03/10/2024
MAMBO 7 YA KUFANYA IKIWA MAFANIKIO YAKO YAMEFUNGWA NA NGUVU ZA GIZA.
1. KUMPA BWANA YESU MAISHA YAKO: Hiki ni kipengele muhimu sana kwa mtu anayetaka kutembea kuishi sawa na kusudi la Mungu. Kuokoka ni kumpokea Yesu k**a Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Pia mwamini Yesu k**a Mfalme wa wafalme (Ufunuo 19:16). Unapookoka, ya kale yanapita na unakua kiumbe kipya (2 Warorintho 5:17). Ukiokoka Mungu anayatupilia mbali maovu yako yote (Mika 7:19) na hakumbuki tena dhambi zako (Isaya 43:25).
Lakini mtu k**a hajaokoka Roho wa Mungu anakuwa hayupo ndani yake na kibiblia mtu huyo anakuwa amekufa (Yakobo 2:26). Biblia inazumgumzia juu ya kufufuliwa pamoja na Kristo (Waefeso 2:6). Huwezi kufufuliwa k**a hujafa. Maandiko yanasema “Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto” (Ufunuo 20:14—15). Je mauti ya kwanza ni ipi?
Nimekuonesha mistari hiyo makusudi kwani mtu k**a hajaokoka kuna vitu Mungu hawezi kukupa katika maisha yao. Lakini ukiwa na Yesu unakuwa mtoto wa Mungu na Roho Mtakatifu anashuhudia pamoja na roho yako (Warumi 8:16). Unapokuwa mtoto wa Mungu, unaingizwa kwenye agano na Mungu lenye muhuri wa Roho Mtakatifu na unapewa kurithi pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho. Yesu anakutoa kutoka katika ufalme wa giza kwenda ufalme wa Mwana wa pendo lake (Wakolosai 1:13).
Unapokuwa ndani ya agano hili, baraka zote za rohoni unapewa (Waefeso 1:3). Lakini kumbuka kupewa baraka na kutembea ndani ya baraka ni vitu viwili tofauti. Siyo kila aliyepewa baraka anazifaidi. Yakobo alikuwa ndani ya baraka za agano lakini Yusufu akaondoka nazo kwenda Misri. Mungu akabariki nyumba ya akida kule Misri badala ya Yakobo aliyeko ndani ya agano. Kuna baraka za kiagano katika Kristo Yesu ambazo huwezi kuzipata mpaka uwe mtoto wa Mungu. Ukiwa mtoto wa Mungu, Roho Mtakatifu anaingia ndani yako na kukufunulia maandiko (Yohana 14:26). Na Roho huyu anakupa macho ya kuona chimbuko la kutokufanikiwa kwako kimaisha.
2. FAHAMU WAPI UMEFUNGWA: Huwezi kujifungua kutoka kwenye kifungo ambacho hukijui. Na huwezi kujua kilichokufunga k**a huijui sheria iliyokufunga katika ulimwengu wa roho. Na huwezi kujifungua k**a hujui sheria inayoweza kuitangua ile sheria iliyokufunga katika ulimwengu wa roho. Na huwezi kujifungua k**a hujui kipengele au vipengele vilivyoko katika ile sheria ambayo shetani ametumia kufunga mafanikio yako. Lakini je, utaijuaje sheria iliyokufunga?
Ili uweze kuijua sheria hii, lazima uwe na neno la Kristo. Kumbuka “imani chanzo chake ni kusikia. Na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Sauti ya Neno la Kristo ndiyo inakupa mafunuo ya kujua eneo au maeneo ambayo umefungwa katika ulimwengu wa roho. K**a huna neno, Mungu anaweza kukuambia kifungo chako kilipo lakini usielewe au usisikie wakati anasema nawe. Hivyo ili uweze kukijua kifungo chako kilipo, lazima uwe na maarifa ya neno la Kristo.
3. TOBA: Ukishajua vifungo vyako vilipo, fanya toba thabiti itayokufungua kutoka kwenye vifungo hivyo. Kushindwa kufanya toba kunaweza kukufanya uendelee kuishi katika kifungo hicho. Lakini je ni toba ipi ambayo unatakiwa uifanye katika kifungo fulani? Utajuaje k**a Mungu amekubali toba yako? Ukisoma habari za wana wa Israel walipoabudu miungu mingine utaona kuwa ilimgarimu Musa toba za 4. Pia soma habari za Gidion katika kitabu cha Waamuzi. Wakati mwingine inakulazimu ufunge na kuomba ili uweze kufunguliwa (Matayo 17:21). Je utajuaje toba ambayo lazima ufunge na kuomba?
ENDELEA HAPA>>>>https://nchiyaukomboziministrytz.blogspot.com/
YOUTUBE>>>youtube.com/channel/UCjXjSSDOweHXL3YE5edBNIg
HAPA>>>>https://noohapou.com/4/8082168
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI KIONGOZI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
MWAJA KITOPE SINGIDA MJINI
PIGA/TUMA MAHITAJI YAKO
0763652896, 0714890889
WHATSAP: 0762756542