02/03/2026
Bismillahi rrahmani rrahim.
Naandika makala haya kwa lengo la kuwaelimisha wasiokua Waislamu (Wakristo) na wengineo.
Jana katika wa Austin huko Texas Marekani mtu mmoja anaejinasibisha na Uislamu amewapiga risasi na kuwaua watu wasio na hatia kwa kigezo kwamba sio waislamu nataka kusema yafwatayo :-
1- Uislamu haukubaliana na Ugaidi wala kuwaua wasio na hatia bila ya sababu , aya zote zinazozungumzia kuua katika Qur'an zinazungumzia vita nitanukuu aya mbili .
ALLAH anasema : {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.} Quran sura ya 2 aya ya 190.
{Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.} Qur'an 60:8
2- Makundi yote ya kigaidi k**a (Al Shabaab), (Al Qaeeda) , (Boko Haram) na kadhalika ni makundi hayauwakilishi Uislamu matendo yao maovu ni yao wala sio mafunzo ya dini yote wanayoyafanya ni ugaidi na hatia na sisi tunayapinga haya makundi.
3- Uislamu unaamrisha kuwafanyia wema hata wanyama na wadudu Mtume Muhammad anasema : {Mwanamke mmoja aliingia motoni (jahanamu) kwa sababu ya paka hakumlisha wala hakumuacha huru akatafute chakula mpaka akafa} k**a kumuua paka mtu anaenda motoni itakuaje kumuua mtu bila hatia.
4- Watu lazima watofautishe kati ya (Muislamu) mtu na (Uislamu) dini , Waislamu wako waovu wahuni walevi washenzi magaidi majambazi na kadhalika , lakini Uislamu haufunzi tabia hizo wala hauamrishi ugaidi na ujambazi , Soma uujue Uislamu sio waislamu.
5- Neno (Ugaidi) lina maana pana na sio waislamu tu wanafanya ugaidi , Waislamu India kila siku wanateswa na kuuwawa , Waislamu Palestina kila siku wanateswa na kuuwawa , Mbona wakiua watu wengine hakuna tatizo lakini akiua Muislamu dunia yote itasimama . Ugaidi huna rangi wala kabila wala dini.