St Jude Catholic Church, Kaptendon

St Jude Catholic Church, Kaptendon Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from St Jude Catholic Church, Kaptendon, Religious organisation, Kaptendon, Kapsabet.

02/09/2026

MASOMO YA MISA, ALHAMISI YA JUMA LA ISHIRINI NA MBILI, KIPINDI CHA KAWAIDA, MWAKA II, KUMBUKUMBU YA MT. GREGORI MKUU, PAPA NA MWALIMU WA KANISA, SEPTEMBA 3, 2026
RANGI YA KILITURJIA: NYEUPE 🤍

SOMO LA KWANZA
1 WAKORINTHO 3:18—23

"Mambo yote ni yenu, nanyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu."

Somo katika barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho

Ndugu: Mtu asijidanganye mwenyewe: k**a mmoja wenu akijiona ni mtu wa hekima nyakati hizi, awe kwanza mjinga, apate kuwa mwenye hekima. Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni ujinga mbele ya Mungu, kwani imeandikwa: Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao." Na tena, "Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima, maana ni ya bure." Basi, mtu asijisifie wanadamu. Kwa maana yote ni yenu: Paulo, Apolo au Kefa, ulimwengu au uzima au mauti; mambo ya sasa au ya baadaye, yote ni yenu. Nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

NENO LA BWANA... TUMSHUKURU MUNGU

ZABURI YA KUITIKIZANA
ZABURI 24:1—2, 3—4ab, 5—6 (K. 1a)

K. Nchi ni yake Bwana na vyote vinavyoijaza.

dunia yote na wakaaji waliomo. Maana Mungu ameweka
misingi yake juu ya bahari; ameisimika juu ya mito ya maji. K.

Nchi ni yake Bwana na vyote vinavyoijaza,
Ni nani atakayeupanda mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama mahali pake patakatifu?
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
asiyeuinua moyo wake kwa mambo ya miungu. K.

Huyo atapata baraka kutoka kwa Bwana.
na tuzo ya Mungu Mwokozi wake.
Hiki ni kizazi cha wenye kumtafuta,
cha wenye kuutafuta uso wako, ee Mungu wa Yakobo. K.

SHANGILIO LA INJILI
MATHAYO 4:19

K. Aleluya. W. Alelya.
K. Njoni mnifuate, asema Bwana, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
W. Aleluya.

SOMO LA INJILI
LUKA 5:1—11

"Waliacha vyote wakamjuata."

† Somo la Injili takatifu ilivyoan dikwa na Luka

Wakati ule: Watu wengi walimsonga wapate kulisikiliza neno la Mungu, [Yesu] alikuwa amesimama kando ya Ziwa la Genesareti. Akaona vyombo viwili vimepwelewa pwani; wavuvi wame shuka, wanaosha nyavu. Akapanda chombo kimoja, ndicho cha Simoni, akamwomba akitenge kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makundi toka chomboni. Baada ya mafundisho, akamwambia Simoni, “Rudisha chombo baharini, shusheni nyavu zenu kwa kuvua samaki." Simoni akajibu, akamwambia, "Bwana, tumejitahidi sana usiku mzima tusipate kitu, lakini kwa neno lako nitashusha nyavu." Walipofanya hivyo, walinasa samaki wengi mno, hata nyavu zao zikaanza kukatika. Wakawaashiria wenzao waliokuwako katika chombo kingine waje kuwasaidia. Wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili hata karibu ya kuzama. Simoni Petro alipoona hayo, alimwangukia Yesu magotini pake, akasema, “Ondoka kwangu, ewe Bwana, kwa maana mimi ni mtu mkosefu."" Maana mshangao ulimshika yeye na wote waliokuwa pamoja naye kwa sababu ya wingi wa samaki waliowanasa, kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, ndio washiriki wa Simoni. Yesu akamwambia Simoni, "Usiogope; tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu." Walipoviegesha vyombo pwani, wakaacha vyote, wakamfuata.

INJILI YA BWANA... SIFA KWAKO EE KRISTO

02/09/2026

MASOMO YA MISA, JUMATANO YA JUMA LA ISHIRINI NA MBILI, KIPINDI CHA KAWAIDA, MWAKA II, SEPTEMBA 2, 2026
RANGI YA KILITURJIA: KIJANI KIBICHI 💚

SOMO LA KWANZA
1 WAKORINTHO 3:1—9

"Sisi ni wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, jengo la Mungu."

Somo katika barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho

Ndugu, hata kwenu sikuweza kusema k**a kwa watu wa kiroho, bali k**a kwa watu wa mwili, k**a kwa watoto wachanga katika Kristo. Naliwalisha maziwa, si chakula kigumu, kwa maana hamkuweza kukiyeyusha. Hata sasa hamwezi. Kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa kawaida, si wa kiroho. Ikiwa kwenu kuna wivu na ugomvi, je, ninyi si watu wa kawaida? Tena mnaishi k**a watu wa kawaida. Mmoja akisema, "Mimi ni wa Paulo," na mwingine, Mimi ni wa Apolo," je, si alama ya watu wa kawaida? Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni watumishi waliowasaidia kupata imani, kila mmoja k**a alivyojaliwa na Bwana. Mimi nilipanda, Apolo anayemwagilia maji, lakini aliyekuza ni Mungu. Hivyo anayepanda na anayemwagilia maji si kitu, ila Mungu anayekuza. Basi, mwenye kupanda na mwenye kumwagilia maji ni wamoja, lakini kila mmoja wao atapata thawabu yake kwa kadiri ya bidii yake. Sisi ni wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, jengo la Mungu.

NENO LA BWANA... TUMSHUKURU MUNGU

ZABURI YA KUITIKIZANA
ZABURI 33:12—13; 14—15, 20—21 (K. 12b)

K. Heri taifa ambalo Bwana amelichagua kuwa urithi wake.

Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wake,
kabila alilochagua kuwa urithi wake.
Toka mbinguni Bwana anatazama;
anawaona wanadamu wote. K.

Toka mahali pa kikao chake anawachungulia
wote wanaokaa duniani,
yeye aliifinyanga mioyo yao wote,
anayaangalia matendo yao yote. K.

Roho zetu zinamngoja Bwana.
Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Naam, mioyo yetu inafurahi katika yeye.
Tunalitumainia jina lake takatifu. K.

SHANGILIO LA INJILI
LUKA 4:18

K. Aleluya. W. Aleluya.
K. Bwana amenituma kuwahubiria maskini habari njema, na kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao.
W. Aleluya.

SOMO LA INJILI
LUKA 4:38—44

"Imenipasa kuihubiria miji mingine pia; kwa maana nimetumwa kwa agizo hilo."

† Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Luka

Wakati ule: Yesu alitoka katika sinagogi, akaingia nyumba ya Simoni. Mkwewe Simoni alikuwa na homa kali, wakamwomba Yesu amsaidie. Akamwinamia, akaikemea homa, nayo ikamwacha. Mara akasimama, akawatumikia. Jua lilipozama, wote walimletea wagonjwa wao wenye shida mbalimbali. Akamwekea kila mmoja mikono, akawaponya. Pia pepo walitoka kwa watu wengi wakigumia na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu." Naye akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, kwa maana walimjua ni Kristo. Kulipopambazuka, alitoka akaenda mahali pa ukiwa. Watu wengi wakamtafuta, na walipomkuta, wataka kumzuia asiondoke kwao. Akawaambia, "Imenipasa kuihubiria miji mingine pia habari njema ya ufalme wa Mungu, kwa maana nimetumwa kwa agizo hilo." Akaendelea kuhubiri katika masinagogi ya Yudea.

INJILI YA BWANA... SIFA KWAKO EE KRISTO

31/08/2026

MASOMO YA MISA, JUMANNE YA JUMA LA ISHIRINI NA MBILI, KIPINDI CHA KAWAIDA, MWAKA II, SEPTEMBA 1, 2026
RANGI YA KILITURJIA: KIJANI KIBICHI 💚

SOMO LA KWANZA
1 WAKORINTHO 2:10b—16

"Mwanadamu asiye na roho hawezi kupokea vipaji vya Roho wa Mungu; mtu wa kiroho hupambanua vitu vyote."

Somo katika barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho

Ndugu: Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Je, ni mwanadamu gani anayajua yaliyo ya kibinadamu, isipokuwa roho ya mwanadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo hakuna ana-yeelewa yaliyo ya kimungu, isipokuwa Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukupewa roho ya ulimwengu, bali Roho atokaye kwa Mungu, tupate kutambua tuliyojaliwa na Mungu. Hayo ndiyo tunayofundisha, si kwa maneno jinsi hekima ya kibinadamu inavyofundishwa, bali kwa maneno yanayofundishwa na Roho. Basi, tunaelezwa mambo ya kiroho kwa maneno ya kiroho.
Mwanadamu katika maumbile yake hawezi kufahamu mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mambo hayo ni upuuzi. Hawezi kuyafahamu, kwa sababu hayatambulikani ila kwa njia ya Roho.Mtu wa kiroho hutambua yote, lakini mwenyewe hawezi kutambuliwa na wengine. Basi, ni nani anayeweza kuifahamu Roho ya Bwana, apate kumfundisha? Lakini sisi tunaye Roho
wa Kristo.

NENO LA BWANA... TUMSHUKURU MUNGU

ZABURI YA KUITIKIZANA
ZABURI 145:8—9, 10—11, 12—13ab, 13cd—14 (K. 17a)

K. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.

Bwana ni mwenye huruma na mpole,
si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa fadhili.
Bwana ni mwema kwa wote,
na huruma yake i juu ya viumbe vyake vyote. K.

Kazi zako zote zinakutukuza, ee Bwana,
wachaji wako wanakusifu.
Wanautaja utukufu wa ufalme wako,
wanauhadithia uwezo wako. K.

Ili wawajulishe wanadamu matendo yako makuu,
na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
Ufalme wako ni ufalme wa nyakati zote;
na utawala wako wadumu kwa vizazi vyote. K.

Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote,
na mwema kwa kazi zake zote.
Bwana huwategemeza wote wanaoanguka,
huwainua wote waliogandamizwa. K.

SHANGILIO LA INJILI
LUKA 7:16

K. Aleluya. W. Aleluya.
Nabii mkubwa ametokea kwetu, na Mungu amewatembelea watu wake.
W. Aleluya.

SOMO LA INJILI
LUKA 4:31—37

"Ninakujua u nani wewe, ndiwe Mtakatifu wa Mungu."

† Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Luka

Wakati ule: Yesu alishukia Kapernaumu, mji wa Galilaya. Akawafundisha siku ya Sabato, na wakastaajabu kwa mafundisho yake, kwa maana alisema kwa mamlaka. Katika sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho wa pepo mchafu, akalia kwa sauti kubwa akisema. "Oh! Kuna nini kati yetu na wewe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani wewe, ndiwe Mtakatifu wa Mungu!" Yesu akamkemea akisema, "Nyamaza! Mtoke!" Pepo mbaya akamtupa chini mbele yao, akamtoka bila kumdhuru. Wote wakashikwa na bumbuazi wakasemezana, "Maana yake ni nini? Awaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na uwezo, nao hutoka." Na sifa yake ikavuma mahali pote pa jirani.

INJILI YA BWANA... SIFA KWAKO EE KRISTO

31/08/2026

MASOMO YA MISA, JUMATATU YA JUMA LA ISHIRINI NA MBILI, KIPINDI CHA KAWAIDA, MWAKA II, AGOSTI 31, 2026
RANGI YA KILITURJIA: KIJANI KIBICHI 💚

SOMO LA KWANZA
1 WAKORINTHO 2:1—5

"Niliwahubiria Kristo msulibiwa."

Somo katika barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho

Nami, ndugu, nilipofika kwenu, sikuja kuwahubiria fumbo la Mungu kwa fahari ya maneno ya hekima. Nilipokaa kwenu nalitaka nisijue lolote, ila Yesu Kristo, ndiye msulibiwa. Hivyo nilifika kwenu kwa udhaifu na hofu na kutetemeka kwingi. Basi, usemi wangu na mahubiri yangu hayakulenga kuwavuta kwa maneno ya hekima, bali kwa onyesho la Roho na nguvu yake, ili imani yenu isitegemee hekima ya wanadamu, bali itegemee nguvu ya Mungu.

NENO LA BWANA... TUMSHUKURU MUNGU

ZABURI YA KUITIKIZANA
ZABURI l19:97, 98, 99, 100, 101, 102 (K. 97a)

K. Jinsi gani, ee Bwana, ninavyoipenda sheria yako!

Jinsi gani naipenda sheria yako, Bwana:
Ninaitafakari mchana kutwa! K.

Maagizo yako yamenipa hekima kuliko adui zangu,
kwani yapo nami siku zote. K.

Nina hekima kuliko walimu wangu wote,
kwa kuwa mafundisho yako ndivo tafakari zangu. K.

Nawapita wazee kwa akili yangu,
kwa kuwa nazishika amri zako. K.

Naiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,
ili nilifuate neno lako. K.

Siendi mbali na mashauri yako;
kwa kuwa wewe mwenyewe umenifundisha. K.

SHANGILIO LA INJILI
TAZAMA LUKA 4:18

K. Aleluya. W. Aleluya.
K. Roho wa Bwana yu juu yangu; amenituma niwahubirie maskini habari njema.
W. Aleluya.

SOMO LA INJILI
LUKA 4:16—30

"Amenituma niwahubirie maskini habari njema... Nabii hakosi heshima isipokuwa mjini mwake."

† Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Luka

Wakati ule: Yesu alikuja Nazareti, pale alikolelewa, na siku ya Sabato, akaingia katika sinagogi k**a ilivyokuwa desturi yake. Akasimama asome; wakampa kitabu cha nabii Isaya, akakifungua, akakuta mahali palipoandikwa: "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenipaka mafuta niwahubirie maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, vipofu kuona tena, kuwaletea wafungwa uhuru, na kutangaza mwaka uliokubalika kwa Bwana." Akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi, na macho ya wote katika sinagogi yakamkazia yeye. Akaanza kuwaambia, "Leo andiko hili limetimia masikioni mwenu." Wote wakamsifu, wakastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake. Wakauliza, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?" Akawaambia, "Bila shaka mtaniambia mithali hii, 'Mganga, jiponye mwenyewe," na mtasema, Tuliyosikia umefanya Kapernaumu, yafanye na hapa kwako.'" Akaendelea kusema, “Amin, nawaambieni, nabii hakosi heshima isipokuwa mjini mwake. Tena, ni kweli ninayowaambia, palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita hata njaa kali ikaingia nchi nzima. Lakini Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mwanamke mjane wa Zarefathi katika nchi ya Sidoni. Kadhalika, walipatikana wakoma wengi katika Israeli wakati wa nabii Elisha, lakini hata mmoja wao hakutakaswa, ila Naamani, mtu wa Shamu." Hapo wote wenye kusikia hayo katika sinagogi walishikwa na hasira. Wakasimama, wakamchukua mpaka nje ya mji kwenye ukingo wa kilima, ambacho mji wao umejengwa, ili wamtupe chini. Yeye lakini, alipita katikati yao, akaenda zake.

INJILI YA BWANA... SIFA KWAKO EE KRISTO

31/08/2026

READINGS FOR MONDAY OF THE TWENTY—SECOND WEEK IN ORDINARY TIME, YEAR II, AUGUST 31, 2026
LITURGICAL COLOUR: GREEN 💚

FIRST READING

"I proclaimed to you Christ crucified."

A reading from the first Letter of Saint Paul to the Corinthians (1 Corinthians 2:1—5)

When I came to you, brethren, I did not come proclaiming to you the testimony of God in lofty words or wisdom. For I decided to know nothing among you except Jesus Christ and him crucified. And I was with you in weakness and in much fear and trembling; and my speech and my message were not in plausible words of wisdom, but in demonstration of the Spirit and power, that your faith might not rest in the wisdom of men but in the power of God.

THE WORD OF THE LORD... THANKS BE TO GOD

RESPONSORIAL PSALM
PSALM 119:97, 98, 99, 100, 101, 102 (R. 97a)

R/. O Lord, how I love your law!

O Lord, how I love your law:
my meditation all the day! R/.

Your command makes me wiser than my foes,
for it is with me always. R/.

I have more insight than all who teach me,
for I ponder your decrees. R/.

R/. O Lord, how I love your law!

I have gained more understanding than my elders,
for I keep your precepts. R/.

I keep my feet from every evil path,
to obey your word. R/.

I have not turned away from your decrees;
you yourself have taught me. R/.

GOSPEL ACCLAMATION
LUKE 4:18

Alleluia. The Spirit of the Lord is upon me; he has sent me to preach good news to the poor. Alleluia.

GOSPEL READING

“He has sent me to preach good news to the poor. No prophet is acceptable in his own country.”

† A reading from the holy Gospel according to Luke (Luke 4:16—30)

At that time: Jesus came to Nazareth, where he had been brought up; and he went to the synagogue, as was his custom, on the sabbath day. And he stood up to read; and there was given to him the Book of the Prophet Isaiah. He opened the book and found the place where it was written, “The Spirit of the Lord is upon me, because he has anointed me to preach good news to the poor. He has sent me to proclaim release to the captives and recovering of sight to the blind, to set at liberty those who are oppressed, to proclaim the acceptable year of the Lord.” And he closed the book, and gave it back to the attendant, and sat down; and the eyes of all in the synagogue were fixed on him. And he began to say to them, “Today this Scripture has been fulfilled in your hearing.” And all spoke well of him, and wondered at the gracious words which proceeded out of his mouth; and they said, “Is not this Joseph’s son?” And he said to them, “Doubtless you will quote to me this proverb, ‘Physician, heal yourself; what we have heard you did at Capernaum, do here also in your own country.”’ And he said, “Truly, I say to you, no prophet is acceptable in his own country. But in truth, I tell you, there were many widows in Israel in the days of Elijah, when the heaven was shut up three years and six months, when there came a great famine over all the land; and Elijah was sent to none of them but only to Zarephath, in the land of Sidon to a woman who was a widow. And there were many lepers in Israel in the time of the prophet Elisha; and none of them was cleansed, but only Naaman the Syrian.” When they heard this, all in the synagogue were filled with wrath. And they rose up and put him out of the city, and led him to the brow of the hill on which their city was built, that they might throw him down headlong. But passing through the midst of them he went away.

THE GOSPEL OF THE LORD... PRAISE TO YOU LORD JESUS CHRIST

CONGRATULATIONS, REV. FR. DR. WILLIAM KOSGEIHeartfelt congratulations to Rev. Fr. Dr. William Kosgei as he celebrates hi...
30/08/2026

CONGRATULATIONS, REV. FR. DR. WILLIAM KOSGEI

Heartfelt congratulations to Rev. Fr. Dr. William Kosgei as he celebrates his Silver Jubilee 25 years of dedicated priestly ministry.

We thank God for your faithful service, spiritual leadership and commitment to His people. May the Lord continue to strengthen you, bless your ministry and grant you many more joyful and fruitful years in His vineyard.

Happy Silver Jubilee, Father! Ad Meliora!

29/08/2026
29/08/2026

*SOMANUTIKAP MISA NE TILIL NEPO JUMAPILI, TARIKIT 30/08/2026*

*JUMAPILITAP TIPTEM AK AENG' NEPO KENYITAP A NEPO KANISA*

*NGORYEETAP MISA: NE NYALIL 💚*
*YAUTIK CHEBO ROSARI 📿: CHEPO KALASUNET*

*SOMANET NE TAI*
*JEREMIAH 20: 7-9*

*_Somanet ne tai koyob kitabutap Maotyot Jeremiah_*

Ee Cheptalel, ki iberbera, ak ki aberberage: ii kiim isiira, ak ki iterteerisye: kaaegu ne kirorechin peetuut komugul, churochura age tugul. Amu kotugul ye ang'alaali, awaache; awaache ale, Koroomnateet ak luuleet: amu kagiyai ng'olyootap Kamuktaindet ne Toroor koek chotisyet eng' anee, ak aegu ne kirorechin eng' peetuut komugul. Ak ngot amwa ale, Ma mwaei kiy agobo ineendet, anan ang'alaal eng' kainennyi, kobiit anyun eng' muguleldanyu ko uu maat ne lalei eng' kawekyuk, ak ang'et eng' muitaet, ak ma muuchi asiis.

_*Ng'olyotab Cheptalel: Kiwekyini Cheptalel kongoi*_

*TYENDAP KALASUNET*
*TYENWOGIKAP KALASUNET 63: 2, 3-4, 5-6, 8-9 (W. 8bc)*

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

Ee Kamuktaindet, inyee ko ii Kamuktaindennyu;
acheeng'in eng' kagiiletapkei;
Amei melelda saboondanyu amu machin, machin kot poortanyu

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

Eng' emet ne yaamaat ne po ng'etatet, ole ma mi peek.
Ara uu nooto koageerin eng' ole-tiliil, si ageer kimnateng'ung' ak toroornateng'ung'.
Amu myee chamyeng'ung' ne tala kosiir saboondo;
ilasun anyun kutinnyu.

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

amu ki iegu toretindennyu, abaibai anyun eng' urwetap kebebaiguk.
Isubotin saboondanyu miising';
nama eung'ung' ne po tai.

*WOLUNET: _Ee Cheptalel, iboorwech rireeneng'ung', ak igoonech yetuneng'ung'_*

*SOMANETAP AENG'*
*ROMANIK 12: 1-2*

*_Somanetap aeng' koyob baruetab koyoktoindet Paulo ne kisirjin Romanik_*

Nooto anyun che kitupche, asoomok miising', eng' rireenosyegap Kamuktaindet ale, ogoite poorwekwok koek tiseiywot ne sabei, ne tiliil, ne taachaksei eng' Kamuktaindet, nooto ko poisyeng'wong' ne nyolu. Amoyaniegei ateptap peetuusyechu: ago ingewalak eng' kaleelitetap kabwaatutikwok, si kobiit onai komyee mageet ne myee ne po Kamuktaindet, ne tachaksei ak kogesunotkei.

_*Ng'olyotab Cheptalel: Kiwekyini Cheptalel kongoi*_

*KATORORETAP LOGOIYWEK CHE MYACH*
*EPESOEK 1: 17-18*

_*Aleluya! Aleluya!*_

Ingogoonech Kamuktaindet ne po Kiptaiyandennyo Jeso Kristo, kokweng'ogis konyegap mugulelwekyok si kobiit kenai kiit ne uu k**ang'unetap kuursennyi

_*Aleluya! Aleluya!*_

✝️ *INJILI* 📖
*MATAYO 16: 21-27*

_*Logoiywek che myach kouu ye kisir Matayo ne Tiliil: Ilosunot ee Kiptaiyat*_

Kobooch yooto anyun, kotoi Jeso koboorchi kasubikyik kole wendi ineendet Jerusalem, ak nyooru kanyaliilet ne oo eng' eunegap poisyek, tisiik che eecheen ak siriik, ak kebar, ak eng' peetuutap somok, king'eet. Ki nam Petero ineendet komut taban ak kotoi koger kong' koleen, “Achicha Kiptaiyat! Ma nyoonjin niito agoi.” Ago kiweleljigei ak koleenji Petero, “Istoenongei, Setani! Ii kanagut eng' anee; amu ma ibwaati inyee tuguugap Kamuktaindet, ago ibwaati che po kipkosabei.”
Kingo pata koleenji Jeso kasubikyik, “Ngo machei chii kosubwo, ko nyolu koeesyogei, ak kosut koip kimurtoiyondennyi, ak kosubwo. Amu age tugul ne machei kosar saboondanyi, kobeeti, ak age tugul ne ibeeti saboondanyi agobo anee, konyooru. Keljino nee ne nyooru chii, ngo nyoor ng'wony komugul, ak kobeet saboondanyi? Anan tos igoito nee chii kowale saboondanyi? Tuun nyoonei Weeriitap chii eng' liilindap Kwandanyi kobooto malaikaisyekyik, ak kogoochi chii age tugul ko uu poisyonikyik. ”

*_Logoiywek che myach chebo Cheptalel: Neng'ung'et katororet ee Kristo_*

THOUSANDS OF CWA MEMBERS IN KAPSABET DIOCESE CELEBRATE THE FEAST OF ST. MONICAThousands of Catholic Women Association (C...
29/08/2026

THOUSANDS OF CWA MEMBERS IN KAPSABET DIOCESE CELEBRATE THE FEAST OF ST. MONICA

Thousands of Catholic Women Association (CWA) members from across the Catholic Diocese of Kapsabet gathered in faith and unity to celebrate the Feast of St. Monica a joyful occasion dedicated to prayer, family and Christian perseverance.

The Holy Mass and celebrations were presided over by Rt. Rev. John Kiplimo Lelei, Bishop of the Catholic Diocese of Kapsabet

The celebration provided an opportunity for the faithful to honour St. Monica, whose life remains a powerful example of persistent prayer, patience, hope and unwavering faith in God.Her witness continues to inspire Christian mothers and families to remain steadfast in prayer, even amid life's challenges.

The occasion also highlighted the important role of Catholic women in nurturing strong families, passing on the faith to future generations and building united, values-driven Christian communities.

May the intercession and example of St. Monica continue to inspire all mothers and families to persevere in faith, hope and prayer, and to strengthen our homes and communities through love, service and devotion to God.

St. Monica, pray for us!

Address

Kaptendon
Kapsabet
30300

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when St Jude Catholic Church, Kaptendon posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to St Jude Catholic Church, Kaptendon:

Shortcuts

Share