St. Francis Xavier Catholic Church Naivasha

St. Francis Xavier Catholic Church Naivasha SUNDAY MASS SCHEDULE
6:45 AM Kiswahili
8:45 AM English
10:45 AM Kiswahili

Some people still say: “Christianity is a white man’s religion.”History must be crying.Long before Europe became fully C...
13/04/2026

Some people still say: “Christianity is a white man’s religion.”

History must be crying.

Long before Europe became fully Christian, the soil of Algeria and the wider North Africa was already producing some of the greatest minds in Christianity.

Think of Saint Augustine of Hippo, one of the most influential theologians in the history of the Church. He was not European. He was African. His thoughts on grace, sin, and salvation still shape Christianity today. Anyone talking about grace today, how we merit nothing without grace, should check well: Augustine already addressed it.

Think of Tertullian, the man who helped give us the language of the Trinity. He was the first to use the term Trinity to explain three Persons in one God. That same Trinity many defend today was clarified by an African mind.

Think of Cyprian of Carthage, who taught the unity of the Church and died for the faith on African soil. Your lessons on ecclesiology are not complete without studying Cyprian of Carthage.

These were not converts from colonial missions. They were foundations of the faith itself.

Today, Christianity in Algeria is small, just a tiny minority, with Catholics numbering under ten thousand, alongside some Protestant communities like the Protestant Church of Algeria. For context, the population of Algeria is around 45 to 48 million people. Catholics are only about 9,000, most of whom are foreign workers or sub Saharan African students. There are four Catholic dioceses in Algeria.

But here is the irony:

A land that once helped define Christianity for the world is now seen by some as a place where Christianity is “foreign.”

This is why history matters.

Christianity did not come to Africa as a stranger. In many places, it grew there, thought there, suffered there, and even died there, long before modern Europe found its full voice.

So the next time someone says, “Christianity is not African,” just remind them:

Africa did not only receive Christianity. Africa helped build it.

Welcome Pope Leo to Africa

Pope Leo XIV Appoints Archbishop Bert van Megen as Apostolic Nuncio to GermanyThe Holy Father, Pope Leo XIV, has appoint...
09/04/2026

Pope Leo XIV Appoints Archbishop Bert van Megen as Apostolic Nuncio to Germany

The Holy Father, Pope Leo XIV, has appointed Archbishop Bert Van Megen, who has served as Apostolic Nuncio to Kenya since 2019, as the new Apostolic Nuncio to Germany.

The appointment, officially announced in Rome on April 9, 2026, at 12 noon (1 p.m. Kenyan time), marks the close of a deeply impactful diplomatic and pastoral mission in Kenya and opens a new chapter of ecclesial service in Europe, with residence in Berlin.

Latest Vatican data shows the Catholic Church is growing fastest in Africa, with baptized members increasing from 281 mi...
04/04/2026

Latest Vatican data shows the Catholic Church is growing fastest in Africa, with baptized members increasing from 281 million in 2023 to 288 million in 2024, a 2.5 percent rise.

This growth is narrowing the gap with Europe, where the Catholic population slightly declined to 20.1 percent of the global Church.

Globally, the Catholic population now stands at 1.422 billion, up 1.14 percent from last year. In contrast, Asia and the Americas have seen slower growth, with Catholics in Asia comprising just 3.3 percent of the continent’s population.

The report also highlights pastoral trends: Africa has fewer clerics, meaning laypeople play a larger role in pastoral work, while Europe, Asia, and Oceania remain more cleric-focused.

Worldwide, there are now 465,048 clerics, including over 407,000 priests. This growth underscores the rising influence of the African Church in global Catholicism.

04/04/2026
03/04/2026

*IBADA YA IJUMAA KUU*

MASOMO, MATESO YA BWANA & MAOMBI.

*KATIKA MATESO YA BWANA*

SALA Tuombe haisemwi
Ee Bwana, kumbuka rehema zako, na, kwa ulinzi wako wa milele, uwatakatifuze watumishi wako, ambao Kristo Mwanao aliwawekea fumbo la Pasaka kwa kumwaga damu yake. Anayeishi na kutawala milele na milele.

AU:
Ee Mungu, kwa njia ya mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo, Mwanao, uliangamiza mauti, urithi wa dhambi ya kale, iliyokuwa ikitawala vizazi vyote vya binadamu. Utujalie ili, kwa kufananishwa naye, k**a tulivyoichukua sura ya mtu wa udongo kutokana na maumbile, kadhalika tuichukue sura ya mtu wa mbinguni, kwa kutakatifuzwa na neema. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

SEHEMU YA KWANZA: LITURUJIA YA NENO
SOMO 1: Isa.52:13-53:12
Tazama, mtumishi wangu atatenda kwa busara, atatukuzwa na kuinuliwa juu, naye atakuwa juu sana. K**a vile wengi walivyokustaajabia, (uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu), ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyas**ia watayafahamu. Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? Maana alikuwa mbele zake k**a mche mwororo. Na k**a mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye s**itiko; Na k**a mtu ambaye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua mas**itiko yetu. Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa. Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote k**a kondoo tumepotea, Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; K**a mwanakondoo apelekwaye machinjoni, Na k**a vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayesimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu. Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya, Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake. Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi; Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake; Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki, Naye atayachukua maovu yao. Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa. Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.

WIMBO WA KATIKATI: Zab.31:1,5,11-13a,14-16,24.(K)Lk.23:46
1. Nimekukimbilia Wewe, Bwana
Nisiaibike milele.
Kwa haki yako uniponye,
Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, ee Bwana, Mungu wa kweli.

(K) Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.

2. Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu,
Naam, hasa kwa jirani zangu;
Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu;
Walioniona njiani walinikimbia. (K)

3. Nimesahauliwa k**a mfu asiyekumbukwa;
Nimekuwa k**a chombo kilichovunjika.
Maana nimes**ia masingizio ya wengi;
Hofu ziko pande zote. (K)

4. Lakini mimi nakutumaini Wewe, Bwana,
Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
Nyakati zangu zimo mikononi mwako;
Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia. (K)

5. Umwangaze mtumishi wako
Kwa nuru ya uso wako;
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
Iweni hodari, mpige moyo konde,
Ninyi nyote mnaomngoja Bwana. (K)

SOMO 2: Ebr4:14-16;5:7-9
Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea Yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akas**ilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii.

SHANGILIO: Flp.2:8-9
Kristo alijinyenyekeza.
Akawa mtii hata mauti,
Naam, mauti ya msalaba.
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno,
Akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina.

INJILI: Yn:18:1-19,42
M. = Msomaji
W. = maneno ya Watu mbalimbali
十 = maneno ya Yesu

M. Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo yalivyoandikwa na Mtakatifu Yohane.

Yesu anak**atwa.
M. Wakati ule Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito Kedroni; palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake. Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake. Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu na makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha. Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia,
十 Ni nani mnayemtafuta?
M. Wao wakamjibu,
W. Ni Yesu Mnazareti.
M. Yesu akawaambia,
十 Ni mimi.
M. Yuda naye, aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja nao. Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. Basi akawauliza tena,
十 Mnamtafuta nani?
M. Wakasema,
W. Yesu Mnazareti.
M. Yesu akajibu,
十 Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi, basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.
M. Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao. Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata s**io la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko. Basi Yesu akamwambia Petro,
十 Rudisha upanga alani mwake; je, kikombe alichonipa Baba, mimi nis**inywee?

Yesu mbele ya Anasi na Kayafa. Petro anamkana Yesu.
M. Basi wale askari na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi walimk**ata Yesu, wakamfunga. Wakamchukua kwa Anasi kwanza; maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule. Naye Kayafa ndiye yule aliyewapa Wayahudi lile shauri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu. Wakamfuata Yesu Petro na mwanafunzi mwingine. Na mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya kuhani Mkuu. Lakini Petro akasimama nje mlangoni. Basi yule mwanafunzi mwingine aliyejulikana na Kuhani Mkuu akatoka, akasema na mngoja mlango, akamleta Petro ndani. Basi yule kijakazi, aliyekuwa mngoja mlango, akamwambia Petro,
W. Wewe nawe, je, hu mwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu?
M. Naye akasema,
W. Si mimi.
M. Na wale watumwa na watumishi walikuwa wakisimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi; wakawa wakikota moto, Petro naye alikuwapo pamoja nao, anakota moto. Basi Kuhani Mkuu akamwuliza Yesu habari za wanafunzi wake, na habari za mafundisho yake. Yesu akamjibu,
十 Mimi nimesema na ulimwengu waziwazi; siku zote nalifundisha katika sinagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi wote; wala kwa siri mimi sikusema neno lolote. Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale walios**ia ni nini niliyowaambia; wao wanajua niliyoyanena.
M. Basi aliposema hayo, mtumishi mmojawapo aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema,
W. Wamjibu hivi Kuhani Mkuu?
M. Yesu akamjibu,
十 K**a nimesema vibaya, ushuhudie ule ubaya; bali k**a nimesema vema, wanipigia nini?
M. Basi Anasi akampeleka hali amefungwa kwa Kayafa, Kuhani Mkuu. Na Simoni Petro alikuwa akisimama huko, anakota moto. Basi wakamwambia,
W. Wewe nawe, je, hu mwanafunzi wake mmojawapo?
M. Naye akakana, akasema,
W. Si mimi.
M. Mtumwa mmojawapo wa Kuhani Mkuu, naye ni jamaa yake yule aliyekatwa s**io na Petro, akasema,
W. Je, mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?
M. Basi Petro akakana tena, na mara akawika jimbi.

Yesu mbele ya Pilato.
M. Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka. Basi Pilato akawatokea nje, akasema,
W. Ni mash*taka gani mnayoleta juu ya mtu huyu?
M. Wakajibu wakamwambia,
W. K**a huyu asingekuwa mtenda mabaya, tusingemleta kwako.
M. Basi Pilato akawaambia,
W. Haya! Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa ile torati yenu!
M. Wayahudi wakamwambia,
W. Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu.
M. Ili litimie lile neno lake Yesu alilolisema, akionesha ni mauti gani atakayokufa. Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia,
W. Je, wewe ni Mfalme wa Wayahudi?
M. Yesu akamjibu,
十 Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?
M. Pilato akajibu,
W. Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?
M. Yesu akajibu,
十 Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. K**a ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.
M. Basi Pilato akamwambia,
W. Wewe u mfalme basi?
M. Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunis**ia sauti yangu.
M. Pilato akamwambia,
W. Kweli ni nini?
M. Naye akiisha kusema neno hilo akawatokea Wayahudi tena, akawaambia,
W. Mimi sioni hatia yoyote kwake. Lakini kwenu kuna desturi ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka; basi, mwapenda niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?
M. Basi wakapiga kelele tena, na kusema,
W. Si huyu, bali Baraba.
M. Naye yule Baraba alikuwa mnyang'anyi. Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu. Akampiga mijeledi. Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. Wakawa wakimwendea, wakisema,
W. Salamu! Mfalme wa Wayahudi!
M. Wakampiga makofi. Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia,
W. Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yoyote kwake.
M. Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia,
W. Tazama, mtu huyu!
M. Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema,
W. Msulibishe! Msulibishe!
M. Pilato akawaambia,
W. Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake.
M. Wayahudi wakamjibu,
W. Sisi tunayo! sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.
M. Basi Pilato alipos**ia neno hilo akazidi kuogopa. Akingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu,
W. Wewe umetoka wapi?
W. Lakini Yesu hakumpa jibu lolote. Basi Pilato akamwambia,
W. Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha?
W. Yesu akamjibu,
十 Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu, k**a usingepewa kutoka juu, kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.

Yesu anahukumiwa kufa.
M. Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua: lakini Wayahudi wakapiga makelele wakasema,
W. Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanye kuwa mfalme humfitini Kaisari.
M. Basi Pilato, alipos**ia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha. Nayo ilikuwa Maandalio ya Pasaka yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi,
W. Tazama, Mfalme wenu!
M. Basi wale wakapiga kelele,
W. Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe!
M. Pilato akawaambia,
W. Je, nimsulibishe Mfalme wenu?
M. Wakuu wa Makuhani wakamjibu,
W. Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.
M. Basi ndipo walipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.

Yesu anasulibiwa.
M. Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha. Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati. Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. Basi wakuu wa Makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato,
W. Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi.
M. Pilato akajibu,
W. Niliyoandika nimeyaandika.

Askari wanagawanya mavazi ya Yesu.
M. Nao askari walipomsulibisha Yesu waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. Basi wakaambiana,
W. Tusiipasue, lakini tuipigie kura iwe ya nani.
M. Ili litimie andiko lile linenalo: Waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.

Yesu na mamae.
M. Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye Mariamu wa Klopa na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake,
十 Mama, tazama mwanao.
M. Kisha akamwambia yule mwanafunzi,
十 Tazama, mama yako.
M. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.

Yesu anakufa.
M. Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema,
十 Naona kiu.
M. Kulikuwako huko chombo kimejaa s**i; basi wakatia sifongo iliyojaa s**i juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile s**i, alisema,
十 Imekwisha.
M. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.

Yesu anatobolewa ubavu.
M. Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli, ili ninyi nanyi mpate kusadiki. Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie: Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko lingine lanena: Watamtazama yeye waliyemchoma.

Yesu anazikwa.
M. Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake. Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na udi, yapata ratli mia. Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, k**a ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. Na pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu yeyote ndani yake. Humo basi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu.

MAOMBI KWA AJILI YA WATU WOTE
I. Kwa ajili ya Kanisa takatifu
Enyi ndugu wapendwa sana, tuliombee Kanisa takatifu la Mungu, ili Mungu na Bwana wetu apende kulijalia amani, kulikusanya na kulilinda popote duniani. Pia atujalie sisi tumtukuze Mungu Baba Mwenyezi, katika maisha ya amani na usalama.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, uliyewafumbulia mataifa yote utukufu wako katika Kristo, uilinde kazi ya huruma yako, ili Kanisa lako, lililoenea popote duniani, liendelee kwa imani thabiti kuliungama jina lako. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

II. Kwa ajili ya Papa
Tumwombee pia Baba mtakatifu wetu J., ili Mungu na Bwana wetu, aliyemteua katika daraja ya uaskofu, amlinde, akae mzima na salama kwa ajili ya Kanisa lake takatifu, apate kuliongoza taifa takatifu la Mungu.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, ambaye vitu vyote huumbwa kwa uamuzi wako, uyas**ilize kwa wema maombi yetu. Umlinde kwa huruma yako huyo Mchungaji mkuu uliyemteua kwa ajili yetu, ili jamii ya wakristo, ambao wewe mwenyewe unawatawala, chini ya huyo Mchungaji mkuu, waongezewe mastahili ya imani yao. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

III. Kwa ajili ya kila daraja na cheo cha waamini
Tumwombee pia askofu wetu J., maaskofu wote, mapadri, mashemasi wa Kanisa, na jamii yote ya waamini.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, ambaye Roho wako hutakatifuza na kusimamia mwili wote wa Kanisa, utus**ilize sisi tunaowaombea watumishi wako, ili wote, kwa msaada wa neema yako, wakutumikie kiaminifu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

IV. Kwa ajili ya wakatekumeni
Tuwaombee pia wakatekumeni (wetu), ili Mungu na Bwana wetu azibue mas**io ya mioyo yao na afungue mlango wa rehema yake, kusudi, wakiisha kupata maondoleo ya dhambi zao zote kwa njia ya maji ya Ubatizo wa kuzaliwa upya, nao pia wawemo ndani ya Yesu Kristo Bwana wetu.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, unayelisitawisha daima Kanisa lako kwa kulipatia wana wapya Uwaongezee imani na akili wakatekumeni (wetu), ili wakiisha kuzaliwa mara ya pili katika kisima cha Ubatizo, wahesabiwe kati ya jamii ya hao uliowafanya watoto wako. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

V. Kwa ajili ya umoja wa Wakristo
Tuwaombee pia ndugu wote wanaomwamini Kristo, ili Mungu na Bwana wetu apende kuwakusanya katika Kanisa lake lililo moja na kuwalinda hao, watendao ukweli.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, unayeyakusanya yaliyotawanyika na kuyalinda yaliyokusanywa, ulitazame kwa wema kundi lake Mwanao, ili, wale waliotakaswa kwa Ubatizo mmoja, waunganishwe kwa umoja wa imani na kifungo cha mapendo. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

VI. Kwa ajili ya Wayahudi
Tuwaombee pia Wayahudi, ambao Mungu Bwana wetu alinena nao kwanza, ili awajalie wazidi kulipenda jina lake na kuwa waaminifu katika kuishi agano lake.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, uliyempa Ibrahimu na uzao wake ahadi zako, us**ilize kwa wema maombi ya Kanisa lako, ili taifa hilo ulilojipatia kwanza lijaliwe kuufikia utimilifu wa ukombozi. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

VII. Kwa ajili ya wasiomwamini Kristo
Tuwaombee pia wale wasiomwamini Kristo, ili, wakiangazwa kwa nuru ya Roho Mtakatifu, wapate nao kuingia katika njia ya wokovu.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, uwajalie wale wasiomwungama Kristo, na wanaenenda mbele ya uso wako kwa moyo mnyofu, waupate ukweli. Nasi, kwa kuzidi daima katika kupendana na kwa kufanya bidii kulifahamu kikamilifu fumbo la uzima wako, utufanye tuwe mashahidi kamili wa mapendo yako ulimwenguni. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

VIII. Kwa ajili ya wasiomwamini Mungu
Tuwaombee pia wale wasiomwamini Mungu, ili, kwa kuyafuata kwa moyo mnyofu yaliyo mema, wastahili kumfikia Mungu mwenyewe.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, umewaumba wanadamu wote, ili wakutafute daima kwa hamu na wakikupata watulie. Tunakuomba utujalie ili, watu wote, licha ya vizuizi vyovyote vya uovu, kwa kuzipokea ishara za wema wako na ushuhuda wa matendo mema ya wale wanaokuamini, wapate kufurahi katika kukuungama wewe uliye peke yako Mungu wa kweli na Baba yetu sisi binadamu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

IX. Kwa ajili ya viongozi wa Serikali
Tuwaombee pia viongozi wote wa serikali, ili Mungu na Bwana wetu aelekeze akili na mioyo yao kadiri ya mapenzi yake, kusudi watu wote wapate amani na uhuru wa kweli.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, mioyo ya watu na haki za mataifa zimo mikononi mwako. Uwaangalie kwa wema wale wenye madaraka ya kutuongoza sisi, kusudi, kwa majaliwa yako, wadumishe popote duniani usitawi wa mataifa, usalama wa amani na uhuru wa dini. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

X. Kwa ajili ya wenye taabu
Enyi ndugu wapendwa sana, tumwombe Mungu Baba mwenyezi, ili atakase ulimwengu na upotovu wowote, aondoe magonjwa, afukuze njaa, ayafungue magereza, azifungue pingu. Wanaosafiri wajaliwe usalama, walio mbali warudi makwao, wagonjwa wapone na wanaokufa waokoke.

Sala katika ukimya. Halafu kuhani anasema:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, ndiwe faraja ya wenye kus**itika, na nguvu ya wanaoteswa. Yafike kwako maombi ya wanaokulilia katika taabu yoyote, ili, kwa rehema yako, wote, kila mmoja katika shida yake, wafurahie kus**ilizwa. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

SALA BAADA YA KOMUNYO:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, umetuhuisha kwa njia ya kifo kitakatifu na ufufuko wa Kristo wako. Tunakuomba, udumishe ndani yetu kazi ya rehema yako, ili, kwa kushiriki fumbo hili takatifu, tupate kuishi katika uchaji siku zote. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

SALA JUU YA WATU:
Ee Bwana, tunakuomba, baraka zako nyingi ziwashukie watu wako, ambao wamekumbuka kifo cha Mwanao kwa kutazamia kufufuka kwao; wapate rehema, wajaliwe kitulizo, waongezewe imani takatifu, na wathibitishiwe ukombozi wa milele. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

_*WAUMINI WOTE KUONDOKA KANISA KIMYA KIMYA KATIKA TAFAKARI KUU*🙏_

03/04/2026

*MASOMO YA MISA YA IJUMAA KUU*

*IJUMAA KATIKA MATESO YA BWANA*

*APRILI 18 2025*

*RANGI YA LITURUJIA: NYEKUNDU* 🟥

*UTANGULIZI*
_Sherehe ya mateso ya Bwana hufanyika karibu saa tisa, isipokuwa sababu za kichungaji zinapendekeza saa nyingine. Sherehe hii ina sehemu tatu, yaani Liturujia ya Neno, Kuabudu Msalaba, na Ekaristi Takatifu. Ijumaa Kuu ya mateso ya Bwana ni siku ya toba kwa Kanisa zima, ambayo inapaswa kuashiria kwa kufunga na kujizuia na nyama. Hakuna misa inayoadhimishwa siku hiyo._

*Tuombe,*
_Kumbuka rehema zako, Ee Bwana, na kwa ulinzi wako wa milele watakase watumishi wako, ambao Kristo Mwanao, kwa kumwaga Damu yake, aliweka siri ya pasaka. Yeye anaishi na kutawala milele na milele._
K/. Amina.

*SOMO LA KWANZA*
Isaya 52:13---53:12

_Aliumizwa kwa sababu ya makosa yetu(Wimbo wa nne wa mtumishi wa Bwana)_

*Somo katika kitabu cha Nabii Isaya*

Tazama, mtumishi wangu atafanikiwa, atatukuzwa, atainuliwa na kusifiwa sana. K**a vile watu wengi walivyoogopa walipomwona, kwa sababu uso wake ulikuwa umeharibiwa, kupita ule wa mwanadamu, ndivyo hivyo mataifa mengi watashtuka; mbele yake wafalme watasimama kimya; kwa kuwa wataona jambo wasiloambiwa , na kutafakari kitu kisichos**ika bado.
Ni nani aliyesadiki habari tuliyois**ia? Na mkono wa Bwana alifunuliwa kwa nani? K**a mche, alikuwa mbele yetu k**a, K**a mzizi katika nchi kavu; Hakuwa na umbo la kuvutia jicho, wala uzuri wa kutuvutia kwake. Alichukiwa na kuepukwa na watu, Mtu wa mateso, ajuaye huzuni, sawa na wale ambao mbele yao twafunika nyuso zetu, alidharauliwa na kufedheheshwa.
Hakika aliyachukua mateso yetu, na alijitwika huzuni zetu. Sisi lakini, tulidhani ameadhibiwa na Mungu, na kupigwa naye, na kuteswa. Ila aliumizwa kwa sababu ya makosa yetu, alipondwa kwa ajili ya maovu yetu. Alibeba adhabu iletayo uzima juu yetu. Alionewa vikali sana, akanyenyekea wala hakufunua kinywa chake; K**a mwanakondoo anayepelekwa machinjoni, na k**a vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake, vivyo hivyo, hakufunua kinywa chake. Alishikwa kwa nguvu na kuhukumiwa; ni nani atasimulia maisha yake? Kweli, walimwondoa kutoka kwa nchi ya walio hai, aliuawa kwa ajili ya makosa ya watu wake.
Walimpa kaburi pamoja na waovu, na pamoja na matajiri katika kifo chake, ingawa hakutenda ukatili wowote, wala haukupatikana udanganyifu wowote kinywani mwake.
Bwana ametaka kumwumiza mtumishi wake, kwa mateso amemhuzunisha; amefanya maisha yake sadaka ya malipo ya dhambi, naye ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, nayo mapenzi ya Bwana yatatimia kwa mikono yake. Kwa ajili ya mateso aliyoyavumilia; yeye ataona mwangaza, atajaliwa mema;
Kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwema atatakasa wengi Yeye atajitwika maovu yao. Ndiyo maana, nitamgawia sehemu kati ya wakuu wa watu, atagawanya nyara pamoja nao walio hodari, sababu alijitoa mwenyewe hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao wakosao, akajitwika dhambi za wengi na kuwaombea wakosaji.

*Neno la Bwana*

*ZABURI YA KUITIKIZANA*
Zaburi 31: 2 na 6, 12-13,15-16, 17 na 25 (K. . Lk 23:46b)

*(K) Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.*

Nakukimbilia wewe, ee Bwana;
Nisiaibike milele.
Uniopoe kwa haki yako.
Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Uniokoe, ee Bwana, Mungu wa kweli.
*(K)*

Kwa adui zangu wote nimekuwa dharau,
Kwa majirani zangu kitu cha kuogofya,
Kitisho kwa rafiki zangu.
Wale wanionao njiani, wananikimbia.
Nimesahauliwa k**a mtu aliyekufa;
Nimekuwa k**a chombo kilichovunjika
*(K)*

Mimi lakini nakutumaini, ee Bwana;
Nasema, "Wewe ndiwe Mungu wangu."
Maisha yangu yamo mikononi mwako;
Uniponye na mikono ya adui zangu / na wadhulumu wangu.
*(K)*

Umwangazie mtumishi wako uso wako;
Uniokoe kwa wema wako.
Muwe hodari, mpige moyo konde,
Enyi wote mnaomtumainia Bwana.
*(K)*

*SOMO LA PILI*
Waebrania 4:14-16; 5:7-9

_Alijifunza utii na akawa chimbuko la wokovu wa milele kwa wote wanaomtii._

Ndugu zangu: Kwa kuwa tuna kuhani mkuu aliyekwisha penya mbingu, ndiye Yesu, Mwana wa Mungu, tuyashikilie maungamo yetu. Maana hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuonea huruma udhaifu wetu, kwani yeye alijaribiwa k**a sisi katika mambo yote, ila hakutenda dhambi. Basi, tukikaribie kiti cha neema kwa matumaini, ili tujaliwe huruma na neema na msaada wakati wa shida.[Yesu]
Alipoishi duniani alimtolea sala na maombi kwa kilio na machozi yeye aliyeweza kumwokoa katika mauti, akas**ilizwa kwa sababu ya uchaji wake. Ingawa ni Mwana alijifunza utii kwa njia ya mateso. Alipokamilika, alikuwa chimbuko la wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.

*Neno la Bwana*

*SHANGILIO LA INJILI*
Wafilipi 2:8-9

*Sifa na utukufu kwako, ee Kristo*
Kristu Yesu alijinyenyekeza mwenyewe, akawa mtii mpaka mauti, yaani mauti ya msalabani. Kwa sababu hiyo Mungu alimtukuza, akampa Jina lipitalo kila jina.
*Sifa na utukufu kwako, ee Kristo*

*INJILI*
Yohane. 18:1 – 19:42

*MATESO YA BWANA WETU YESU KRISTO YALIVYOANDIKWA NA YOHANE*

*M*= Msomaji
*✝️* =maneno ya Yesu
*W* = maneno ya watu mbalimbali

*M*: Wakati ule: Yesu aliondoka pamoja na wafuasi wake, kwenda ng’ambo ya kijito Kidroni, pale palikuwa na bustani, akaingia yeye na wafuasi wake. Kadhalika Yuda, yule aliyemsaliti, alijua mahali pale, kwa maana mara nyingi Yesu alikusanyika huko pamoja na wafuasi wake. Basi, Yuda alipokea kikosi cha askari na walinzi waliotumwa na makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko, walishika mienge, na taa, na silaha mikononi. Yesu akijua yote yatakayompata, akatoka, akawaambia,

*✝️*: "Mnamtafuta nani?"

*M* : Wao wakamjibu,

*W* : "Yesu Mnazareti."

*M* : Yesu akawaambia,

*✝️* : "MIMI NDIYE."

*M* : Yuda, aliyemsaliti, alisimama pamoja nao. Alipowaambia, ‘MIMI NDIYE,’ walirudi nyuma, wakaanguka chini. Akawauliza tena,

*✝️*: "Mnamtafuta nani?"

*M*: Wakasema,

*W*: "Yesu Mnazareti."

*M*: Yesu akajibu,

✝️: "Nimekwisha kuwaambia ya kwamba MIMI NDIYE. Basi, ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao."

*M*: Hayo alisema, Ili neno lake litimie, yaani: '‘Sikumpoteza hata mmoja wa hao ulionipa.’' Basi Simoni Petro, alikuwa na upanga, akauchomoa, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata s**io la kulia. s**io lake la kulia. Na yule mtumishi jina lake ni Malko. Yesu akamwambia Petro,

✝️: "Rudisha upanga alani mwake. Je, nisinywe kikombe alichonipa Baba?"

*M*: Hapo kikosi cha askari na jemadari wake na walinzi wa Wayahudi walimk**ata Yesu, wakamfunga na wakampeleka kwanza kwa Anasi. Maana huyo alikuwa mkwewe the Kayafa, naye alikuwa kuhani mkuu wa mwaka ule. Kayafa huyo ndiye aliyewapa Wayahudi shauri kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya taifa. Petro na mfuasi mwingine wakamfuata Yesu. Huyo mfuasi mwingine alijulikana na kuhani mkuu, akaingia pamoja na Yesu katik ukumbi wa kuhani mkuu. Lakini Petro alisimama nje karibu na mlango. Basi yule mfuasi mwingine, aliyejulikana na Kuhani Mkuu, akatoka akasema na mgoja mlango, akamleta Petro ndani. Kijakazi yule aliyekuwa mgoja mlango, akamwambia Petro,

*W*: "Je, Wewe si mmojawapo wa wafuasi wa mtu huyu?"

*M*: Naye akasema,

*W*: "Si mimi".

*M*: Watumishi na walinzi walisimama huko na walikuwa wamewasha moto wa makaa, maana kulikuwa baridi, nao wakaota moto.Na Petro pia alisimama nao akiota moto. Kuhani Mkuu akamhoji Yesu juu ya wafuasi wake na mafundisho yake. Yesu akamjibu,

✝️: "Mimi Nilisema waziwazi mbele ya wote. Siku zote nilifundisha katika sinagogi na hekaluni wanapokutana Wayahudi wote, Kwa siri sikusema neno. Ya nini kuniuliza mimi? Waulize wale walios**ia niliyowafundisha. Bila shaka wanajua niliyosema."

*M*: Aliosema hayo, mmoja wa mlinzi aliyesimama karibu alimpiga Yesu kofi akisema,

*W*: "Wamjibu hivyo kuhani mkuu?"

*M*: Yesu akamjibu,

✝️: K**a nimesema vibaya, ushuhudie huo ubaya; bali k**a nimesema vema, bona unanipiga?"

*M*: Hapo Anasi alimpeleka hali amefungwa kwa Kayafa, kuhani mkuu. Simoni Petro alisimama huko akiota moto. Basi wakamwuliza,

*W*: Je, Wewe si mmoja wa wafuasi wake?"

*M*: Naye akakana, akasema,

*W*: "Si mimi."

*M*: Mtumishi mmoja wa kuhani mkuu, ndiye jamaa wa yule aliyekatwa s**io na Petro, akasema,

*W*: "Je, mimi sikukuona pamoja naye bustanini pamoja naye?"

*M*: Petro akakana tena. Mara hapo jogoo akawika.
Kutoka kwa Kayafa walimpeleka Yesu Praitorio. Kulikuwa asubuhi mapema. Wenyewe hawakuingia Praitorio, wasije wakajinajisi, maana walitaka kuila Pasaka. Basi, Pilato akawaendea nje, akasema,

*W*: "Mnaleta mashtaka gani juu ya mtu huyu?"

*M*: Wakajibu, wakamwambia,

*W*: K**a huyu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako."

*M*: Pilato akawaambia,

*W*: Haya! Mchukueni ninyi, mkamhukumu kwa sheria yenu."

*M*: Wayahudi wakamjibu,

*W*: Sisi hatuna ruhusa ya kumwua mtu,"

*M*: Hivyo maneno aliyoyasema Yesu kuonyesha namna ya kifo chake yalipata kutimia. Basi, Pilato akaingia tena katika Praitorio, akamwita Yesu, akamwuliza,

*W*: "Je, wewe u Mfalme wa Wayahudi?"

*M*: Yesu akajibu,

✝️: "Unasema hii kwa nafsi yako, au ni watu wengine waliokupa habari yangu,"

*M*: Pilato akajibu,

*W*: "Ni Myahudi mimi? Ni taifa lako na makuhani wakuu waliokuleta kwangu. Umefanya nini?"

*M*: Yesu akajibu,

✝️: "Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. K**a ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatolewa kwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu si wa hapa.

*M*: Basi Pilato akamwambia,

*W*: "Wewe u mfalme basi?"

*M*: Yesu akajibu,

✝️: Wewe unasema ya kuwa, mimi ni mfalme. Nia ya kuzaliwa mimi na nia yab kuja ulimwenguni mimi ndiyo nishuhudie ukweli. Kila aliye wa ukweli hus**ia sauti yangu."

*M*: Pilato akamwuliza,

*W*: "Ukweli ni nini?"

*M*: Baada ya maneno hayo, alikwenda nje tena kwa Wayahudi, akawaambia,

*W*: Mimi sioni kosa kwake. Lakini kuna desturi kwenu niwafungulie mfungwa mmoja kwa sikukuu ya Pasaka. Je, mwataka niwafungulie Mfalme wa Wayahudi?"

*M*: Wakapiga kelele na kusema,

*W* "Si huyu, bali Baraba!"

*M*: Na Baraba alikuwa mnyang'anyi. Hapo Pilato alimtwaa Yesu, akampiga mijeledi. Nao askari wakasuka taji la miiba, wakamtia kichwani, wakamvisha joho la zambarau, wakamjongea, wakisema,

*W* : "Salaam, Mfalme wa Wayahudi!"

*M*: wakampiga makofi. Kisha Pilato akaenda tena nje, akawaambia,

*W*: "Tazameni, ninamleta nje mpate kutambua ya kuwa sioni kosa kwake."

*M*: Hapo Yesu alitoka nje, amevaa taji la miiba kichwani na lile joho la zambarau. Pilato akawaambia,

*W*: "Mtazameni mtu!"

*M*: Makuhani wakuu na watumishi walipomwona walipiga kelele,

*W*: "Msulibishe! Msulibishe!"

*M*: Pilato akawaambia,

*W*: Mchukueni ninyi wenyewe, mkamsulibishe. Kwa maana mimi Sioni kosa kwake."

*M*: Wayahudi wakamjibu,

*W*: Sisi tuna sheria, na kwa kadiri ya sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu amejidai kuwa Mwana wa Mungu.

*M*: Pilato alipos**ia hayo, akazidi kuogopa, akaingia tena Praitorio, akamwambia Yesu,

*W*: "Umetoka wapi?"

*W*: Yesu hakumjibu. Pilato akamwuliza,

*M*: "Husemi nami? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukufungua, na nina mamlaka ya kukusulubisha?"

*M*: Yesu akamjibu,

✝️: Usingekuwa na mamlaka yoyote juu yangu mimi, k**a usingepewa kutoka juu. kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana kosa kubwa zaidi.

*M*: Toka hapa, Pilato akajaribu kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema,

*W*: Ukimfungua huyu, wewe si rafiki wa Kaisari. Kila mtu ajifanyaye mfalme, anamuasi Kaisari."

*M*: Pilato alipos**ia maneno hayo, akamleta Yesu nje na akaketi katika kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabbatha. Ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, mnamo saa sita. Akawaambia Wayahudi,

*W*: "Tazameni Mfalme wenu!"

*M*: Nao Wakapaza sauti,

*W*: "Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe!"

*M*: Pilato akawaambia,

*W*: "Je, nimsulubishe Mfalme wenu?"

*M*: Makuhani wakuu wakajibu,

*W*: Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.

*M*: Hapo Pilato alimtoa kwao ili asulibiwe. Nao wakamchukua Yesu, naye mwenyewe alichukua msalaba njiani toka mjini mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania Golgotha. Huko wakamsulibisha, na pamoja naye wengine wawili, mmoja kushoto na mmoja kulia, na Yesu katikati.
Pilato akaandika hati, akaiweka juu ya msalaba. Ilikuwa imeandikwa, "Yesu Mnazareti, Mfalme wa Wayahudi." Wayahudi wengi walisoma hatu hiyo, maana aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; Lugha ya hati ilikuwa Kiebrania, Kilatini, na Kigiriki. Makuhani wakuu wa Wayahudi wakamwambia Pilato,

*W*: "Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali ya kwamba alisema, 'Mimi ni 'Mfalme wa Wayahudi.'"

*M*: Pilato akajibu,

*W*: "Niliyoandika nimeyaandika."

*M*: Baada ya kumsulibisha Yesu, askari waliyachukua mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu moja. Pia walichukua kanzu; nayo kanzu ilikuwa nzima bila mshono, yaani mfumo mmoja toka juu mpaka chini.
Basi wakaambiana,

*W*: Tusiipasue, afadhali tuipigie kura na hivyo kuamua itakuwa ya nani,"

*M*: Kwa namna hii yalitimia Maandiko yasemayo: "Waligawanya nguo zangu, wakalipigia kura vazi langu." Hayo ndiyo waliyofanya askari.
Karibu na msalaba wa Yesu walisimama mama yake, na ndugu wa mama yake, Maria mke wa Klopa, na Maria Magdalena. Basi, Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye yule mwanafunzi aliyempenda, alimwambia mama yake,

✝️: "Mama, tazama mwanao."

*M*: Kisha akamwambia mfuasi,

✝️: "Tazama mama yako."

*M*: Toka saa ile yule mfuasi huyo alimpokea nyumbani kwake. Baada ya hayo, Yesu akijua ya kuwa yote yaliyotakiwa kwa kutekeleza Maandiko yametimia, akasema,

✝️: "Naona kiu."

*M*: Huko kulikuwako chombo kilichojaa s**i. Basi, wakalowesha sifongo katika s**i, wakaipachika kwenye mwanzi, wakakigusa kinywa chake. Baada ya kuipokea s**i, Yesu alisema,

✝️: "Yametimia."

*M*: Akainama kichwa, akatoa roho.

_(Wote wanakaa kimya kwa muda, ama kwa kupiga magoti)_

Siku ile ilikuwa siku ya kuandaa Pasaka.Kwa hiyo Wayahudi walimwomba Pilato, waliosulibiwa hiyo wavunjwe miguu na kuondolewa, ili miili yao isikae msalabani siku ya Sabato, kwa maana Sabato ile ilikuwa sikukuu kubwa. Basi askari wakaja, wakamvunja miguu yule wa kwanza na wa pili waliosulibiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu na kumwona amekwisha kufa, hawakumvunja miguu, ila askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki, mara ikatoka damu na maji. Aliyeyaona hayo, ameyashuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli, ili ninyi pia mpate kusadiki. Maana hayo yametendeka, ili aandiko litimie lisemalo, "hatavunjwa mfupa hata mmoja." Tena andiko lingine lasema, "Watamtazama yule waliyemchoma."
Baada ya hayo, Yosefu wa Arimathea, ndiye mfuasi wa Yesu, lakini mfuasi wa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato ruhusa auondoe mwili wa Yesu. Pilato akampa ruhusa. Basi ,akaenda, akauondoa mwili wake. Akaja Nikodemo, yule aliyemwendea Yesu mara ya kwanza usiku, akaleta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata ratili mia. Kisha wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na manukato, k**a ilivyo desturi kwa Wayahudi kuzika. Pale aliposulibiwa palikuwa na bustani, na katika bustani kulikuwa na kaburi jipya, ambamo hajazikwa bado mtu. Basi, humo ndani wakamweka Yesu kwa sababu ya Maandalio ya Pasaka ya Wayahudi, na kaburi lilikuwa karibu.

*Injili ya Bwana*

Address

PO BOX 9
Naivasha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when St. Francis Xavier Catholic Church Naivasha posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share