ST. Charles Borromeo Catholic Church

ST. Charles Borromeo Catholic Church Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ST. Charles Borromeo Catholic Church, Religious organisation, Muguga, Kikuyu.

Time to celebrate the season of spring and advent of Jesus in our lives
10/04/2022

Time to celebrate the season of spring and advent of Jesus in our lives

40 days of fasting, giving , praying and preparing.
14/03/2022

40 days of fasting, giving , praying and preparing.

Congratulations to the newly wed  💒 coupleMR and Mrs Charles Maina
08/01/2022

Congratulations to the newly wed 💒 couple
MR and Mrs Charles Maina

MASOMO YA MISA, MEI 15, 2021JUMA LA 6 LA PASAKA, JUMAMOSI SOMO 1Mdo. 18:23-28 Paulo, akiisha kukaa Antiokia siku kadha w...
14/05/2021

MASOMO YA MISA, MEI 15, 2021

JUMA LA 6 LA PASAKA, JUMAMOSI



SOMO 1

Mdo. 18:23-28



Paulo, akiisha kukaa Antiokia siku kadha wa kadha aliondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwathibitisha wanafunzi. Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzaliwa wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohane tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.



Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe; naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.



Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.



WIMBO WA KATIKATI

Zab. 47: 1-2, 7-9 (K) 7



(K) Mungu ndiye mfalme wa dunia yote.

Au: Aleluya.



Enyi watu wote, pigeni makofi,

Mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe,

Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya,

Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. (K)



Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,

Imbeni kwa akili.

Mungu awamiliki mataifa,

Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. (K)



Wakuu wa watu wamekusanyika,

Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu.

Maana ngao za dunia zina Mungu,

Ametukuka sana. (K)



SHANGILIO

Yn. 10:27



Aleluya, aleluya,

Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.

Aleluya.



INJILI

Yn. 16:23-28
Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambayo sitasema nanyi tena kwa mithali; lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. Na siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba.



Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.



-------------------------

Copyright © 2021
St Charles Barromeo.

Address

Muguga
Kikuyu
STCHARLESBORROMEO HTTPS://MAPS.APP.GOO.GL/3NLHC1F1QB6N2XCZ6

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ST. Charles Borromeo Catholic Church posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to ST. Charles Borromeo Catholic Church:

Share