Moravian Church Zanzibar

Moravian Church Zanzibar Kanisa la Moravian Tanzania
Jimbo la Mashariki
Eneo la Misheni Zanzibar
Ushirika wa Zanzibar

08/08/2026
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya kutujalia ibada njema ya Jumapili iliyofanyika tarehe 02 Agosti, 2026 katika Ka...
05/08/2026

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema ya kutujalia ibada njema ya Jumapili iliyofanyika tarehe 02 Agosti, 2026 katika Kanisa la Moravian Zanzibar–Mwera.

Ibada iliongozwa na Mchungaji Japhet Mtafya, Mwenyekiti wa Eneo la Misheni Zanzibar, huku mahubiri ya Neno la Mungu yakitolewa na Mchungaji Ntufye Simon Mbukwa, Katibu Mkuu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki.

Kupitia ibada hii, waumini walipata nafasi ya kumwabudu Mungu, kusikiliza Neno lake na kuimarishwa katika imani. Tunaendelea kumshukuru Mungu kwa watumishi wake na kuomba azidi kulibariki Kanisa lake na kueneza Injili yake.

Amen!

Sikukuu ya Idara ya Uinjilisti – Kanisa la Moravian Zanzibar 🙏❤️Leo tumeshiriki kwa furaha Ibada ya Sikukuu ya Idara ya ...
26/07/2026

Sikukuu ya Idara ya Uinjilisti – Kanisa la Moravian Zanzibar 🙏❤️

Leo tumeshiriki kwa furaha Ibada ya Sikukuu ya Idara ya Uinjilisti ya Kanisa la Moravian Zanzibar. Ibada iliongozwa na Mchungaji Onesmo Kasyama, huku Neno la Mungu likihubiriwa na Mama Mchungaji Japhet Mtafya, Mwenyekiti wa Eneo la Misheni Zanzibar, Mama yetu Chanda Ngwenya.

Mgeni rasmi wa maadhimisho haya alikuwa Ndugu Edgar Teacher, Mkurugenzi wa Tanzania Mwangaza, ambaye alituunga mkono na kushiriki nasi katika siku hii ya pekee.

Pia tulibahatika kutembelewa na Dada Bettina Nasgowitz kutoka HMH, jambo lililoongeza baraka na ushirika katika maadhimisho yetu.

Ujumbe mkuu wa siku ulitukumbusha kumtegemea Mungu pekee, kumwamini kwa moyo wote, na kutoweka tumaini letu kwa mwanadamu.

«"Amebarikiwa mtu yule anayemtumaini BWANA, ambaye tumaini lake ni BWANA." — Yeremia 17:7»

Tunamshukuru Mungu kwa siku hii yenye baraka, ushirika na mafundisho yenye kujenga imani. Mungu aendelee kuibariki Idara ya Uinjilisti, Kanisa la Moravian Zanzibar, na kila anayejitoa katika kuieneza Injili ya Kristo.

"Mungu ameunganisha, mwanadamu asitenganishe." (Mathayo 19:6) 🤍💍Leo tumeshuhudia ibada takatifu ya ndoa ya Mpoki Jordan ...
25/07/2026

"Mungu ameunganisha, mwanadamu asitenganishe." (Mathayo 19:6) 🤍💍
Leo tumeshuhudia ibada takatifu ya ndoa ya Mpoki Jordan Juma na Patricia Innocent Joseph, iliyofanyika katika Kanisa la Moravian Tanzania, Ushirika wa Mwera – Zanzibar. Ibada hii iliongozwa na kufungwa rasmi na Mchungaji Onesmo Kasyama.
Tunawatakia wanandoa hawa maisha yenye upendo wa kweli, amani, uaminifu, na baraka tele katika safari yao mpya ya ndoa. Mungu aendelee kuwa msingi wa familia yao siku zote.
Hongereni sana Bwana na Bi. Jordan! 💒❤️

14/07/2026

Wote mnakaribishwa...

08/07/2026

Mahubiri ya ibada ya Jumapili yalitolewa na Onesmo Kasyama ambaye alisisitiza kutokukata Tamaa..

SIKUKUU YA IDARA YA WANAWAKE – KANISA LA MORAVIAN ZANZIBAR 💐🙏Leo tumepata neema ya kuabudu pamoja katika Sikukuu ya Idar...
28/06/2026

SIKUKUU YA IDARA YA WANAWAKE – KANISA LA MORAVIAN ZANZIBAR 💐🙏

Leo tumepata neema ya kuabudu pamoja katika Sikukuu ya Idara ya Wanawake. Ibada iliongozwa na Mch. Onesmo Kasyama, huku Neno la Mungu likituimarisha kupitia kauli mbiu:

"Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." (Mathayo 11:28)

Tumekumbushwa kumkabidhi Kristo mizigo yetu yote, kwa kuwa ndani yake kuna pumziko, faraja na tumaini la kweli.

Mungu aendelee kuibariki Idara ya Wanawake na Kanisa la Moravian Zanzibar. Tuwe watu wa kumtegemea Kristo katika kila hali.

Matukio mbalimbali kutoka katika Ibada iliyofanyika tarehe 21 Juni 2026, iliyoongozwa na Mch. Onesmo Kasyama k**a mwenye...
22/06/2026

Matukio mbalimbali kutoka katika Ibada iliyofanyika tarehe 21 Juni 2026, iliyoongozwa na Mch. Onesmo Kasyama k**a mwenyeji. Mahubiri yalitolewa na Mch. Japhet Mtafya, Mwenyekiti wa Eneo la Misheni Zanzibar, ambaye alisisitiza waamini kufuata mafundisho ya Yesu Kristo na si mafundisho ya wanadamu. Tumehimizwa kusimama katika Neno la Mungu na kuishi kulingana na mapenzi yake. Mungu aendelee kutuongoza katika kweli yake. 🙏✨

Wote mnakaribishwa..
16/06/2026

Wote mnakaribishwa..

Address

Mwera Mahak**ani Zanzibar
Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Moravian Church Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share