22/05/2026
ENGLISH SWAHILI LESSON
WHY KEEP THE DAY OF PENTECOST? KWANINI TUADHIMISHE SIKU YA PENTEKOSTE?
INTRODUCTION
Those who question the keeping of the Day of Pentecost often ask with scorn, “Why do you keep it? Do you receive the Holy Spirit every year?” Yet Pentecost is not about repeating the outpouring but remembering and honouring the Almighty Heavenly Father’s appointed time, the fulfilment of His promise in the outpouring of the Holy Spirit, the connection to the giving of the law at Sinai, and the testimony of His grace and power in the lives of believers.
UTANGULIZI
Wale wanaopinga kuhusu kuadhimisha Siku ya Pentekoste mara nyingi huuliza kwa dharau, “Kwa nini mnaiadhimisha? Je, mnampokea Roho Mtakatifu kila mwaka?” Hata hivyo, Pentekoste si kuhusu kurudia kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, bali ni kukumbuka na kumheshimu mpango uliowekwa na Elohim, kutimizwa kwa ahadi Yake katika kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, uhusiano wake na utoaji wa Sheria katika Mlima Sinai, na ushuhuda wa neema na nguvu Zake katika maisha ya waumini.
1. To remember, honour, and testify of the mighty works, grace, and power of Elohim in the lives of believers (Psalm 111:4; Acts 1:8; Titus 3:5-6; Deuteronomy 16:9-12).
Kukumbuka, kuheshimu, na kutoa ushuhuda wa kazi kuu, neema, na nguvu za Elohim katika maisha ya waumini (Zaburi 111:4; Matendo ya Mitume 1:8; Tito 3:5-6; Kumbukumbu la Torati 16:9-12).
2. To commemorate the giving of the Ten Commandments at Mount Sinai (Exodus 19:1-20; Exodus 20:1-17).
Kukumbuka kutolewa kwa Amri Kumi katika Mlima Sinai (Kutoka 19:1-20; Kutoka 20:1-17).
3. To remember the outpouring of the Holy Spirit upon His people (Acts 2:1-4; Joel 2:28-29).
Kukumbuka kumwagwa kwa Roho Mtakatifu juu ya watu wake (Matendo ya Mitume 2:1-4; Yoeli 2:28-29).
4. To remember the fulfilment of the promise that the law of Elohim would be written in the hearts of His people (Jeremiah 31:33; Hebrews 8:10).
Kukumbuka kutimizwa kwa ahadi kwamba sheria ya Elohim itaandikwa katika mioyo ya watu wake (Yeremia 31:33; Waebrania 8:10).
5. To celebrate with gratitude for being part of the firstfruits of the Holy Spirit’s outpouring (James 1:18; Romans 8:23).
Kusherehekea kwa shukrani kwa kuwa sisi ni sehemu ya malimbuko ya Kwanza ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu (Yakobo 1:18; Warumi 8:23).
6. To show reverence and loyalty to the Creator (Ecclesiastes 12:13; John 14:15).
Kuonyesha heshima na uaminifu kwa Muumba (Mhubiri 12:13; Yohana 14:15).
DID APOSTLE PAUL KEEP THE DAY OF PENTECOST?
YES. The Apostle Paul continued to observe the Day of Pentecost in his ministry work, as seen in Acts 20:16 and 1 Corinthians 16:8. This shows that Pentecost remained meaningful and part of the observance of worship and service in the early Church.
JE, MTUME PAULO ALIKUWA AKIADHIMISHA SIKU YA PENTEKOSTE?
NDIYO. Mtume Paulo aliendelea kuadhimisha Siku ya Pentekoste katika huduma yake, k**a inavyoonekana katika Matendo ya Mitume 20:16 na 1 Wakorintho 16:8. Hii inaonyesha kwamba Pentekoste iliendelea kuwa na maana na ilikuwa sehemu ya ibada na utumishi katika Kanisa la mwanzo.
THE JERUSALEM CHURCH KEPT THE DAY OF PENTECOST
From Judah Magazine (June 1975, pages 5 and 7), Elder A.N. Dugger recorded that the Jerusalem Church observed Pentecost on Friday 16th May 1975 (Sivan 6). The account describes worship, singing, testimonies, and preaching. This serves as a modern historical example of Pentecost being observed on Sivan 6 rather than a fixed Sunday, reinforcing the Sivan 6 counting tradition (Isaiah 66:10).
KANISA LA YERUSALEMU LILIADHIMISHA SIKU SIKU YA PENTEKOSTE
Kutoka Judah Magazine (Juni 1975, ukurasa wa 5 na 7), Mzee A.N. Dugger anarekodi kwamba Kanisa la Yerusalemu liliadhimisha Siku ya Pentekoste Ijumaa, tarehe 16 Mei 1975 (Sivan 6). Walisherehekea siku hiyo kwa kuabudu, kwa kuimba, kwa kutoa ushuhuda, na kwa mahubiri. Hii inatoa mfano wa kihistoria wa kisasa unaoonyesha uadhimishaji wa Pentekoste katika Sivan 6 badala ya Pentekoste ya Jumapili, na hivyo kuimarisha kuhesabu majuma hadi Sivan 6, ambayo si lazima iwe Jumapili peke yake (Isaya 66:10).
CONCLUSION
In conclusion, the Day of Pentecost stands as a sacred memorial of Elohim's appointed time, a testimony of His fulfilled promises, and a reminder of the outpouring of the Holy Spirit upon His people. It is not a ritual of repetition, but a living witness of covenant history from Sinai to Zion, calling believers to reverence, gratitude, and faithful obedience. In remembering it, the saints reaffirm their identity as a people shaped by His Word, empowered by His Spirit, and set apart for His glory.
HITIMISHO
Kwa kuhitimisha, Siku ya Pentekoste inasimama k**a kumbukumbu takatifu ya wakati uliowekwa na Elohim, ushuhuda wa ahadi Zake zilizotimizwa, na ukumbusho wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu juu ya watu Wake. Si ibada ya kurudia tukio, bali ni ushuhuda hai wa historia ya agano kutoka Sinai hadi Sayuni, ukiwaalika waumini katika heshima, shukrani, na utii wa uaminifu. Kwa kuikumbuka, watakatifu wanathibitisha tena utambulisho wao k**a watu walioundwa na Neno Lake, waliojazwa nguvu na Roho Wake, na waliotengwa kwa ajili ya utukufu Wake.
This Post has been prepared by
Bro Mutonga (Pipeline Church, Nakuru, Kenya, East Africa, Africa)
[email protected]
+254722808047
Permission granted to freely share it widely in whatever form (Matthew 10:8)