22/08/2026
Wanaume wengi hujiandaa kwa
dakika 10 za tamaa, Lakini hawajiandai kwa miaka 10 ya matokeo.
Kuna kitu wanaume wengi hawafundishwi, Hujifunza namna ya kumshawishi mwanamke. Lakini.
"Hawajifunzi namna ya kubeba
matokeo ya maamuzi yao" Hapo ndipo wanaume wengi huangukia pua.
Dakika chache kabla hujamgusa...huyu bint jiulize. Je, Ninamwona k**a binadamu mwenye ndoto...Au K**a fursa ya kutuliza tamaa yangu.? Hapa, Majibu yako yatatawala
matendo yako.
Broo...Kuna mwanamke anakutazama k**a sehemu Sahihi na salama.
Anakuamini kuliko anavyoonyesha. Kamwe usithubutu kuchanganye imani yake na udhaifu wake.
Jiulize?! Kesho akiniambia "Nahitaji uwe pembeni yangu." Je, nitabaki..? Au nitaanza kuzima simu. Kubadili njia..Na kujifanya simfahamu..?
Kuna wanaume wanaoshinda vita vya
kumshawishi mwanamke, Lakini wanashindwa vita vya dhamiri zao.
Kwa sababu ni rahisi kuvua nguo Lakini ni ngumu mno kuvua hatia moyoni mwake.
Broo...Usiombe Mungu akupe mwanamke mwema, Wakati wewe bado hujawa
mwanaume salama kwa mwanamke yeyote
Anza kujijenga kwanza.
Jiulize swali moja tu..K**a huyo angekuwa dada yako. Ungejisikia salama kumuacha na
mwanaume mwenye tabia k**a zako leo?
K**a jibu ni "HAPANA" Bado una safari ya kuwa mwanaume wa kweli.
Watu watasahau ulikuwa na pesa kiasi gani...Watasahau ulivaa nini. Lakini kuna mwanamke hataisahau namna ulivyobadilisha maisha yake, Kwa heshima Au kwa maumivu, Broo Uamuzi ni wako.
Broo...Baada ya kusoma post hii Usijiulize "Huyu binti anastahili kuwa na mimi?" Jiulize
"Mimi ninastahili kuaminiwa na binti wa mtu.?"
Kwa sababu Siku ambayo utaanza kujiuliza swali hilo, Hutakuwa umebadilisha mahusiano
yako Tu, Utakuwa umeanza kubadilika wewe mwenyewe.
Na hapo ndipo mwanaume halisi huzaliwa Broo.mwanaume halisi hajivunii idadi ya wanawake aliowahi kuwa nao.
Anajivunia maamuzi aliyofanya bila kuharibu maisha ya mwingine, Hekima kabla ya tamaa
Heshima kabla ya maamuzi.