Thewinners TZ

Thewinners TZ HIKI NI KIKUNDI CHA VIJANA WALIOOKOKA NA WANAMPENDA YESU' DHAMIRA YA KIKUNDI HIKI NI KUINJILISHA JAMII KUPITIA VIPAJI VYA VIJANA WALIVYO JALIWA NA MUNGU.

SALAMU YETU INATOKA KITABU CHA WAFILIPI 1:16

02/01/2022

SHALOM WANA WA MUNGU

MAANDALIZI YA MKUTANO WA INJILI  UNAOTARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA KESHO ALHAMISI YA TRH 02/12-04.12/2021 MAJENGO- MOSHI
01/12/2021

MAANDALIZI YA MKUTANO WA INJILI UNAOTARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA KESHO ALHAMISI YA TRH 02/12-04.12/2021
MAJENGO- MOSHI

SHALOOM
01/12/2021

SHALOOM

21/10/2021

SHALOOM

“Mkeo amefariki Msiba uko hapa nyumbani?” Denis alipokea ujumbe mfupi kwenye simu yake, kuangalia ulitoka kwa Mama yake ...
13/10/2021

“Mkeo amefariki Msiba uko hapa nyumbani?” Denis alipokea ujumbe mfupi kwenye simu yake, kuangalia ulitoka kwa Mama yake mzazi. Nguvu zilimuishia, alikuwa akiongea na mteja ofisini kwake lakini sauti ilikauka.
Bila kujijua alijikuta ananyanyuka na kuanza kutembea. tembea ofisini kwake akiwa hajitambui. Wafanyakazi wake walimuuliza bosi vipi lakini hakuwa na jibu la maana la kuwapa.
Akili yake ilikumbuka maneno ambayo alimwambia mkewe asubuhi wakati anaondoka, mkewe alimwambia sukari imeisha na kwa dharau alimjibu, “Sasa unaniambia mimi ili nini? Kwani ni lazima unywe chai, huko kwenu mlikua mnakunywa chai kila siku?”
Alikumbuka namna usiku wake alivyompiga makofi baada tu ya mboga kuungua alipochelewa kuepua kwani alikua ananyonyesha mtoto wao wa mwisho ambaye yeye mwenyewe ndiyo alimuita amnyonyeshe kwani alikuwa analia sana.
Alikumbuka namna siku mbili kabla mkewe alisema amechoka kupigwa na kunyanyaswa, anakumbuka namna alivyomjibu kwa dharau kuwa k**a amechoka aondoke amuachie watoto wake.
“Ameniachia wanangu!” Alijikuta anaropoka na machozi yalianza kumtoka. Alishindwa hata kutembea hivyo alikaa chini kabisa sakafuni. Wafanyakazi wake walikuja na kumnyanyua na baada ya kumuuliza ndipo alipowaambia mkewe amefariki.
Walimchukua mpaka kwenye gari na safari ya kurejea nyumbani ilianza, walifika nyumbani, kila kitu kilikuwa kimya, nyumba ilikua imefungwa na hakukuwa na mtu.
Denis alizidi kuchanganyikiwa zaidi asijue nini cha kufanya ndipo alipokumbuka kuwa Mama yake alimwambia msiba uko nyumbani hivyo alidhani kuwa ni nyumbani kwao.
********************

Safari nyingine ilianza, Dennis alikuwa na mawazo, hayakuwa mawazo tu ya kufiwa bali ya aibu. Pamoja na kumiliki kampuni kubwa akiajiri watu zaidi ya kumi lakini mkewe alimnyanyasa na kumtesa k**a kinyago, mbali na kumpiga lakini alikua hamhudumii vizuri.
“Atakuwa amefia kwa Mama wakati ameenda kuomba hela ya matumizi…” Aliwaza kwani mara nyingi alipokuwa akimnyima pesa Mama yake mzazi ndiyo alikuwa akimsaidia na ndiye alizuia mara nyingi mkewe asiondoke.
Alifika mpaka nyumbani kwao, kweli kulikuwa na msiba, maturubai yalishawekwa, watu walishaanza kupika na watu walishaanza kujaa taratibu. Alijitahidi kushuka kwenye gari na kuanza kutembea kuelekea nyumbani.
Watu walikua wakimsalimia na kumpa pole, aliipokea kwa aibu huku akiwaza ni kitu gani kiliwasukuma wazazi wake kufanyia msiba pale na ni nini kilikuwa kimesababisha mauti ya mkewe.
“Ameumwa sana muacheni apumzike..” Ilikuwa ni sauti ya Baba yake mzazi ikimwambia jirani yao mmoja. Hapo ndipo alichanganyikiwa zaidi akiwaza ni kwa namna gani mkewe alikuwa anaumwa bila yeye kujali.
Lakini alikumbuka ni mara nyingi mkewe alimwambia anaumwa lakini alidharau na ni mara nyingi Mama yake alimsema kuhusu kutokumsikiliza mkewe na mara nyingi tu Mama yake aliongozana na mkewe hospitalini.
Yeye kwake yote hayo hakujali, kila mke alipomwambia anaumwa yeye alidai haki yake ya ndoa, alizidi kumpiga na alianza kukumbuka namna ambavyo alimpiga mpaka kulazwa lakini bado hakujali.
Aliwaza, "Labda ndiyo ilikuwa sababu ya kifo chake? Au alikuwa anaumwa kimya kimya halafu hasemi akaja kusema nyumbani?” Alitembea mpaka kufika ndani, alikaa na kusalimiana na ndugu wengine ambao nao walikuwa wanampa pole kwa msiba.
Alizipokea huku akijaribu kujizuia machozi yasitoke. Mara mtoto wake wapili wa miaka minne alikuja. Alikuwa akilia akimtaka Mama yake watu wakimwambia asubiri Mama yake anakuja.
Mtoto alimkimbilia Dennis na kuanza kulia "Baba namtaka Mama, namtaka Mama." Denis alichaganyikiwa kwani hakuwa na jibu la kumpa, hakujua amwambie nini kuhusu Mama yake.
Mara mtoto mwingine mkubwa kidogo wa miaka saba alikuja, alikuwa amembeba mtoto wao mdogo mchanga wa miezi sita. Alimfuata Baba yake na kumuuliza, "Baba, Mama yuko wapi Jack anataka kunyonya."
Hapo ndipo aliishiwa nguvu kabisa, maneno yake ya “Ondoka niachie wanangu" yalizunguka kichwani kwake. Aliwaangalia wanawe na kusema, "Kweli nimeachiwa, umeniweza Juddy mke wangu."
Alijikuta anaanza kulia k**a mtoto kitu ambacho kiliwafanya na wanawe wote kulia. Dennis alichanganyikiwa, kila mtu aliyekuwa anakuja nyumbani alienda kumpa pole, nguvu zilimuishia alikata tamaa, na majuto ya hali ya juu, kila tendo baya alilokuwa akimfanyia mkewe lilimjia kichwani.
*********************
“Mama Jose njoo umnyonyeshe mtoto analia toka muda mrefu.” Ilikua ni sauti ya Mama yake. Dennis alishtuka na kunyanyuka kuangalia, Mama Jose ni mkewe na hakujua ni kwa nini Mama yake alikuwa anamwambia aje kumnyonyesha mtoto wakati alishafariki dunia.
Kabla hajasema chochote Mama yake aliingia kisha, “Ohhh Dennis umekuja? Nikajua utakuja baadaye kazi zimekubana, mkeo alisema hupatikani kwenye simu.”
Dennis alizidi kuchanganyikiwa, alibaki na mshangao. Mara mkewe aliingia, hapo ndipo alichanganyikiwa zaidi, alishtuka k**a vile ameona mzimu, kidogo amdondoshe mtoto aliyekuwa amempakata.

“Vipi Baba Jose…” Mkewe alimuuliza kwa maana namna alivyokuwa akimuangalia haikuwa kawaida yake. “Uko hai mke wangu?” Alijikuta anauliza. “Ndiyo kwani vipi ulitaka nife?” Mkewe alijibu kwa kebehi kidogo kwani alijua ni dharau ya mumewe.
“Lakini Mama......” Dennis aliongea kwa kushangaa huku akimuangalia Mama yake. Mama yake alitabasamu na kumwambia, "Aliyefariki ni Bibi yako si ndiyo alikuwa anakuita mume wangu?
"Wewe mbona kila siku ukipiga simu unaulizia mke wangu hajambo." Dennis alipumua kwa nguvu huku akikaa chini, mkewe alimchukua mtoto kwenda kumnyonyesha. Denis alimfuata huko huko chumbani, alipiga magoti mbele yake na kusema, “Samahani mke wangu nilikuwa sijajua thamani yako mpaka leo. Yaani leo ndiyo nilichanganyikiwa, nilijua umekufa na tayari nilishaona maisha hayawezekani bila wewe. Ninaahidi nitabadilika nitakuwa mume mwema na kamwe sikunyanyasi tena."
Mama yake ambaye alisimama mlangoni alitingisha kichwa na kucheka huku akisema, “Unavyoringa uachiwe watoto kila siku, unajua uchungu wa kulea wewe au unataka uachiwe ili uje kunitupia wanao hapa nianze kulea wajukuu?!”
Hakusubiri hata jibu aliondoka akimuacha mwanaye akiendelea kuomba msamaha akiwa haamini kuwa mkewe yu hai. Siku ile ndiyo ilikuwa siku ya Mabadiliko kwa Dennis kwani hakuwahi kumpiga wala kumnyanyasa tena mkewe.
*****MWISHO******
K**a umejifunza chochote niachie Comments kisha sambaza iwe Fundisho kwa wengine pia walio na tabia k**a ya Dennis.

Encouraging Line
12/10/2021

Encouraging Line

02/10/2021

MUNGU AKUBARIKI JIONI YA LEO
WEWE UTAKAYE TYPE AMINA!!

*DONDOO ZA UCHUMBA HADI NDOA*Wakati tukiendelea kuombe watu ili kuwapata wenzi wao wakuwafanana!!Lipo jambo la mhimu lim...
28/09/2021

*DONDOO ZA UCHUMBA HADI NDOA*

Wakati tukiendelea kuombe watu ili kuwapata wenzi wao wakuwafanana!!

Lipo jambo la mhimu limejificha katika uchaguzi wa nani anafaa kuwa mwenza bora kabisa na siri hiyo iliyojificha, _ndiyo huwenda ni sahihi kuliko moyo uliojaa matamanio ya uwongo uliowazi katika kiini cha moyo_

Ikumbukwe kuwa, Uchaguzi wa mke/mume hufanywa mara moja tu, kwa hiyo jambo hili lisichukuliwe kirahisi rahisi tu kwa sababu ni la maisha ya mtu

Siri iliyojificha na ndiyo ukweli ulio wazi, ni....! *_Unayempenda, yeye hakupendi ila anampenda mwingine, ila usiyempenda ndiye anayekupenda_*

👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿

Ukifanyia research hiyo salsafa, utakuja gundua kuwa huo ndio ukweli uliojificha vifuani mwa watu wengi!

Kwa kuwa mabinti kwa mila zetu, ndio huwa wanafuatwa kuambiwa anapendwa, kwa hiyo, wao ndio huamua kwamba akubali au akatae! shauri hilo hubakia katika hiari yake

Kunakuwaga na mambo mawili hapo, Anaweza akatokea kijana akimwambia anampenda , ila yeye binti asimpende na ingawa kweli huyo kijana anaupendo wa dhati kabisa kwa binti huyo, atafuatilia na kufuatilia lakini wapi!

Nyie mabinti huwa hamjui tu, kijana anayekupenda kwa moyo wote kabisa, na anampango mzuri na wewe, ni rahisi sana kumgundua,

*Hilo hapo ni somo lingine*

Leo somo letu ni, *Unayempenda naye anampenda mwingine, ila anayekupenda wewe humpendi*

Mungu awasaidie sana vijana kung'amua hicho kitendawili ili muwe na ndoa njema na ya furaha

Mwanadada haupaswi kumfanya kijana wa kiume akupende, isipokuwa yeye ndiye anapaswa autafute upendo wako ulipojificha ijapokuwa unaweza kuwa unampenda!

Binti, ukijipa kazi ya ya wewe umfurahishe kijana eti mpaka amsahau sjiui nani anaye mpenda na akuoe wewe, mwaka hautaisha ndoa yenu itakuwa na kila aina ya migogoro

Somo litaendelea

Address

Vijana
Old Moshi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Thewinners TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share