15/01/2023
Mchungaji Felisiana christopher mwingira.
SOMO:MATARAJIO YA MLANGO WA KUPOKEA.
Ebrania11:1.'Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana".
Katika imani tunatarajia kupokea jambo toka mungu. Mwaka huu ni mwaka wa kudunda dunda juu
Yale waliyokuumiza yaone k**a si kitu kwako ,mungu wetu yupo na anaweza.Imani ni mungu na chochote utakachokiomba leo kitatokea.
Tarajio langu ni kusoma hadi chuo kikuu na kupata kazi nzuri na kuwalea wazazi wangu kwasababu mungu anaweza kufanya.
Warumi.1:20-22 .Na k**a walivyokataa kuwa na mungu katika fahamu zao mungu aliwaacha wafuate hakiakili zao sisizofaa.
Kwasababu ya mawazo ya hakili isiyofaa inakupa wewe kutokuwa na matarajio yako katika maisha, lakini ukikubali hakili yako iongozwe na mungu ba si utakuwa na mawazo na matarajio mazuri na yenye kutimia
Na changamoto kubwa ni kwamba sisi wenyewe huwa tunajiwazia na kujitamkia vibaya kuhusu maisha yetu, lakini k**a ukijitamkia na kujiwazia mema kila iitwapo leo utapokea kile unachokitarajia.
Maneno yako lazima yakubaliwe na tena lazima yaendane nakile unachokifanya.
Zaburi 19:14.Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu yapate kibari mbele zako ee BWANA mwamba wangu na mwokozi wangu.