04/06/2026
Wakati mwingine tunaweza kuhisi tumesahaulika kutokana na changamoto na majaribu ya maisha, lakini Biblia inatukumbusha kuwa yupo Mungu anayewakumbuka watu wake. K**a alivyomkumbuka Hana na kubadilisha kilio chake kuwa ushuhuda, ndivyo anavyotukumbuka nasi leo. Endelea kuomba, kuamini na kusubiri kwa uvumilivu, maana wakati wa Mungu ukifika, kile kilichoonekana kuwa hakiwezekani kitakuwa ushuhuda wa neema yake.