05/12/2020
KUISHI MAISHA MAPANA (LARGER LIFE)
Ni mapenzi ya Mungu kwamba watu wake waishi maisha mazuri yaliyo panuka. 2 Samueli 22:37 Daudi alielewa neno hili na akamwambia Mungu hivi " Umezifanyia nafasi hatua zangu wala miguu yangu haikuteleza."
Ili tupige hatua tunahitji nafasi ya kusonga mbele.
Kusonga mbele kihekima, kimali na hata mipaka iliyopanuka.
Mungu alimpanulia Sulemani mipaka yake. 1 Wafalme 4:29 - Mungu akampa Sulemani hekima na akili nyingi sana na moyo mkuu, K**a mchanga ulioko pwani.
Akamzidishia na Mali pia.
Mungu alimpanulia Isaka mipaka yake na pia uzao wake. Mwanzo 26:4 akamwahidi haya-- " Nitazidisha uzao wako k**a nyota za mbinguni, na nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote watajibarikia.
Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu,akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
Ufunguo wa kufungua baraka zetu ni kusikia sauti ya Mungu wetu aliye mbinguni.
Kupanuliwa kuna kanuni zake za muhimu sana.
Yabesi alizielewa kisawasawa akamwomba Mungu naye akamsikiliza.
1 Mambo ya Nyakati 4:10 -- " Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema,
-- Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli
-- na kunizidishia hozi (milki, nchi) yangu
-- na mkono wako ungekuwa pamoja nami,
-- nawe ungenilinda na uovu,
-- ili nisiwe kwa huzuni yangu!
-- Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Zaburi 113: 5 - 9 -- Mungu " Humwinua mnyonge kutoka mavumbini na kumpandisha maskini kutoka jaani.
Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake.
-- Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa awe mama wa watoto wenye furaha.
Isaya 54:2 - 3 ahadi ya Mungu kwetu Ni hii -- " Panua mahali pa hema yako,
na yatandaze mapazia ya maskani yako;
usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako;
vikaze vikingi vya hema yako;
-- kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto;
na wazao wako watawamiliki mataifa;
wataifanya miji iliyoachwa ukiwa kukaliwa na watu."
Mungu wetu anatuahidi kuenea, kupanua hema zetu, uzao wetu, mali zetu na roho zetu.