Efatha Ministry Ukunda

Efatha Ministry Ukunda Healing and Deliverance by the blood of Jesus Christ

SOMO: KUSUDI MAALUM LA MWANADAMUWarumi 8:30"Na wale aliowachagua tangu mwanzo, hao pia aliwaita..."Mimi na wewe tumechag...
21/07/2026

SOMO: KUSUDI MAALUM LA MWANADAMU

Warumi 8:30

"Na wale aliowachagua tangu mwanzo, hao pia aliwaita..."

Mimi na wewe tumechaguliwa kabla ya kuumbwa kwa dunia. Mungu alikuwa na kusudi na maisha yetu tangu mwanzo.

Mwanzo 1:26–27

"Na Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu..."

Mimi na wewe tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Pia tumeumbwa kwa kusudi la Mungu. Sisi ni miungu wadogo, mbona sasa tunakata tamaa? Huku kuvunjika moyo kunatoka wapi?

Viumbe vyote alivitamka vikawa, lakini sisi Mungu alitufinyanga, akatupulizia pumzi ya uhai. Uhai wetu na wa wanyama haufanani, maana sisi tuna pumzi ya Mungu.

Kwa ajili ya kuumbwa na kufinyangwa, tuna kazi ya kufanya. Tunapotoka hapa, tutoke tukiwa hatujioni wadogo tena. Tamka: “Nimebarikiwa.”

Mungu alipotuumba alitubariki na akasema tuzae, tuongezeke. Tulipewa kuijaza nchi na kuitiisha. Chochote unachokitaja kiko chini ya uweza wako.

Tumepewa kutawala viumbe vyote vya angani na majini. Tuna mamlaka ya kila kitu: kuumba, kuharibu na kutengeneza. Tambua kuwa una kazi ya kumwakilisha.

Ambia moyo wako kwamba ni lazima uende sawasawa na kusudi la Mungu, maana tumepewa vyote. Mungu anangoja mimi na wewe tujitambue kuwa tunaweza.

Mungu hampi mtu jaribu asiloliweza. K**a ulijaribu kufanya vitu vikashindikana, usife moyo; endelea mbele. Hakuna mwenye kusudi la Mungu ambaye hapitii mapito.

1 Wakorintho 10:13

"Jaribu halikuwapata isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu... lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea..."

Kila jaribu, mlima au changamoto, jua kwamba haiko pale kukumaliza. Iko pale ili upate ushuhuda na Mungu ajitukuze.

Katika hali ya kushindwa, usichoke; ng’ang’ana mpaka utoboze. Chochote ambacho ni mlima, kisambaratishwe kwa maombi.

Kila jaribu lina mlango wa kupitia. Usikate tamaa mpaka siku ile mlango utakapotokea. Usichoke kuomba, kufanya ibada na kutumika.

Ili uweze kukitunza ulichopokea, ni lazima uombe. Chochote kigumu unachopitia, tengeneza toolbox, ukiweke ndani na umpige Ibilisi.

Esta 4:11–16

"...Na ni nani ajuaye k**a hukufikilia ufalme kwa wakati k**a huu?"

Popote ulipo, tambua una kazi ya kufanya. Mungu hakupi kazi kwa sababu anaweza, bali kwa sababu yeye anafanya ndani yako na kukuwezesha. Kile ambacho unakiona hakiwezekani, kifanye.

MAMBO UNAYOHITAJI KATIKA WITO

1. Uwe mtu wa maombi.
Elisha alikaa katika nafasi ya maombi hadi akajibiwa. Mngoje Bwana kwenye maombi.

2. Tengeneza watu wanaofanana na wewe.
Esta alitengeneza watu wa kufunga pamoja naye.

3. Soma Neno.
Nguvu ya maombi itakuja yenyewe.

4. Vua roho ya uoga, vaa roho ya mamlaka.

IBADA YA JUMAPILI

©️ASKOFU: DINA ADUO


Efatha Ministry Ukunda

In the presence of God, pouring our hearts of worship...🎶 Wema wako tumeona, eee Baba tumeuona... 🎶 🎵
21/07/2026

In the presence of God, pouring our hearts of worship...
🎶 Wema wako tumeona, eee Baba tumeuona... 🎶 🎵

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA, UKUNDATarehe: 19.07.2026Kiongozi wa Ibada: Felista ShadrackZaburi 25:6–11"Ee ...
21/07/2026

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA, UKUNDA
Tarehe: 19.07.2026

Kiongozi wa Ibada: Felista Shadrack

Zaburi 25:6–11
"Ee Bwana, zikumbuke rehema zako na fadhili zako, maana zimekuwapo tangu milele... Kwa ajili ya jina lako, Ee Bwana, unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi..."

Zaburi 27:13–14
"Naam, naamini nitaona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai. Umngoje Bwana; uwe hodari, na moyo wako upate nguvu; naam, umngoje Bwana."

SOMO: SISI NI ASKARI WA YESUMaombolezo 3:22–23“Ni kwa huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi....
14/07/2026

SOMO: SISI NI ASKARI WA YESU

Maombolezo 3:22–23
“Ni kwa huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila asubuhi; uaminifu wako ni mkuu.”

Mara nyingi tunajikwaa na kumtendea Mungu dhambi, lakini hatuangamii kwa sababu ya huruma na rehema zake. Kabla hatujaokoka tulikuwa hatufai, lakini yeye ametustahilisha kwa neema yake.

Zaburi 55:22
“Mtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza; Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.”

Je, umekuja ukiwa umelemewa na mizigo? Leo Bwana anasema umtwike mizigo yako, maana anajua mapito unayopitia.

Mathayo 11:28
“Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”

Yesu anasema atakupumzisha mizigo yako.

2 Timotheo 2:1
“Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.”

Sisi ni askari wa Yesu, na kuna vita tunapaswa kupigana. Askari lazima afanyiwe recruitment kwa sababu anaenda vitani. Wakati wote askari anatakiwa kuwa tayari na kuwa makini. Pia askari hupitia safari ya taabu na kuvumilia. Sisi ni raia wa mbinguni na ni askari wa Yesu.

Askari wa Yesu si wa kawaida, maana tumepakwa mafuta kwa ajili ya kuukuza Ufalme wa Mungu. Askari wa Yesu anajua kujituma na hasukumwi. Hakuna askari anayepewa taji k**a si halali. Tuwe na stamina katika wokovu. Unapopitia shida, tafakari neno la Mungu. Tunapaswa kuwa na bidii.

Sisi ni wana wa Mungu na ni barua inayosomeka. Ukizingatia kuwa hodari na shujaa, Mungu atakupa uelewa. Sisi ni vyombo vya Mungu; je, wewe ni chombo cha aina gani? Je, ni cha mbao, chuma, au dhahabu? Je, ni vita gani unaweza kustahimili k**a mwana wa Mungu? Askari wa Yesu anaweza kustahimili vita zote. Yesu akija leo, utapewa thawabu gani kwa kazi ya Mungu uliyofanya?




IBADA YA JUMAPILI
©️ MTUMISHI MWANGI

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA UKUNDAKIONGOZI WA IBADA: ASKOFU DINA🎶 Eee Bwana, uniumbie moyo safi. 🎶Wafilipi...
14/07/2026

IBADA YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA EFATHA UKUNDA

KIONGOZI WA IBADA: ASKOFU DINA

🎶 Eee Bwana, uniumbie moyo safi. 🎶

Wafilipi 4:4–8

"Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno, kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu. Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yote yenye staha, yote ya haki, yote yaliyo safi, yote yapendezayo, yenye sifa njema, ukiwapo wema wowote na ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo."

KARIBU MWEZI JULAIMwezi huu wa Saba ni Mwezi Wako wa Kudunda, Kufanikiwa, Kustawi, Kushinda na Kuvuna, hivyo Ninaamuru M...
01/07/2026

KARIBU MWEZI JULAI

Mwezi huu wa Saba ni Mwezi Wako wa Kudunda, Kufanikiwa, Kustawi, Kushinda na Kuvuna, hivyo Ninaamuru Muujiza wako ukujie sasa, ustawi wako ukujie sasa, Mafanikio yako yakujie sasa, ili upate kumchezea Yesu.

Mwezi Huu utapokea Muujiza wako, Uponyaji wako, Ukombozi wako, Mafanikio yako na Utajiri wako katika Jina la Yesu.

28/06/2026

Kambi ya Vijana iliyoanza tarehe 17 hadi 20 Juni mwaka huu 2026 haikuishia kuwa mkusanyiko wa vijana tu, bali ilikuwa mahali pa kugundua na kuwasha vipaji.

Kijana huyu anashuhudia jinsi ambavyo kupitia mashindano yaliyofanyika kambini, kipaji chake cha kuhubiri kilivyopata nafasi ya kung'aa na kuwaka zaidi. Leo anamrudishia Mungu utukufu kwa kile alichokifanya katika maisha yake.

🔥 Mungu bado anainua vijana na kuwaandaa kwa ajili ya kusimama katika wito wao.

Je, ni kipaji gani unaamini Mungu ameweka ndani yako? Tuambie kwenye maoni. 👇
❤️ Like | 💬 Comment | 📲 Share ili ushuhuda huu uwatie moyo vijana wengi zaidi.




'swill

Usipitwe na  tukio hili la kumpata  mshindi kwenye  Categories mbalimbali  zilizokuwa zikishindaniwa kwa siku tatu.LIVE ...
20/06/2026

Usipitwe na tukio hili la kumpata mshindi kwenye Categories mbalimbali zilizokuwa zikishindaniwa kwa siku tatu.

LIVE ON Don't Plan to Miss




'swill

⏰ HATIMAYE NI LEO! 🔥Siku tuliyoisubiri kwa hamu kubwa imewadia! Karibu kwenye Kambi ya Vijana inayofanyika Precious Cent...
17/06/2026

⏰ HATIMAYE NI LEO! 🔥
Siku tuliyoisubiri kwa hamu kubwa imewadia! Karibu kwenye Kambi ya Vijana inayofanyika Precious Centre, Kibaha.

📍 K**a unatoka mjini au mkoani, shuka Kituo cha kwa Matias na utaelekezwa moja kwa moja kwenye eneo la kambi.

USIKOSEEEE, KUMENOGA WEWEEEEH🔥🔥🔥



'swill

17/06/2026

Address

Ukunda

Opening Hours

Wednesday 17:30 - 18:30
Friday 22:00 - 05:00
Sunday 10:00 - 13:00

Telephone

+254721936884

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Ministry Ukunda posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share