07/02/2026
49. *ISRAEL NA NYAKATI ZA MATAIFA* 7 _/2/ 2026 /20th of Sh’vat._
Somo Kuu: *Luka 21:24-38.*
Fungu la Kukari: *Luka 21:36.*
1. Yahshua alisema nini kuhusu dhiki ya Wayahudi na kipindi cha kutawanywa kwao? Luka 21:24.
2. Kadiri nyakati za Mataifa zinavyokaribia mwisho, ni hali gani zitakazoenea duniani? Mstari wa 25, 26.
Maelezo: - Nyakati za Mataifa hazikuanza kwa siku moja, au hata mwaka
fulani, lakini kwa kipindi cha muda mrefu. Waisraeli walipopoteza hamu
kwa Yahweh na polepole wakawa hawana imani, watu wa Mataifa walipata
hamu kwa Yahweh polepole. Leo hii inafanyika kinyume chake: Watu wa
Mataifa wanamwacha Yahweh haraka, na Israeli nao wanamtamani
Yahweh tena .
3. Je, Yahrusalemu ingekanyagwa na watu wa mataifa kwa muda gani? Luka 21:24.
4. Je, kipindi cha upofu kilibakia kwa Israeli na Wayahudi kwa muda gani? Warumi 11:25.
5. Je, Yahweh atawapokea Wayahudi na kuwapandikiza tena kwenye mzeituni wao wa shamba? Waroma 11:23, 24 .
6. Je, kuwapokea tena kunahusiana vipi na ufufuo? Mstari wa 15.
7. Kulingana na nabii Ezekieli, Israeli watakaporudi katika nchi yao, je, wao pia watapewa Roho wa kweli na badiliko la moyo? Ezek. 36:24-26
8. Ni hali gani zitakuwepo katika nchi ya Israeli kuhusu kunyunyiziwa maji safi (Neno) kwa Wayahudi? Mstari wa 25.
9. Yahshua atakaporudi kwenye Mlima wa Mizeituni, Je, Atakuja kwa watu wanaoishi katika dhambi, au atakuja kwa watu ambao tayari wameacha makosa yao? Isaya 59:20.
10. Je, itakuwa ni baada ya Yahshua kuja ndipo Israeli watamtafuta Yahweh hapa Yahrusalemu? Au itakuwa “katika siku za mwisho”? Hosea 3:4, 5:5:15 .
11. Baada ya Yahweh kuwakusanya Wayahudi kurudi katika nchi ya Israeli, je, atawatuma Wachungaji ili kuwafundisha njia za haki? Yeremia 3:14, 15 .