OLQP SouthB

OLQP SouthB This is the official page for Our Lady Queen of Peace catholic church located in SouthB , Na

06/09/2026

MASOMO YA MISA
JUMATATU, SEPTEMBA 7, 2026
JUMA LA 23 LA MWAKA

SOMO 1
1Kor. 5:1 – 8

Habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe, nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.

Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima? Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, k**a vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; basin a tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 5:4 – 6, 11 (K) 8

(K) Bwana, uniongoze kwa haki yako.

Unawachukia wote watendao ubatili.
Utawaharibu wasemao uongo;
Bwana humzira mwuaji na mwenye hila. (K)

Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;
Mtu mwovu hatakaa kwako;
Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako. (K)

Nao wote wanaokukimbilia watafurahi;
Watapiga daima kelele za furaha.
Kwa kuwa Wewe unawahifadhi,
Walipendao jina lako watakufurahia. (K)

SHANGILIO
Zab. 19:8

Aleluya, aleluya,
Amri ya Bwana ni safi,
huyatia macho nuru.
Alelluya.

INJILI
Lk. 6:6 – 1

Ilikuwa siku ya sabato nyingine Yesu aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kuume umepooza. Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumsh*takia. Lakini yeye atakayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama.

Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza? Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

06/09/2026

“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu, Septemba 7, 2026.
Juma la 23 la Mwaka

1 Kor 5: 1-8;
Zab 5: 5-7, 12;
Lk 6: 6-11

WATU WASIO TIWA CHACHU!

“Mahusiano hayawezi kufa hivi hivi bila sababu. Yanakufa kwacsababu ya ubinafsi na kukosa uelewa”. Kukiwa na upendo na uelewa uhusiano hauwezi kufa kamwe. Katika Injili ya Leo tunamsikia Yesu akimponya mtu aliye na mkono ulio pooza akiwa katika Sinagogi siku ya Sabato. Katika hali ya kukosa uelewa, kuwa na ubinafsi, na umimi wa viongozi wa Wayahudi, Waandishi na Mafarisayo hawakuruhusu akili zao na mioyo yao kuelewa maneno na matendo ya Yesu. Walianza kumlaumu. Viongozi hawa walikuwa wanajali zaidi kushika sheria za Sabato zaidi ya kuleta nafuu kwa wanao teseka. Waliweza kuokoa mnyama aliyeanguka shimoni siku ya sababu zaidi ya kuonesha huruma kwa mwanadamu mwenzao.

Yesu alikuwa na haki ya kumuokoa yule mgonjwa sio tu kwa kumponya mkono wake lakini hata kumsamehe makosa yake na kumpa neema, Amani na furaha. Mt. Paulo anatuonya sisi tugeuze hali zetu, tuzirekebishe. Tuadhimishe uwepo wetu na Yesu, si kwakurudia chachu ya kale, chachu ya chuki na uovu bali tukiwa donge jipya lisilochachuka ambalo Paulo anasema ni weupe wa moyo na kweli. Tusiwe watu wasio eleweka katika maisha yetu ya ufuasi, tumgeukie Yesu kweli na tuweke lengo la kuacha maisha ya kale. Achana na kiburi, wivu, kushengenya wengine, kufurahia uovu, ubinafsi, uchoyo! Kwani hizi sio sifa za mfuasi wa Yesu. Tuombe neema ya Mungu ituongoze ili daima tuweze kufurahi jirani zetu wanapofanikiwa, tusiwazibie milango tusije tukawa k**a mafarisayo na waandishi.

Sala: Ee Bwana, tusaidie tuweze kusafisha chachu ya kale na kuiondoa, tunaomba utufanye donge jipya la uaminifu na kweli. Amina

06/09/2026

*Readings at Mass*
*Monday, 7th September 2026*
*Twenty Third Week in Ordinary Time*
*Liturgical Colour: Green*
________
*First reading*
1 Corinthians 5:1-8

I have been told as an undoubted fact that one of you is living with his father’s wife. This is a case of sexual immorality among you that must be unparalleled even among pagans. How can you be so proud of yourselves? You should be in mourning. A man who does a thing like that ought to have been expelled from the community. Though I am far away in body, I am with you in spirit, and have already condemned the man who did this thing as if I were actually present. When you are assembled together in the name of the Lord Jesus, and I am spiritually present with you, then with the power of our Lord Jesus he is to be handed over to Satan so that his sensual body may be destroyed and his spirit saved on the day of the Lord.

The pride that you take in yourselves is hardly to your credit. You must know how even a small amount of yeast is enough to leaven all the dough, so get rid of all the old yeast, and make yourselves into a completely new batch of bread, unleavened as you are meant to be. Christ, our passover, has been sacrificed; let us celebrate the feast, then, by getting rid of all the old yeast of evil and wickedness, having only the unleavened bread of sincerity and truth.
_______
*Responsorial Psalm*
Psalm 5:5-7,12

Lead me, Lord, in your justice.

You are no God who loves evil;
no sinner is your guest.
The boastful shall not stand their ground
before your face.

You hate all who do evil;
you destroy all who lie.
The deceitful and bloodthirsty man
the Lord detests.

All those you protect shall be glad
and ring out their joy.
You shelter them; in you they rejoice,
those who love your name.
______
*Gospel Acclamation*
Jn 10:27

Alleluia, alleluia!
The sheep that belong to me listen to my voice,
says the Lord,
I know them and they follow me.
Alleluia!
________
*Gospel*
Luke 6:6-11

On the sabbath Jesus went into the synagogue and began to teach, and a man was there whose right hand was withered. The scribes and the Pharisees were watching him to see if he would cure a man on the sabbath, hoping to find something to use against him. But he knew their thoughts; and he said to the man with the withered hand, ‘Stand up! Come out into the middle.’ And he came out and stood there. Then Jesus said to them, ‘I put it to you: is it against the law on the sabbath to do good, or to do evil; to save life, or to destroy it?’ Then he looked round at them all and said to the man, ‘Stretch out your hand.’ He did so, and his hand was better. But they were furious, and began to discuss the best way of dealing with Jesus.

06/09/2026

“SPRINGS OF LIVING WATER”
Daily Spiritual Reflections
7th SEPTEMBER 2026
------------------------------------------------
MONDAY, TWENTY THIRD WEEK IN ORDINARY TIME

1 Cor 5: 1-8 Ps 5: 5-7, 12 Lk 6: 6-11
------------------------------------------------

LOVE OR LAW?

We live in the 21st century, a world that prides in its progress and technological advancements. With the advent of artificial intelligence and algorithms, we seem to have moved forward much in our lifestyle and standards. Yet how often do we find ourselves clinging to outdated rituals, rigid regulations and legalistic attitudes that suppress the spirit of love and mercy? The external progress seems not to have spilled into our interior lives. Jesus our Master gave us one eternal commandment - love one another as I have love you, as the pattern to live our lives by, the golden rule of human living.

The third commandment in the decalogue calls us to keep the sabbath holy. Which means to rest or cease. Over time, the Pharisees and Sadducees worsened it with a complex web of rules losing sight of the commandment’s original intent: communion with God and compassion for others. It is here that Jesus challenges these traditions. In today’s Gospel, Jesus heals a man suffering from paralysis of the right hand, even though it is the sabbath. Jesus acts with compassion. He teaches us a profound truth: love is never out of season. The sabbath, for Jesus is not merely a day of rest, it is a day of restoration, making space for goodness, mercy and human connection.

As Christians our Sunday, the Lord’s Day is not just for attending mass and retreating into personal rest. The church teaches us that Sunday is traditionally consecrated by Christian piety to good works and humble service of the sick, the infirm and the elderly (CCC 2186). So, the question before us is not merely whether we observe the law but how we live love. Will we be people of cold rules or warm hearts? Do we choose to enter into our own personal cocoons on the day of the Lord, and hide human charity? Or are we willing to step out of our comforts and share – receive and give – the love for which we are created? Let us choose the way of Christ: the way of love.

Response: Lead me, Lord, in your justice.

04/09/2026

*Readings at Mass*
*Sunday 6th September 2026*
*Twenty Third Week in Ordinary Time*
*Liturgical Colour: Green*
________
*First reading*
Ezekiel 33:7-9

The word of the Lord was addressed to me as follows: ‘Son of man, I have appointed you as sentry to the House of Israel. When you hear a word from my mouth, warn them in my name. If I say to a wicked man: Wicked wretch, you are to die, and you do not speak to warn the wicked man to renounce his ways, then he shall die for his sin, but I will hold you responsible for his death. If, however, you do warn a wicked man to renounce his ways and repent, and he does not repent, then he shall die for his sin, but you yourself will have saved your life.’
________
*Responsorial Psalm*
Psalm 94(95):1-2,6-9

O that today you would listen to his voice! ‘Harden not your hearts.’

Come, ring out our joy to the Lord;
hail the rock who saves us.
Let us come before him, giving thanks,
with songs let us hail the Lord.

Come in; let us bow and bend low;
let us kneel before the God who made us:
for he is our God and we
the people who belong to his pasture,
the flock that is led by his hand.

O that today you would listen to his voice!
‘Harden not your hearts as at Meribah,
as on that day at Massah in the desert
when your fathers put me to the test;
when they tried me, though they saw my work.’
________
*Second reading*
Romans 13:8-10

Avoid getting into debt, except the debt of mutual love. If you love your fellow men you have carried out your obligations. All the commandments: You shall not commit adultery, you shall not kill, you shall not steal, you shall not covet, and so on, are summed up in this single command: You must love your neighbour as yourself. Love is the one thing that cannot hurt your neighbour; that is why it is the answer to every one of the commandments.
________
*Gospel Acclamation*
Jn 17:17

Alleluia, alleluia!
Your word is truth, O Lord:
consecrate us in the truth.
Alleluia!
________
*Gospel*
Matthew 18:15-20

Jesus said to his disciples: ‘If your brother does something wrong, go and have it out with him alone, between your two selves. If he listens to you, you have won back your brother. If he does not listen, take one or two others along with you: the evidence of two or three witnesses is required to sustain any charge. But if he refuses to listen to these, report it to the community; and if he refuses to listen to the community, treat him like a pagan or a tax collector.

‘I tell you solemnly, whatever you bind on earth shall be considered bound in heaven; whatever you loose on earth shall be considered loosed in heaven.

‘I tell you solemnly once again, if two of you on earth agree to ask anything at all, it will be granted to you by my Father in heaven. For where two or three meet in my name, I shall be there with them.’

04/09/2026

“SPRINGS OF LIVING WATER”
Daily Spiritual Reflections
6th SEPTEMBER 2026
------------------------------------------------
SUNDAY, TWENTY THIRD WEEK IN ORDINARY TIME

Ez 33: 7-9 Ps 95: 1-2, 6-9 Rom 13: 8-10 Mt 18: 15-20
------------------------------------------------

CALLED TO WATCH, CALLED TO LOVE

The Word of God this Sunday presents us with a challenging yet deeply beautiful truth: love is not merely a feeling; it is a responsibility. Through the prophet Ezekiel, the teaching of St. Paul, and the words of Jesus Himself, we are reminded that every Christian is called both to watch and to love; to remain attentive to God and to care for the spiritual well-being of one another. In the first reading, God appoints Ezekiel as a watchman for Israel. A watchman stands alert, scanning the horizon for danger. If he sees danger approaching and remains silent, he becomes accountable for the loss that follows. God therefore entrusts Ezekiel with a sacred duty: to speak His word faithfully, even when it may be unwelcome. At first glance, this responsibility seems to belong only to prophets.

Yet through baptism, every Christian shares in Christ's prophetic mission. We too are called to be watchmen, but not over cities or kingdoms, but over our own hearts and, in a spirit of charity, over the communities to which we belong. We are called to notice when a brother or sister is struggling, drifting away from God, or burdened by sin. Love does not close its eyes to danger. Yet there is a great difference between vigilance and judgment. This is where the second reading becomes essential. Love is the fulfilment of the law because genuine love always seeks the good of the other. Christian concern is never rooted in superiority or control. It springs from a heart that desires another person's growth in holiness and happiness. The saints of Carmel understood this deeply. St. Teresa of Avila often insisted that progress in the spiritual life depends upon humility and self knowledge. Before we attempt to guide another, we must first allow God to reveal our own weaknesses. A soul that knows its need for mercy becomes gentle in offering correction. It speaks not as a judge but as a fellow pilgrim.

This wisdom sheds light on the Gospel. Jesus teaches a path of fraternal correction that begins quietly and personally. The goal is not to expose, embarrass, or defeat another person. The goal is reconciliation. Jesus desires that relationships wounded by sin be healed through honest conversation and patient charity. How different this approach is from the spirit of our age. We live in a culture where criticism is often public and swift, while forgiveness can be slow and reluctant. Social media encourages exposure rather than encounter. Jesus proposes another way: the way of personal dialogue, discretion, and sincere concern for the other person's dignity.

For Carmelites, this Gospel carries an additional invitation. Before speaking to another, we must first enter the silence of prayer. Elijah encountered God not in the wind, earthquake, or fire, but in a gentle whisper. The Carmelite learns that every important word should emerge from a listening heart. If correction is not first purified by prayer, it can easily become harsh or self-righteous. But when it is born of prayer, it can become an instrument of healing. St. Thérèse of Lisieux understood that true charity often consists in small acts of patience, hidden sacrifices, and persistent prayer for others. She knew that souls are changed not merely by arguments but by grace. Her "little way" reminds us that love is often most powerful when it is humble.

The Gospel concludes with one of Christ's most consoling promises: "Where two or three are gathered in my name, there I am amidst them." These words remind us that reconciliation is never merely a human achievement. Christ Himself is present among those who seek unity and peace. Whenever believers come together in prayer, forgiveness, and mutual support, the Lord stands among them. This promise lies at the heart of Carmelite spirituality as every community is sustained specifically by the presence of Christ. Whether in a monastery, an OCDS community, a parish, or a family, relationships flourish when Christ remains at the centre.

Today's readings invite us to examine our own lives. Do we watch over our hearts with vigilance? Do we care enough about others to tell the truth when necessary? Do we pray for those whom we find difficult? The watchman of Ezekiel, the charity of St. Paul, and the teaching of Jesus all point toward the same vocation. We are called to watch with loving concern. We are called to love with courage and commitment.

Response: O that today you would listen to his voice! Harden not your hearts.

04/09/2026

MASOMO YA MISA,
JUMAPILI, SEPTEMBA 6, 2026
JUMA LA 23 LA MWAKA
________

MWANZO
Zab. 119:137, 124

Ee Bwana, wewe ndiwe mwenye haki, na hukumu zako ni za adili. K**a zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako.
________

SOMO I
Eze. 33:7-9

Basi wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 95:1-2, 6-9 (K) 7-8

(K) Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake!

Tusifanye migumu mioyo yetu.
Njoni tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele yake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi. (K)

Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake. (K)

Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu;
K**a vile huko Meriba;
K**a siku ile ya Masa jangwani,
Hapo waliponijaribu baba zetu;
Wakanipima, wakayaona matendo yangu. (K)
________

SOMO 2
Rum. 13:8-10

Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sharia. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani, na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako k**a nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya, basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

SHANGILIO
Yn. 14:23

Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda, atalishika neno langu;
Na baba yangu atampenda; Nasi tutakuja kwake.
Aleluya.
________

INJILI
Mt. 18:15-20

Siku ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, k**a hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako k**a mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.

Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

04/09/2026

“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila Jumapili
Jumapili, Septemba 6, 2026

Dominika ya 23 ya Mwaka

Ez 33: 7-9;
Zab 94: 1-2, 6-9;
Rom 13: 8-10;
Mt 18: 15-20

KUJENGA JUMUIYA YENYE KUWA NA TAHADHARI!

Wakati watu wameshakutana na ugumu fulani, wanakuwa wanatoa kiashirio kwa wengine kwamba muelekeo sio mzuri, viashirio vyao mara nyingi wengi hawa vitilii maanani. Lakini katika hali ya kweli, wengi hupenda kuwatazama wengine wakiwa katika njia isio faa. Mara nyingi wanawachukia, kuwatania na kuwaona wajinga. Mungu analinganisha kazi ya nabii Ezekieli na ya mlinzi. Alikuwa apewe onyo kutoka kwa Mungu naye alipeleke onyo hilo kwa kila mtu. Kazi ya Kanisa na ya kila mkristo ni sawa sawa. Ni kuwaongoza watu kwa ujumbe wa neno la Mungu. Siku hizi tunatumia teknolojia yenye nguvu kuwapa watu ishara ya hatari ya kujisahau kushika neno la Mungu. Tunachofanya leo na teknolojia kilifanyika katika Biblia, ambapo waliwaweka walinzi katika sehemu Fulani ili aweze kutoa ishara ya hatari wakati aduia anataka kukaribia.

"Mtu mmoja alikuwa akishanga shangaa aliokota ufunguo bondeni karibu na mlima mkubwa. Ulikuwa ni ufunguo wa ajabu, ufunguo ambao ulikuwa na uwezo wakufungua kila aina ya nyumba yenye hazina ulimwenguni. Kwa ufunguo huu alikusanya dhahabu na almasi kutoka katika sehemu mbali mbali alizopenda duniani. Akiwa njiani akirudi alisikia sauti ikimwambia kutoka chini ya mlima: “kabla haujatoka nje, hakikisha hausahau kitu muhimu kuliko vyote. Gafla mlango ukafunga moja kwa moja. Alikuwa amesahau kuchukua ufunguo.”

Mwanadamu daima anatafuta kupata ufunguo wa furaha, Amani na kujitosheleza. Sisi wote tunatafuta ufunguo wa urafiki, kueleweka, kuwa na jina na uzuri, na kuwa na kazi nzuri yenye kuvutia na faraja. Wengine wanatafuta furaha kwa fedha, madaraka nk. Lakini hivi vyote vinatufunga na kujikuta tunapotelea huko. Vinatufunga kiasi ambacho tunasahau kitu muhimu ziadi nacho ni ufunguo wa maisha. Maisha ya Ukristo yanatufundisha kwamba dunia hii itapita, hiki ndicho tunacho paswa kuzingatia kwa macho yetu na kutazama “maisha ya umilele”. Hii inamaana kwamba maisha yetu hapa duniani yana lengo zaidi ya lengo la kawaida. Furaha tulio nayo hapa sio kitu, ni kivuli tu cha furaha halisi ambayo tutakuwa nayo huko mbinguni. Lakini ufunguo wa furaha ya maisha haya uko wapi?

Katika somo la Injili ya leo Yesu anatuonesha picha nzuri ya jumuiya ya mapendo na yenye kujali. Inatuonesha ni kwa jinsi ghani tunaweza kuanzisha jumuiya ya kweli ya Kikristo na yenye kupendana.

1. K**a mtu akikukosa, tunapaswa tumwendee kwa upendo wa Kimungu na kumrudisha kundini. Tofauti kabisa na kumlaumu na kuanza kumlaumu, tunapaswa kumfuata kwa mapendo na kumsihi katika mapendo yetu. Injili inatushauri kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja, kwa utulivu na katika hali ya upekee, katika hali ya kurekebishana kindugu, ili kuanzisha tena urafiki uliyo vunjika. K**a hili litashindikana inashauriwa kuchukuwa watu wenye hekima na kumfuata kumuonesha kwamba jumuiya nzima inakuhitaji kurudi kundini katika mapendo yote.

2. Yesu anasisitiza nguvu ya sala. Anasema “pale wawili au watatu walipokusanyika kwa ajili yangu, Baba atakuwa katikati yao”. Huu ni uhakika anaotoa Yesu kwamba wale wanaosali yeye atakuja katikati yao na kuwa kati yao na kushiriki katika sala yao. Wayahudi walikuwa na Imani kubwa katika sala za pamoja. Iliandikwa “wawili walipo kusanyika na wanajihusisha na kujifunza Torati, utukufu wa Mungu upo katikati yao” sala za jumuiya huweka magomvi mbali na kuleta umoja. Agano, jumuiya, ukarimu, msamaha hizi ni sifa za dini ya Kibiblia. Uzoefu wa haya yote vinafanya maisha yetu kuwa na furaha, na kuishi vizuri. Haya yote yanawezekana tu pale ambapo tuna upendo. Kwa mfano,

"Mfungwa mmoja alikuwa anarudi nyumbani, kutoka katika mahabusu ya mbali akiwa kwenye treni. Alikuwa akiona aibu kwa kufungwa kwake na alikuwa akidhani familia yake itakuwa imemsamehe. Kwa ishara ya kuonesha kwamba wamemsamehe, walipaswa wafunge riboni nyeupe kwenye mti ambao ulikuwa karibu na gari nyumbani kwake. Hivyo k**a hataona riboni nyeupe kwenye mti, yeye atapitiliza na treni aelekee kokote atakapo kwenda. Wakati treni ilivyofika karibu na nyumbani, akawa na wasi wasi mkubwa kiasi ambacho hakuthubutu kutazama kupitia dirishani. Marafiki zake wakaamua kubadilisha nafasi wakisema tunafahamu tu ataangalia mti uliokaribu na gari. Ghafla akanyanyua kichwa bila kujua na tazama sio roboni moja iliyowekwa kwenye mti bali mti wote ulikuwa umejaa riboni"

Amani na mshik**ano unawezekana tu, pale ambapo watu wanaishi kwa roho ya upendo na msamaha. Mungu ni upendo na penye upendo Mungu yupo. Upendo wa Mungu unabeba pia upendo kwa jirani. Upendo tunaweza kuupata tu tunapo amua kuishi na wenzetu, kwa mshik**ano katika jumuiya. Hili halimuumizi mtu yeyote, bali linakamilisha kila kitu na kufanya maisha yafikie katika kilele cha hali ya juu.

Mungu ametufanya sisi tuwe walinzi wa dunia sasa. Tunapaswa kuwa walinzi, kutangaza kwa kila mmoja, jumuiya zetu, na ulimwengu wa ukweli katika Yesu Kristo. Tunaitwa kusimama pamoja, bila kuachana katika Imani bila kuogopa kuitwa tusio na maana au mafundisho potofu, bali tutangaze kwa jirani na jumuiya zetu, ili watu wafahamu katika kutokufahamu kwao, kumuamini Yesu, na kukuwa katika neema na utakatifu. Tunapaswa kuwasaidia wengine watambue makosa yao, hasa tukiwa na kazi k**a ya wazazi kwa mtoto, mwalimu kwa wanafunzi, wazee na vijana.

Tutumie njia sawa ya kuwasaidia wengine watoke katika makosa yao bila ya kuwaumiza au kuwadhalilisha na kuwaachia makovu. Badala ya kuponya tukakuza kidonda zaidi. Katika vikao vyetu tuangalie njia njema ya kumsadia mtu na kumuonya badala ya kumwanika hadharani mbele ya watu wote, k**a kuna njia nzuri ya mtu mmoja kumfuata kwa hekima utamsaidia zaidi, kuliko kumkosoa mtu mbele ya watu wengi au katika kikao, hili haliponyi kwani mmoja hujisikia amedhalilishwa na utu wake kudharauliwa. Mfano tusisubiri mpaka mtu afe ndio tupate muda wa kukaa pamoja tuje kumrekebisha mtu mbele ya kikao cha ukoo, badala yake tutumie njia mbadala ya kutuma mtu mwenye hekima amsaidie na kupatana kabla ya kukaa pamoja. K*tangaza dhambi ya mtu mbele ya kikao, daima haina lengo la kuleta upatanisho wa kweli badala yake humuachia mtu maumivu na kisasi moyoni. Hakuna hata mmoja wetu angependa dhambi yake itajwe mbele ya watu. Ndio maana sakramenti ya kitubio husaidia kweli. Tumuige Yesu aliyekuwa na huruma kwa wadhambi.

Sala: Bwana, upo nasi katika jumuiya yetu, tukishikana pamoja kwa mapendo, huruma na msamaha. Tunakuomba tuwe watu wakutafuta furaha, upendo na Amani. Tunakuomba tuwe tayari kusamehe na kupatana na kila mtu. Yesu, ninakuamini wewe. Amina

04/09/2026

MASOMO YA MISA
JUMAMOSI, SEPTEMBA 5, 2026
JUMA LA 22 LA MWAKA

SOMO 1
1Kor. 4:6 – 15

Ndugu zangu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe. Maana ni nani anayekupambanua na mwingine? Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea, wajisifia nini kana kwamba hukupokea? Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laity mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi! Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, k**a watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu tumekuwa tamasha kwa dunia; kwa malaika na wanadamu.

Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima. Hata saa hii ya sasa, tuna njaa na kiu, tu uchi, twapigwa ngumi, tena hatuna makao; kasha twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twastahimili; tukisingiziwa twasihi; tumefanywa k**a takataka za dunia, na tama ya vitu vyote hata sasa.

Siyaandiki hayo ili kuwatahayarisha; bali kuwaonya k**a watoto niwapendao. Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:17 – 21 (K0 18

(K) Bwana yu karibu na wote wamwitao.

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu. (K)

Atawafanyia wamchao matakwa yao,
Nay atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Bwana huwahifadhi wote wammpendao,
Na wote wasio haki atawaangamiza. (K)

Kinywa change kitazinena sifa za Bwana;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu
Milele na milele. (K)

SHANGILIO
Zab. 119:18

Aleluya, aleluya,
Unifumbue macho yangu niyatazame
maajabu yatokayo katika sharia yako.
Aleluya.

INJILI
Lk. 6:1 – 5

Ilikuwa siku ya sabato moja Yesu alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao. Basi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato? Yesu akawajibu akawaambia, Hamkulisoma, hata hilo alilolifanya Daudi, alipokuwa na njaa, nay eye na wale aliokuwa nao? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya Wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao. Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo

04/09/2026

“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Septemba 5, 2026
Juma la 22 la Mwaka

1 Kor 4: 6-15;
Zab 144: 17-21;
Lk 6: 1-5

KUFANYA LISILO HALALI SIKU YA SABATO?

Sabato ilikuwepo hata kabla Torati haijatolewa katika Mlima Sinai (K*t 19). Wayahudi walifundishwa “kukumbuka siku ya Sabato” na kuifanya takatifu. Siku ya sabato ilitegemewa kuwa siku ya mapumziko na siku ya kuabudu, muda wa kukumbuka siku aliyo pumzika Mungu baada ya kazi ya uumbaji, siku ya saba. Mafarisayo walichukulia kitendo walichofanya wafuasi kwenye Injili kuwa ni kufuru kuhusu Sabato. Walivyomlaumu Yesu kuwa ameikufuru Sabato, Yesu aliwajjibu vyema. Yesu alimtumia Daudi k**a mfano, wakati Daudi akimkimbia Sauli alikula mikate ile ya Wonyesho (iliobarikiwa) inayotumika tu pale Mahali Patakatifu (tabernacle) ambayo ililiwa na makuhani pekee. (Sam 21: 1-6). Yesu anasema wazi kwamba Sabato sio Bwana, bali Mwana wa mtu (Yesu mwenyewe) ndiye. Ni yeye mwenyewe mwenye mamlaka ya kubadili torati na sheria ya Sabato.

Yesu anatufundisha tusifungwe mno na sheria tushindwe kuonesha upendo kwa jirani zetu. Pamoja na kutimiza majukumu yetu, tusisahau kwamba sisi tunayo sheria ya Kristo ambayo ni upendo, sheria isiyo na upendo si sheria ya Kristo. Mt. Greogori mkuu, alitambua hilo ndio maana alitoa huduma bora katika kanisa, na zaidi sana upendo wake kwa fukara uliomdhihirisha kuwa yeye ni kiongozi na mchungaji wa kweli. Tumuombe atuombee kwa Mungu ili nasi tuweze kuwa na roho ya kuwapenda wote wasiojiweza tuwe na moyo wakuwahudumia kwa upendo bila kujali jamii inaniona je. Ndugu zangu sisi tunalo deni, na deni letu ni Upendo kwa Mungu na jirani zetu, tujaribu kulilipa kila siku tuwapo hapa duniani.

Sala: Bwana, naomba nikuheshimu katika kazi yangu na katika mapumziko yangu na niwatendee jirani zangu kwa heshima na upendo. Niweke mbali na roho ya mabishano na ubinafsi ili niweze kutafuta uzuri wa jirani zangu katika hali zote. Amina

Address

P. O. Box 60311 Nairobi City Square
Nairobi South
002000

Opening Hours

Monday 07:00 - 19:30
Tuesday 07:00 - 19:30
Wednesday 07:00 - 19:30
Thursday 07:00 - 19:30
Friday 07:00 - 19:30
Saturday 07:00 - 19:30
Sunday 07:00 - 19:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when OLQP SouthB posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to OLQP SouthB:

Shortcuts

Share

Category