05/12/2020
*MASOMO YA MISA,DECEMBA 06, 2020*
*DOMINIKA YA 2 MAJILIO MWAKA B.*
*MWANZO:*
*Isaya 30:19,30*
*_Enyi watu wa sayuni, Tazama Bwana anakuja kuziokoa Nchi.na Bwana atafanya utukufu wa sauti yake isikike ndani ya mioyo yenu._*
*SOMO 1.*
*Isaya 40:1-5,9-11.*
Watulizeni mioyo, watulizeni mioyo, watu wangu, asema Mungu wenu.
Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake zote.
Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye,
Itengenezeni nyikani njia ya BWANA;
Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Kila bonde litainuliwa,
Na kila mlima na kilima kitashushwa;
Palipopotoka patakuwa pamenyoka,
Na palipoparuza patasawazishwa;
Na utukufu wa BWANA utafunuliwa,
Na wote wenye mwili watauona pamoja;
Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.
Wewe uuhubiriye Sayuni habari njema,
Panda juu ya mlima mrefu;
Wewe uuhubiriye Yerusalemu habari njema,
Paza sauti kwa nguvu;
Paza sauti yako, usiogope;
Iambie miji ya Yuda, Tazameni, Mungu wenu.
Tazameni, Bwana Mungu atakuja k**a shujaa,
Na mkono wake ndio utakaomtawalia;
Tazameni, thawabu yake i pamoja naye,
Na ijara yake i mbele zake.
Atalilisha kundi lake k**a mchungaji,
Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake;
Na kuwachukua kifuani mwake,
Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.
*Neno la Bwana.......Tumshukuru Mungu.*
*ZABURI YA KUITIKIZIANA.*
*Zaburi 85:8-13*
*(K).Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, utupe wokovu wako.*
Na nisikie atakavyosema Mungu BWANA,
Maana atawaambia watu wake amani,
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.(K).
Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amani zimehusiana.
Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni.(K).
Naam, BWANA atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia.(K).
*SOMO 2.*
*2 Petro 3:8-14.*
Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamb