Jesus Power Ministry

Jesus Power Ministry Jesus power ministry ni huduma ya Mungu yenye makusudi ya kurejesha hatima za watu wake mahala alipo

2025 MWAKA WA KUANGAZA.Ndugu zangu kherini nyote na mwaka mpya wa 2025.Nakukumbusha tu k**a unajua ulijitayalisha kwa ja...
14/01/2025

2025 MWAKA WA KUANGAZA.
Ndugu zangu kherini nyote na mwaka mpya wa 2025.
Nakukumbusha tu k**a unajua ulijitayalisha kwa jambo flani kwa kipindi kadhaa basi mwaka huu ni majira yake.

Unapoambiwa mwaka wa kuangaza siyo wote watakaongaza Bali wale walijitayalisha,walikubali kupita kwenye milima na mabonde kwa imani na kwa subila ili majira Yao yakifika wapate kuwaangazia wengi walio gizani.

Siku zote Nuru uwaangazia waovu na wema.
Ukawe Nuru kwa waliokupinga,kubeza,kukucheka,kukudharua,kukutenga wakata unaendea ndoto zako Ili wote wapate kuona upendo wa MUNGU kupitia wewe.

Yusuph alifanyika Nuru si tu kwa misri pekee Bali kwa mataifa yote walikuja misri kununua chakula.

God bless you abundantly.

THE DIVINITY LEADERSHIP (UONGOZI WA KIUNGU)Bwana Yesu afisiwe wana Mungu popote pale mlipo.Bwana Yesu anasema mtu akikup...
21/09/2024

THE DIVINITY LEADERSHIP (UONGOZI WA KIUNGU)

Bwana Yesu afisiwe wana Mungu popote pale mlipo.

Bwana Yesu anasema mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto,wengi sana hawajui kwanini Bwana Yesu alitumia neno hili kuwa mojawapo ya kiungo muhimu kwenye uongozi.

Hapa Bwana Yesu alikuwa anamaanisha kunyamaza nyakati za hatari,kwenye hatari yoyote huwezi kuhimili hisia zako binafsi lazima utataka kujipambania iwe utapona au hautapona.

Ikimbukwe kwenye uongozi wa Bwana Yesu, aliletewa habari ya kukatwa kichwa kwa mtu wake wa karibu sana ambaye ni Yohana mbatizaji.
Bwana Yesu alijitenga kwa Muda kwenye kundi kubwa la watu.
Kwanini alijitenga kwa muda baada ya kuletewa taarifa hiyo.
Yeye alienda kufanya tafakuri binafsi na Baba yake aliyemtuma alafu baada ya kuludi hakuja na jawabu la kwamba waingie mtaani yeye,wanafunzi wake na wafuasi wake kuandamana dhidi ya ukatili aliyofanyiwa mtumishi wake Yohana,akaendelea na shughuli yake k**a kawaida.

Hapa ibilisi alikuwa anatafuta hisia binafsi za Bwana Yesu namna atakavyoweza kuonyesha ghadhabu yake dhidi ya ukatili ule lakini matokeo yake akanyamaza,shetani alikuwa anampima yeye ambaye anasema vita yake si katika mwili bali ni katika ulimwengu wa roho je ataweza kuhimili kuzuia hisia zake kwa huyu mpendwa wake.?

Ndugu zangu tunapozungumzia uongozi wa kiungu ni uongozi teule,usiondeshwa na mihemko bali unaendeshwa kwa ufahamu,hekima na akili,haya mambo makuu matatu yanakusaidia kujua chanzo halisi cha tatizo na kutokea hapo unajua chanzo sahihi cha suruhisho.

Watumishi wa Mungu wakijitokeza kwenye vyombo vya habari wakihamaki k**a ulimwengu unavyoenda manake unalivunja daraja la amani,upendo na ustahimilivu katika Taifa.

Watumishi wa Mungu wao wamepewa neema ya kuonyeshwa mambo yaliyoko sirini yanayotendeka na ambayo yataweza kutendeka baadae,na kwahivyo siyo watu wa kukulupuka hovyo hovyo kutoa majawabu na majawabu yao huleta suluhisho la kweli kiasi cha aliyetenda uovu huo kujiona yu uchi ndicho kilichofanyika kwa mtumishi wa Mungu Suleiman dhidi ya mabinti wawili makahaba waliokuwa wakigombania mtoto ile kesi ilisuluhishwa kihakili sana na amani ikatawala pande zote.

Bila kujua chanzo cha tatizo ni ngumu kupata utulivu wa kweli wa kudumu kwa mtu binafsi,jamii,au hata Taifa.

PUT GOD FIRST FOR EVERYTHING YOU DO!!!.

Geofrey Julius-Jesus power ministry Tz

🎉 Happy Birthday to Me! 🎉I’m incredibly grateful for all the wonderful people in my life—friends, colleagues, and follow...
17/09/2024

🎉 Happy Birthday to Me! 🎉

I’m incredibly grateful for all the wonderful people in my life—friends, colleagues, and followers—who make each day special. Your support, kindness, and positivity mean the world to me. As I celebrate another year, I want to take a moment to thank my Almighty God Jesus and each of you for being a part of my journey.
Here’s to another year of shared experiences, growth, and joy. I hope your day is filled with as much happiness as you bring into my life!
Thank you for the birthday wishes, the love, and for being such an amazing part of my life. Cheers to many more moments together!

Warmest thanks and best wishes.

UNAJIONA UKIWA WAPI KWA MIAKA 30 IJAYO?K**a una miaka 30 Leo na bado haujapata kujua nafasi uliyonayo sasa inakupa picha...
01/04/2024

UNAJIONA UKIWA WAPI KWA MIAKA 30 IJAYO?

K**a una miaka 30 Leo na bado haujapata kujua nafasi uliyonayo sasa inakupa picha ipi au matokeo yapi baada ya miaka 30 ijayo,Kuna shida mojawapo inayokusumbua kati ya hizi

1.Kutokujua k**a mahala ulipo ni sahihi na kwasababu hiyo kujikutaka unapoteza muda mwingi pasipo kuona matokeo.

MUNGU akamwambia Ibrahim atoke nyumbani kwa baba yake akiwa na takribani miaka 70.Mungu alimwelekeza Ibrahim njia sahihi ya kufanikiwa kwake,k**a neema hiyo isingemjia Ibrahim anegishia kuridhi kasehemu kadogo kwenye Mali ya baba yake na hako kasehemu kadogo ndiko angekagawanya kwa watoto wake.

Yakobo alikaa kwa mjomba wake Rabani kwa zaidi ya miaka 17 bila kuona matokeo halisi ya maisha yake anaona anaongeza watoto katika nyumba ya baba yake bila kujua hatima ya watoto itakuwaje baada yake mpaka pale alipofanya maamuzi ya kusema maisha haya yatosha.

2.Kutokuwa na ufahamu wa kutosha wa kile unachokifanya kwa sasa.

K**a unafanya biashara na hauoni biashara hiyo katika picha ya mafanikio kwa miaka 30 ijayo maana yake hiyo biashara utaiua.Kuwa na ufahamu wa kutosha na kuwa na mikakati endelevu dhidi ya hiyo biashara yako usipojituma katika kuilisha biashara yako maarifa huwe na hakika biashara hiyo itadumaa.

Uko kwenye ndoa,k**a hauoni mafanikio kwenye ndoa yako kwa miaka 30 ijayo maana yake unachokifanya sasa ni kazi bure.Kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu chanzo Cha amani kwenye ndoa yako,na chanzo Cha kipato kwenye ndoa yako.

MUNGU akawaambia Adamu na Hawa wazae na kuijaza Dunia,Neno wazae maana yake ni mbegu na neno kujaza maana yake ni matokeo ya mbegu wanayoipanda wao,kwa lugha nyingine Kila mbegu unayopanda lazima izae na kwasababu ya kuzaa kule ndoa hiyo itakuwa Bora na yenye heshima.Mungu anaposema mzae hamaanishi tu watoto watokao kwenye viuno vya Mwanaume,anamaanisha kuibua mawazo mapya yaletayo uchumi kwenu, kwahiyo lazima muazimie nyie wawili kushik**ana kwenye zao la kiuchumi.

3.Kusikiliza mawazo ya watu wengine kuliko mawazo yako mwenyewe.

Unapotumia muda mwingi kufanyia kazi mawazo ya watu wengine maana yake unageuka mtumwa, na hakuna mtumwa yeyote duniani aliyewahi kuwa huru.

4.Hofu.

K**a haujioni mtu mwenye thamani sana kwa miaka 30 ijayo,ujue umezingirwa na hofu ya maisha inayokupelekea kutofanya maamuzi ya kukabili kesho yako.Mtu yeyote mwenye hofu ni ngumu sana kuleta mabadiliko yoyote.
Na kwasababu hiyo miako 30 ijayo utakuwa msumbufu sana kwa wale unaohisi unawasaidia Leo maana na wao watakuwa na majukumu pia.

Hofu inafukuza Imani,na mahala pasipokuwa na Imani hapana mavuno.

Zaidi ya yote k**a unajiona mtu flani kwa miaka 30 ijayo.
Zingatia haya mambo muhimu.

1.Jifunze namna ya kuomba kimkakati.
2.Funga kimkakati
3.Jifunze kuweka muda wa utekelezaji wa mipango yako.
3.Kuwa sahihi kwenye malengo yako.
4.Jifunze kuhimili hisia binafsi.(Usiwe mtu wa kuhama hama hivyo.
5.Jibidishe katika elimu
6.Uwe mtu wa Imani
7.Ambatana na mtu sahihi anayeweza kuwa Mwalimu wako au mshauri wako. Na
8 Always stay positive (Daima waza chanya na siyo hasi)

God bless you
Geofrey Julius-Jesus power ministry Tz

Kufanikiwa kwa Ibrahim kulitokana na utii,kupoteza kwa Mfalme Saul kulitokana na kutokutii, Malikia Vashti alipoteza naf...
19/08/2023

Kufanikiwa kwa Ibrahim kulitokana na utii,kupoteza kwa Mfalme Saul kulitokana na kutokutii, Malikia Vashti alipoteza nafasi yake ya kuwa mke wa Mfalme Ahusuelo kwa kosa la kutokutii.

Weka akilini mwako kwamba sehemu yoyote inayokuwa na kuongezeka sana chanzo chake ni utii,ndio maana utii unachukua nafasi kubwa kuliko sadaka.

By Geofrey Julius

ISRAEL NI AFRICASerikali ya Ufalme wa Pharaoh yaani mawazili,Makatibu wakuu na washauri wengine wa Pharaoh wakaandaa mku...
05/08/2023

ISRAEL NI AFRICA

Serikali ya Ufalme wa Pharaoh yaani mawazili,Makatibu wakuu na washauri wengine wa Pharaoh wakaandaa mkutano wa kuwajadili waisrael hoja kubwa ilikuwa ni mbili
1.Wana nguvu kuwazidi
2.Wanazaliana sana

Haya mambo makuu mawili yalikuwa tishio kwenye nchi nzima ya Misri.

Kwenye mkutano huo wakaja na hoja moja kuu ya kuwatenda kwa akili kwa namna gani

1.Kuwafanyisha kazi ngumu.Kwa lugha nyingine walitengwa na mifumo ya elimu,elimu waliokuwa wanapata wamisri siyo waliokuwa wanapata waisrael.

2.Ikatolewa walaka kwa Kila mwanamke wa Israel atakaejifungua mtoto wa kiume huyo mtoto auwawe.

Sasa baada ya nchi za Africa kujipatia uhuru,wazungu wakaandaa tena mkutano utaokuibua hoja za namna ya kubaki Africa, kwasababu Africa ni bara lenye utajiri.

Hoja walizokuja nazo mojawapo ni namna ya kukukontro uchumi Ili mwafrika asipate kusimamia mwenyewe rasilimali zake.
Wakaibua na hoja ya namna ya kukontro uzao kwasababu waafrica wanazaliana sana na pia Wana nguvu.Hapa wakaja na agenda za uzazi wa mpango na agenda za ushoga kwa nini ushoga mwanaume akifanyiwa huo uchafu hawezi kufanction kwahiyo atapoteza nguvu ya kuachilia uzao.

Pia kuzalisha mfumo mpya wa ulaji kwasababu vyakula vya Africa vinachochea nguvu.

Sasa elewa kitu kimoja moja hapa, Israel nchi na Israel mteule ni vitu viwili tofauti.
Wakati Serikali ya Pharaoh ikipanga mambo ya Siri dhidi ya mteule Israel Mungu akaachilia uzao wa Siri kwa ajili ya kumkomboa mteule Israel ambaye ni Musa.

Kwa hapa Africa viongozi wengi walionyesha kwenda kinyume na sera mpya zilizoletwa baada ya ule mkutano mkuu wa wazungu baada ya uhuru viongozi walikufa kikatili na wazungu wakajitahidi sana kutengeneza mamluki wengi wa kutosha ambao ni waafrica wenyewe wakiamini kwamba hao hao watahusika kupindua au kuchochea ghasia kwenye nchi zao wenyewe.Na ndivyo tunavyoona Leo.

Je nani mkombozi wa Africa.Miongoni mwa vijana katika miaka hii wapo au yupo kijana Mungu amekwisha waandaa au kumwandaa kwa Siri na kufanikisha ile ndoto ambayo baba zetu walijitahidi kuifanikisha lakini waliishia njiani kwa nini kwasababu hawakuwa na nguvu ya kweli ya kuwalinda.
Ndio maana nyakati hizi unazidi kuona vuguvuga la wazi kwa viongozi wetu wakiwa kwenye mikutano Yao wakipigia kelele kuachiwa Africa Yao.

Cha muhimu sana hakikisha unawafundisha watoto wako mambo muhimu ya uongozi na namna ya kufanya mambo muhimu na sahihi pamoja uzalendo katika nchi yake.Epuka kuhamishwa akili na matukio mbalimbali yanayoweza kutokea ndani ya nchi yako au Africa.Wakati waisrael wakipitishwa kwenye pagumu bible inasema MUNGU alisikia kilio cha Israel manake walikuwa wanaomba., walikuwa wanaomba lakini hawakuwa wanajua wanatokaje, MUNGU ilibidi amwandae Musa kielemu,kiujasili,na udhubutu.

Hii ni kumaanisha kwamba tusibaki tu kwenye maombi peke yake, tupambane kujua mambo mengi kuhusu Africa,fundisha watoto wako vizuri mambo ya ujasiri na himiza uzao wako umjue Mungu sana.

Time has come to rescue Africa.
From Geofrey Julius

DON'T LOOSE YOUR FOCUS 2023.(Usipoteze mwelekeo wako 2023)Kherini ya mwaka mpya rafiki zangu,ndugu zangu ongereni sanaaa...
02/01/2023

DON'T LOOSE YOUR FOCUS 2023.(Usipoteze mwelekeo wako 2023)

Kherini ya mwaka mpya rafiki zangu,ndugu zangu ongereni sanaaa MUNGU wetu ni mwema sana Kila wakati

Ujumbe wangu katika mwaka huu kwenu.
Kumbuka kwamba Mungu anapokupa kusudi lake hakulupuki,anakuwa amekwisha lipeleleza na kudhibitisha kuwa litawezekana.

Mungu alimuuliza Yeremia unaona nini mbele yako alichokiona Yeremia Mungu akamwambia umeona vema maana naliangalia neno langu nipate kulitimiza.

Sekiliza hicho ulichokiona miaka minne,au mitano,au miwili iliyopita bado kipo na wewe ndie wa kukifanikisha.

Wana wa Israel walitumia miaka 40 kuifikia nchi ya haadi lengo lao moja ilikuwa ni kuifikia nchi ya haadi basi.

Yusuph kusudi lake lilikuwa moja ni kudhibitishwa kwenye nafasi yake ambayo ilitoka kwa MUNGU mwenyewe.
Ayubu licha yay changamoto zake zote hakuhama kwenye kusudi la kumtumainia MUNGU.

Ile ndoa nzuri uliyoiona miaka kadhaa iliyopita utaifikia,ile kazi uliyoendea na ukaamua kuisomea utaiona.Hilo deni unalodaiwa miezi kadhaa,miaka kadhaa utalilipa

NOTE: REMEMBER THE GOAL, DON'T QUITE THE PROCESS,GOD IS WATCHING.(Muhimu:Kumbuka lengo,usikimbia mchakato Mungu anakutazama.)

REMAIN PURE-Baki Msafi.Bwana Yesu asifiwe,na ongera sana kwa majukumu yako ya kila siku,wote twastahili kulitukuza jina ...
30/08/2022

REMAIN PURE-Baki Msafi.

Bwana Yesu asifiwe,na ongera sana kwa majukumu yako ya kila siku,wote twastahili kulitukuza jina la Bwana wakati wote kwasababu yeye ndiye anaetuwezesha kuwa hivi tulivyo leo.

Kwakweli inafurahisha sana Taifa lenye mtu,au watu wanaomtumikia Mungu kwa mioyo yao yote wakitenda yale ambayo Bwana wao ataka wayatende.Ongera sana ikiwa wewe huu miongoni mwao.
Karibu sana kwenye somo letu la leo.Remain Pure ( Baki Msafi).
Katika hali ya kawaida kila mtu hupenda usafi iwe kwenye nyumba yake mwenyewe,mwili wake,mazingira yake n.k,yaani kuna watu kwa mambo ya mwili tu ni wasafi kweli kweli,ongera yako katika wewe ikiwa ni msafi katika mambo hayo ya mwilini,lakini somo letu zaidi limelenga usafi katika mambo yote.

Remain Pure,au Baki msafi,kisafi chochote huwa kinapendwa kwasababu ya kupendwa kinaganganiwa na katika kuganganiwa kule chaweza kuchafuliwa muda wowote na watakaosema hakifai tena ni wale waliokuwa wakikigangania,.
Leo hii kwa sababu ya maarifa kuibuka mengi,kuna maji tunayokunywa leo lakini chimbuko lake siyo kwenye chemichemi bali yanatolewa kwenye madimbwi mabaya alafu yanafanyiwa mchujo kupitia vifaa maalum na hatimae yanakuwa maji safi yanayostahili kunyweka.

Biblia inasema najua asili ya imani yako,manake Bwana anakutambua kuwa wewe ni wake ijapokuwa upo katikati ya watu waliokuchafua,yaani kuna watu unakaa nao lakini hawakuthamini tena,kwa maana ya kwamba wewe siyo wa muhimu kwao lakini mko pamoja,pengine ni aina yako ya maisha unayoishi,kuvaa kwako,wamezoe maneno yako,ahaadi zako,n.k.
Sasa anapokuja yule wa sirini atambue kuwa wewe ni safi,ili akufanye uwe safi Bwana Yesu anasema atakupitisha kwenye moto k**a mtu apitishavyo dhahabu kwenye moto,manake ataanza kusafisha nafsi yako na akikwisha kamilisha hivyo atakutambulisha katika jamii na watu watakuona unafaa kwa ajili ya kesho zao.

Sasa Bwana akikwisha kufanya msafi,usifikili wenye nia ya kukuchafua watakoma,sikiliza,Yesu katika wanafunzi wake kumi na mbili alikuwepo mmoja ambae yeye licha ya mambo yote aliyokuwa anayashuhudia kwa macho yake kutoka kwa Bwana Yesu bado ndani mwake nia yake haikuwa njema huyo ni Yuda Eskariot,hii ni kumaanisha kwamba yeyote uliyekaribu nawe anaweza kutumika kwamba kila ulifanyalo yeye anaona ni baya tu,kuna wanawake wameolewa kila analolifanya kwa mme wake bado mmewe maneno ya kejeli yatatoka kinywani mwake tu,au kila mwanaume analolifanya bado mwanamke haoni k**a mmewe ni shujaa kwake,ili uwepushwe na watu wa aina hii,kazi yako siyo kuugeuza moyo wako k**a watakavyo wao bali jukumu lako ni kuendelea kuwa safi moyoni mwako.
Kuna watu wamechafuliwa na wamekubali kujiona kuwa wao ni wachafu,wamekuwa na hisia za kujiona si kitu kwenye maisha,wameishia kujichafua moja kwa moja,wamefuta uaminifu wao kwa kila mtu,hawapendi tena,hawafanyi kazi kwa bidii tena,hawavai vizuri tena,hawasaidii watu tena,k**a ni kujukumika vizuri kwenye tendo la ndoa hawawezi tena n.k.

Ninachotaka nikwambie Yesu alitambua mapema sana nia ya Yuda eskariot kuwa ni mpinzani wake,yaani ni k**a mfano umeoa unakuja kutambua mkeo au mmeo hayuko upande wa maono yako ya shughuli zako,licha ya kwamba shughuli hiyo unayoifanya sasa,inamlisha,inamvisha nk lakini huwezi kusikia maneno mazuri kutoka kwa mkeo au meo akikupongeza,sasa ukiona hivyo usije ukaanza kudanganywa na watu wa nje unaokutana nao mfano katika shughuli zako unakutana na mdada yaani kuongea kwake kutenda kwake unaona angefaa kuwa mkeo au unakutana na mkaka anasema anakukubali sana kwenye kujituma kwako lakini neno hilo hujawai kulisikia kwa meo,usikulupuke kuanza mahusiano ya siri kati ya aina ya watu hao wawili kwasababu nia ya ibilisi ni kukuondoa kwenye kusudi nyuma ya mtu.

Jitahidi sana kudumisha nia njema kwa huyo mtu akupingae,asiyethamini uwepo wako,kuna vitu vingine Mungu uruhusu viwepo ili ajitwalie utukufu katika hayo,atakapomwondoa huyo mtu usiangalie nyuma tena,na kuingiza huruma zako za kijinga,Mungu atamleta mtu aliyekwisha guswa moyo kwa ajili ya kusudi lake mwenyewe,usije ukaangalia macho ya watu watakuonaje wewe songa mbele na timiza wajibu uliokwisha pewa.
Kwenye kitabu cha Samweli biblia inasema waliomchukia Sauli baada kupakwa mafuta teule ya kifalme wakaonekana si kitu,Mungu akamwinulia Sauli watu walioguswa moyo kuambatana na Sauli.

Ngoja nikwambie kitu baadhi ya vitu au taratibu zilizowekwa na wanadamu ili katika taratibu hizo kusudi la Mungu lizuiliwe kwa urahisi kabisa ni taratibu za kufunga ndoa kanisani,sikiliza kuna watu wanataka kuagwa vizuri nyumbani kwao ili waende kufanana k**a mama zao au baba zao huko wanakoenda,wengine wanataka tu waonekane wamevaa shera yaani hawana haja na kusudi ndani ya ndoa wanazoziendea,sasa usije ukatishwa na mtu awaye yote pale ambapo Mungu atakutaka ufanye maamuzi kwa ajili ya kusudi lake,kitakachokufanya ubaki salama dhidi ya maneno yao na vita yao ni kwasababu Mungu hakuona hatia juu yako.

Nihitimishe kwa kusema hivi,kubambwa kwa Yesu msalabani hakukutokana na kisasi cha adui zake walio mpinga,bali Mungu aliluhusu kwa ajili ya mimi na wewe tukombolewe,weka hofu pembeni muweke Mungu awe mtetezi wako kwenye kila hatua unayoikabili,.
God bless you.
Geofrey Julius-Jesus power ministry Tz

BRING BACK YOUR MIND -Rudisha akili yako.Bwana Yesu asifiwe,na ongera kwa majukumu yako ya kila siku bilashaka tunastahi...
10/06/2022

BRING BACK YOUR MIND -Rudisha akili yako.

Bwana Yesu asifiwe,na ongera kwa majukumu yako ya kila siku bilashaka tunastahili kumtukuza Mungu wetu sana kwa ajili ya neema zake na upendo wake mkuu sana usioelezeka kabisa.

Unajua ni raha sana Taifa kuwa na Vijana waliowekeza mioyo yao kwa Mungu taifa hilo hakika linalindwa na kubarikiwa kwa ajiri tu ya vijana hao,Kwasababu ya Yusuph pekee Misri yote ilipata chakula na mataifa mengi walikuja kununua chakula Misri.Kijana endelea kumtumainia Mungu hakika hatakuacha.

Okay somo letu leo hii linaeleza kuludisha akili zetu,kwa lugha ya wenzentu wanasema (BRING BACK YOUR MIND)

Paul anaeleza kwamba kwasababu watu wamemuacha Mungu akili zao zimepolwa na ibilisi,kwenye dunia leo tunaishi chini ya makundi makuu mawili ( Conscious and Unconscious mind group) yaani makundi ya watu wenye akili ya ufahamu na makundi ya watu wenye akili isiyokuwa na ufahamu.Wote hawa tunaishi nao kila siku na makundi ya watu wenye akili isiyo na ufahamu ni wengi na kwasababu ya wingi wao matatizo hayakomi katika jamii.

Ufahamu ukipolwa kinachotawala ni ujinga na roho hii ya ujinga kazi yake ni kuharibu huwa haina nafasi ya kufikilli mara mbili,chunguza sana watu wanaofanya matukio ya kutisha kwenye jamii wakikwisha fanya ujinga wao ule ufahamu ulejea kwa muda na mtu huyo ubaki kwenye majuto wengine wameishia jela kwasababu ya kukosa ufahamu,wengine wamepoteza nafasi zao za kazi,wengine ndoa zao,wengine marafiki wa karibu n.k

Jiulize Suleiman k**a asingepewa akili na ufahamu angewezaje kukaa na watu ambao miongoni mwao upuuzi ulikuwa mwingi,fikilia wale makaaba wawili mmoja wao anadanganya,analazimisha uongo uwe ukweli na ilipotolewa la kumkata mtoto katikati yeye alikwisha kukubaliana na uhamzi huo,kumbuka nilikwambia ujinga kazi yake ni kuharibu,ufahamu na akili alizopewa Suleiman ulimnusuru mtoto.
Watu waliopolwa ufahamu wanakuwaga wepesi kutafuta msaada kutoka nje hawako tiyali kutatua matatizo yao wenyewe kwanini kwasababu wanaamini wakiwa na kundi la kwatetea watatimiza kwa wepesi kusudi lao.Ooh God tizama kundi lilomkataa Kristo Bwana linainua mashtaka ambayo Yesu alifanya kweli lakini yanageuzwa kuwa siyo halali na wote waliona siyo halali Yesu kujiita mwana wa Mungu wakati ni halali yake.

Tizama hapa Daniel 4: 34 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;

Mfalme Nebukadreza fahamu zinamrejea,alafu zinamrejea akiwa peke yake,hana mke,wala watoto,wala marafiki,wala mtu yeyote aliyekuwa karibu naye,yuko peke yake msituni,mtu aliyekuwa akiongoza kundi kubwa la watu,anakaa kwenye kiti cha kifalme cha maamuzi lakini ghafla kwasababu ya ujinga wake kumzidi na kuanza kutamka maneno ya kujisifu ona hapa Daniel 4:30-31 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?
31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.

Mara nyingi ujinga kuondoa kwenye nafasi yako,weka akilini mwako kwamba leo hii roho hii iliyomvaa Mfalme Nebukadreza ya ujinga imewakaba wengi sana leo hii wakubwa kwa wadogo,walio na ufahamu wanamhitaji Mungu sana wapate kuishi.
Huwezi ukaishi kwa maana ya kwamba upate mlo wako,uvae,ulale salama k**a huna nguvu za Mungu,nenda kasome habari za Modekai katika kitabu cha Esta dhidi ya adui yao naamani.

Inahitajika hekima na akili itokayo kwa Bwana kuweza kutambua ujinga ulioko nyuma ya mtu,kwasababu kuna uwezekano mkubwa wa kumuita mwenzako mjinga wakati na wewe roho ile ile ya ujinga iko ndani mwako,ndio maana watu wenye ufahamu siyo wepesi kuongeza neno juu ya neno,huwa wanasikiliza alafu wanakaa kimya,Mungu anaposema usilipize kisasi,kisasi ni juu yangu,ni kweli unaweza kuona unahaki ya kulipiza kisasi lakini kitendo cha kujitwalia mkono wako wa kisasi Mungu anakaa pembeni,yaani aibu iliytakiwa kumpata huyo mtu inakugeukia wewe kiasi cha kushangaza wengi.mfano mkeo anaweza kukuletea jambo flani ukamsikiliza alafu ukaishia kunyamaza kimya usimjibu k**a alivyotalaji kujibiwa,kwa kunyamaza kwako kimya unampa mwana wa kujiludi na kutafakari upya jambo hilo.kwanini unahitaji kutulia kabla haujatoa maamuzi ni kwasababu ya kuipa nafasi akili uliyopewa na Mungu ipate kuchagua ukweli na uongo juu ya jambo hilo,ndicho kilichofanyika kwa Daniel,Daniel hakutoa majibu papo kwa papo aliomba apewe muda na alipokuja akaleta uhalisia wa jambo lenyewe.

leo hii unasikia kesi za watu kufungwa bila hatia,wengine kuuawa bila kosa,wengine kutengenezewa hila za uongo ndicho kilichotokea kwa Yusuph,kumbuka kitu kimoja kesi iliyomwingiza gerezeni Yusuph siyo kesi iliyomtoa gerezani Yusuph.
Okay nihitimishe hivi daima usiluhusu akili zako na ufahamu wako uliopewa na Mungu uondoshwe nyuma ya taarifa unazozisikia kwasababu huo ndio uzima wako,imeandikwa ishike sana elimu usiache iende zake,kitakachokusaidia utoke kwenye mtego uliotengenezewa ni ufahamu wako na akili,watu watasema unalinga,unadharau la hasha siyo kulinga ni kwasababu unajua.Yesu anasema imani yako imekuponya manake kujua kwako kumekusaidia.

GOD BLESS YOU
Geofrey Julius

HIDEN FOR PURPOSE,FOR A REASON AND FOR A SEASON. (Kufichwa kwa kusudi,kwa sababu and kwa Muda.Hujambo na Shalom,ongera s...
18/05/2022

HIDEN FOR PURPOSE,FOR A REASON AND FOR A SEASON. (Kufichwa kwa kusudi,kwa sababu and kwa Muda.
Hujambo na Shalom,ongera sana kwa majukumu yako ya kila siku,nafurahishwa sana jinsi ambavyo Mungu anavyotupenda na zaidi ya yote anavyotulinda.

Leo roho wa Bwana ametupenda tushirikishane kwa pamoja kuhusu utendaje wa Mungu kwa walio wake na wanaotaka kufahamu habari zake za kweli na kuja kwake karibu tujifunze pamoja yawezekana mimi na wewe tukapata kitu muhimu kuhusu somo hili.
Okay Somo letu linasema kufichwa kwa kusudi,kwa sababu na kwa muda.
Bwana wetu Yesu Kristo anatambua kabisa kwamba kila amfuataye hana budi kukinywea kikombe chake na kwasababu hiyo,miiba na michongoma imeandaliwa mbele yake lakini zaidi ya yote anasema tusiogope kwa ajili ya hiyo.

Tukianza na neno KUSUDI(YAANI KIPAJI CHAKO AU JUKUMU LAKO LA NDANI) kwenye eneo hili ndio Ufalme wa Mungu uliko,unahitaji kufunzwa taratibu na kanuni zake kuhusu kusudi lako na namna utakavyoliishi ni eneo ambalo unafunzwa na kuonyeshwa maono jinsi jukumu lako litakavyokuwa siku za usoni,unafunzwa jinsi ya kulihudumia na siyo lenyewe kukuhudumia.

Kwenye eneo hili Mungu anaweza kukutenga na jamaa zako yawezekana ni mkeo,watoto wako,baba na mama yako,ndugu zako na hata marafiki unakuwa ni k**a vile mtu usiyekuwa na ndugu,kipindi hiki kinahitaji utulivu wako mkubwa sana.Yusuph katika biblia ilibidi Mungu amtenge kabisa na familia kwasababu kusudi lilokwisha wekwa ndani mwake ni takatifu na linahitaji kutunzwa kwa kiwango cha juu,ndio maana Yesu anapokwambia jihadharini sana nafsi zenu si tu uende mbinguni hapana bali kusudi lilokwisha wekwa ndani mwako lidhihilishwe kwa wengi.Ndio maana Yusuph alipoingizwa mtegoni mwa mke wa boss wake Potifa,Yusuph alisema nifanyeje uovu huu ni mkose Mungu wangu,manake ndani mwake lipo kusudi na kusudi hilo ni takatifu,angefanya jambo hilo la kulala na mke wa Potifa manake angemkosa Mungu na angekosa maisha yake ya baadae.

Yesu anapenda sana muungano na familia,anapenda uhusiano mwema ndani ya familia lakini panapokuja eneo la kusudi Yesu aweki roho ya chuki kwa mtu aliyekwisha mchagua na kuwa tiyali kumtenga kulingana na mazingira aliyonayo kwamba asiwe na ugomvi wa moyo dhidi ya watu aliowagundua kuwa ni wabaya wake,ndio maana kusudi la Yusuph lilipodhihishwa kwa wengi,alipotambua ndugu zake alisamehe na kuwaleta wote katika nchi alikokuwa akiishi.

hapa chunga sana roho ya kicho yaani roho ya huruma utaliua kusudi kabla halijazaliwa Mungu anasema usiwe na kicho yaani usifikili una huruma kuliko Mungu,una upendo kuliko Mungu,ukiweza katika hapa Mungu atakuwa tiyali kuambatana nawe.

NENO KWA SABABU.
Wengi tumeokoka katika mazingira yaliyokwisha hatamiwa na ibilisi,.Gidion mtumishi wa Mungu alitengwa kwa Muda na kuanza kufunzwa na Bwana,Gidion asingeweza kuharibu madhabahu ya baba yake k**a ndani mwake hajatengenezwa kwa maana ya kuvuviwa nguvu ya kushinda nguvu nyingine,hapa panahitaji utulivu ni eneo ambalo utakuwa unazungumza na Mungu mara kwa mara,inakuwa ni eneo la kufunzwa namna ya kudili na mafundo,vifungo na nira nyingi kuhusu wewe mwenyewe au kuhusu watu wengine,unapitishwa kwenye moto wa hali ya juu sana.Yakobo aliposema sitoki hapa mpaka unibariki,haikuwa battle ya kawaida,wengi watasema ni batlle ya usiku mzima lakini ilikuwa na zaidi ya usiku mzima,usiku uliobadili maisha yake na kupewa jina jipya na katika yeye leo tunaitwa wana wa Israel (yaani kizazi teule cha Yakobo). Mungu akisema usifenye jambo flani hakikisha haufanyi hata k**a kuna presha nyingi kutoka kwa watu wengine.Haya ninayokueleza nimeyaona na nimeyapitia.

Moja ya sababu nyingine Mungu anajua ya kwamba watu waliokuzunguka wamekusudia kukatisha maisha yako kwa muda flani,kwahiyo kabla ya jambo hilo kutimia Mungu anakuondoa na ukuwekea roho nyingine ya kumtambua yeye.Mungu alizungumza na Yusuph mme wake Mariam kwamba mchukue mtoto huyu mpeleke Misri kwani Pharao amekusudia kumuua,manake hakuna namna nyingine ya kunusuru kusudi hilo la ndani zaidi ya kukutoa kwenye mazingira flani,epuka kushawishiwa na jambo lolote lile hapa hakika utamuona Mungu na kusudi hilo litaendelea kulindwa,hutakufa licha ya wale waliokuwa na kusudi lao baya kukuandama kwa wingi lakini Yesu anasema usiogope ashuru zao.Yeye anawaita mbweha hahaha.

NENO KWA MUDA.
Kila kitu Mungu amekipa muda wake,muda aliyouweka yeye ukifika umefika,kila hatua ya mufunzo yana muda wake,mashuleni tunawekewa muda wa kufunzwa,kazini kadhalika,mtoto ana muda wake wa kukaa tumboni mwa mama yake,ukiweza kutoka huko kote na kuhusubili muda utaona kila ulichokiona kwenye maono na kitabaki kuwa ndoto.Ibrahim na Sarah mkewe walifichwa kwa muda wa miaka 25 kabla ya kuupata uzao wao ISAKA,Daudi alifichwa kwa miaka 17 kabla ya kuketishwa kwenye kiti cha Ufalme,Yusuph alifichwa miaka 13 kabla ya kufanywa waziri mkuu.

Nimalizie kwa kusema umuhimu wa maisha yako ni kusudi lako,watu wengi wanasema watu ni mali lakini watu hawaji kwako bila kusudi,kwahiyo kusudi ni mali na huo ndio ufalme wenyewe.
Usiogope kwa kuwa peke yako kwa muda wa miaka kadhaa,Yohana alitengwa akapelekwa msituni akila nzige na asari,Yesu alipelekwa jangwani akizungukwa na mbweha wengi lakini maraika walikuwa wakimlinda.

AMINI MUNGU YUPO.
God bless you .
Geofrey Julius

Bwana Yesu asifiwe,usikose kujiunga nami katika semina yetu leo jioni kupitia mtandao wa zoom saa kumi na moja za jioni ...
23/03/2022

Bwana Yesu asifiwe,
usikose kujiunga nami katika semina yetu leo jioni kupitia mtandao wa zoom saa kumi na moja za jioni 5:00
Ili iweze kushiriki vyema kuwa na app ya zoom kwenye simu yako au kwenye computa yako.
Karibuni.

Geofrey Julius is inviting you to a scheduled Zoom meeting.
Topic: PROTECT YOUR BELOVED SON -SECOND EDITION
Time: Mar 23, 2022 05:00 PM Nairobi
Join Zoom Meeting
https://us04web.zoom.us/j/9924392382...
Meeting ID: 992 439 2382
Passcode: 860616

PROTECT YOUR BELOVED SON.(MLINDE MWANAO MPENDWA).Bwana Yesu asifiwe na ongera sana kwa majukumu yako ya kila siku,lakini...
17/03/2022

PROTECT YOUR BELOVED SON.(MLINDE MWANAO MPENDWA).

Bwana Yesu asifiwe na ongera sana kwa majukumu yako ya kila siku,lakini pia kumshukuru Mwenyezi Mungu yeye anaetuwezesha kuwa hivi tulivyo leo hii.
Leo roho mtakatifu amenikumbusha nikushirikishe jambo hili na pengine kuna vitu inakuhitaji uvijue kuhusu watoto wako au mwanao ajae au aliyekwisha kuwepo.
Somo letu la leo linaitwa Protect your beloved son( mlinde mwanao mpendwa).

Ni ukweli usiopingika mzazi au wazazi wanaweza kuwa na watoto kumi au watano n.k lakini mzazi katika hao watano yupo mmoja apendwae sana,wakati mwingine mzazi anaweza kujitahidi kuficha upendo huo lakini mara nyingi ushindikana mpaka wote mle ndani mnajua baba au mama anampenda nani.
Sasa wazazi hawa wawili yaani baba na mama baba anaweza kuonyesha upendo wa wazi kwa mtoto flani lakini mama nae akawa na mtoto wake anaempanda.Unaweza ukawa hautoki katika familia za zaidi ya wake watatu au wawili unatoka kwenye familia ya baba mmoja na mama moja lakini baba asiposimama imara mzao wake wa kwanza wa haki atachukuliwa anaweza akafa ghafla,au madhabahu ya mama ya siri ikamfanya kuwa wa mwisho waswahili wanasema kupigwa zongo (mzee anapigwa zongo upendo unahama ghafla yaani mzee anahamisha uridhi wake kwa mtoto mwingine lakini si kwasababu anampenda huyo bali madhabahu ya mkewe imeamua kufanya hivyo.) Biblia inasema enyi waume ishini na wake zenu kwa akili,kitendo cha kuhamishwa fahamu mzee wa nyumba ukoo wako wote unauingiza mateka chini ya madhabu ya mkeo ambae yeye anauwakilisha ukoo wa nyumbani kwake,uzao wako na ukoo wako utaitegemea madhabu ya ujombani.

Sikiliza Mungu alimwambia Ibrahim kwamba uzao wake utaingizwa matekani kwa muda ya miaka arobaini,lakini lilibaki fumbo kwa Ibrahim hakuambiwa kwasababu gani wataingizwa mateka watu hao. Okay,uzao wa Ibrahim wa haki yaani ISAKA akapata mke,na huyo mke aliyepata Mungu alihusika kabisa asilimia miamoja,.Isaka akapata uzao katika uzao ule ISAKA akampenda sana Esau kuliko yakobo na mkewa akalijua hilo,jambo hilo halikufanyika baraka kwa mkewe ISAKA, Yakobo akajikuta anapendwa sana na mama yake kuliko baba yake.Swali ni je kwa nini upendo wa ISAKA ulionekana mkubwa kwa Esau ni kwasababu Esau alikuwa akimletea mzee chakula kitamu alichokiwinda mwenyewe.
Bilashaka mawindo ya Esau yalikuwa yanaliwa na familia yote,je kwa nini hilo halikumpendeza mama yake Esau,mama akaona afanye hila kwa mtoto wake mwenyewe aliyemzaa tena na uchungu alipata lakini akaigeuza kesho ya Esau kwa hila.

Sasa tizama madhabahu za giza zilizo na nguvu,ni kitu gani kiliuteka moyo wa mama yake Esau na kuona kwamba anaestahili kupata mbaraka wa haki ni Yakobo.kumbuka mama yake Yakobo alikuwa na kaka yake anaitwa Laban na huyu kaka yake yeye alikuwa mshirikina kwahiyo madhabu ya kaka ikaukaba moyo wa dada yake,yaani Mama yake Esau alipokwisha kufanya tendo hilo la hila akamtuma kwa haraka Yakobo akae kwa mjomba wake Laban ajipatie mjtaji huko.
Lakini kwa sababu madhabahu ile ndio ilihusika kugeuza moyo wa dada yake Yakobo hakuweza kufanikiwa kwa mjoba wake matokeo yake akaingizwa mateka na mjomba wake.Yaani Laban akawa anahusika kula kwa Yakabo,kuvaa kwake,kulala kwake lakini pia kulisha wake zake na watoto wake kumbuka ni ujombaniiiiiiii.

Chunguza sana katika familia za kiafrika wajomba wanahusika sana kulea watoto wa dada zao upande wa baba wengi wao nguvu ya kiuchumi huwa ni changamoto k**a yuko mmoja anaonyesha kamwanga kwenye ukoo huo akifa ndio imeisha hiyo.
Nguvu ya Yakobo kutoka mikononi mwa mjomba wake ni Mungu mwenyewe,tena mjomba alipotaka kuinua kisasi dhidi ya Yakobo Mungu akamwambia usijaribu kumfanya chochote Yakobo,haikuwa mizimu ya baba yake ISAKA au mzimu wa ISAKA mwenyewe alikuwa ni Mungu mwenyewe.
Ninachotaka utambue hapa nini ni kwamba mtoto wako mpendwa anaweza kupolwa haki yake ya uridhi na akaashiria kupoteza mwelekeo kabisa lakini k**a Mungu anahusika katika upendo huo siku wasiyodhania watu huyo mtoto wako mpendwa Mungu atamkumbuka na sasa atahamisha upendo wake wote kwa huyo mtoto na atafanyika kuwa mridhi wake yaani YESU KRISTO BWANA ndicho kilichofanyika kwa Yakobo,Mungu anamwambia Yakobo hutaitwa Yakobo tena bali utaitwa Israel,neno hutaitwa Yakobo tena manake yakobo alikuwa mkiwa,tasa anajiona yuko na watu,familia alifikili yuko mahali salama kumbe alikwisha polwa na nafsi imefichwa kwenye vitunguli za mjomba wake.

Nakumbuka siku moja miaka imekwisha pita kidogo nikaona njozi katika njozi hiyo niliona mwanga mkubwa sana ukitoka mbinguni na nilikuwa naonekana niko kwenye msitu alafu katika mwanga ule ndani yake kunatoka sauti na sauti hiyo ilikuwa nzito sana na likatamkwa jina jipya () nimeliweka kwenye mabano niliposhtuka sikutaka kuifuatilia sauti hiyo kwasababu nilikuwa nakula,nakunywa,nalala bure kabisa sina mawazo lakini baada ya kuanza maisha yangu na nikaokoka ndio sasa sauti hiyo nikaweza kuitambua.

Nihitimishe kwa kusema hivi,kuna watu ni watumishi leo lakini kabla ya utumishi wao hawakuwa wanajua wanastahili kufanya nini katika maisha yao,ukipolwa haki yako ya upendo kwa mzazi wako au wazazi wako iwe umezaliwa kwenye familia ya zaidi ya moja,majira yako yatafika ya kuitambua sauti ya Mungu ambaye yeye ni mtoa uridhi usioweza kufananishwa wala kulinganishwa na jamii ya kwenu,mara nyingi fikra za wanafamilia wengi zipo katika kile wanachokiona na kwasababu ya hicho upendo wa kinafiki ni mwingi ndani mwake kukuua,kukufanya mgonjwa wa kudumu kwao siyo shida,sikiliza mama yake Yakobo hakuna mahali biblia inasema alijutia uovu wake yeye aliona ni sawa kufanya hivyo na hukuna mtu wa kumuuliza,lakini kwasababu ya kosa hilo uzao wa yakobo ukaingizwa mateka miaka arobaini.
K**a yupo mtoto unampenda ukijua kesho ya mtoto huyu ni ya wengi hakikisha unamshika Mungu,kwasababu madhabahu inayopinga upendo huo inamtafuta mwanao ipate kummeza.

Mungu akubariki sana.
Geofrey Julius

Address

Usa-River
Arusha
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jesus Power Ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Jesus Power Ministry:

Share

Category