14/07/2024
Kanisa la Adonai Pentecostal Church International-Dzaleka Adonai pentecostal church Dzaleka
NENO LA LEO 14-07-2024
Mhubiri: Ev. K**ALEBO
Nehemia 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Habari za Nehemia, mwana wa Hakalia. Ikawa katika mwezi wa Kisleu, mwaka wa ishirini, nilipokuwapo Shushani ngomeni,
…
⁶ tega sikio lako, macho yako yakafumbuke, upate kuyasikiliza maombi ya mtumishi wako, ninayoomba mbele zako wakati huu, mchana na usiku, kwa ajili ya wana wa Israeli, watumishi wako; hapo ninapoziungama dhambi za wana wa Israeli, tulizozifanya juu yako; naam, mimi na nyumba ya baba yangu tumefanya dhambi.
NENO:
Nehemia alikuwa Muyahudi ambaye alikwenda utumwani huko BABELI,Wana wa Israeli walitenda zambi mbele za Mungu naye Mungu akawaazibu nakumtuma Mfalme Nebukandeneza huko Babeli naye akawapiga nakuwapeleka watu huko Babeli.
ZERUBABELI
Baada ya miaka 60 kundi la pili likatoka kuongozwa na mtumishi wa Mungu EZDRA
Baada ya miaka 80 chini ya mfalme ALTASHASTA kundi la tatu likaongozwa na mtumishi wa Mungu NEHEMIA mnamo mwaka wa 4444
Aliyelijenga Hekalu la Yerusalemu ni kundi lile la pili la EZDRA
NEHEMIA naye huko alikua na mnywesha mfalme divai ama kinywaji,
Sasa akiwa huko Shushani watu wakutoka Yerusalem naye Nehemia akawauliza habari na hali za Yerusalem,naye HANANI akamjibu NEHEMIA kwamba mji uko katika hali ya mateso na Yerusalem iko katika hali mbaya saana,ukuta ama ulinzi wa Yerusalem umebomolewa na kwamba malango yake yamechomwa na moto.
Ukuta huo ulikuwa ni ulinzi juu ya mji mkubwa,hata adui hakuwa na njia yakupitia lakini ulipobomolewa kila adui alikua naingia mara kwa mara,
Alipoambiwa habari hio,NEHEMIA akauguwa rohoni,akakosa amani,Biblia inasema kwamba
NENO: ISHI MAONO ULIYO YABEBA, ISHI MALENGO
K**a vile maneno ya Mungu inasema Tusiyasikie tuh maneno bali tuyatende
NEHEMIA akaomba Mungu
Hio ilikuwa hatuwa ya kwanza,na maombi yake hayakukuwa ya kawaida,alitubu zambi zake,zambi zamababu zake...
Siku ya pili alipoenda kwa Mfalme kumnywesha naye Mfalme akamuona Nehemia akaona kwamba hali yake sio nzuri,
“Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.”
— Nehemia 2:2 (Biblia Takatifu)
SWALI: KWANINI NEHEMIA ALIHUZUNIKA KWA AJILI YA YERUSALEM?
Kwasababu ndani yake mulikua Upendo na Huruma ndani yake,
Sio sisi wakristo mwenzako anapopatwa na shida wewe unafurahia,mwenzenu anateseka wewe unacheka.
2. WIVU WA KAZI YA MUNGU: Wengine hawana wivu wa kazi ya Mungu,kwamfano wewe ni muimbaji hauwezi furahia uimbaji unaenda vibaya,
3. HAKUA MUBINAFSI: hakujifungia ako kazi yote hio
4. ALIKUWA ALIBEBA MISINGI YA YERUSALEM NDANI YAKE: Kiukweli kulikuwa watu wenye nguvu nyingi,wenye pesa,ma injenia mafundi wakubwa lakini misingi hio ilikua nabebwa na NEHEMIA,
MPENDWA acha nikuambie kwamba wewe sio wakawaida,Nehemia hakukua fundi,hakukua nanguvu zakuijenga Yerusalem
MFALME AKAMUULIZA,NIFANYE NINI? NEHEMIA hakuishia kuomba tuh lakini alifanya hatua
“Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni.”
— Nehemia 2:4 (Biblia Takatifu)
ALIMUOMBA MFALME RUHUSA NA MFALME AKAMPA VITU VILIVYOKUA NA ITAJIKA...
Tumesikiya habari za ujenzi wa Yerusalem,nasi mioyo yetu imeharibika,familia zetu zimeharibika,kuna watu wanaoishi katika nyumba moja,katika kanisa moja lakini hawaongeyi,hawana mahusiano ya sawa,Leo nisiku ya kujenga familia zetu,leo nisiku yakujenga kanisa zetu,
Nehemia alimweka Mungu mbele na hata mfalme akamsaidia Mpendwa,wakati unamuweka Mungu Mbele anatumikisha hata adui yako ili akusaidie katika mambo unayoyafanya.
KUNA MAOMBI YAKIPEKEE AMBAYO UNAITAJIKA KUOMBEWA ILI UJUWE MAONO ULIYOYABEBA, NA UISHI MALENGO UWE K**A NEHEMIA.
Muhubiri: **alebo
Mwandishi: Prince Malipo Gedeon Prima