27/10/2022
1
Nisikilizeni, Enyi visiwa, sikieni hili, ninyi mataifa mlio mbali: Kabla sijazaliwa BWANA aliniita, tangu kuzaliwa kwangu amelitaja jina langu.
2
Akafanya kinywa changu kuwa k**a upanga ulionolewa, katika uvuli wa mkono wake akanificha; akanifanya kuwa mshale uliosuguliwa na kunificha katika podo lake.
3
Akaniambia, “Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika yeye nitaonyesha utukufu wangu.”
4
Lakini nilisema, “Nimetumika bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida. Hata hivyo linalonistahili liko mkononi mwa BWANA, nayo ijara yangu iko kwa Mungu wangu.”
5
Sasa BWANA asema, yeye aliyeniumba tumboni kuwa mtumishi wake kumrudisha tena Yakobo kwake na kumkusanyia Israeli, kwa maana nimepata heshima machoni pa BWANA, naye Mungu wangu amekuwa nguvu yangu;
6
anasema: “Je, ni jambo dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kurejeza upya makabila ya Yakobo, na kuwarudisha wale Waisraeli niliowahifadhi? Pia nitakufanya uwe nuru kwa ajili ya watu Mataifa, ili upate kuleta wokovu wangu hata miisho ya dunia.”
7
Hili ndilo asemalo BWANA, yeye Mkombozi na Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwake yeye ambaye alidharauliwa na kuchukiwa na taifa, kwa mtumishi wa watawala: “Wafalme watakuona na kusimama, wakuu wataona na kuanguka kifudifudi, kwa sababu ya BWANA, aliye mwaminifu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, ambaye amekuchagua wewe.”
8
Hili ndilo asemalo BWANA: “Wakati wangu uliokubalika nitakujibu, nami katika siku ya wokovu nitakusaidia; nitakuhifadhi nami nitakufanya kuwa Agano kwa ajili ya
Send a message to learn more