22/07/2025
𝗕𝗨𝗦𝗧𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗘𝗗𝗘𝗡𝗜 – 𝗠𝘂𝗻𝗴𝘂 𝗮𝗹𝗶 𝗮𝗻𝗱𝗮𝗮 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝗸𝗶𝘁𝘂 𝗸𝗮𝗯𝗹𝗮 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗸𝘂𝘂𝗺𝗯𝗮 !
Kabla Mungu kuumba mwanadamu, alitengeneza kwanza Bustani ya Edeni, akajaza humo kila kitu mtu angehitaji. Hakukuwa na ombi, shida, au mahitaji—byote bilikua tayari.
Na hata leo, byote unabyomwomba Mungu biko tu hapa duniani : mke mwema, kazi, afya, nyumba, heshima, amani—biko. Mungu alishaviweka tayari.
Lakini angalia : Adam na Eva waliishi humo, hadi walipomkorofisha Mungu. Ndio, wakaondolewa. Na kuanzia hapo, malaika mwenye upanga aliwekwa kulinda bustani, ili asiingie tena mtu yeyote atakaye tumia baraka hizo bila kumpa Mungu nafasi yake.
➡️ Edeni ni jumla ya byote Mungu alitengeneza kwa ajili ya mwanadamu kuishi maisha mazuri chini ya jua. Lakini kila mtu ana “malaika wa kuzuia”, na huyo malaika anakuzuia kufikia vitu fulani kulingana na nafasi unayompa Mungu ndani ya maisha yako.
Usinieleze k**a watu wa dunia wana mali—wanaipata, lakini hawaifurahii. Ni baada ya kuwa na utajiri ndipo magonjwa yanakuja : diabète, cancer, goutte, tension...
🚫 Uko na ng’ombe 500, lakini daktari amekuzuia kula nyama.
🚫 Uko na magari kibao, lakini afya imechoka—umeambiwa utembee kwa miguu.
🚫 Una pesa, lakini hakuna mtoto wa maana wa kukurithi; au ulionao hawana hekima—wataharibu yote uliojenga.
Lakini wewe sikiya !
Kitabu cha Mhubiri kinasema:
« Hakuna jambo jema chini ya jua k**a kula, kunywa na kufurahia matunda ya kazi yako… maana hiyo ndiyo sehemu Mungu aliyompa mwanadamu. »
Lakini usisahau kwamba ili kufurahia maisha kikamilifu, ni lazima umpe Mungu nafasi yake k**a Mwokozi na Bwana wa maisha yako — Yeye ndiye atawale juu yako, siyo ukabila, siyo uchoyo, siyo wivu, wala tabia mbaya yeyote ile.
Pia wekeza katika mambo ya thamani kweli: kazi ya Mungu. Weka hazina yako mbinguni, kwa maana unapo pita majaribu, Mungu atakumbuka maombi na sadaka zako ulizo zifanya kwa moyo.
Matendo ya mitume 10:4
Kumbukumbu hii maalum hugusa moyo wa Mungu, na kumu shawishi kuingilia kati katika nyakati zako ngumu.
🙌 Mungu akupe raha, ule kubyako, ufurahie kazi ya mikono yako. Upate vyote unavyohitaji na uvitumie kwa utukufu Wake, bila masharti wala mateso.