Joy of the Catholic Life

Joy of the Catholic Life Reflections and Articles to renew and inspire Catholic Living. Page Editors:
Fr. Regan D'souza,

Contributors:
Fr. Regan D'souza, OCD, Carmelite
Fr.

Sandeep Kumar, OCD, Carmelite

Design Lead: Fr. Regan D'souza,

ASALI ITOKAYO MWAMBANI”Tafakari ya kila sikuIjumaa, Januari 27, 2023Juma la 3 la Mwaka wa KanisaEbr 10: 32-39;Zab 37: 3-...
26/01/2023

ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Januari 27, 2023
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa

Ebr 10: 32-39;
Zab 37: 3-6, 23-24, 39-40;
Mk 4: 26-34

MBEGU ZA UFALME WA MUNGU!

Leo Yesu anaelezea habari ya mtu anaye mwaga mbegu zake ardhini. Ikisha oteshwa, anasubiri mpaka itakavyo ota na kukuwa na kutoa mavuno. Haelewe ni kwa jinsi ghani zinavyokuwa, lakini siku ya mavuno ifikakapo anavuna. Yesu pia anaongea kuhusu mbegu ya haradali. Hii ni ndogo sana lakini ina utajiri ndani yake. Hii mbegu pamoja na kwamba ni ndogo sana ina utajiri ndani yake ya kuweza kuwa mti mkubwa, na kuwa chanzo cha chakula kwa ajili ya ndege na sehemu ya kupumzikia ya ndege.

Huu ni ni kukweli unao dhihirisha kwamba Yesu anapenda kumtumia kila mmoja wetu katika kujenga ufalme wake. Tunaweza kujisikia kwamba hatuwezi kufanya mengi sana, na kwamba hatuja pewa vipaji vingi k**a wengine, na kwamba hatuwezi kuleta mabadiliko makubwa, lakini hii sio kweli. Ukweli ni kwamba kila mmoja wetu amepewa vipaji vingi vya ajabu na Mungu ambavyo Mungu anapenda vizae matunda. Anataka alete kutoka ndani mwetu vitu vya utukufu kwa ajili ya Ulimwengu. Tunachopaswa kufanya ni kumruhusu yeye afanye kazi ndani yetu. K**a mbegu, tunapaswa tujiruhusu wenyewe kujiotesha kwenye udongo wa huruma yake kwa njia ya Imani na kujikabidhi kwenye mapenzi yake. Tunapaswa tujimwagilie kwa sala za kila siku na kuruhusu mwanga wa wake utuangazie ili aweze kuvuna matunda apendavyo kutoka ndani yetu na alicho otesha tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Ametufanya sisi kwa lengo la kuleta Ufalme wake ndani yetu. Ni jukumu letu kumruhusu Mungu afanye yote ndani yetu ambayo amepanga katika maisha yetu.

Sala: Bwana, nakupenda na ninakushukuru kwa yote uliotenda katika maisha yangu. Ninakushuru kwa namna ya pekee, kwa yote, ambayo najua utatenda katika maisha yangu. Ninakuomba ili niweze kujikabidhi kwako, ili uweze kunitakasa mimi kwa neema yako, naomba ulete katika maisha yangu matunda mema. Yesu nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2017 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

26/01/2023

MASOMO YA MISA, JANUARI 27, 2023
IJUMAA, JUMA LA 3 LA MWAKA

SOMO 1
Ebr. 10:32 – 39

Zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu; pindi mlipotwezwa kwa mashutumu na dhiki, na pindi mliposhirikiana na wale waliotendewa hayo. Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. Basi msiutupe ujasiri wetu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa Imani; naye akisitasita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na Imani ya kutuokoa roho zetu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 37:3 – 6, 23 – 24, 39 – 40 (K) 39

(K) Wokovu wa wenye haki una Bwana.

Umtumaini Bwana ukatende mema,
Ukae katika nchi upendezwe na uaminifu.
Nawe utajifurahisha kwa Bwana,
Naye atakupa haja za moyo wako. (K)

Umkabidhi Bwana njia yako pia umtumaini
Naye atafanya;
Ataitokeza haki yako k**a nuru,
Na hukumu yako k**a adhuhuri. (K)

Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana,
Naye aipenda njia yake.
Ajapojikwaa hataanguka chini,
Bwana humshika mkono na kumtegemeza. (K)

Wokovu wa wenye haki una Bwana,
Yeye ni ngome yao wakati wa taabu.
Naye Bwana huwasaidia na kuwaopoa,
Huwaopoa na wasio haki na kuwaokoa,
Kwa kuwa wamemtumaini Yeye. (K)

SHANGILIO
1Thes. 2:13

Aleluya, aleluya,
Lipokeeni neno la Mungu, siyo k**a neno la wanadamu, bali k**a neno la Mungu.
Aleluya.

INJILI
Mk. 4:26-34

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Ufalme wa Mungu, mfano wake ni k**a mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. Hata matunda yakiiva, mara aupeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika.

Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? Ni k**a punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi, lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.

Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulisikia; wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

26/01/2023
20/12/2022

VISIT https://www.facebook.com/Furaha.Katoliki for future posts

Ukurasa huu ni marejeo ya uwezo wa furaha ya Kikristo. Itakuwa na nukuu za Baba Mtakatifu Fransisko pamoja na mahubiri na masomo ya kila siku na mambo mbalimbali ya Kikatoliki. Kikatoliki.

Ukurasa Wahariri:
Pd. Regan D'souza, (Mkarmeli)
Pd. Sandeep Kumar (MKarmeli),

Design Meneja:
Pd. Regan D'souza, (Mkarmeli)

Address

Bangalore

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Joy of the Catholic Life posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Place Of Worship

Send a message to Joy of the Catholic Life:

Share