14/05/2024
VITA VYA KI-MIUNGU VILIVYOPO KWA MZALIWA WA KWANZA, K**A LANGO LA WAZALIWA WENGINE
BWANA YESU ASIFIWE WANA WA MUNGU, Namshukuru Mungu sana kwa ajili ya wakati huu mzuri na kwa ajili yako wewe uliyekuwa tayari kusoma fundisho hilo, ambalo baada ya kujifunza hautabaki k**a jinsi ulivyo katika jina la Yesu Kristo.
Wote tunajua tunaposema mzaliwa wa kwanza ni nani, katika familia yako uliyozaliwa kuna mzaliwa wa kwanza yamkini ni wewe unayesoma ujumbe huu, tunasema mzaliwa wa kwanza ni lango kwa sababu anakuwa yeye ndiye wa kwanza kufungua tumbo la mama yake na kuwa lango, kuruhusu wazaliwa wengine kufuatia. Katika ulimwengu wa roho kuna maana kubwa sana na watoto hawa wanakuwa wamebeba Baraka kubwa sana ambazo zinatiririka hadi kwa wazaliwa wanaofuata. Kwa kuwa wamebeba umaana wa Baraka za Mungu. Kitabu cha KUTOKA 13:1-2 “Bwana akasema na Musa, akamwambia Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israel, wa binadamu na wa mnyama;ni wangu huyo.” Mungu, anasema na Musa awatakase wazaliwa wa kwanza wote, akisema wote hao ni wa kwake, wazaliwa wa kwanza wamebeba umaana mkubwa sana mbele za Mungu kwa sababu kupitia mzaliwa wa kwanza Mungu anapata uhalali wa kutawala familia ile yote.
Kwa nini watoto hawa wanakuwa na vita sana, ni kwa sababu wanapiganiwa/wanatafutwa na pande tatu (3), pande ya kwanza mtoto huyu anapiganiwa na Mungu mwenyewe aliye hai, pande ya pili, anatafutwa na miungu upande wa baba yake, na pande ya tatu anatafutwa na miungu ya upande wa mama yake. Mzaliwa wa kwanza anapitia vita vikubwa kwa sababu amebeba vifuatavyo:- amebeba Nembo ya familia, familia hiyo hutambulishwa kupitia yeye, Ni mteule wa Mungu, amebeba kusudi (Israel), mzaliwa wa kwanza husahihisha makosa ya familia, kuwasaidia wadogo zake, Mungu humpa kipawa cha uongozi, kuwaongoza wanamfuata njia iliyo sahihi, ana neema ya utajiri, ila aweze kuwainua wadogo kimaisha kwa ujumla.
Ukisoma kitabu cha Kutoka 4:22-23 “Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israel ni mwanangu mimi, MZALIWA WA KWANZA WANGU, nami nimekuambia, mpe ruhusa aende ili apate kunitumikia nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako. ‘’ …….kwa Mungu, Israel ni mzaliwa wa kwanza, huyu ndiye aliyebeba ukombozi wa ulimwengu, ukisoma maandika utaona Bwana wetu Yesu Kristo ametoka katika ukoo wa Daudi, ambapo asili ni mzaliwa wa kwanza, Israel. Vita hivi vya mzaliwa wa kwanza havijaanza leo, vipo tokea enzi ya ukombozi wa wana wa Israel. Kiroho, unaweza kuona Farao aling’ang’ana na kuwak**atia wana wa Israel ili wafanyike kuwa watumwa, hapana, alipambana ili kuzuia kusudi la Mungu lililobebwa ndali ya wana wa Israel, katika harakati za ukombozi wa ulimwengu mzima, kupitia Yesu Kristo.
Ukisoma tena, Kumbu. La torati 12:2..”Vunjeni kabisa mahali pale walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki”………..hii ni maadhi ya amri alizokuwa anatoa Bwana kwa wana wa Israel, mzaliwa wa kwanza wake….katika koo nyingi katika maisha ya sasa bado kunakutawaliwa na miungu, miungu hii inaweza ikawa ni ya upande wa baba au wa mama, ambayo bado imebema ile vita ya mzaliwa wa kwanza, miungu inapambana na mzaliwa wa kwanza katika familia kwa sababu amebeba Baraka ambazo zinashuka kwa wanaofuata na familia mzima.
Kuna baadhi ya familia, wazaliwa wao wa kwanza wanapitia katika changamoto kubwa za kimaisha, maisha yake hayaeleweki, hana kinachoendelea katika maisha yake, na wengine hata kuachia shule njiani, wengine wamesoma lakini hawana wanachojivunia, wengine ni maprofesa kabisa lakn ukiangalia maisha wanayoishi huoni k**a vinaendana, wengine wamek**atwa kwenye uzizi, wengine kwenye magonjwa, wengine kwenye mitala, kwenye pombe kupita kiasi, umasikini, utasa, nk. Kuna watoto Mungu ameachilia Baraka kubwa katika kuzibeba familia zao, kuzisaidia, lakini maisha ya huyo mtu yameshikiliwa na kuruhusu familia kubaki masikini, kuna watu ni wakubwa sana katika nchi hii, yamkini kwenye siasa, biashara, kwenye huduma, kazi, nk. lkn huoni wakiishi maisha yale Mungu amekusudia kuishi.
Mzaliwa huyu wa kwanza, anakuwa amek**atwa na miungu, kwa sababu akik**atwa yeye familia nzima inakuwa imek**atwa ili kuharibu lile kusudi la Mungu lilibebwa na familia husika. Mtoto huyu akifunguliwa, basi wote wanaofuta wanakuwa wemefunguliwa hata wale wa uzao wake. Wakati mwingine wadogo wanamuangalia mkubwa wao mzaliwa wa kwanza, wanaiga maisha yake, hivyo k**a anaishi maisha ya Baraka, hivyo wadogo wanarithi matendo ya mkubwa wao, ikitokea sasa maisha anayoishi ya hovyo, wadogo nao yamkini wakafuta hivyo, kwa sababu ya ile roho ya laana aliyeachiwa mzaliwa wa kwanza. je,? ulishawahi kuona mzazi anaishi maisha ya mitala, na watoto wanaishi maisha hayohayo?
Nini ufanye, fanya maombi ya kuita damu ya Yesu ipite kila mahali uliposhikiliwa, ita damu ya yesu ikutenganishe wewe na nguvu za kimiungu zilizokushikilia, Wakolosai 1:19-20 “kwa kuwa katika yeye (Yesu) ilipendeza utimilifu wote ukae, na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiishakufanya amani kwa DAMU ya msalaba”, Damu ya yesu Kristo hutengeneza agano jipya kati yako na Mungu, ukiisha kufanya agano kwa damu ya Yesu, miuungu haitakuwa na uhalali tena katika maisha yako..kitabu cha Marko 14:24 “akawaambia, hii ndiyo DAMU yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi”…….maombi yako yaambatane na kutoa SADAKA, toa sadaka kwa ajili ya ukombozi wako, k**a wewe nimzaliwa wa kwanza, pia unaweza kutoa sadaka kwa ajili ya mwanao ambaye ni mzaliwa wa kwanza…soma KUTOKA 13:13 “kila mzaliwa wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana- kondoo, na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa”. Unadhani kwa nini Mungu alisema haya? Mungu anajua mzaliwa wa kwanza amebeba uthamani gani kwake yeye Mungu kwanza lakini pia kwa familia kwa ujumla. Soma pia. Kumbu. 21:16,17
Nikurudishe katika neno hili KUTOKA 13:1-2 “Bwana akasema na Musa, akamwambia Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israel, wa binadamu na wa mnyama;ni wangu huyo.”…hapa mnyama ametajwa katika mzaliwa wa kwanza, mnyama hapa anaweza pia kuwa kiwakilishi cha mali zako zote unazozianzisha kwa mara ya kwanza, mfano unataka kufungua biashara, biashara inaweza kuwa mzaliwa wa kwanza katika maisha yako, je, unatoa sadaka ya ukombozi kwa ajili ya hiyo biashara? Inaweza ikawa ni biashara, kazi, ndoa yako, mifugo nk. Hivyo, katika kuomba sio tu unaomba kwa ajili ya binadamu, omba na toa sadaka kwa ajili ya dhughuli zako unazozianzisha.
MUNGU AKUBARIKI MWANA WA MUNGU.
SOMO LINALOFUATA, VITA VYA ROHONI VILIVYOPO JUU YA MTU ANAYEPATA NEEMA YA WOKOVU NA NINI AFANYE ILI KUSHINDA VITA HIVYO. Usiapange kukosa.
HAULE JP-0767 565834