Spirit into the wilderness to be tempted of the devil.
Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
[2]And when he had fasted forty days and forty nights, he was afterward an hungred.
Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
[3]And when the tempter came to him, he said, If thou be the Son of God, command that these stones be made bread.
Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.
[4]But he answered and said, It is written, Man shall not live by bread alone, but by every word that proceedeth out of the mouth of God.
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
[5]Then the devil taketh him up into the holy city, and setteth him on a pinnacle of the temple,
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
[6]And saith unto him, If thou be the Son of God, cast thyself down: for it is written, He shall give his angels charge concerning thee: and in their hands they shall bear thee up, lest at any time thou dash thy foot against a stone.
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
[7]Jesus said unto him, It is written again, Thou shalt not tempt the Lord thy God.
Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
[8]Again, the devil taketh him up into an exceeding high mountain, and sheweth him all the kingdoms of the world, and the glory of them;
Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
[9]And saith unto him, All these things will I give thee, if thou wilt fall down and worship me.
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
[10]Then saith Jesus unto him, Get thee hence, Satan: for it is written, Thou shalt worship the Lord thy God, and him only shalt thou serve.
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
[11]Then the devil leaveth him, and, behold, angels came and ministered unto him.
Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia. Yesu Aanza Huduma yake katika Galilaya

Shalom

Address

Arumeru
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jukwaa la Maombi Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Jukwaa la Maombi Tanzania:

Share