19/07/2024
GHADHABU YA MUNGU (1)
JE! MUNGU ANA HASIRA?
Biblia imejaa lugha ya picha na kwamba wema wa Mungu ulioandikwa chini ya vitabu vya Agano la Kale unaonekana katika lugha ya picha.
“Ghadhabu ya Mungu” ni moja ya dhana zinazohitaji uchunguzi wa karibu.
Maneno “ghadhabu ya Mungu” ambayo wakati mwingine yamefasiriwa k**a “hasira ya Mungu” ni maneno yaliyotumika katika vitabu vya Agano la Kale ambayo pia yalitumika katika maandiko ya Agano Jipya.
Tazama jinsi yalivyotumika;
Kutoka 32:11 Musa akamsihi sana Bwana, Mungu wake, na kusema, Bwana, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?
Kumbukumbu la Torati 9:7 Kumbuka, usisahau ulivyomtia Bwana, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hata mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya Bwana.
Ezra 8:22 Maana naliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni kinyume cha wote wamwachao.
Ezra 10:14 Basi maakida wetu na wawekwe kwa ajili ya mkutano wote, na watu wote walio katika miji yetu, waliooa wanawake wageni, na waje nyakati zilizoamriwa, tena pamoja nao na waje wazee wa kila mji, na makadhi wa miji hiyo, hata ghadhabu kali ya Mungu wetu itakapotuondokea mbali, jambo hili lik**alizike.
Zaburi 78:31 Hasira ya Mungu ikapanda juu yao, Akawaua waliokuwa wanono; Akawaangusha chini vijana wa Israeli.
Neno “ghadhabu” pia lilitumika katika vitabu vya Agano Jipya vya Biblia.
Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Warumi 2:5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.
Waefeso 5:6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.
Wakolosai 3:6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.
Ufunuo wa Yohana 14:10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
Ufunuo wa Yohana 14:19 Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.
Sasa neno “ghadhabu” linapaswa kueleweka katika muktadha ambao limetumika.
Lilitumika kwa ajili ya mwanadamu.
Yakobo 1:19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika.
Waefeso 4:26 Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.
Lilitumika kwa ajili ya Mungu.
Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Warumi 1:18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
Waefeso 5:6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.
Lilitumika kwa kile kitakachokuja; tukio la wakati ujao.
Warumi 5:9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Wakolosai 3:6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.
1 Wathesalonike 1:10 na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.
Hebu tuchunguze “ghadhabu” kuhusiana na Mungu, katika Yohana 3.
Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Neno “ghadhabu” lilitafsiriwa kutoka katika neno la Kigiriki “orge” .
Linamaanisha adhabu au kisasi.
Neno mzizi wake ni “orago”.
Neno “orago” linamaanisha hasira iliyotulizwa.
Kwa hiyo, hasira inaweza kumaanisha kuitikia matendo ya mtu kwa kulipiza kisasi au adhabu.
Katika kitabu cha Mwanzo, huwezi kuona ghadhabu ikielezewa k**a mwitikio wa Mungu kwa sababu ya dhambi.
Musa aliandika katika sura ya kwanza ya kitabu cha Mwanzo (Mwanzo 1) kwa kurudia neno “vyema, chema au njema” mara saba (7) katika sura ya kwanza.
Mwanzo 1:4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
Mwanzo 1:10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mwanzo 1:12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema .
Mwanzo 1:18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mwanzo 1:21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mwanzo 1:25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Tazama kwamba mstari wa 31 unatoa muhtasari wa kila kitu ambacho Mungu aliumba kwamba ni chema.
Pia tazama kwamba katika Mwanzo 1, hapakuwa na neno baya lililonenwa.
Ukweli huu unamdhihirisha Mungu kuwa ni mwema.
Neno “vyema, chema au njema” linamaanisha kitu kamili pasipo uovu au chochote cha kudhuru.
Katika Mwanzo 2, hatuoni pia ghadhabu k**a mwitikio wa Mungu katika dhambi. Tazama simulizi la Musa.
Mwanzo 2:16-17 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Haya yamesemwa kabla mwanadamu hajatenda dhambi.
Kumbuka imesemwa mapema katika sura zilizotangulia kwamba utambuzi wa Mungu juu ya dhambi hauthibitishi ushiriki ama kuhusika kwake katika dhambi.
Pia kumbuka kwamba mauti ni kutokuwepo kwa uzima.
Kile ambacho Mungu alimpa mwanadamu katika Mwanzo 1 kilikuwa uzima na katika Mwanzo 2, uliitwa “mti wa uzima”.
Mwanzo 2:9 Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Mwanzo 2:16-17 kwa hiyo ni taarifa ya upendo wa Mungu kumjulisha mtu kabla ya kutojihusisha na dhambi (kutozingatia maagizo yake) na kifo (kutokuwepo kwa maisha yake).
Kwa hiyo inatosha kusema kwamba dhambi na mauti haviwezi kutambulika nje ya mapenzi ya Mungu (nuru na uzima).
Kwa maneno mengine, kinachotafsiri dhambi na mauti ni Mungu.
Tunapoendelea kuchunguza hili itawekwa wazi kwa nini inaitwa “ghadhabu ya Mungu” ingawa yeye hahusiki nayo.
Kwa hiyo Mwanzo 2:16-17 si kauli au tishio la kuua, lakini ni kauli inayoonyesha matokeo ya matendo ya mwanadamu; uzima (Mwanzo 2:9) au mauti (Mwanzo 2:17).
Hivyo mwanadamu alipofanya uchaguzi wa kutenda dhambi katika Mwanzo 3, Mungu alisema matokeo ya kutokutii kwake.
Mwanzo 3:14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Zingatia maneno “umelaaniwa” na “ardhi imelaaniwa”.
Neno “~laaniwa” lilitafsiriwa kutoka katika neno la Kiebrania “arar”.
K**a vile ilivyo kwamba giza ni kutokuwapo kwa nuru na mauti ni kutokuwepo kwa uzima, laana inarejelea kutokuweza; kushindwa.
Ikiwa ardhi imelaaniwa kwa ajili ya mwanadamu, inamaanisha kwamba dhambi ya mwanadamu iliiathiri ardhi hiyo.
Kwa hivyo katika Mwanzo 3 Mungu hakuwa akiitikia dhambi ya mwanadamu, badala yake, Mungu alikuwa akitamka matokeo ya dhambi ya mwanadamu.
Sasa sura inayofuata Mwanzo 4; ndipo neno “ghadhabu” linatajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Mwanzo.
Mwanzo 4:2-5 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
Neno “~ghadhibikia” lilitafsiriwa kutoka katika neno la Kiebrania “charah”.
Lilitumiwa mara 91 katika maandishi ya Kiebrania ya Biblia.
Ni neno lenye nguvu sana linalomaanisha kukasirika, kuchemka, kutofurahishwa au kuwaka.
Tazama jinsi ilivyoelezwa baada ya tukio hili la Kaini.
Mwanzo 18:30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.
Mwanzo 30:2 Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?
Mwanzo 31:35 Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya k**e. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
Mwanzo 31:36 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N'nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii?
Kutoka 4:14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Musa, akasema, Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake.
Kutoka 22:24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.
Kutoka 32:10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.
Kutoka 32:19 Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile michezo. Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.
Kutoka 32:22 Haruni akasema, Hasira ya bwana wangu isiwake, wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya.
Hesabu 12:9 Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.
Hesabu 32:13 Na hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huku jangwani muda wa miaka arobaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa Bwana kikaisha angamia.
Waamuzi 2:14 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.
1 Samweli 18:8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme?
2 Samweli 12:5 Ndipo hasira ya Daudi ikawaka sana juu ya mtu yule; akamwambia Nathani, Aishivyo Bwana, mtu huyo aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa.
Lilielezewa k**a kitu kinachochemka au kuwaka.
Rudi kwenye Mwanzo 4,
Nafasi ya Mungu katika tukio hilo inapaswa kuzingatiwa.
Mwanzo 4:6-8 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 K**a ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. 8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
K**a vile katika Mwanzo 2-3, Mungu alimtahadharisha Kaini; “dhambi iko, inakuotea mlangoni”.
Mwanzo 4:9-11 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? 10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako.
Katika mstari wa 11, neno “~laaniwa” liliandikwa tena.
Tazama njeo ya neno “umelaaniwa”.
Neno hilo lipo katika wakati uliopita.
Hili linaonyesha kwamba Mungu alikuwa akieleza tu mambo yaliyo dhahiri, uhalisia wa kilichofanyika.
Hakuwa akimtamkia Kaini alaaniwe.
Ingawa Kaini alionyesha ghadhabu, hasira yake haipunguzi wema na rehema za Mungu.
Mwanzo 4:13-14 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
Kaini mwenyewe alijua matokeo ya kitendo chake.
Aliomba wema na rehema za Mungu.
Mwanzo 4:15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Simulizi hilo linamaanisha kwamba Mungu alimrehemu Kaini.
Hakuna kitu kilichosemwa k**a ghadhabu ya Mungu, kinachoonekana hapa ni wema na huruma ya Mungu.
Hata hivyo kinachoonekana ni ghadhabu ya mwanadamu.
Ghadhabu ya mwanadamu kwa kuwa Kaini alikuwa na ghadhabu na kumuua ndugu yake.
Kwa hivyo mfano wa kwanza wa mauti ya mwili wa damu na nyama, mauaji na ghadhabu hupatikana kwa mwanadamu.
Yesu alirejelea ukweli huu katika kitabu cha Yohana.
Yohana 8:44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
Neno “Ibilisi” limetafsiriwa kutoka katika neno la Kigiriki “diabolos”.
Neno hili limeonekana hapo awali kurejelea mdanganyifu; Shetani.
Yesu alirejelea kitabu cha Mwanzo. Neno “mwuaji” linamaanisha mchinjaji.
Hii ina maana kwamba katika Mwanzo 4, Shetani alikuwa nyuma ya tukio.
Kwa hiyo alikuwa pia nyuma ya tukio katika Mwanzo 3, ndiyo maana Musa alitumia maneno “nyoka” na “mwerevu”.
Mwanzo 3:1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Paulo alitumia maneno haya kumuelezea Shetani pia.
2 Wakorintho 11:3 Lakini nachelea; k**a yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
Muktadha wa maelezo ya Paulo ulikuwa ni mafundisho ya uongo; wale wanaopotosha ukweli wa Neno la Mungu.
Katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, nyoka; Shetani alielezewa pia.
Ufunuo wa Yohana 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ufunuo wa Yohana 20:2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu.
Kwa hivyo Shetani anaelezewa k**a mwenye hila na k**a muuaji tangu mwanzo.
Kwa hiyo, alikuwa nyuma ya tukio katika kitabu cha Mwanzo.
Hii inaeleza kwa nini mauti na ghadhabu vilipotajwa katika maandiko ya vitabu vya Agano la Kale, havikutajwa bila Mungu.
Hii ni kwa sababu Mungu ndiye anaetafsiri dhambi, mauti na giza ni nini; kwamba hiki ni dhambi na hiki si dhambi, ama hili ni giza na hii ni nuru.
Hata hivyo Mungu ni mwema na mwenye rehema.
Kwa hiyo mwanadamu anapotenda dhambi na kupatikana na matokeo ya dhambi, inarejelewa k**a ghadhabu ya Mungu kwa sababu wema wa Mungu na rehema au uwezo wa kuokoa haupo katika dhambi hiyo.
Kumbuka kutoka katika sura iliyotangulia kwamba neno “dhambi” lilitafsiriwa kutoka katika neno la Kiebrania “chattah” ambalo linamaanisha kwamba kuna kitu kinakosekana.
Tazama zaidi kwamba ilikuwa ni kukataa kutii na kupokea ahadi ya Mungu.
Kwa hivyo, "dhambi" ina maana ya upungufu au kuna kitu kinakosekana ambacho ni MUNGU.
Sasa kumbuka kutoka katika utangulizi wa kitabu hiki kwamba, matumizi ya tamathali za semi yaliongelewa na moja ya tamathali hizo ni “metonimia”.
Metonimia ni tamathali ya semi ambapo kisehemu huwakilisha kitu kizima au kitu kizima huwakilisha kisehemu fulani.
Kutokutenda kwa Mungu katika dhambi; kutokuamini na matokeo yake ndiyo huitwa ghadhabu ya Mungu.
Kwa hiyo “ghadhabu ya Mungu” ni tamathali ya semi inayoitwa “metonimia”.
Baada ya kuona hakuna ghadhabu kwa Mungu tangu mwanzo, basi baadhi ya matukio yanahitaji kuwekwa wazi.
MAPIGO YA MISRI
Musa alielezea neno “mwenye kuharibu” wakati wa Pasaka.
Hebu tutazame maandio ya Musa.
Kutoka 12:23 Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.
Kutoka 6:1 Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.
Kutoka 7:17 Bwana asema, Katika jambo hili utanijua ya kuwa mimi ndimi Bwana; tazama, nitayapiga haya maji yaliyo mtoni kwa fimbo hii niliyo nayo mkononi mwangu, nayo yatageuzwa kuwa damu. 18 Na hao samaki walio mtoni watakufa, na huo mto utatoa uvundo; nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni. 19 Bwana akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Shika fimbo yako, kaunyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya mito yao, juu ya vijito vyao, na juu ya maziwa ya maji yao, na juu ya visima vyao vyote vya maji, ili yageuke kuwa damu, nako kutakuwa na damu katika nchi yote ya Misri, katika vyombo vya mti, na katika vyombo vya jiwe.
Kutoka 8:1 Bwana akamwambia Musa, Ingia kwa Farao, ukamwambie, Bwana asema hivi, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia. 2 Tena k**a ukikataa kuwapa ruhusa, tazama, nitaipiga mipaka yako yote kwa kuleta vyura; 3 na huo mto utafurika vyura, nao watakwea juu na kuingia ndani ya nyumba yako, na ndani ya chumba chako cha kulala, na juu ya kitanda chako, na ndani ya nyumba ya watumishi wako, na juu ya watu wako, na ndani ya meko yako, na ndani ya vyombo vyako vya kukandia unga.
Kuna pigo moja kubwa ambalo tunaweza kulichunguza katika Kutoka 11.
Kutoka 11:1 Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa... 4 Musa akasema, Bwana asema hivi, K**a usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati ya Misri; 5 na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. 6 Ndipo kutakuwa na kilio kikuu katika nchi yote ya Misri, ambacho mfano wake haujakuwa bado majira yo yote, wala hautakuwako mfano wake tena kabisa.
Pigo hili k**a jinsi ilivyo katika mapigo mengine yote lilihusishwa na Mungu.
Katika Kutoka 12, maagizo yaliyotolewa kwa Israeli kuhusu pigo hili yanaweza kuonekana.
Kutoka 12:3 Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwanakondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja; 4 na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo. 5 Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. 6 Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. 7 Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla. 8 Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. 9 Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani. 10 Wala msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. 11 Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana. 12 Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. 13 Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.
Maagizo yaliyotolewa kwa Waisraeli hapa ni kwamba wanapaswa kuchinja mwana-kondoo na kuitia damu katika miimo ya mlango katika kizingiti cha juu katika nyumba ili kuzuia madhara ambayo yangetokea.
Katika tukio hili, ulinzi kutoka katika uovu ulihusishwa na Mungu hata hivyo uovu wenyewe pia ulihusishwa na Mungu.
K**a vile ilivyoonekana katika kitabu cha Mwanzo, kuna nafsi nyuma ya tukio.
Na hiyo ndiyo iliyoitwa “mwenye kuharibu” (Kutoka 12:23).
Sasa huyu hawezi kuwa Mungu kwa sababu Mungu aliumba vitu katika kitabu cha Mwanzo; hakuharibu.
Katika Septuagint (tafsiri ya Kigiriki ya maandiko ya Kiebrania) neno “mwenye kuharibu” ni neno “olothreuo”.
Neno hilo lilielezwa katika Nyaraka.
Tazama jinsi lilivyoelezwa:
1 Wakorintho10:10 Wala msinung'unike, k**a wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.
Waebrania 11:28 Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao.
Neno la Kigiriki “olothreuo” linamaanisha kuharibu; kuua.
Tazama kwamba mwandishi wa kitabu cha Waebrania hakusema Mungu alikuwa akiwaua wazaliwa wa kwanza wala Paulo hakusema kwamba Mungu ndiye mharibifu.
Hata hivyo, tazama muktadha wa mjadala wake.
1 Wakorintho 10:1-5 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
Paulo alisema kwamba hawakumpendeza Mungu.
Kwa hiyo sababu ya kuangamizwa ama kuharibiwa kwao ilikuwa ni kwa sababu hawakuwa katika imani na hivyo hawakuwepo katika uwezo wa Mungu uokoao.
Hii ni sawa na maelezo ya mwandishi wa kitabu cha Waebrania.
Alifundisha kwa kutumia neno “kwa imani”.
Kwa hiyo ukosefu wa imani ambao ni kutokuamini ni kutokuwepo katika nguvu za kuokoa za Mungu.
Tazama rejea nyingine za neno hilo.
1 Wakorintho 5:5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.
1 Wathesalonike 5:3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, k**a vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
2 Wathesalonike1:8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu.
2 Wathesalonike 1:9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.
1 Timotheo 6:9 Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
Zingatia kwamba kila rejea hapo juu ilihusiana na dhambi.
Uharibifu ni uharibifu wa dhambi.
Tazama mistari ya awali katika 1 Wakorintho 10: 10.
1 Wakorintho 10:7 Wala msiwe waabudu sanamu, k**a wengine wao walivyokuwa; k**a ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze. 8 Wala msifanye uasherati, k**a wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. 9 Wala tusimjaribu Bwana, k**a wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
Neno “~jaribu” linamaanisha kuomba kile ambacho mtu hawezi kufanya.
Kushinikiza zaidi ya uwezo wa mtu.
Ni neno lile lile linalopatikana katika Mathayo 4:7.
Mathayo 4:7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Luka 4:12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Linamaanisha kwenda nje ya mipaka ya mtu.
Yakobo alikuwa wazi kwamba Mungu hajaribiwi na maovu katika Yakobo 1:13.
Linapatikana pia katika Injili ya Luka.
Luka 10:25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?
Kwanini Paulo alisema wasimjaribu Bwana?
Hapo awali alisema yafuatayo.
1 Wakorintho 10:3-4 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
Alikuwa akirejelea ujumbe; ujumbe wa Kristo yaani, walikuwa wakisisitiza ama wakishinikiza zaidi ya ujumbe.
Kwa hiyo maneno “~jaribu Bwana” yanarejelea kutokuamini.
Kumjaribu Bwana maana yake walikwenda zaidi ya uwezo wake.
K**a vile mwandishi wa kitabu cha Waebrania alivyoandika.
Waebrania 4:1 Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. 2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile k**a hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. 3 Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; k**a vile alivyosema, K**a nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.
Kudumu kwao katika kushinikiza na kutokuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini ilikuwa ni kujaribu.
Walitoka katika uwezo wake wa kuokoa ambako ndiko kunaitwa ghadhabu ya Mungu.
Katika ghadhabu hiyo, anasema kulikuwa na “mwenye kuharibu”.
Huyu mwenye kuharibu si Mungu lakini kwa hakika Shetani alijificha nyuma ya dhambi na kutokuamini.
Kumbuka:
2 Wathesalonike 1:9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.
Walikuwa “wametengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake” na kwa sababu hii, wataangamizwa.
Ni matokeo ya kutokuamini.
Katika 2 Wafalme 1:10-14, tunaweza kuona Eliya akikutana na watu kadhaa.
2 Wafalme 1:10 Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake 14 Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi. 12 Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. 13 Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako. 14 Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako.
Watu kadhaa walikufa kwa sababu ya tukio hili.
Kumbuka kutoka katika utangulizi wa kitabu hiki kwamba wanafunzi walifikiri wangekuwa wanamtumikia Mungu kwa kutuma moto kuwateketeza watu (Luka 9:51-56).
Hili lilitokana na kile ambacho Eliya alisema; “ikiwa mimi ni mtu wa Mungu…”.
Hii ina maana kwamba Eliya alimhusisha Mungu katika uwezo wake wa kuua.
Kutoka katika maneno ya wanafunzi katika Luka 9, ni dhahiri kwamba kile Eliya alifanya hapa kilichukuliwa k**a kazi au matendo ya Mungu.
Hii inaelezea kwa nini wanafunzi wa Yesu walimwomba awaruhusu kufanya jambo lile lile; kuharibu au kuangamiza watu kwa sababu hawakumpokea Yesu.
Tazama mwitikio wa Yesu tena.
Luka 9:55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] 56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Neno “akawakanya” limetafsiriwa kutoka katika neno la Kigiriki “epitimao” ambalo lilirejelewa mara 29 katika vitabu vya Agano Jipya vya Biblia.
Linamaanisha kushutumu; kukosoa; kukemea vikali.
Lilielezewa kila wakati katika maana mbaya au hasi.
Mathayo 17:18 Yesu akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.
Mathayo 8:26 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.
Inaweza kuonekana kwamba k**a Yesu alikemea vikali hatua iliyokusudiwa na wanafunzi wake.
Kwa hivyo kitendo cha Eliya katika maangamizi ya watu (2 Wafalme 1) kwa hakika kingeleta mwitikio huo huo.
Ni wazi kwamba Yesu alikuwa akisahihisha kitendo cha Eliya.
Tazama mstari wa 55b hadi 56 katika Luka 9.
Luka 9:55 [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] 56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
Hii ina maana kwamba alichofanya Eliya hakikuwa kwa uwezo wa Roho wa Mungu.
Yesu hakumhusianisha Mungu na maangamizi ya maisha ya watu kutokana na mwenendo wao.
Suala hapa ni kwamba kwa karne nyingi kabla ya wakati huo na hata katika akili ya Eliya mwenyewe, tendo la Eliya na tendo la uharibifu wa maisha ya watu lilikuwa limehusianishwa na Mungu; kwamba ni kwa uwezo wa Mungu.
Kwa hivyo kuenea na kukubalika kwa mfumo fulani wa imani hakufanyi mfumo huo wa imani kuwa kweli.
Athari ya hili ni kwamba, hakuwezi kuwa na uelewa wa Mungu au tabia yake kwa kuangalia tu katika maandiko ya Agano la Kale.
Ili kupata ufahamu ama uelewa kamili mtu anatakiwa kutazama tu katika Kristo; matamshi na matendo yake.
Ilikuwa dhahiri kwamba kumekuwa na dhana potofu iliyo wazi kumhusu Mungu wakati wote huo.
Felician Makarios Phos
Kainos Creation Church (KCC)
0742107009