15/08/2026
KILE NILICHOJARIBIWA NACHO
Kuna nyakati kwenye maisha Mungu hutaka tujifunze na kuhubiri sio kile tukisikiacho au tukisomacho tu, Bali kile ambacho tumekiishi au tunakiishi - experienced - ( Ayubu 42:5 ).
Leo ni jumapili, ndugu Mchungaji twende tukahubiri alichotupa "Baba wa mianga" hata k**a unaona Bado hakijatokea kwako wewe hubiri; ndio ! kila MTU ANA MAJIRA YAKE; tambua tu kuwa, Kuna mtu Hilo neno litamsaidia kwa kuwa litakutana na majira yake, yaani leo ndio majira yake ya kukutana na Bwana kwa neno hilo.
Hubiri uzima hata k**a unahisi ugonjwa ndani yako, hubiri kuinuka hata k**a huoni dalili yoyote ya kutoka hapo ulipo, hubiri nasema tena hubiri wakati ukufaao na wakati usio kufaa ( 2 Timotheo 4:2 ).
Mtume Paulo katika barua ya Wagalatia ( 4:14 ) anaonesha kuwa alikuwa katika jaribu la kiafya, lakini katika nyaraka zake, tunaona Mungu akimtumia katika karama , vipawa na madhihirisho mengi ya roho mtakatifu ( 1 Wakorintho 2:1-5 ).
Kuna wakati utapewa neno la faraja wakati wewe mwenyewe una huzuni kuu, Kuna wakati utapewa neno la Imani wakati hofu imetawala moyo wako, ndio Kuna wakati utapewa neno la uponyaji wakati ukiwa hauwezi ( wewe hubiri ).
Kuna nyakati nilifundisha kuwa Mungu anajibu maombi walakini nikiwa na Mimi nasubiri niliyoomba yajibiwe,
Kuna wakati nilifundisha Kusamehe lakini wakati huo na Mimi natamani kuwa na moyo wa msamaha,
Kuna wakati nilifundisha utoaji katikati ya vipindi ambavyo nilipambana na roho mtakatifu mara anioneshapo mahali pa kupeleka hazina yangu,
Kuna nyakati nilihubiri kuhusu maombi lakini Mimi pia nikiwa na struggle ili niwe na maisha ya maombi ( nazikumbuka nyakati hizo ).
Katika mambo yote nimejifunza, kuhubiri ni jambo Moja ila kuhubiri ulichokiishi ni jambo lingine. Na kila mhubiri ni lazima apite kwenye kipimo Cha kupimwa katika Yale anayohubiri.
Waebrania 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
¹⁶ Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
____________
Michael FOJ
T.A.G - Valley Of Blessing - BLB
Mwanza, Tanzania.
+255 (0) 757 129 776.