Groupe De Prière et D'Evangélisation AGAPE

Groupe De Prière et D'Evangélisation AGAPE Vitu Ambavyo Tulipaswa Kujua Tangu Utoto Wetu Katika Kristo, Yesu ni Rafiki Asiyeondoka Kamwe.

Isaya 60 : 1-5
15/11/2024

Isaya 60 : 1-5

Majira yanapobadilika haitafsiri kuwa umelaaniwa. Mungu alisema Usiku na Mchana havitakoma Kadri nchi idumupo, kazi yetu...
12/05/2023

Majira yanapobadilika haitafsiri kuwa umelaaniwa. Mungu alisema Usiku na Mchana havitakoma Kadri nchi idumupo, kazi yetu ni kujua ikiwa mchana tufanyenini ili usiku ukija tusikose kuona.

Zaburi 1:2-3
[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

[3]Naye atakuwa k**a mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.

Tunapoitafakari sheiria haibadilishi majira ila kutafakari kunatubadilisha sisi tunakuwa k**a mti uliopandwa kando ya mto uzaao MATUNDA yake kwa MAJIRA yake na wala Jani lake halinyauki in all seasons, na kila tufanyalo LITAFANIKIWA.

Ndugu zangu niwatie moyo TAABU yetu ya KUMTAFUTA MUNGU sio BURE, Wengine mmesimama mwanzo wa ibada mpaka mwisho, nawaambia kweli one day it will show, Mungu anaiona kiu yetu na anaiona bidii yetu ya kumpenda, kokote ulipokaa kwenye ibada Neema ya Mungu imeachiliwa juu yetu na tutamuona Bwana.

Kuna sababu kwanini Yesu anashughulika na mioyo ya watu kuliko matendo yao. Injili haiendi kwenye kukemea vitendo peke y...
05/05/2023

Kuna sababu kwanini Yesu anashughulika na mioyo ya watu kuliko matendo yao. Injili haiendi kwenye kukemea vitendo peke yake injili inaenda kwenye moyo na kuupa moyo habari njema ya tumaini nakuuonesha moyo kuna maisha bora kuliko haya ya sasa unayoyazalisha.

Watu wengi tusichojua MOYO ni CHEMCHEM ya yote yanayotendwa na mtu, Biblia inasema Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo.... mpaka anasema hivyo maana yake tunapaswa tulinde mioyo ya watoto wetu kuliko hata maadili yao, Linda moyo wa mtu kuliko mwili wake, Linda moyo maana huko ndiko zitokako Chem Chem za uzima(issues of life) Mithali 4:23.

Haya maneno ya Linda sana moyo aliyasema king 🤴 Solomon, huyu hakuwa kiongozi wa kidini ila ni kiongozi wa kisiasa kwenye nchi ambayo Mungu aliichagua iwe kioo cha namna ambavyo anaishi na kanisa lake, this man was give alot of wisdom na Mungu kiasi kwamba alikuwa anauwezo wa kuwa na majibu ya maswali mengi sana duniani na watu walitafuta maji kutoka kwenye kinywa chake sasa huyu ni zaidi ya philosophers waliosoma vitabu vingi sana vya research na hapa anatoa ushauri anasema LINDA SANA MOYO WAKO...

Anajua kinachomfanya mtu akengeuke ni issue za moyoni. Nchi hii siku watu wakaacha kuumizana mioyo tutakuwa na taifa bora sana. Nchi za watu vijana wamekengeuka wamekuwa wa hovyo si kwasababu hawana maadili Nooo, most of them mioyo imeumizwa so wanaamua kufanya wanayoyataka, broken-hearted person ni mbaya kuliko mtu yoyote, so unaweza ukawa una address issue ya ujambazi, USHOGA, Ulevi, USAGAJI ,uzinzi au unyanyasaji wa kijinsia kumbe issue ni mioyo. Tiba ikipatikana moyoni watu wanabadilika. Tabia haitengenezwi kwenye ubongo tabia inatengenezwa moyoni.

Yesu alikuja kuikoa mioyo kwanza. Mahali pengine neno linasema "Mwanangu nipe MOYO wako Nikuokoe" mtu aliye na ulevi Akipona moyo, pombe Ina kata yenyewe. Kuna watu mioyo imejaa hofu so wanalazimika kufanya vitu viovu ili tu kuridhisha hofu ya moyo. Nchi hii people are bullying each other, watu wanaona ni furaha kudhalilishana ili tu waonekane wananguvu, hii yote ni kuiua mioyo, bila kujua tunazidi kuuana. Biblia inasema KWA MOYO mtu huamini, sio kwa Ubongo....

Just a Polite Reminder...2WAKORINTHO 1:11-12
04/05/2023

Just a Polite Reminder...
2WAKORINTHO 1:11-12

Mara nyingi, mwanzo wa safari zetu, mambo yanaweza yasiwe mazuri sana au yasiende jinsi tulivyotarajia. Wakati mwingine,...
02/05/2023

Mara nyingi, mwanzo wa safari zetu, mambo yanaweza yasiwe mazuri sana au yasiende jinsi tulivyotarajia.

Wakati mwingine, maendeleo yanaweza yasiwe ya kutia moyo na tunahisi kukatishwa tamaa, kudharauliwa, kufadhaika na tunakaribia kukata tamaa.

Kuna wakati tunajisikia huzuni tunapoanza kupima maendeleo yetu na ya wengine na tunachokiona ndani yetu ni kushindwa.

Sikia!
Acha nikutie moyo usiku wa leo, haijalishi ulianza vipi...kinachojalisha ni jinsi unavyomaliza!

Mchakato wa safari na matokeo ya mafanikio sio sawa kwa kila mtu.

Usijilinganishe na wengine ... kwa sababu, hujui jinsi walivyoanza, wawezeshaji na vifaa vilivyopatikana kwao kufanya safari yao kuwa laini k**a unavyoona.

Au hata k**a unajua na unavyo vyote, kuna kitengo kinachoitwa “WAKATI”. Kila mtu ana wakati wake..

Kuwa mvumilivu na mchakato wako mwenyewe, jitolee kwenye kazi zako na uwe na bidii ... muda si mrefu, utastaajabishwa na jinsi mambo yatakavyokuwa, na utaangalia mchakato jinsi ulivyoanza, na kuwa na furaha sana jinsi safari inavyoisha.

Mwisho wake "utakuwa" bora kuliko mwanzo wake ... kuwa mwangalifu ili umalize vizuri.

Endelea kusonga mbele hadi ufikie mwisho uliofikiria. Kuna ukuu mkubwa mwishoni k**a utaendelea hadi mwisho.

Kwa sababu ya MUNGU chochote kitakachojaribu kusimama kinyume chako hakitafanikiwa kwa jina la Yesu...!Kwa sababu ya MUN...
13/04/2023

Kwa sababu ya MUNGU chochote kitakachojaribu kusimama kinyume chako hakitafanikiwa kwa jina la Yesu...!

Kwa sababu ya MUNGU kila mipango ya siri inayopangwa na adui zako, kila mipango ya siri inayopangwa na kuzimu ili ikudhoofishe kiroho, kimwili, ki-akili, ki-uchumi haitafanikiwa kwa jina la Yesu...!

Kwa sababu ya MUNGU kila mishale iliyoelekezwa kwako kujeruhi na kushambulia nafsi, moyo, mwili, familia yako, ndoa yako, uchumi wako, mahusiano yako, elimu yako, taaluma yako n.k ....INARUDI KWA ALIYEITUMA KWA JINA LA YESU...!

Kwa sababu ya MUNGU utaishi kutimiza kusudi lake na lako hapa duniani...Maisha yako hayatakatishwa kabla ya kutimiza kusudi lake na lako.

Kwa sababu ya MUNGU utafika walikosema hutafika na Mungu atakupa hatua kubwa za kiroho na kimwili ambazo hawakutarajia....

Kwa sababu ya MUNGU UTASHINDA VITA VYOTE...Haijalishi ni vita ya kiroho au ya kimwili,...UTASHINDA KWA KISHINDO kwa jina la YESU...!

USIOGOPE....INUA KICHWA CHAKO NA TEMBEA KWA UJASIRI UTIMIZE NDOTO YAKO, MAANA MUNGU YU PAMOJA NAWE KUKUSAIDIA...🙏🙏!

●Kumbukumbu la Torati 28:7,"BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba."

●Zaburi 7:15-16,"Amechimba shimo, amelichimba chini sana, akatumbukia katika handaki aliyoifanya.Madhara yake yatamrejea kichwani pake, na dhuluma yake itamshukia utosini."

●Isaya 54:17,"Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa..."

Isaiah

Vitu ambavyo tulipaswa kujua tangu utoto wetu katika Kristo,  Yesu ni rafiki asiyeondoka kamwe. In the matter of Fact si...
08/03/2023

Vitu ambavyo tulipaswa kujua tangu utoto wetu katika Kristo, Yesu ni rafiki asiyeondoka kamwe. In the matter of Fact sisi wajibu wetu ni kuuamini uwepo wake tusiouona kwa macho ila upo katika maisha yetu.

Kwake Yesu tunalo Tumaini la kuona kesho zilizo njema. Imani yetu kwake na kwa Jina lake inatuachilia sisi nguvu iliyofichwa ndani ya hilo Jina lake. Jina la Yesu sio tu NOMINO(NOUN) bali Jina la Yesu ni CHEO(RANK) Ambacho kila aliyepewa hilo Jina anauwezo wa kupata matokeo yale yale ambayo yule mtu wa kwanza aliyepokea hilo Jina alipata.

Biblia inaeleza wazi Mungu alimkirimia Jina Yesu Jina lipitalo Majina Yote and the good thing is Mungu alimkirimia hilo Jina mapema sana tangu akiwa tumboni mwa mama yake na kwajina hilo Yesu Ali accomplish mambo mengi sana yaliyokuwa impossible...

Petro baada ya kumnyanyua kiwete anaulizwa anajibu ni jina gani na kwa nguvu gani mmefanya haya...anasema hakuna Jina jingine tulilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo, isipokuwa Jina la Yesu...Jina la Yesu ni asset ya kimbingu tuliyopewa ndio maana Petro anaujasiri wa kusema sina fedha wala dhahabu bali nilichonacho ndicho nikupacho then anasema "kwa Jina la Yesu simama uende".

Niko hapa Leo kukwambia Pokea Jina la Yesu na kwa Jina hili kila kilichokwama kwako na kiende kuanzia sasa, kila kilichosimama mbele yako na kipige goti lake kwako kwa Jina la Yesu. Jina la Yesu likakuinue na kukuweka Panapo heshima.

Address

Bujumbura

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Groupe De Prière et D'Evangélisation AGAPE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share