21/05/2026
๐จ๐ง๐๐ ๐๐จ๐๐๐ฆ๐๐ข ๐ช๐ ๐ ๐ช๐๐ ๐๐ก๐ ๐ก๐ ๐ง๐๐๐ฅ๐๐๐ ๐ญ๐ ๐จ๐๐๐๐ ๐ ๐ช๐ ๐ ๐จ๐ก๐๐จ.
๐จ๐๐ฎ๐ป๐ด๐๐น๐ถ๐๐ถ:
Maisha ya Mwamini yanaongozwa na kile anachokijua na kukiamini kuhusu Mungu na ufalme Wake. Taarifa ambazo mtu anazo ndizo zinazounda mtazamo wake, maamuzi yake, mwenendo wake, na hata kiwango chake cha kufaidika na neema ya Mungu ndani ya Kristo. Ndiyo maana adui hupambana sana na ufahamu wa Mwamini ili aishi chini ya kiwango ambacho Mungu amemkusudia.
๐ญ. ๐ ๐ฎ๐ถ๐๐ต๐ฎ ๐๐ฎ ๐ ๐๐ฎ๐บ๐ถ๐ป๐ถ ๐ป๐ถ ๐บ๐ฎ๐๐ผ๐ธ๐ฒ๐ผ ๐๐ฎ ๐๐ฎ๐ฎ๐ฟ๐ถ๐ณ๐ฎ ๐ฎ๐น๐ถ๐๐ผ๐ป๐ฎ๐๐ผ.
Namna Mwamini alivyo ni udhihirisho wa taarifa alizo nazo juu ya ufalme wa Mungu. Mtu hawezi kuishi tofauti na kile anachokiamini moyoni mwake. K**a ufahamu wake ni mdogo, hata maisha yake yatabaki katika mipaka hiyo.
Biblia inasema:
> โWatu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa...โ
โ ๐๐ผ๐๐ฒ๐ฎ ๐ฐ:๐ฒ
Tatizo kubwa mara nyingi si ukosefu wa Mungu, bali ni ukosefu wa maarifa sahihi kuhusu Mungu na ufalme Wake.
๐ฎ. ๐ง๐ฎ๐ฎ๐ฟ๐ถ๐ณ๐ฎ ๐๐ถ๐๐ถ๐๐ผ ๐๐ฎ๐ต๐ถ๐ต๐ถ ๐ต๐๐๐ฎ๐ฎ ๐บ๐๐ฒ๐ป๐ฒ๐ป๐ฑ๐ผ ๐๐๐ถ๐ผ ๐๐ฎ๐ต๐ถ๐ต๐ถ.
Mwamini anapokuwa na taarifa zisizo sahihi kuhusu ufalme wa Mungu, lazima ataishi na kuenenda kwa msingi wa taarifa hizo. Kwa sababu hiyo, hawezi kufaidi kikamilifu yote aliyopewa ndani ya Kristo.
๐ช๐ฎ๐ฝ๐ผ ๐๐ฎ๐ฎ๐บ๐ถ๐ป๐ถ ๐ฎ๐บ๐ฏ๐ฎ๐ผ:
-wanaishi katika hofu badala ya imani,
-wanaona hawawezi kushinda dhambi,
-hawaelewi mamlaka waliyopewa ndani ya Kristo,
-wanaamini maisha yao yanaamuliwa na mazingira kuliko Neno la Mungu.
Sababu kubwa ya hali hizi mara nyingi si kukosa kumpenda Mungu, bali ni kukosa ufahamu sahihi wa Neno la Mungu.
๐ฏ. ๐๐๐๐ถ๐ธ๐ถ๐น๐ถ๐๐ฎ ๐บ๐ฎ๐บ๐ฏ๐ผ ๐๐ฎ๐๐ถ๐๐ผ ๐๐ฎ ๐๐ณ๐ฎ๐น๐บ๐ฒ ๐ต๐๐ต๐ฎ๐ฟ๐ถ๐ฏ๐ ๐๐ณ๐ฎ๐ต๐ฎ๐บ๐ ๐๐ฎ ๐ ๐๐ฎ๐บ๐ถ๐ป๐ถ.
Waamini wengi wameharibiwa ufahamu wao kwa sababu ya kus**iliza mambo yaliyo kinyume na ufalme wa Mungu na kila kitu chema kilicho ndani ya Kristo. Mtu anapolisha akili yake kwa taarifa za hofu, kushindwa, tamaa za dunia, na falsafa zisizotoka kwa Mungu, taratibu moyo wake huanza kuamini vitu hivyo.
Biblia inasema:
> โAngalieni mtu asiwafanye mateka kwa njia ya elimu ya dunia na madanganyo matupu...โ
โ ๐ช๐ฎ๐ธ๐ผ๐น๐ผ๐๐ฎ๐ถ ๐ฎ:๐ด
Na tena:
> โImani chanzo chake ni kus**ia...โ
โ ๐ช๐ฎ๐ฟ๐๐บ๐ถ :๐ญ๐ณ
K**a imani huja kwa kus**ia, basi hata mashaka, hofu, na mitazamo mibaya huingia kupitia kile mtu anachos**iliza kila siku.
Ndiyo maana waamini wengi leo wanaongozwa na:
-hali za maisha,
-mazingira wanayopitia,
-uchumi,
maoni ya watu,
hisia zao,
na vitu vinavyoonekana kwa macho,
badala ya kuongozwa na ukweli wa Neno la Mungu na Roho Mtakatifu.
Mwamini anapoishi kwa kuongozwa na mazingira, maisha yake yatabadilika kulingana na mazingira hayo. Lakini anapoongozwa na Neno la Mungu, anakuwa imara hata katikati ya changamoto.
๐ฐ. ๐ ๐ถ๐๐ฎ๐๐ฎ๐บ๐ผ ๐๐ฎ ๐๐ฎ๐ฎ๐บ๐ถ๐ป๐ถ ๐ต๐๐๐ผ๐ธ๐ฎ๐ป๐ฎ ๐ป๐ฎ ๐๐ฎ๐ฎ๐ฟ๐ถ๐ณ๐ฎ ๐๐ฎ๐น๐ถ๐๐ผ๐ป๐ฎ๐๐ผ
Ukiangalia hali ya waamini wengi leo, mitazamo yao inatokana na taarifa walizonazo. Mtu akijazwa taarifa za kushindwa ataishi maisha ya kushindwa; lakini akijazwa ukweli wa Mungu ataenenda katika ushindi.
Biblia inasema:
> โWala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu...โ
โ ๐ช๐ฎ๐ฟ๐๐บ๐ถ ๐ญ๐ด:๐ฎ
Kubadilika kwa maisha ya Mwamini huanza kwanza kwa kubadilika kwa ufahamu wake.
๐ฑ. ๐๐ฟ๐ถ๐๐๐ผ ๐๐ฎ๐๐ฎ๐ฟ๐ถ ๐ฎ๐บ๐ฒ๐๐๐ฝ๐ฎ๐๐ถ๐ฎ ๐ธ๐ถ๐น๐ฎ ๐ธ๐ถ๐๐ ๐ฐ๐ต๐ฒ๐บ๐ฎ.
Ndani ya Kristo, Mwamini amepewa uzima, ushindi, mamlaka, haki, na urithi wa kifalme. Lakini mtu hawezi kufaidika na kitu asichokijua.
> โKwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa...โ
โ ๐ฎ ๐ฃ๐ฒ๐๐ฟ๐ผ ๐ญ:๐ฏ
Maarifa sahihi humsaidia Mwamini kuishi katika uhalisia wa kile ambacho tayari amepewa ndani ya Kristo.
๐๐ถ๐๐ถ๐บ๐ถ๐๐ต๐ผ:
Mwamini anapaswa kujenga maisha yake juu ya ukweli wa Neno la Mungu na si juu ya hisia, mazingira, au mafundisho yasiyo sahihi. Kadiri ufahamu wa Mwamini unavyokuwa sahihi kuhusu ufalme wa Mungu, ndivyo maisha yake yatakavyozidi kuonyesha utukufu wa Kristo.
Kwa hiyo, vita kubwa kwa Mwamini si vya nje tu, bali pia ni vita vya taarifa na ufahamu. Maana taarifa sahihi huzaa maisha sahihi, na maisha sahihi humdhihirisha Kristo ๐ฑ๐๐ป๐ถ๐ฎ๐ป๐ถ.
๐จ๐บ๐ฒ๐ฏ๐ฎ๐ฟ๐ถ๐ธ๐ถ๐๐ฎ ๐บ๐ถ๐น๐ฒ๐น๐ฒ.
๐๐๐ฎ ๐บ๐ฎ๐ณ๐๐ป๐๐ผ ๐ป๐ฎ ๐๐๐ต๐ฎ๐๐ฟ๐ถ ๐๐ฎ๐ถ๐ฑ๐ถ wa ๐ป๐ฑ๐ผ๐ฎ:
๐ง๐ฒ๐บ๐ฏ๐ฒ๐น๐ฒ๐ฎ ๐๐ธ๐ฎ๐ฟ๐ฎ๐๐ฎ ๐๐ฒ๐๐ NDOA NZURI Hujengwa ๐๐ฎ๐ฐ๐ฒ๐ฏ๐ผ๐ผ๐ธ ๐ป๐ฎ ๐๐ป๐๐๐ฎ๐ด๐ฟ๐ฎ๐บ.
๐ ๐ช๐ฎ๐๐ถ๐น๐ถ๐ฎ๐ป๐ฎ ๐ป๐ฎ๐๐ถ:
๐ ๐๐ฎ๐น๐ถ๐บ๐ ๐ง๐๐บ๐ฎ๐ถ๐ป๐ถ ๐ก๐ฒ๐น๐๐ผ๐ป ๐๐ถ๐ฏ๐ผ๐ป๐ฎ ๐ป๐ฎ
๐ ๐ฐ๐ต๐๐ป๐ด๐ฎ๐ท๐ถ ๐๐ฎ๐๐ต๐ฒ๐ฟ๐ถ๐ป๐ฒ ๐ง๐๐บ๐ฎ๐ถ๐ป๐ถ ๐๐ถ๐ฏ๐ผ๐ป๐ฎ
๐ฑ 0714 553 780 / 0742 120 119 / 0678 739 090
๐ง [email protected]
Jesus is the Way, the Truth and the Life Ministry.