12/05/2026
TO OUR OWN WONDERFUL SPIRITUAL MOTHER
MAMA MARY AMRI Mary Amri 💘❤️🥰🥰❗️
Katika kusherehekea siku hii ya Mama Duniani, kwanza kabisa tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha yako. Umekuwa mama wa kipekee mwenye upendo wa dhati kwa watoto wako wa kiroho; upendo usiochoka, moyo wa kujitoa, na huduma yako ya unyenyekevu mkubwa kiroho na kimwili imekuwa baraka isiyoelezeka kwa wengi.🙌🏻🙌🏻❤️
Wanawake wote wa AKUZAMU, kwa upendo mkubwa na heshima ya pekee, wameona wakupatie tuzo hii ya k**a ishara ndogo tu ya kuthamini huduma yako, maombi yako yasiyokoma, na malezi yako ya kiimani na kimwili kwetu sote. Kwa kweli, namna ambavyo umegusa maisha ya kila mmoja wetu haiwezi kuelezewa kwa maneno.😭😭😭
Umekuwa chanzo cha faraja kwa waliovunjika moyo, umejenga ujasiri kwa waliokuwa wamekata tamaa, na umeonyesha upendo wa kweli wa Kristo kwa kila anayepata nafasi ya kukutana nawe. Hukuwahi kumdharau wala kumkatia mtu tamaa; badala yake, unamwinua, unamtia nguvu, na unamfanya ajione wa thamani mbele za Mungu na mbele za watu. Si kwa wanawake pekee, bali kwa kila mtu anayekuja katika maisha yako, umeacha alama ya upendo, matumaini, na imani.1📌❗️
Mama, tunasema asante kwa machozi uliyolia kwa ajili yetu kwenye maombi, kwa ushauri wako wenye hekima, kwa upendo wako usio na ubaguzi, na kwa moyo wako wa kipekee wa kuhudumia wengine. Wewe ni zawadi kubwa sana kwetu.🙏🏻
Mungu azidi kukubariki kwa wingi mama, akupe afya njema, nguvu mpya kila siku, na akuongezee neema katika kila hatua ya maisha yako.📌 Tunakuombea maisha marefu yenye furaha, afya njema, amani, na tumaini kuu katika Mungu wetu wa Mbinguni tunayemtumikia.🙏🏻
Tunakupenda sana na tutaendelea kukuenzi siku zote, Mama yetu kipenzi💘 💖🙏