ZGA Mwanza

ZGA Mwanza Zion Gospel Assembly Church Tanzania

Ibada ya jumapili 02/08/2026Mhubiri : Pastor Boniphace mkamiNdugu ameshiriki neno la Mungu na kanisa juu ya moyo wa daud...
04/08/2026

Ibada ya jumapili 02/08/2026
Mhubiri : Pastor Boniphace mkami

Ndugu ameshiriki neno la Mungu na kanisa juu ya moyo wa daudi ambao ulimpendeza Mungu kwa namna ambavyo daudi alienenda na kuishi hapa duniani.
Kumtumikia Mungu ni faida kwa kuwa ni hazina mbele za Mungu kwaio inatupasa kuutafuta uso wa Mungu kwanza katika maisha yetu.

K**a vile paulo alivomsihi timotheo kuilinda imani ileile aliyojifunza kwake na utumishi usio na maswali wala mashaka, vivyo hivo imetupasa kulinda imani na matendo yetu na kumwamini Mungu juu ya maisha yetu ili safari yetu ya wokovu isiwe bure.

k**a Paulo alivowaambia wakorintho isiwe yeye anawahubiri wengine na mwisho yeye akaja kukataliwa, kwaio yatupasa kumaanisha kabisa katika hii safari hii ya mbinguni.

Zaburi 139: 1-3, 50:3-6,16-23 || 1Timotheo 6:11-16 || 2Timotheo 3 : 10-12 || Wakorintho 9:27

02/08/2026

KARIBU KATIKA IBADA YA JUMAPILI 02/08/2026

Ibada ya jumapili 15/03/2026Muhubiri : Pastor OkwalingaNdugu ameliasa kanisa ya kwamba Yesu anakuja kuchukua kanisa lisi...
21/03/2026

Ibada ya jumapili 15/03/2026
Muhubiri : Pastor Okwalinga

Ndugu ameliasa kanisa ya kwamba Yesu anakuja kuchukua kanisa lisilokua na madoa wala makunyanzi analisafisha kwa injili yake, Kwa neno lake ambalo ni YESU mwenyewe.
Kuokoka sio mwisho, baada ya kuokoka
tunatakiwa tuendelee kuishi katika injili ili tuendelee kubadilishwa kumfaa Kristo.

Ndugu amelitia moyo kanisa ya kwamba kuna maeneo mengi tunaweza kujaribiwa nayo ili kuonyesha hali ya mioyo yetu na hapo ndipo nguvu ya msalaba inapohitajika kuyafia mambo ili kuendelea kumfaa Kristo.

Ndugu ameendelea kulitia moyo kanisa kuukumbatia ujumbe wa msalaba kwasababu
ndiyo nguvu ya Mungu na haki ya Mungu inatupa changamoto ya kuishi kwa imani kwa kumtegemea yeye peke yake.
Mtume paulo anasema Hasha asione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana Yesu
Kristo.

Mwisho amemaliza kwa kusema sisi k**a waamini tudhamirie moyoni kwamba tusione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Yesu Kristo.

VITABU
1Yohana 2:15 || 2Wakorintho 4:3-11 || Wagalatia 6:14 || Warumi 1:16-17 || Waefeso 5:25 || Waebrania 4:12 || Mathayo 13:44-46 || 1Wakorintho17-18

Ibada ya jumapili : 25/01/26Muhubiri: Pastor Elia TambeMtumishi wa Mungu ametukumbusha kua siku ya mwisho kila mtu atato...
30/01/2026

Ibada ya jumapili : 25/01/26
Muhubiri: Pastor Elia Tambe

Mtumishi wa Mungu ametukumbusha kua siku ya mwisho kila mtu atatoa hesabu ya maisha yake mwenyewe, ametukumbusha ile kiu na shauku tuliyokua nayo kwajili ya Bwana na ule upendo wa kwanza uliokua ndani ya mioyo yetu.

Ndugu aamelitia moyo kanisa tujihadhali tusijekua k**a mafarisayo, kwa nje tunaonekana tunaendelea kumbe tumekwama na k**a tunataka kurudi kwenye unyoofu basi turudi kwenye Unyenyekevu, utiifu, hofu ya Mungu na kuweka maisha yetu chini, na k**a tukitaka kanisa lipate raha basi inatupasa wote turudi katika utaratibu wa kanisa, utaratibu wa Mungu.

Mwisho kabisa ndugu ametusihi ya kwamba sisi k**a wana wa kristo imetupasa tutembee na
tushik**ane k**a kanisa.

Math 22:34-46 || Luk 10:25-28 || Waebrani 10:32-36

Address

Mwanza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ZGA Mwanza posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share