08/03/2024
NENO LASIKU
Na, Mama Eliakunda Mwingira- Kanisa la Efatha
Tarehe 08/03/2024
SOMO: BWANA NIUMBIE TABIA YAKO KATIKA MAISHA YANGU
Zaburi 20:1-9 “Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. Bwana akutimizie matakwa yako yote……..”
Bwana akaonekane katika maisha yako, wewe uliyekuwa umeinama ukainuke na Bwana akakupelekee msaada wakati unaohitaji, maana ni ahadi na mpango wake kwamba yeyote anayemkimbilia anamshika mkono na kumtegemeza.
UKIRI:
•Bwana nipe kutii sheria na maagizo yako maana ndipo utatii yale ninayokuomba, niondolee tabia ya maswali maswali na uniumbie tabia ya utii.
•Baba yangu wa mbinguni niumbie tabia ya uaminifu katika kukupenda wewe, uaminifu katika matoleo yangu, utumishi wangu na katika maisha yangu kwa ujumla. Umba tabia ya uaminifu ndani yangu na iwe ndio maisha yangu maana hivi ndivyo ulivyo wewe BABA yangu, k**a alivyo baba ndivyo alivyo mwana nipe kufanana na wewe Bwana.
•Eeh! BABA nipe kujitoa kwa ajili ya utukufu wa Jina lako, umeonesha mfano kwangu pale ulipomtoa mwanao wa pekee Yesu akafa msalabani kwa ajili yangu mimi niliyekuwa nimepote na leo nimepatikana, tabia hii iwe ya kwangu. Nipe kujitoa kwa ajili ya kazi yako na kwa ajili ya wengine, kutoa nguvu, mali zangu na kila nilichonacho kwa maana kila nilichonacho ni cha kwako, wewe umenipa ili nivitunze nakubali BWANA kuvitoa kwako wakati unaofaa na usiofaa.