Efatha Church Same.

Efatha Church Same. EFATHA CHURCH SAME
🌏

HABARI NJEMA ZA UFALME.Wema wa Mungu kupitia nguvu za kuhubiri injili kwa jina lake Yesu kristo umetupatia neema nyingin...
27/08/2026

HABARI NJEMA ZA UFALME.
Wema wa Mungu kupitia nguvu za kuhubiri injili kwa jina lake Yesu kristo umetupatia neema nyingine mpya kwaajili ya Urejesho wa talanta ya mwanamke bila kubagua umri na lika.

Tunawakaribisha wanawake wote ili Mungu akajazilize kiu ndani yako

Usikose ni siku ya kesho📌

UNAWEZAJE KUIKOMBOA AU KUIPONYA NDOA YAKO?.Wanandoa mnatakiwa kujiuliza je mwenzako ana furaha na wewe? Jenga tabia ya k...
26/08/2026

UNAWEZAJE KUIKOMBOA AU KUIPONYA NDOA YAKO?.

Wanandoa mnatakiwa kujiuliza je mwenzako ana furaha na wewe? Jenga tabia ya kumuuliza mwenzako Je, anakufurahia?. Kwa kuuliza huku kutakusaidia kuomba msamaha na kuweka mambo sawa. Ni vizuri sana ukawa na tabia ya kuomba msamaha hata k**a hujakosea. Hii itakusaidia sana.

Wewe baba, huyo uliye naye yaani huyo mkeo ameletwa na Mungu kwenye maisha yako kwahiyo kuishi naye kwa kumsumbua, humkumbatii, humwambi nakupenda halafu unasema unampenda Mungu sio kweli. Unampendaje Mungu wakati mkeo hujamwambia unampenda?.

Wewe baba, unatakiwa kuwa na tabia ya kumnunulia mkeo zawadi. Sio tangu kipindi cha uchumba ulivyo mnunulia zawadi basi hujamnunulia tena au mpaka akuombe huo sio upendo.

Kwenye ndoa ni mahali pa mashangilio yaani mkeo hatakiwi akukwaze. Ukiona mkeo anakukwaza basi jua wewe unakwaza.

Una mkwaza nani?
Unamkwaza Mungu. Ukiona mkeo k**a vile hakuheshimu, anakubishia maana yake wewe ni mbishi kwa Mungu. Siku wewe baba ukiacha ubishi utaona mambo yatakavyo kunyookea.

K**a mnataka kuona ustawi na maongezeko katika familia hakikisheni furaha na amani vinakaa katika ndoa yenu, msikubali kumpa ibilisi nafasi.

Mkiona mambo hayajakaa sawa hakikisheni mnayashughulikia ili yakae sawa na amani irudi, amani ikisha rudi mshughulikieni adui shetani aliyeyaleta hayo.

MUNGU AWABARIKI WANANDOA WOTE MKAISHI MAISHA YA FURAHA NA SHANGWE, MKASTAWI SANA.

MCHUNGAJI ANDREW SANGA

MKESHA WA MWANAMKE‼️Usikose mkesha maalum wa kusimama mbele za Mungu katika maombi ya KUINUA NGUVU YA MWANAMKE Kuna nguv...
26/08/2026

MKESHA WA MWANAMKE‼️

Usikose mkesha maalum wa kusimama mbele za Mungu katika maombi ya KUINUA NGUVU YA MWANAMKE Kuna nguvu katika kuomba na Mungu husikia kilio cha watu wake.

NI IJUMAA hii,‼️
Saa 3 Kamili usiku!
Kanisa la Efatha Same, Kilimanjaro
location barabara ya mahuu kituo cha Sabasaba

Njoo tumtafute Bwana pamoja, tukiweka mbele zake maisha yetu, familia, kazi na kila hitaji. Kwa Mungu yote yanawezekana!

Karibu sana — usije peke yako, mwalike na mwingine.

UKIRI WA SIKU. NAIBARIKI JUMANNE YANGU. Namshukuru BWANA kwa kuwa ni Mwema; kwa maana Fadhili zake ni za Milele. Sisi ni...
25/08/2026

UKIRI WA SIKU.

NAIBARIKI JUMANNE YANGU.

Namshukuru BWANA kwa kuwa ni Mwema; kwa maana Fadhili zake ni za Milele. Sisi ni Nuru ya Ulimwengu, Mimi na Familia yangu tutaangaza. Familia yangu itasonga mbele, kwetu kutakuwa Kwema, hakutakuwa na magomvi wala magonjwa wala vifo wala ukata. Maisha yetu yatakuwa Mazuri kwa kuwa Tumebarikiwa na BWANA.

Asante YESU, YESU ni Mzuri.

MAOMBI1. Muombe Mungu akurejeshee kila kilicho liwa na aina zote za maaduiMadumaduPalaleNzigeTunutu2. Rejesha kila ulich...
24/08/2026

MAOMBI
1. Muombe Mungu akurejeshee kila kilicho liwa na aina zote za maadui
Madumadu
Palale
Nzige
Tunutu

2. Rejesha kila ulicho badilishiwa

3. Rejeshe afya, mtoto , utumishi n.k

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME 23/8/2026SOMO: UNA NINI MKONONIHapa duniani hakuna kitu ambacho Mungu hajampa mt...
24/08/2026

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME 23/8/2026

SOMO: UNA NINI MKONONI

Hapa duniani hakuna kitu ambacho Mungu hajampa mtu.
Kila mtu anacho kitu kwaajili ya Mungu na maisha yetu hapa duniani
mfano, yule mwanamke aliulizwa una nini akajibu ana chupa ya mafuta.
mfano 2;YESU aliwauliza wanafunzi wake wana nini mkononi wakajibu mikate miwili na samaki.

NDIPO SASA TUNAULIZWA TUNA NINI MKONONI?
-Kuna wapiga vyombo
-waimbaji
-waombaji
-wanao jitoa kwa kazi ya kuujenga ufalme wa Mungu kwa njia mbali mbali.
Hicho ulicho nacho lazima kisaidie wengine, SWALI linakuja wewe una nini unachofanya kimeinua watu? Mfani Malkia Esther yeye alicho nacho kilikuwa kukomboa taifa zima alitumia hekima mpaka mambo kukaa vizuri.

Uthamani wako upo katiks kupanda, uthamani wa kile ulicho nacho wewe, hakuna kitu utafanya ambacho Mungu amekupa na ukafanya kazi usipate kitu.

Naongelea wewe unafanya nini hapa kanisani na kwa watu?

1 Petro 2 5
Ninyi nanyi, k**a mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
Mimi ni dhabihu kamili, na neno lasema huwapa mema wampendao kwa sababu hiyo kila aliyekuwepo duniani Mungu amemkusudia awepo.
2 Timotheo 3 17
ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Utakuwa kamili hapo utakapo fanya hicho ulichopewa.
Unapohubiri injili ya kristo mweleze mtu habari za Yesu sio habari ingine.
1 kolosai 1;29

©️MTUMISHI WA MUNGU TOGOLANI MJEMA

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME TAREHE 23/8/2026MATUKIO KATIKA PICHA  WANA WA MUNGU WAKIABUDU
24/08/2026

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME TAREHE 23/8/2026

MATUKIO KATIKA PICHA WANA WA MUNGU WAKIABUDU

MCHUNGAJI RACHEL SUSULE ANAWAKARIBISHA MKESHA WA AINA YAKE HII SIO YA KUKOSA KWA WANAWAKE ..MKARIBISHE NA JIRANI YAKO.
18/08/2026

MCHUNGAJI RACHEL SUSULE ANAWAKARIBISHA MKESHA WA AINA YAKE HII SIO YA KUKOSA KWA WANAWAKE ..MKARIBISHE NA JIRANI YAKO.

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME TAREHE 16/8/2026MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHAIBADA YA NENOMithali 16 1  Maand...
16/08/2026

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME TAREHE 16/8/2026

MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA

IBADA YA NENO
Mithali 16 1
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

©️MTUMISHI WA MUNGU REUBEN ISHIKE

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME TAREHE 16/8/2026MAOMBI MAALUMU1. Mshukuru Mungu kwaajili ya ndoa za wana Efatha ...
16/08/2026

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA EFATHA SAME TAREHE 16/8/2026

MAOMBI MAALUMU
1. Mshukuru Mungu kwaajili ya ndoa za wana Efatha kote
-kwa NDOA nzuri
-kwa MKE/MUME
-Kwa pendo lililo katika ndoa

2. Tangaza kuridhiwa kwa ndoa zetu, zilizokufa zikafufuke, kwa jina la Yesu.

3. Nenda kambi ya Adui inayo fanya uharibifu katika ndoa za wana Mungu, sambaratisha hizo silaha za uharibifu

4. Silaha zao k**a maneno, uongo, njaa, uchonganishi n.k wanacho tumia kuingilia ndoa tuma moto Yeremia 23:29

5. Omba Mungu aimalishe ndoa za Efatha
-Aimarishe mume/mke
-Aimarishe afya, vipato, utumishi wao

6. Omba Mungu kila mke aliye katika ndoa asimame katika kweli ili wasimamie majukumu yao vema.

7. Chochea nguvu ya ziada iliyopo ndani ya mwanamke ili afanye kwa ubora katika kusudi.

TANGAZA
8. Hakuna uchungu kwa wanandoa.
-Hakuna ugomvi
-Hakuna hasira
-Hakuna magonjwa
-Hakuna giza kwa jina la Yesu

Address

Same Saba Saba
Same
301

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Efatha Church Same. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share