TAG Sayuni Christian Centre

TAG Sayuni Christian Centre God loves you/Mungu anakupenda

17/05/2026

Philippians 4:4
[4]Rejoice in the Lord alway: and again I say, Rejoice.

Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

TANZIA💔😭 : ASKOFU MKUU WA KWANZA WA KANISA LA TAG MCH. DR. IMMANUEL LAZARO AFARIKI DUNIA  Makamu Askofu wa Kanisa la TAG...
18/05/2025

TANZIA💔😭 : ASKOFU MKUU WA KWANZA WA KANISA LA TAG MCH. DR. IMMANUEL LAZARO AFARIKI DUNIA

Makamu Askofu wa Kanisa la TAG Taifa,Dkt. Magnus Muhiche athibitisha kifo cha Mzee wetu wa Imani Askofu wa Kwanza wa Kanisa la TAG Taifa, Mch. Dr. Immanuel Lazaro ambaye amefariki mnamo Mei 17,2025,Majira ya Saa tano Asubuhi wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali Ya KCMC.

Ikumbukwe Marehemu,Mzee wetu, Mch. Dr. Immanuel Lazaro ameliongoza kanisa letu kwa muda wa miaka 24.

"2Timotheo 4:7 - Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda."

13/01/2025
Luke/Luka 2:12-14We hope you have a beautiful Christmas!Tuna imani umesherehekea vyema Christmas Luke 2:12-14: And this ...
27/12/2023

Luke/Luka 2:12-14

We hope you have a beautiful Christmas!
Tuna imani umesherehekea vyema Christmas

Luke 2:12-14: And this will be a sign for you: you will find a baby wrapped in swaddling cloths and lying in a manger. And suddenly there was with the angel a multitude of the heavenly host praising God and saying, 'Glory to God in the highest, and on earth peace among those with whom he is pleased!'

Luka 2:12-14:Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.

Katika kuadhimisha sikukuu ya Christmas na mwaka mpya tunapenda kuwatambulisha na muufatilie/follow ukurasa wa "Global t...
27/12/2023

Katika kuadhimisha sikukuu ya Christmas na mwaka mpya tunapenda kuwatambulisha na muufatilie/follow ukurasa wa "Global teen challenge-Manyoni" na uweze kujiunga nao Kwa taarifa mbali mbali kuhusu waraibu wa madawa ya kulevya

Teen challenge ni Nini?
Ni program iliyoandaliwa kuwasaidia wanaume na wanawake kupata suluhisho la matatizo ya uraibu wa pombe ,madawa ya kulevya ,ngono ,wizi nk

Teen challenge inawasaidia kina Nani?
Mtu yeyote mwenye miaka 18 na kuendelea mwenye tatizo la

1:uraibu wa madawa ya kulevya kwa muda mrefu

2:Pombe- ulevi wa kupindukia

3:matatizo ya kihisia- mfano msongo wa mawazo kutokana na uraibu

4:matatizo ya kitabia mfano -kutowajibika , utovu wa nidhamu ,uvivu, kutojitambua nk

Zaidi ya watu 5000 duniani wameweza kusaidiwa kuachana na uraibu uliowatesa kwa muda mrefu kupitia program hii yenye matawi sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

Mungu akubariki kwa kusoma ujumbe huu .

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa simu namba

+255 755 376 212
+255 658 336 878
+255 716 161 683

Au barua pepe [email protected]

Global teen challenge wakishirikiana na SOS adventures walifanikiwa kuhubiri injili mitaa kwa mitaa eneo la mbagala na m...
12/06/2023

Global teen challenge wakishirikiana na SOS adventures walifanikiwa kuhubiri injili mitaa kwa mitaa eneo la mbagala na maeneo mengine mbalimbali ya Dar es salaam, watu zaidi ya 130,000 walihubiriwa neno la Mungu

20,161 walilikiri jina la Yesu na kuokoka

633 walifunguliwa kutoka kwenye vifungo vya mapepo,Magonjwa nk

Mungu awabariki Sana watumishi wa Mungu kutoka TAG sayuni- Manyoni ambao walituwakilisha vyema katika kumtumikia Mungu kwa siku 10 huko mbagala Zakhiem-Dar es salaam

Pastor Raymond Gumbo, pastor John Daud ,Pastor Emmanuel yohana & Joel john ambaye ni kiongozi kutoka Manyoni teen challenge ndio waliokuwa mabalozi wa Yesu huko mbagala.

MUNGU AKUBARIKI KWA KUSOMA UJUMBE HUU

07/06/2022

IBADA YA JUMAPILI 5.6.2022

MUHUBIRI: MCH ILUMINATA MAKULE

SOMO: KUISHINDA HALI YA KUVUNJIKA MOYO

KIINI :KUJITIA NGUVU KATIKA BWANA.

NINI UFANYE ILI UJITIE NGUVU KATIKA BWANA

1.kukaa uweponi mwa Bwana Isaya 40:31,41:10

2.Tafuta ushirika na watu wa Mungu Ebrania 10:21

3.Ng'ang'ana na ahadi za Mungu 2korintho 1:20

MAMBO YA KUZINGATIA PALE UNAPOVUNJIKA MOYO

1.Kuwa na uwezo wa kukabili Ile Hali

2.Kumkaribia Mungu

3.Kutokutazama Hali ya mazingira uliyo nayo

4.Kumbuka uumbaji wa Mungu Isaya 49:14-16

31/05/2022

IBADA YA JUMAPILI 29.5.2022

MUHUBIRI: Askofu Maxwel

SOMO: Utambue nguvu ya utoaji kwa ajili ya Umisheni

MAANDIKO: Mwanzo 4:4-8 , Mwanzo 22:1-3

DALILI ZA KUWA UMESHINDWA UMISHENI

1. Kutokujitoa mwenyewe kwa Mungu

2.kutokuwa na shauku ya kumtolea Mungu

3.Kutokutoa kabisa Malaki 1:6

Siku ya Jeshi kubwa TAG Sayuni Christian Center-ManyoniPastore Debora seleli amekuwa Baraka Sana kwa kanisa letu ,karibu...
14/03/2022

Siku ya Jeshi kubwa TAG Sayuni Christian Center-Manyoni

Pastore Debora seleli amekuwa Baraka Sana kwa kanisa letu ,karibu Tena Pastor

Address

P. O. Box 137 Sayuni Street, Manyoni
Singida

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TAG Sayuni Christian Centre posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share