05/02/2018
MSINGI WA MAISHA YA MKRISTO NI NENO LA MUNGU
Msingi wa maisha ya mkristo ni neno la Mungu . Hauwezi ukasema umeokoka na unampenda Yesu ikiwa unasoma neno la Mungu kila jumapili na mama unasoma gazeti tena kwa mazoea . Ili uweze kukua katika kumjua Mungu (kukua kiroho) si kwa kwenda kanisani, si kwa kuwa na namba za watumishi mbalimbali si kujua kuombea na watu wanaanguka mapepo si kufanya au kuona miujiza mingi la hasha utaweza kukua kiroho k**a utasoma neno la Mungu, utalitafakari na kuliingiza ktk matendo. Mfano unaumwa na mauti imekuzunguka unaweza ukatumia andiko hili "SITAKUFA BALI NITAISHI "ukawa unalikiri mpaka linajengeka katika nafsi yako na mauti inauachia.
Ishi ndani ya neno la Mungu maana vitu vyote vitapita, fedha, magari, nyumba, miujiza na vingine vyote lakini neno la Mungu kamwe litabaki milele.
Mathayo 4:4
Yohana 10:35
1Koritho 1:18
Waefeso 6:17
Wakolosai 3:16
Waebrania 4:12 , 13:7
Ubarikiwe.