Nchi ya ukombozi ministry

Nchi ya ukombozi ministry KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA

SADAKA INAKOMESHA LAANAKaribu katika mfululizo ya masomo yahusuyo matoleo!(Ifahamu Nguvu iliyopo katika Sadaka)Tangu Ada...
02/12/2025

SADAKA INAKOMESHA LAANA

Karibu katika mfululizo ya masomo yahusuyo matoleo!
(Ifahamu Nguvu iliyopo katika Sadaka)

Tangu Adamu aanguke ardhi ilianza kulaaniwa; kila siku laana ilikuwa inajiongeza juu ya laana, ndio maana utaona Mungu alimwambia Adamu ardhi imelaaniwa kwaajili yake yeye na uzao wake (Mwanzo 3:17), lakini ukizidi kusoma utaona tena ardhi inalaaniwa mara ya pili kwa Kaini (Mwanzo 4:11).

Na desturi hiyo iliendelea juu ya wanadamu, (Maana yake kila kukicha ardhi ilikuwa inalaaniwa juu ya wanadamu, kutokana na maasi).
Lakini tunasoma alipozaliwa Nuhu maandiko yanamtaja k**a mwana wa Faraja, atakayeikomesha laana iliyo juu ya ardhi.

Mwanzo 5:28 “Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
29 Akamwita jina lake Nuhu, AKINENA, HUYU NDIYE ATAKAYETUFARIJI KWA KAZI YETU NA KWA TAABU YA MIKONO YETU KATIKA NCHI ALIYOILAANI BWANA”
Sasa unaweza kujiuliza ni wakati gani ambao Nuhu alileta faraja katika Nchi aliyoilaani Bwana?
Tusome Mwanzo 8:20-22.

Mwanzo 8:20 Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
21 Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, SITAILAANI NCHI TENA BAADA YA HAYO KWA SABABU YA WANADAMU, MAANA MAWAZO YA MOYO WA MWANADAMU NI MABAYA TANGU UJANA WAKE; WALA SITAPIGA TENA BAADA YA HAYO KILA KILICHO HAI K**A NILIVYOFANYA.

22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa k**i, mchana na usiku, havitakoma”
Umeona hapo? Baada ya Nuhu kumjengea Bwana madhabahu na kumtolea Bwana sadaka nzuri na ya kumridhisha, ndipo akaikomesha ile laana yote iliyokuwa inaendelea juu ya ardhi, kukawa hakuna tena kulaaniwa kwa nchi baada ya hapo!, ndio maana mpaka leo tunaona misimu ya mvua ipo, misimu ya kiangazi cha mavuno ipo, majira ya kuvuna na kupanda bado yapo, k**a isingelikuwa ile sadaka Nuhu aliyoitoa huenda leo tungekuwa dunia ingekuwa mahali pabaya.

Lakini siri ya KUIKOMESHA HIYO LAANA!, Nuhu alifahamu ni kwa NJIA YA MATOLEO TU!..Na ni kanuni gani Nuhu aliyoitumia kutoa sadaka mpaka kufikia kuvunja misingi ya laana ya ardhi?

1.Alijenga Madhabahu.
Na sisi ni lazima tujenge madhabahu kwanza, na Madhahabu ya sasa, Agano jipya si ile ya mawe bali ni MIOYO YETU, Hiyo inapaswa iwe misafi kabla ya kufikiri kumtolea BWANA sadaka. Kwasababu maandiko yanasema sadaka ya mtu mbaya ni machukizo kwa Bwana (Mithali 15:8).

2. Kutoa vilivyo safi.
Baada ya Nuhu kutoka kwenye safina alitwaa wanyama walio safi tu na kumtolea Mungu, Na sisi ni lazima tumtolee Mungu vitu vilivyo visafi, hatupaswi kumtolea Mungu vitu vilivyopatikana kwa njia haramu k**a ukahaba, dhuluma, rushwa, wizi, utapeli, na njia nyingine zote zinazofanana na hizo.
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili.”

3. Kutoa katika KILA kilicho safi!
Hii ni kanuni ya mwisho na ya muhimu sana, Ni lazima kutoa katika “KILA” kilicho safi, na si katika “BAADHI ya vilivyo safi”. Nuhu hakutoa tu Ng’ombe pekee yake k**a sadaka, na kuwahifadhi mbuzi kwaajili ya chakula chake na biashara yake, au hakutoa kondoo pekee yake, na kuwaacha kuku na mbuzi…bali alitoa katika vyote vilivyo safi, ikiwemo kondoo, mbuzi, ng’ombe, njiwa, kuku na vinginevyo.. kila kimoja kwa sehemu yake..Hiyo ikafanya sadaka yake kumridhisha Mungu, na hivyo kufuta laana zote zilizokuwepo juu ya nchi, ambapo mpaka leo tunakula matunda yake.
Na wewe una vitu gani vilivyo safi mbele za Mungu?, je katika vyote unavyovifanya huwa unafikiri kumtolea Mungu katika hivyo?, Je katika zawadi unazopewa ulishawahi kufikiri kumtolea Mungu sehemu ndogo katika hiyo?, au unafiki ni sehemu ya mshahara tu ndio Mungu anaitaka?!
Je katika mifugo yako yote ulishawahi kufikiri kumtolea Mungu sehemu ya hiyo? Usimtolee Mungu kuku na kuacha Mbuzi!.. Jaribu siku moja kumtolea mbuzi na kuku kwa pamoja, na uone matokeo yake, (Mungu ameruhusu tumjaribu kwa njia hiyo, Malaki 3:10).
Utaona laana zinavyoondoka juu yako!!.
Bwana akubariki.

KWA MSAADA ZAIDI AU MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI KIONGOZI

BISHOPLAURENT MPOMA

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

MWAJA KITOPE – SINGIDA MJINI, BARABARA YA KWENDA MWANKOKO

0714890889

WHATSAP: 0762756542

MAOMBI YA KUVUNJA VIAPO NA MAAGANO YA MAUTI KWENYE MIKONO YAKO. Inawezekana Kila Unalolifanya halifanikiwi kwa Sababu ya...
02/12/2025

MAOMBI YA KUVUNJA VIAPO NA MAAGANO YA MAUTI KWENYE MIKONO YAKO.

Inawezekana Kila Unalolifanya halifanikiwi kwa Sababu ya Viapo vya Mauti vilivyoachiliwa na Ufalme wa Giza kwenye Mapito yako wakaweka Maagano kwamba Hautamiliki, Uchumi, Kazi na Biashara Nzuri na hata Ukimiliki hautafanikiwa bali utaandamwa na Roho za Uaribifu hivyo Njoo kwenye Maombi Alhamis hii.

Inawezekana Ndoa yako inapita Maali pagumu, Inawezekana Familia yenu imefungwa na Roho ya Ulevu, Magonjwa na Umasikini kutokana na Maagano na Viapo vilivyofanyika kwajili yenu, Hivyo Njoo Alhamis Hii ni Siku yako ya Kwenda kufanya Agano na MUNGU la Kufanikiwa kwenye kila eneo la Maisha yako.

Zaburi 25:14. Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha Agano lake.

KWA MSAADA ZAIDI AU MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI KIONGOZI

BISHOP LAURENT MPOMA

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

MWAJA KITOPE – SINGIDA MJINI, BARABARA YA KWENDA MWANKOKO

0714890889

WHATSAP: 0762756542

02/12/2025

MAAGANO
Mithali 11:9b, Yak 5:14.
Agano (covenant)-makubaliano baina ya pande mbili yanayoweza kushinikizwa kisheria.

Agano linaweza kuwa katika mfumo ufuatao
Kutoka 34:12-16
• MAMBO YA MSINGI KATIKA KUSABABISHA AGANO
1. Watu
2. Maneno
3. Sababu
4. Mahali
5. Baraka/ adhabu ya kuvunja agano
• Kuvunja maagano hupelekea mambo yafuatayo
1. Mauti 2 sam 21:1-9
2. umasikini
3. majanga
4. kifo cha ghafula
5. balaa
6. utasa : fuatilia wake za Ibrahimu, Isaka na Yakobo Mwanzo 20:17–18,Mwanzo 25:21, Mwanzo 30:1
7.
• KUVUNJA MAAGANO
Vifungu vya kutumia: Isaya 28:15 , Isaya 28:18, 2 Wakorintho 3:6, Marko 14:24 , Waebrania 13:20 , Waebrania 12:24, Zaburi 94:11
Agano la uovu (shetani) ni makubaliano kati ya pande mbili au zaidi zinazoshikiliwa na nguvu za giza na k**imamiwa na roho za mashetani. Ni kati ya shetani na mwanadamu. Isaya 28:15,18
• AINA ZA MAAGANO YA UOVU (SHETANI)
1. Maagano ya uovu ya asili, tambiko etc….
2. Maagano ya kurithi.
• Maagano ya kulazimishwa ndotoni na nguvu za giza
1. Maagano ya kuamua mwenyewe na shetani…. Kujitakia
2. Maagano ya kuingia bila kujua ( hufanywa na nguvu za giza).

• MIFANO YA MAAGANO YA UOVU (MAPEPO).
1. Maagano dhidi ya sanamu
2. Maagano dhidi ya uchawi
• Maagano ya kwenye maji(mito, bahari, maziwa n.k
1. Maagano ya ardhini.
2. Maagano ya nguvu tatu nazo ni jua, mwezi, nyota.
3. Maagano ya mawakala wa shetani, freemasons, iluminati, n.k
• Maagano dhidi ya aina Fulani ya chakula… allergy.
• Maagano dhidi ya roho za kuzimu
1. Maagano dhidi ya roho za miamba., madini n.k
2. Maagano dhidi ya mume au mke wa kiroho ( majini mahaba)
3. Maagano dhidi ya roho za uovu, majini k**a vile shamsi, subiani,makata, zaituni, etc.

• JINSI YA KUVUNJA MAAGANO
1. Mkabidhi Yesu Maisha RUMI 10:9-10
2. Weka wazi/ chunguza na tambua chanzo cha tatizo 2 Fal 2:19-22
3. Kataa, vunja /pinga maagano hayo ya shetani Kutoka 34:12-16
4. Jitoe kwenye maagano kwa kukiri kwa Kinywa chako
5. Amua na chukua hatua kutoka kwenye maagano
6. Maombi ya kiu na mzigo husaidia kukutoa kwenye maagano haraka na kwa urahisi.. weka bidii katika maombi. Yakobo 5:15-16
7. Kiri na kubali kulitumia NENO la Mungu mara kwa mara. Waebrania 12:29, 4:12
8. Ishi maisha ya kufunga na kuomba. Isaya 58:5, Mathayo 17:21
9. Fanya maombi ya kujikomboa toka asili.
10. Fanyiwa ukombozi kwa maombi
11. Jazwa Roho mt.
12. Acha kula kula hovyo hovyo. Shetani hutumia muda huu kumrudisha mtu ktk maagano kwa njia ya chakula.


• Maombi
1. Maagano yeyote niliyoingizwa na mababu, miziu na wazee wa eneo langu la sili katika damu ya Yesu ninayavunja katika Jina la Yesu.
2. Kila agano lililojificha linalosumbua maisha yangu, ninakutangazia sasa, ninakukataa na kukuamuru vunjika sasa katika Jina la Yesu.
3. Kila agano linalopatilizwa katika kizazi change, vunjika/ toka katika maisha yangu katika Jina la Yesu.
4. Agano lolote lililolazimishwa kuingia kupitia ndoto au kutokuelewa kwangu, ninakuvunja katika Jina la Yesu.
5. Agano lolote nililofanya na nguvu za giza kwenye maji, miamba, jua, mwezi, nyota n.k ninayavunja katika Jina la Yesu.
6. Agano kati yangu na Sanamu yeyote na roho za uovu/pepo wabaya ninayavunja katika Jina la Yesu.
7. Agano kati yangu na Majini mahaba ninavunja katika jina la Yesu.
8. Agano lolote katika ardhi ya asili yangu inayoathiri mafanikio yangu na maisha yangu, ninayavunja kwa damu ya Yesu katika Jina la Yesu.
9. Agano lolote katika nyumba ninayoishi na asili yake kuanzia sasa, au nyumba niliyowahi kuishi huko nyuma linaliathiri mafanikio yangu na maisha, ninayavunja kwa damu ya Yesu katika Jina la Yesu.
10. Nguvu yeyote inayorudisha/huisha /kuleta maagano ya mashetani katika maisha yangu, ninaivunja na kuitowesha katika Jina la Yesu.
11. Kila mkataba wa kipepo na mashetani unaopelekea/ kushinikiza agano katika maisha yangu na familia, kufa katika jina la Yesu.
12. Kila agano lililojificha na lisilojulikana linalosumbua mustakabali wa masiha yangu, katika Jina la Yesu ninakuvunja sasa.
13. Ahsante Yesu kwa ushindi katika Jina la Yesu.

KWA MSAADA ZAIDI AU MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI KIONGOZI

BISHOP LAURENT MPOMA

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

MWAJA KITOPE – SINGIDA MJINI.

0714890889

WHATSAP: 0762756542

KUNA WAKATI UNAPITIA MAGUMU, NIKUTIE MOYO SASA UTAINUKA TENA WIKI HII KATIKA JINA LA YESU.AMINAAA
02/12/2025

KUNA WAKATI UNAPITIA MAGUMU, NIKUTIE MOYO SASA UTAINUKA TENA WIKI HII KATIKA JINA LA YESU.AMINAAA

NAKUOMBEA MUNGU AKUPE NEEMA YAKUKUTANA NA WATU SAHII WIKI HII .
02/12/2025

NAKUOMBEA MUNGU AKUPE NEEMA YAKUKUTANA NA WATU SAHII WIKI HII .

SIFA NA KUABUDU IKIENDELEA , NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY  (HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
27/08/2025

SIFA NA KUABUDU IKIENDELEA , NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY (HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

BONYEZA " SUBSCIBE" HAPO CHINI

Liko tumaini kwa wanao msubiri BWANA YESUVIDEO HII HAPA
27/08/2025

Liko tumaini kwa wanao msubiri BWANA YESU

VIDEO HII HAPA

BONYEZA "KU-SUBSCIBE" HAPO CHINI

Yote Yanawezekana Kwa Mungu aliye hai.Namshukuru Mungu kwa kutupa faraja ya maandiko yanayoonyesha kwamba yote yanawezek...
16/07/2025

Yote Yanawezekana Kwa Mungu aliye hai.

Namshukuru Mungu kwa kutupa faraja ya maandiko yanayoonyesha kwamba yote yanawezekana kwake. Leo nimetafuta mistari michache ambayo naamini itaijenga imani yako ikiwa utaisoma na kuitafakari. Isome, irudie rudie na kuisema ,kisha utaanza kuona moyoni Mungu anaweza yote.
1. Mwanzo 18:14
Mungu alionyesha kwa Sara hakuna neno la kumshinda, atapata mtoto.
2.Yeremia 32:27
Mungu aliuliza kuna neno gani gumu la kumshinda? Kwa wenye mwili.
3.Ayubu 42:2
Ayubu alimsema Mungu kwamba anaweza yote na makusudi yake hayazuiliki.
4.Mathayo 3:9
Yohana mbatizaji alionyesha Mungu anao uwezo wa kugeuza mawe yawe watoto wa Ibrahim! Hii yaonyesha anaweza yote.
5.Warumi 4:21
Ibrahimu alijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
6.Luka 1:37
Malaika alisema hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu, akimaanisha, hakuna ahadi ya Mungu isiyo na nguvu ya kujitimiza au kutimia.
7.Mathayo 19:26
Yesu alisema yote yawezekana kwa Mungu!
8.Yohana 15:5
Yesu alisema pasipo yeye hatuwezi lolote, kwa hiyo pamoja naye tunaweza yote.
9.Luka 17:20-21
Yesu alisema tukiwa na imani k**a chembe ya haradali, imani inayokuwa na kusema tunaweza kuamisha mlima wala hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwetu. Imani hii hutokea katika maombi na kufunga.
10.Marko 9:23
Yesu alisema yote yawezekana kwa aaminiye, Yote yawezek**a kwa mtu aiwekaye imani yake kwa Mungu awezaye yote, anaanza kuweza k**a Mungu awezavyo.
Unaweza Pamoja na Mungu.

MAMA ALIYEFUNGWA NA MAPEPO MUDA MREFU AFUNGULIWA NA MUNGU KUPITIA MADHABAHU YA NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY.
17/05/2025

MAMA ALIYEFUNGWA NA MAPEPO MUDA MREFU AFUNGULIWA NA MUNGU KUPITIA MADHABAHU YA NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY.

ELIM PENTEKOSTE-NCHI YA UKOMBOZI - MUHAWA SINGIDA

17/05/2025

ELIM PENTEKOSTE-NCHI YA UKOMBOZI - MUHAWA SINGIDA

Address

S. L. P 618
Singida
0000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nchi ya ukombozi ministry posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share