inuka tena

inuka tena Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from inuka tena, Religious Center, Nzega.

13/05/2026

INUKA TENA.

K**A HUWEZI KUJIKUBARI HIVYO ULIVYO,

HATA KUKIWA VILE 👉
UTAKAVYO HUWEZI KUJIKUBARI,

ACHA KUSHINDANA NA WAKATI
WAKATI UTAKUKUTA JIANI

EV,Meshack c mlenga

INUKA TENA
ANZA UPYA.

12/05/2026

:INUKA
TENA:...

KUMBUKA HII... HAKUNA MTU AWAE YOTE ATAKAE SIMAMA KUPAMBANIA HATIMA YAKO & KUTETEA HATIMA YAKO
SIMAMA PAMBANA MWENYEWE

MENEJA WA KAMPUNI YOYOTE HASIMAMI KUPAMBANIA HATIMA YA TAJIRI YAKE WALA YA KAMPUNI!!

ISIPOKUWA YEYE...

ANASIMAMA KUPAMBANIA MSHAHALA WAKE (ILI MSHAHALA UMUFIKISHE KWENYE HATIMA YAKE

KINYONGA AKIFIKA KWENYE RANGI NYEUSI KIJANI N.K
ANAFANANAZO,HAIMANISHI NIMWOGA ISIPOKUWA ANAFANYA HIVYO IWERAHISI KUWINDA NA KUTO ONEKANA KIRAHISI NA ADUI
NAE ANAPAMBANIA HATIMA YAKE

MAZINGIRA YASIKUFANYE USHINDWE, KUTOKANA NA UKOSEFU WA MIUNDO MBINU YABADILISHE MAZINGIRA, WEWE MWENYEWE YAWE NA MWELEKEO WAKO,

YAGEUZE MAZINGIRA YAWE FULSA, YAFANANE NA WEWE KUFIKIA HATIMA YAKO.

JAMBO LA KUZINGATIA FULSA
NI MAPUNGUFU YALIYOKO KWENYE ENEO LAKO
HAYO MAPUNGUFU NDIYO HATIMA YAKO.

Ev,Meshack c mlenga.

INUKA TENA
ANZA SAFARI YA MATUMAINI.

30/04/2026

SOMO: ANGUKO LA KANISA
Msingi wa Biblia: Ufunuo 2–3, Mathayo 24:4–13, 2 Timotheo 4:3–4
Utangulizi
Kanisa ni mwili wa Kristo (Waefeso 1:22–23), lakini Biblia inaonyesha wazi kuwa kanisa linaweza kuanguka kiroho hata k**a lina majengo, waumini wengi na shughuli nyingi.
Yesu mwenyewe alionya makanisa saba ya Asia Ndogo juu ya hatari ya anguko.
1. Maana ya Anguko la Kanisa
Anguko la kanisa si kufungwa kwa jengo, bali ni:
Kupoteza Nguvu ya Mungu,
Kukosa radha ya ibada, upendo kupungua sana na ibada za maigizo au (sanaa madhabahuni) kanisani (Ufunuo 2:4)
Kuacha kweli ya Neno la Mungu
Kuongozwa na mapokeo, tamaa na dunia na kutotambua nafasi ya Roho mtakatifu ndani ya kanisa .
👉 Kanisa linaweza kuonekana hai, lakini mbele za Mungu likawa limekufa ibada mufu (Ufunuo 3:1).
2. Sababu Kuu za Anguko la Kanisa
(a) Kuacha Neno la Mungu
“Watajiepusha na kuisikiliza kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.”
— 2 Timotheo 4:4
Mahubiri ya kuburudisha badala ya kuonya
Wachungaji kuogopa kupoteza washirika kwa sababu ya maonyo
Mavazi machafu huwezi tofautisha kahaba na alieko kanisani.
Injili ya baraka bila toba
Kuchagua maandiko yanayopendeza masikio
(b) Upendo wa Dunia
“Mtu ye yote akiupenda ulimwengu, kumpenda Baba hakumo ndani yake.”
— 1 Yohana 2:15
Fedha kuwa lengo kuu
Umaarufu kuliko utakatifu
Kanisa kuwa biashara

25/04/2026
22/04/2026

Bwana asifiwe wateule wa bwana Yesu.
hivi unajuwa sababu kuu zinazo pelekea Kuanguka kiroho?
kuanguka kiroho siyo jambo la ghafla tu—mara nyingi huanza kidogo kidogo mpaka mtu unajikuta umepoteza moto wa rohoni.
Hizi ni baadhi ya sababu kuu zinazopelekea mtu kuanguka kiroho:
1. Kuacha maombi
1 Wathesalonike 5:17 — “Ombeni bila kukoma.”
Maombi ni pumzi ya roho. Ukiacha kuomba, uhusiano wako na Mungu unadhoofika haraka.
2. Kutosoma biblia au unasoma hauliishi Neno la Mungu
Hosea 4:6 — “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.”
Bila Neno la Mungu, mtu anakuwa dhaifu kiimani na rahisi kushindwa na dhambi.
3. Dhambi ya siri
Zaburi 66:18 — “Kama ningaliangalia uovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.”
Dhambi ndogo ndogo zisizoshughulikiwa hujenga ukuta kati ya mtu na Mungu.
4. Kiburi
Mithali 16:18 — “Kiburi hutangulia uangamivu.”
Mtu anapoanza kujiona anajitosheleza, anaacha kumtegemea Mungu.
5. Kukosa ushirika na roho mtakatifu
Waebrania 10:25 — “Tusiache kukusanyika pamoja…”
Kujitenga na waamini wengine kunapunguza nguvu ya kiroho.

6. Kupenda dunia kuliko Mungu
1 Yohana 2:15 — “Msiipende dunia…”
Moyo unapojazwa na vitu vya dunia (fedha, tamaa, anasa), upendo wa Mungu hupungua.
Kiburi na kuto onathamani kwa wengine
Kujihesabia haki huondoa kabisa hata kale kaliko baki maana nichukizo kwa mungu kujihesabia haki.
Ev,meshack mlenga

20/04/2026

ITUKA TENA INAKUKARIBISHA KUJIFUNZA PAMOJA FACEBOOK

20/04/2026

MOYO ULIOUMIZWA

1. Moyo wa mwanadamu ni nini?
Katika Biblia, “moyo” siyo tu kifaa cha mwili, bali ni:
Kituo cha hisia
Chanzo cha mawazo
Mahali pa maamuzi ya maisha
đź“– Mithali 4:23
“Linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”
👉 Maisha ya mtu hutoka kwenye hali ya moyo wake.

2. Hali halisi ya moyo wa mwanadamu
đź“– Yeremia 17:9
“Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote…”
👉 Hii inaonyesha:
Moyo unaweza kujeruhiwa
Moyo unaweza kubeba uchungu
Moyo unaweza kupotea bila Mungu

3. Moyo ulio umizwa ni nini?
Ni moyo uliobeba:
Uchungu
Maumivu ya zamani
Kukataliwa
Usaliti
Kukosa upendo
đź“– Zaburi 147:3
“Huponya waliovunjika moyo na kufunga jeraha zao.”
👉 Mungu anatambua moyo uliovunjika.

4. Dalili za moyo ulio umizwa
Mtu mwenye moyo ulioumia anaweza:
Kukosa amani
Kuwa na hasira za haraka
Kuwa na chuki au kisasi
Kujitenga na wengine
Kukosa imani au matumaini
👉 Mara nyingi hujificha kwa nje lakini ndani kuna vita.

5. Madhara ya moyo ulio umizwa
Huzuia maombi kujibiwa
Huvunja mahusiano
Hufungua mlango wa dhambi
Huzuia ukuaji wa kiroho
đź“– Waebrania 12:15
“Mzizi wa uchungu usije ukamea ukawasumbua.”

6. Yesu – mponyaji wa moyo
đź“– Luka 4:18
“Ametumwa kuwaponya waliovunjika moyo.”
👉 Yesu ana nguvu ya:
Kuondoa maumivu ya ndani
Kurejesha furaha
Kujaza amani

7. Njia ya kupona moyo ulio umizwa
(a) Kubali maumivu yako
Usijifanye uko sawa wakati unaumia.
đź“– Zaburi 34:18
(b) Samehe kwa moyo wako wote
Kusamehe ndiyo ufunguo wa uponyaji.
đź“– Waefeso 4:31-32
(c) Mwagie Mungu moyo wako
đź“– Zaburi 62:8
“Miminyeni mioyo yenu mbele zake.”
(d) Jaza moyo wako Neno la Mungu
👉 Neno linasafisha na kuponya ndani.
(e) Jitenge na vitu vinavyoongeza maumivu
Marafiki wabaya
Mazingira ya sumu
Mawazo mabaya
🔥 MFANO WA MAOMBI
“Bwana Yesu,
Moyo wangu umeumia, umebeba uchungu mwingi.
Ninakuletea kila maumivu niliyopitia.
Ninachagua kusamehe leo.
Niponye ndani yangu, ondoa uchungu wote.
Nijaze amani yako.
Nifanye mpya kuanzia leo.
Amina.”
Ev,Meshack mlenga.

18/04/2026

TATIZO TUBWA KWA SASA NIWACHUNGAJI WANAFUNDISHA DINI ZAO WATU WANAHITAJI MUNGU SIYO DINI

18/04/2026

Haleluya
UNASALI
NIKWELI
UMEJIZUIA KUZINI NI KWELI,

KWELI UMEJIZUIA KUNYWA POMBE

UMEJIZUIA KUIBA

Lakini bado unavaa sikuku nyima

Night dress ndiyo nguo zako za mtoko

BAADO Muongo

Ujuwe sehemu yako ni Jehanum
KUMBUKA ULIPO ANGUKA UTENGENEZE
KISHA
INUKA TENA

EV.MESHACK C MLENGA

Address

Nzega
123

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when inuka tena posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share