12/09/2023
MUNGU NI NANI?
: Kuna Mungu wangapi?
: Kuna Mungu mmoja tu.
👉Kumbukumbu la Torati 6:4
Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja.
: Je huyu Mungu Mmoja ana nafsi ngapi?
: Huyu Mungu mmoja ambaye ni BWANA ana nafsi moja tu.
👉Yeremia 22:5
Lakini k**a hamtaki kusikia maneno haya, mimi naapa kwa , asema BWANA, ya kuwa nyumba hii itakuwa ukiwa.
K**a Mungu ana nafsi 3, Basi angesema naapa kwa Nafsi , Lakini amesema naapa kwa Nafsi ikimaanisha ni Mmoja.
: Je huyo Mungu Mmoja ni Nani?
: Biblia inaposema Kuna Mungu mmoja Ina maana ya Baba.
👉Waefeso 4:6
Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
: K**a Mungu Mmoja ni Baba Je, Yesu ni Nani?
: Yesu ni Mwana wa Mungu,
👉Mathayo 16:16
Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
: Je Roho Mtakatifu ni Nani?
: Roho Mtakatifu Ni Roho wa Mungu na pia ni Roho wa Yesu Kristo.
👉Warumi 8:9
Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
: K**a Mungu ni Mmoja ambaye ni Baba, inakuwaje katika Uumbaji kuna nafsi zaidi ya moja?
: Katika Uumbaji, Mungu alikuwa na Mwanaye Yesu Kristo na ndiye alimwambia "Na tumfanye mtu kwa mfano wetu"
👉Mithali 8:30
Ndipo nilipokuwa pamoja naye, k**a stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake;
: huyo ni Yesu ndio anasema alikuwa pamoja na Mungu.
: Je, 1Yohana 5:8 haina maana Mungu ana nafsi 3?
: hilo fungu halisemi yupo Mungu mwenye nafsi 3 anayeshuhudia Mbinguni, Bali fungu linasema wako watatu wanaoshuhudia Mbinguni Baba(ambaye ni Mungu mwenyewe), Neno(ambaye ni Mwana wa Mungu) na Roho(ambaye ni Roho wa Mungu na pia ni Roho wa Mwana wa Mungu)
: Mbona MATHAYO 28:18,19, inasema tukawabatize watu kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu?
#