24/05/2026
IBADA YA SUNDAY SCHOOL.
24.05.2026
SOMO LA 21,MEI 24.
Mwalimu wa somo:Katibu Binwa.
Kichwa cha Somo:Paulo akiwa Yerusalemu.
Maandiko ya somo: Matendo 20:22-24,21:10-11,17,30-31,33.
Kweli ya Biblia: Lazima tujiandae kuufuata uongozi wa Roho hata tunapojua kuwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha taabu na mateso.
Msitari wa kukumbuka:
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu k**a kumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyoipokea kwa Bwana Yesu,kuishihudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
Matendo 20:24