19/08/2026
🌙🔥 MAOMBI YA USIKU
USILALE NA MZIGO AMBAO MUNGU ANAWEZA KUKUBEBEA!
✨ UTANGULIZI
Mpendwa, kabla hujalala usiku huu, simama kidogo mbele za Mungu.
Huenda leo umepitia mengi.
Umecheka mbele za watu, lakini ndani yako umeumia.
Umejaribu kuwa na nguvu, lakini moyo umechoka.
Umeomba, lakini bado unasubiri jibu.
Usilale ukiwa umebeba yote hayo.
Mkabidhi Mungu usiku wako.
Mkabidhi familia yako.
Mkabidhi kesho yako.
Kwa amani nitajilaza na kulala; kwa kuwa Wewe, BWANA, ndiwe unikalishaye salama.” — Zaburi 4:8
Sasa tulia...
Tufanye maombi. 🙏
🙏 MAOMBI
Baba katika jina la Yesu,
nakushukuru kwa kunifikisha mwisho wa siku hii.
Asante kwa ulinzi wako.
Asante kwa rehema zako.
Asante kwa mambo niliyoyaona na hata yale ambayo sikuyajua kuwa umenilinda nayo.
Bwana, nisamehe dhambi zangu.
Nisafishe moyo wangu.
Ondoa ndani yangu kila uchungu, hofu, hasira na mawazo yasiyokupendeza.
🌙 Usiku huu naweka maisha yangu mikononi mwako.
Linda nilipo.
Linda familia yangu.
Linda wapendwa wangu.
Kila mpango wa adui dhidi yangu,
naubatilisha kwa jina la Yesu.
Kila jambo lililokwama katika maisha yangu,
Bwana, lifungue kwa nguvu zako.
Kila mlango uliokuwa umefungwa,
funguka kwa jina la Yesu! 🔥
Kila moyo uliovunjika,
leta uponyaji.
Kila anayelia kwa siri,
mfariji.
Kila anayesubiri jibu,
mpe tumaini jipya.
Na pale ambapo nimeishiwa nguvu,
Bwana, nipe nguvu mpya.
🔥 TAMKO LA USIKU
Ninatamka usiku huu:
Sitakufa kabla ya kuona wema wa Mungu.
Sitatawaliwa na hofu.
Sitatawaliwa na kukata tamaa.
Sitatawaliwa na kushindwa.
Mungu ananitangulia.
Mungu ananilinda.
Mungu ananipigania.
Kesho yangu iko mikononi mwa Mungu!
Baba, nipe usingizi wa amani.
Niamshishe kesho nikiwa na nguvu mpya,
neema mpya,
fursa mpya,
na ushuhuda mpya. 🔥
Kwa jina la Yesu Kristo,
AMEN! 🙏🔥
❤️ K**a umeomba pamoja nami, andika AMEN kwa imani.
📲 Mshirikishe mtu mmoja unayetaka Mungu amlinde usiku huu.